Monday, August 18, 2014

MAZITO YAIBUKA NDOA YA GARDNER NA JIDE


Stori: WAANDISHI WETU
Jambo limezua jambo! Nyuma ya habari ya madai ya kuvunjika kwa ndoa ya Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na Mtangazaji wa Radio Times FM, Gardner G Habash, kuna mambo mazito yameibuka, mara baada ya habari hiyo kuripotiwa na gazeti pacha la hili, Ijumaa la wiki iliyopita.
Uzio wa nyumba ya Staa, ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’Gardner G Habash, ikiwa umezungukwa na nyasi.
Katika habari hiyo, ilielezwa kwamba mitandao mingi ya kijamii ndani na nje ya Bongo ilipambwa na sakata la mastaa hao kudaiwa kutengana huku Gardner akikanusha kwamba hakuna kitu kama hicho.
Mara baada ya habari hiyo kwenda hewani, wikiendi iliyopita gazeti hili lilipokea simu nyingi zikianika undani wa kile wanachokijua.
“Gardner atuambie ukweli maana hata huku nyumbani (Kimara-Temboni, Dar) tuna zaidi ya miezi miwili hatuwaoni,” alisema mmoja wa wapiga simu hao.
Geti la nyumba hiyo likiwa na vumbi.
Ili kuthibitisha kilichosemwa, gazeti hili lilifika nyumbani kwa mastaa hao na kushuhudia geti na nyumba vikiwa na mavumbi ya kutotumika huku kukiwa hakuna hata alama za tairi za gari.Wanahabari wetu walishinda eneo hilo bila wawili hao kurejea nyumbani ambapo kwa mujibu wa majirani, Gardner alionekana akiingia nyumbani hapo akiwa na gari aina ya Toyota Coaster la bendi yao ya Machozi na alipoondoka ndiyo ikawa kimoja.
“Ninyi angalieni mazingira. Ona maua na miti ilivyoweka vichaka na pori. Ni vigumu kuamini kama staa mkubwa kama Jide anaishi kwenye mazingira kama haya,” alisema mmoja wa majirani zao.
Gazeti hili liliweka ‘patroo’ ya jirani huyo ambaye hadi tunakwenda mitamboni, wawili hao walikuwa hawaonekani nyumbani hapo.
Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na Mtangazaji wa Radio Times FM, Gardner G Habash wakiwa katika picha ya pamoja.
Pamoja na yote hayo na ishara mbaya zinazoonekana juu ya wawili hao ikidaiwa kila mmoja anaishi kivyake, bado Gardner amekuwa akisisitiza hakuna chochote kinachoendelea na kwamba hajui anayeeneza habari hizo ana lengo gani.
Kwa upande wake Jide, wikiendi iliyopita alitupia mtandaoni picha ya kidole chenye pete ya ndoa huku akiombwa chondechonde na mashabiki wake aendelee kutetea ndoa yake.

WATU 4 WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA JIWE USIKU WA MANANE JIJINI MWANZA

Screen Shot 2014-08-19 at 9.04.45 AM

Watu wanne wa familia mbiili tofauti wakazi wa mtaa wa Nyerere A, eneo la Mabatini jijini Mwanza wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na mawe wakiwa wamelala.

Tukio hilo limetokea majira ya saa Nane usiku wakati mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali pamoja na radi ilipokuwa ikinyesha.
Mwandishi amefika katika eneo la tukio na kushuhudia wananchi wakishirikiana na jeshi la uokoaji na zimamoto pamoja na askari polisi wakiendelea na kazi ya kufukua miili iliyonasa chini ya jiwe kubwa.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyerere A, mabatini jijini Mwanza Hassan Maulid amewataja waliofariki dunia kuwa ni Sayi Otieno na Kwinta Kweko ambao ni mume na mke huku watoto wawili Kelfine Masalu na Emanuel Joseph wa familia ya Bw.Joseph William nao pia wakipoteza maisha baada ya chumba walichokuwa wamelala kuangukiwa na jiwe lililoporomoka kutoka juu mlimani.
Kaimu kamanda wa jeshi la uokoaji na zimamoto mkoa wa Mwanza inspekta Augustino Magere amewashauri wakazi wa jiji la Mwanza waishio maeneo ya milimani kuchukua tahadhari ili kuepusha maafa kama yaliyojitokeza.
Wakisimulia tukio hilo katika hali ya majonzi na simanzi, baadhi ya wakazi wa mtaa huo wa Nyerere A, wanaeleza namna walivyoupokea msiba huo mkubwa.
Huyu ndiye mtoto pekee aliyenusurika kifo baada ya wazazi wake kufariki dunia kufuatia nyumba yao kuangukiwa na jiwe kubwa.


