Tuesday, October 21, 2014

POLISI WAMUUA MUHALIFU WA UGAIDI ARUSHA

Polisi mkoani Arusha yamuua kwa risasi mtuhumiwa Namba Moja wa milipuko ya mabomu katika mikusanyiko jijini humo na umwagiaji watu tindikali baada ya kujaribu kutoroka akiwa njiani kwenda kuonesha bomu alilokuwa amelificha maeneo ya Kondoa mkoani Dodoma.
  
KIongozi wa  matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary (Pichani)ameuawa na jeshi la polisi wakati  akijaribu kukimbia.
Inaelezwa kuwa
Yahaya Hassan ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha,SACP Liberatus Sabas (pichani) Alisema kuwa tukio hilo limetokea  Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa tano na nusu  katika barabara ya Babati mkoani Arusha wakati  akijaribu kuwakimbia polisi.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita  huko mkoani Morogoro  mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma  kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.

"Mtuhumiwa huyo alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani Morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyiwa mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko Kondoa na jana alikuwa akipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia triki zake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga judo na kutaka kuwakimbia askari ndipo akapigwa risasi mbili"alisema Sabas.

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu  ili kuweza kuteketeza matukio ya uhalifu.

TARIME WABUNI NJIA RAHISI YA KUKAMATA WEZI


Watu saba kati ya 100 Kijiji cha Kenyamanyori, Kata ya Turwa, Wilaya ya Tarime walioshiriki kunywa dawa ya mganga wa kienyeji aliyeletwa kutoka Busia nchini Kenya wameingia kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kulipa Sh3 milioni kila mmojaWanakijiji hao walikusanyika juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji kugongwa na uongozi, huku wakieleza kwamba ilikuwa siku ya nne kwa kengele hiyo kugongwa lengo likiwa ni kuzungumzia wizi unaoendeshwa na watu wasiojulikana.Inadaiwa wizi wa kuvunja maduka umekithiri kijijini hapo, baada ya wanakijiji hao kuwasili eneo la mikutano, walielezwa kusudio la kengele kuwa ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu.


Miongoni mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu Wambura, anayedaiwa kuleta mganga kutoka Busia nchini Kenya kuwabaini wahusika, hivyo kila mmoja aliombwa kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari.
Hata hivyo, walitahadharishwa kwamba kama aliyeshiriki hatakunywa dawa hiyo, itamuumbua maana aliyeibiwa atakuwa amekunywa.
Kabla ya kuanza kunyweshwa, mganga huyo aliomba wanakijiji iwapo kuna mhusika, ni vyema ajitokeze kabla ya kuingia gharama za kuwarejesha hali yao ya kawaida hazijaongezeka watakaponaswa.
Hata hivyo, wanakijiji walidharau wakidai ni mbabaishaji huyu hawezi lolote kwani hivyo ni vitisho.
Ilipotimu saa 5:00 asubuhi, mganga aliwaeleza ndani ya saa mbili tangu mtu anywe dawa yake atakuwa ameanza kuonyesha vitendo alivyokuwa akifanya wakati anaiba dukani.
Saa 6:00 mchana tayari dalili zilikuwa zimenza kuonekana kwa watu saba wakiwamo wafanyabiashara wenzake, pia yumo mwanamke wakiwa wamelewa wanafanya vioja, huku wengine wakila nyasi na kutafuna midomo.
Wambura alisema anachotaka ni kurejeshewa Sh12 milioni, zikiwamo gharama za mganga huyo, huku walionaswa na dawa hiyo wakitakiwa kulipa Sh3 milioni na kupewa siku tatu vinginevyo watageuzwa vichaa.
“Nimeibiwa sana ila ninavumilia, hii ni mara ya tano sasa, nimechoka na ninachotaka wanirudishie Sh12.5 milioni gharama niliyotumia ikiwamo mali zangu walizochukua, waliwahi kunivamia na mke wangu tunatoka dukani wakatukata mapanga hadi mke wangu akafa,” alisema Wambura.
Pia, tukio hilo lilishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Vanance Mwamengo, madaktari wa Hospitali ya Mji wa Tarime, madiwani na polisi na kwamba kutokana na wananchi kutokuchukua sheria mkononi, masuala hayo yatamalizwa kimila.

KIBAKA APOKEA KICHAPO BAADA YA KUPORA SIMU

KIBAKA ALIYECHAPWA NA WANANCHI

Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Omar mkazi wa Mafisa Morogoro,ambaye ni dereva wa boda boda mwishoni mwa wiki iliyopita alipokea  kichapo  kutoka kwa wananchi wenye hasir akidaiwa kumpora simu mwanamke mmoja nayedaiwa kuwa mwanafunzi wa chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine’ SUA’ 
Tukio hilo limetokea ijumaa iliyopita  Eneo  Mazimbu  FK  ambapo Mwanafunzi  huyo alikuwa akitembea kuelekea chuoni huku akiongea na simu hivyo Omar aliyekuwa amempakia mwenzake kwenye pikipiki walimpora simu kwa kutumia pikipiki hiyo.







