Monday, November 24, 2014

MTOTO ATUMIWA KUMWIBA MTOTO MWENZAKE, AKAMATWA..



Mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake. Tukio hilo la kushangaza lililonaswa na Ijumaa Wikienda lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 mchana maeneo ya Majengo Mapya, Kata ya Kihonda jirani na nyumbani kwa aliyekuwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, marehemu Alberth Keneth Mangweha ‘Ngwea’.Hatari! Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Kihonda mjini hapa anayesoma darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi Noto Sosario, anadaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake kisha kukamatwa na kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira zaidi ya 300.
Raia wenye hasira kali wakimsubiri kwa hamu mtoto huyo nje ya nyumba aliyohifadhiwa. 
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa kwa jirani yangu, Asha Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo kwa njia za kichawi hivyo mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia mwizi. 
Kamanda akimbana mtoto huyo kwa maswali. “Mtoto alikuwa amevaa nguo nyeusi ndipo umati ukajitokeza na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku wengine wakimpiga vibaya na kutishia kumuua.
Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto huyo kwa usalama zaidi. “Baada ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani kwangu.“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
Mtoto huyo akichukuliwa kwenye 'Defender' kuelekea kituo cha Polisi.Kwa upande wake, mtoto huyo alisema: “Bibi ndiye huwa ananituma. Kwa sasa niko kwenye ulimwengu wa giza na mateso makubwa.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Vicent alisema: “Mwanangu nilimzaa akiwa salama lakini tangu atoke Moshi (Kilimanjaro) kwa bibi yake amekuwa wa ajabu hivyo nimepanga kumpeleka kwenye maombi.”

MZEE WA MIAKA 75 AMPA MIMBA BINTI WA MIAKA 13


Matukio ya mimba za utotoni yamekuwa yakijitokeza kila kukicha yakiwa na sura tofauti, mengi yametajwa kuharibu maisha na kupoteza ndoto za wasichana wengi.

Kutoka Nigeria Mzee mwenye umri wa miaka 75 anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.Mzee huyo Pa Alabi ambaye ni fundi seremala aliombwa na binti huyo kumtengenezea kiboksi cha kuhifadhia pesa zake, baada ya kumpa kiboksi hicho akaanza kumtongoza na kujenga ukaribu nae hadi binti akakubali. 
“..Siku yenyewe nilimwelezea hisia zangu na akaahidi kulifikiria suala hilo na baadae akakubali, tulikutana kimwili pale nilipomuomba na tulikuwa tukiheshimiana, ghafla akaacha kuja kwangu baada ya siku tano baada ya ile siku ya kwanza tulipokutana kimwili. Siku moja akaja na kuniambia Bibi yake alimwambia ni mjamzito ndipo alipoacha kuja kwangu na sikumuona tena hadi Polisi walipokuja kunikamata..– Pa Alabi. 
Siku ya kwanza msichana huyo kukutana na Alabi alimpatia hela Naira 200 na kumnunulia simu ya mkononi yenye thamani ya Naira 150 pesa za Nigeria na baada ya kukamatwa na kuhojiwa alijitetea kuwa hakujua kama ni kosa kukutana kimwili na binti huyo mdogo na kueleza kuwa lengo lake ilikuwa ni kumuoa na kumtunza yeye na mtoto wake.

TARATIBU ZA TIBA ZA RAIS ZAKAMILIKA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taratibu za Tiba za Rais zakamilika
Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.
Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.
Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.
Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Novemba,2014

MWIGULU NCHEMBA ATEMA SUMU,WEZI WA ESCROW/IPTL WAKAMATWE,WAFILISIWE,WAFUNGWE.KUJIUZULU TU HAITOSHI.


VIONGOZI WA SPLM KUTOKA SUDANI KUSINI WAMFUATA KINANA MASASI


 Jenerali James Kok ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu, SPLM, Mbunge , amewahi kuwa Waziri wa masuala ya kijamiii na bisahara katika serikali ya umoja wa kitaifa  Sudan,SPLM - IG akiwasalimu wananchi wa Masasi. Msafara wa viongozi hao kutoka Sudani kusini ulifika wilayani Masasi kwa lengo la kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye shati la kijani) pamoja na viongozi wa chama cha SPLM kutoka Sudani Kusini wakiwa wameinua mikono juu kama ishara ya umoja na mshikamano,Masasi mkoani Mtwara.
Kutoka Kushoto ni Dkt. Cirino Hiteng,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Bw.Goy Jooyul na Jenerali James Kok.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa chama cha SPLM kutoka Sudani ya kusini waliomfuata Masasi mkoani Mtwara ambapo Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara ya kukijenga na kukiimarisha chama mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Jenerali James Kok kutoka chama cha SPLM Sudani ya Kusini ambaye yeye pamoja na viongozi wenzake wamefika mpaka Masasi kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM

HII NI NOMA KULIKO ZOTE

THIS is not fair (Hii siyo sawa)! Tunaweza kufumba macho na kuacha kusema kinachoendelea katika baadhi ya ‘madudu’ serikalini, lakini linapokuja suala la uchotwaji wa Sh. bilioni 306 za umma kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, tuache masihara, minoti hiyo iliyoibwa na wajanja wachache, inauma sana, Ijumaa Wikienda linakudadavulia zaidi.
Mfano wa burungutu la fedha yaliyochotwa Benki Kuu.
KWANZA ESCROW NI NINI?
Tunajua wengi wanafahamu kinachoendelea kuhusu Escrow ambapo sasa limekuwa gumzo ndani ya bunge na kwenye mijadala mbalimbali ya wananchi wa kada tofauti lakini si vibaya tukaijua zaidi kwani inadaiwa sakata hilo linampa wakati mgumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa na serikali ili kuhifadhi fedha za umma baada ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kuingia mkataba wa kununua nishati ya umeme kutoka Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) mapema miaka ya 2000.
Baadaye Tanesco iligundua kwamba, bei ya umeme wanayouziwa na kampuni hiyo ni kubwa, hivyo walikwenda kuipinga katika mahakama ya kibiashara.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
ILIVYOFUNGULIWA SASA
Wakati mvutano huo ukianza, ndipo serikali ilifungua akaunti hiyo kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambako Tanesco iliweka fedha ilizokuwa ikizilalamikia kwa ajili ya kuilipa IPTL kama tozo ya umeme (capacity charges) hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi juu ya kama kweli bei hiyo ilikuwa halali kwa Tanesco au la!
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
WAJANJA WAZICHOTA
Lakini wakati shauri hilo likitua kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (UCSID) na uamuzi ukiwa bado haujatolewa, inadaiwa Wizara ya Nishati na Madini iliidhinisha fedha hizo zitolewe BoT na kulipwa Kampuni ya PAP ambayo ilishainunua IPTL, wizara ilidaiwa kuamini Tanesco wangeshindwa kesi hiyo.
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Hukumu ilipotoka, Tanesco waliibuka na ushindi na kutakiwa kulipwa fedha kibao lakini walipokwenda kuchungulia kwenye akaunti walikuta hakuna kitu, sakata likaanzia hapo sasa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
NI FEDHA NYINGI KIASI GANI?
Kwa utafiti uliofanywa na gazeti hili, shilingi bilioni 306 ni fedha nyingi kiasi kwamba kama zikipangwa katika chumba chenye ukubwa wa futi 10 kwa 10, vitahitajika vyumba viwili vilivyojaa kuanzia chini hadi juu pasipo na pangaboi.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.
INAUMA JAMANI
Kama hiyo haitoshi, hesabu zinaonesha, endapo kijana mwenye umri wa miaka 18 sasa, aliyemaliza elimu ya kidato cha nne na yupo tayari kuanza maisha, akipewa sehemu ndogo tu ya fedha hizo halafu akafanya matumizi ya kufuru bila kufanya kazi wala biashara yoyote, ataweza kufa akiwa na miaka 75 huku akibakisha chenji kubwa.
Kwamba, endapo kijana huyo atatumia shilingi laki tano (500,000) kila siku (watumishi wengi wa serikali wanalipwa chini ya kiwango hiki) kwa mwaka mzima wenye siku 365, atakuwa ametumia shilingi milioni 182.5 tu!

UFAFANUZI WAKE
Maana yake ni kwamba hadi atakapofikisha umri wa miaka 75, ikiwa ni miaka 57 tangu aanze kutumbua fedha hizo akiwa na miaka 18, atatumia shilingi bilioni 10.4 tu, sawa na asilimia chini ya sifuri ya mabilioni hayo ambayo baadhi ya wakubwa ‘wamejisevia’. Kweli inauma sana!

WABUNGE WALIOICHARUKIA
Kashfa hiyo imeshikiwa bango na wabunge karibu wote wa kambi ya upinzani na baadhi kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), ingawa wanaoonekana kuwa vinara ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye ndiye aliyeibua kashfa hiyo.
Kafulila, ambaye Jumamosi iliyopita alifunga ndoa nyumbani kwao Kigoma, alisababisha purukushani kubwa ndani ya bunge alipoibua sakata hilo kiasi cha kutaka kupigwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

KINA NANI KIKAANGONI?
Sakati hili limewakalia vibaya baadhi ya vigogo serikalini, akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anayedaiwa kutumika ili kuifunika ripoti ya CAG isijadiliwe bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndullu na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka.
Wengine wanaohusishwa na kashfa hiyo baada ya kubainika kupewa mgao wao kupitia kwa mmoja wa watuhumiwa ni pamoja na waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mwanasheria Mkuu wa serikali wa zamani, Andrew Chenge.

KITAELEWEKA KESHOKUTWA
Hatima ya vigogo wanaotuhumiwa kuchota mabilioni hayo ya fedha inatarajiwa kujulikana Novemba 26, mwaka huu (keshokutwa) wakati ripoti ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itakapopiga hodi bungeni na waheshimiwa kuanza kuijadili.
CREDIT: GLOBAL PUBLISHERS

MBUNGE WA KIGOMA KUSINI,MHE DAVID KAFULILA NA JESSICA KISHOA WAUNGANA NA KUWA MWILI MMOJA



 Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma,  jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila akiwa kanisani  na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa  kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
 Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi 
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba  harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe  Zitto Kabwe na Mhe David  Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma
Mkoko waliotembelea siku hiyoHammer

RAIS KIKWETE ATOLEWA NYUZI KATIKA MSHONO, AFYA YAKE YAZIDI KUIMARIKA


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri.

MAUAJI YA KENYA YANALENGA KUZUA UHASAMA WA KIDINI


Baadhi ya miili ya abiria waliouawa jana na Al-Shabaab eneo la Mandera, Kenya.
Basi lililotekwa na Al-Shabaab eneo la Mandera likiwa njiani kuelekea Nairobi.
MSHAURI wa Rais Uhuru Kenyatta wa nchini Kenya, Abdikadir Mohammed amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi nchini humo jana yalilenga kusababisha vita vya kidini.Kwenye mahojiano na BBC Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa Wakenya kutoka madhehebu yote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri ambao walishindwa kukariri Koran.Al-Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani wa Mombasa.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.
Wanajeshi wakiwa eneo la tukio.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Baadhi ya miili ya watoto ambao nao waliuawa katika shambulio hilo.
Miili ya marehemu ambao wengi walikuwa siyo waislamu.
Ndugu wa marehemu wakiwa na simanzi wakati wa kupokea miili ya wapendwa wao jijini Nairobi.