Screen Shot 2014-08-19 at 9.04.53 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.00 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.07 AM

Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.46 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.53 AM

 

WAPINGA NDOA KATI YA MUARABU NA MYAHUDI



     Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel
Wayahudi wanne wenye msimamo mkali wamekamatwa nchini Israeli baada ya kuzua rabsha katika      sherehe ya kuadhimisha harusi ya mwanamke myahudi aliyebadili dini na kuwa Muislamu na kisha  kuolewa na mwanamume Mwarabu rai ya wa Israeli. Mamia ya watu waliandamana nje ya ukumbi uliotumika kwa sherehe hiyo katika mji wa Rishon LeZion Jumapili wakipinga ndoa hiyo licha ya kuwepo kwa maafisa wa Usalama.
Bwana harusi , Mahmoud Mansour, alikuwa amechukua hati ya mahakama ya kupinga kufanyika kwa maandamano ya kupinga nikaha yake lakini maafisa wa usalama wakashindwa kuzima maandamano hayo


  Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel

Bi Harusi Morel Malka, alikuwa amewaalika wageni 500 katika hafla hiyo.
Bi Malka, 23, alikuwa amesilimu kabla ya sherehe hiyo kuambatana na desturi za kiislamu.
"Kwa kweli tunaishi pamoja kwa amani na sielewi kwanini ndoa hii inawahusu watu." alisema bwana Mansour, 26.
Rais Rivlin alifananisha maandamano hayo dhidi ya ndo hiyo na ''panya anayengata msingi wa unaoliunganisha taifa hilo la Israeli''.



 Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel

Rais wa Israeli Reuven Rivlin amekashifu upinzani dhidi ya ndoa hiyo .
Muungano wa wayahudi wenye msimamo mkali Jewish Lehava walipewa ruhusa ya kuandamana kupinga ndoa hiyo ilimradi tu wasikaribie chini ya mita 200 karibu na ukumbi wa sherehe hiyo.
Kundi hilo linapinga ndoa kati ya Wayahudi na Waarabu.
Waandamanaji wanne walikamatwa na polisi kwa kukiuka masharti yao kulingana na mtandao wa habari wa kiyahudi.
Sadfa ni kuwa kundi lingine linalounga mkono ndoa kati ya Waarabu na Wayahudi lilifanya maandamano kuunga mkono ndoa hiyo na hivyo kuwalazimu maafisa wa usalama kufanya kazi ya ziada kuzuia makabiliano baina ya makundi hayo hasimu.

UKAWA WAMTESA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, AWABEMBELEZA KURUDI BUNGENI DODOMA.


Mwanasheria Mkuu akizungumza wakati wa mkutano na waandishi jijini Dar es Salaam jana. Picha na Salim Shao.

Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amesema mchakato wa Katiba Mpya ukikwama kufika mwisho kutokana na mvutano unaoendelea wa makundi mawili kushikilia misimamo yao, kutafanyika marekebisho ya 15 katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977 ili kuruhusu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Pia, ameipongeza iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuandaa Rasimu bora na kuwaomba wajumbe wake kuwa na ngozi ngumu ya uvumilivu katika kipindi hiki na waepuke kurushiana maneno na watu wanaowakejeli.


Jaji Werema aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea mchakato huo ulipotoka, ulipofika na unakokwenda huku akitumia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Rasimu ya Katiba kufafanua baadhi ya mambo.


Mwanasheria huyo, akijibu swali aliloulizwa kuwa Bunge Maalumu la Katiba linaendelea wakati wajumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiwa hawashiriki, Je, ikishindikana kupatikana kwa theluthi mbili itakuaje? Alisema: “Katika kamati theluthi mbili inatosha, lakini kule mwisho (katika kura ya maoni ya kuipitisha Katiba itakayopendekezwa) kama tutafika darajani, hilo ni suala la siku za usoni.


