Askari wa jiji wakiwapakia wafanyabiashara kwenye ‘Karandinga’ ya askari polisi.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, aliyezungumza , alifafanua chanzo cha
askari kutumia nguvu hiyo, ambapo alisema ni baada ya wananchi kuwapiga
mawe wakati wakitekeleza zoezi lao.
“Majuzi askari wa jiji walikwenda maeneo ya Segerea kwa ajili ya
kufanya oparesheni ya kuwaondoa wafanya biashara kandokando mwa
barabara, wananchi wakaanza kuwapiga mawe na kufanya zoezi hilo kuwa
gumu. Ndiyo maana leo baada ya kuanza kupigwa mawe, nao wakaamua kutumia
mabomu ya machozi katika kuwatawanya.’’
No comments:
Post a Comment