“Kama tutafika huko na kukuta hakuna pa kutokea, tutarudi bungeni (Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na kufanya marekebisho ya 15 katika Katiba ya sasa ya mwaka 1977 kama uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi, mgombea binafsi na kupunguzwa kwa mamlaka ya Rais, vitu ambavyo vimekuwa vikizungumzwa sana na wananchi,” alisema Jaji Werema.


Kuhusu madaraka ya Rais kulivunja au kulisitisha Bunge hilo, Jaji Werema alisema “Sheria haimruhusu Rais kulivunja au kulisitisha na katika maongezi yangu na yeye (Rais Kikwete) nilimweleza kwamba hana madaraka hayo.”


Aliongeza: “Nimemwambia hana mamlaka ya kusimamisha, hana mamlaka ya kulivunja na wala asifikirie kwani Sheria haikumpa mamlaka na akifanya hivyo atakuwa anavunja Katiba.”


Jaji Werema alisema mamlaka ya Bunge hilo inatokana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayolitaka kujadili na kupitisha Rasimu iliyopendekezwa na Tume kisha kuandaa Katiba na kuipeleka kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.


“Kisheria maana ya kujadili ni kuboresha, kubadilisha na kuweka jambo vizuri na hii siyo mimi bali tulikubaliana wote na kanuni zikaandaliwa,” alisema Jaji Werema.


Kuhusu mabadiliko ya kanuni ilizozifanya Bunge hilo wakati Ukawa wakiwa hawapo alisema: “Tulifanya hivyo kwani Rais (Kikwete) amesema siku 60 alizoongeza zikiisha hawezi kuongeza tena, hivyo tumefanya hivyo ili kuwezesha siku hizo zitoshe.”


Aprili 16 mwaka huu, wajumbe wa Ukawa kutoka vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la 201 walisusia kushiriki shughuli zote za Bunge hilo hadi pale Rasimu iliyowasilishwa na Jaji Warioba iheshimiwe kutokana na kubeba maoni na mapendekezo ya wananchi.


Hata hivyo, Bunge hilo liliendelea na vikao vyake hadi lilipoahirishwa Aprili mwaka huu kupisha Bunge la Bajeti na Agosti 5 mwaka huu. Lilirejea tena na kuanza vikao vyake huku wajumbe wa Ukawa wakiwa wameendelea kushikilia msimamo wao.


Mvutano mkubwa wa Ukawa na Tanzania kwanza (wajumbe kutoka CCM) ulianza wakati Kamati 12 za Bunge hilo zilipokuwa zikiwasilisha maoni ya Sura ya Kwanza na ya Sita inayohusu muundo wa muungano kuwa wa Serikali tatu kama ulivyo katika Rasimu hiyo, huku CCM wakitaka Serikali mbili.


Jitihada zimefanyika za kutafuta maridhiano baina ya makundi hayo, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta aliteua kamati ya mashauriano, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi aliwakutanisha Ukawa na Tanzania Kwanza na wanaharakati kadhaa kuandaa meza ya mashauriano kwa kumwita Mkurugenzi wa Shule ya Sheria Kenya, Profesa Patrick Lumumba lakini jitihada hizo zimegonga mwamba.


Jaji Werema akizungumzia maridhiano alisema: “Huwezi kupata maridhiano wakati kila upande unashikilia msimamo wake hivyo kinachotakiwa tuijadili Rasimu hii na wananchi ndiyo wataamua ni serikali mbili au tatu na tusiwabeze kwani wao ndiyo wenye uamuzi wa mwisho.


Akiizungumzia iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema, “Hawa wazee walifanya kazi nzuri sana jambo hili linachukua hisia sana, hivi sasa wanajibishana. Mimi nawaomba wawe wasuluhishi kwani baadhi walikataa na mimi niliwashauri wakakubali na leo yanayowatokea ndiyo hayo waliyoyakataa.”


Aliongeza: “Wavumilie, haya mambo ya umma ni lazima uwe na ngozi ngumu na kama unajibu jibu kidogo tu.”


Mwanasheria huyo aliyebobea katika masuala ya usuluhishi wa migogoro aliwaomba wajumbe wa Ukawa kurejea bungeni kujadili sura zilizosalia ambazo zinagusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

MWANANCHI