Na Dustan Shekidele,Morogoro.
 Wakihojiwa na Mwandishi wetu eneo la tukio mashuhuda wa tukio hilo wasliema”huyu dada alikuwa akieleka SUA huku akiongea na simu ghafla boda boda huyu aliyekuwa amembeba mwenzake nyuma walimpitia  kumpora simu dada huyu na kukimbia nayo ambapo dada alipiga kelele za mwizi na boda boda wa kijiwe la FK waliwasha pikipiki zao na kuwafukuza ambapo walifanikiwa kuwakamata eneo hili la mazimbu reli ya pili ambapo mwenzake aliyempakia nyuma alifanikiwa kuruka katika pikipiki na kukimbia na kumuachia msara mwenzake.  
Katika hatua nyingine mmoja wa boda boda aliyefanikisha kukamtwa kwa kibaka huyo alisema' Hii ni kazi ya boda boda ni kazi  kama kazi nyingine na tunashukuru serikali inatutambua lakini kuna baadhi ya bodaboda wanatupaka matoke kw akufanya mambo ya wizi huku wakitumia mgongo wa boda boda ndio maana tulivyoshuhudi tukio hili tumeamu kuteketeza mafuta yetu na kuwafukuza vibaka hawa na kufanikiwa kuwakamata"alisema  Bw Juma ldd

Mwandishi wa mtandao huu alipiga simu polisi kwa lengo la kumuogoa mwizi huyu ambapo fasta Defenda lilifika na kumchukua kibaka huyu ambapo baadhi ya watu wanaomfahamu walidai anaegesha pikipiki wake kijiwe cha Tumbaku lringa Road  na kwamba pikipiki hiyo alikabidhiwa kwa mkataba wa kwama mmoja ambapo mwaka ukimaliki pikipiki ni mara yake na kwamba alibakiza miezi miwili kukamilisha mkataba huo.

 Afisa mmoja wa jeshi la polisi aliyeom,ba hifadhi ya jina lake alimtonya mwandishi wetu kwamba boda boda huyo alikata roho siku iliyofuata

MREMA AWAFUKUZA KAZI MADIWANI WAWILI VUNJO..


[mrema.JPG]MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, amekunjua upya makucha yake yaliyowahi kurarua viongozi wenzake akiwa katika NCCR-Mageuzi na TLP, na sasa amefukuza hadharani madiwani wawili wa chama chake waliounga mkono nia ya Mbunge wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambaye ametangaza kugombea ubunge wa Vunjo. 
 
Mrema amewavua uanachama wa TLP, Meja Mstaafu Jesse Makundi, aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya Mrema; na Yorolanda Lyimo, Diwani wa Kilema Kaskazini.

Jimbo hilo linawakilishwa na Mrema tangu 2010, na amesema mara kadhaa kwamba hataki kusikia mtu akitaka ubunge katika jimbo lake. Tayari amemlalamikia Mbatia kwa rais na katika Bunge Maalumu la Katiba.

Kilichowaponza Makundi na Lyimo ni kushiriki harambee iliyoongozwa na Mbatia ya ujenzi wa maabara na mabweni katika shule za Sekondari za Pakula, Kiluani na Mwika, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika harambee hiyo, Makundi alisema anatambua uwezo wa Mbatia na kwamba, kwa sababu hiyo, anamuunga mkono katika azima yake ya kuwa mbunge mwakani.

Alisema kwa kuwa alipokea tochi ya kumulikia wana Vunjo kutoka kwa Mbatia, ameona ni busara kuirudisha kwa yule aliyemkabidhi tochi hiyo.

“Leo nimefikia uamuzi ambao naamini ndio hitaji la wana Vunjo, kwa kuwa Jimbo hili nililipokea kutoka kwa Mbatia na kwa kuwa yeye ndiye aliyenikabidhi hii Tochi, natamka hadharani kuwa Mbatia ndiye chaguo langu, yeye ndiye atakayemulika wana Vunjo,” alisema Makundi.

Yorolanda naye alidai kuwa uamuzi wa kumuunga mkono Mbatia ni wa Mungu.

“Tunamuomba Mungu amuinue aweze kuwa Mbunge wetu. Mimi ni Diwani wa TLP, nina Mbunge wangu, namuheshimu sana (Mrema), lakini namuomba Mungu amteue Mbatia chaguo letu Wana Vunjo.

 Nafahamu wapo watakaonukuu maneno yangu lakini kama mbaya acha iwe mbaya,” alisema.

Mrema amekerwa na kauli hizo, akawavua uanachama akidai wameonyesha utovu wa nidhamu na wamekiuka katiba ya chama chao kuunga mkono mtia nia wa ubunge wa chama kingine, katika jimbo lake ambalo naye ameshatangaza kuwania nafasi hiyo tena mwakani.

Alikuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Mwanjeni, Kata ya Mwika Kusini.

Hata hivyo, Makundi amesema uamuzi wa Mrema ni batili, kwani mwenyekiti wake huyo hana mamlaka hayo.

Mrema amekuwa analalamikia hatua ya Mbatia kutaka ubunge wa Vunjo, akisema kinachomtia kiburi ni ubunge wa kuteuliwa aliopewa na Rais Jakaya Kikwete.

Analaumu pia vyama vya NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ambavyo vimetangaza kuweka mgombea mmoja mmoja kila jimbo kwa ushirikiano.

Hata hivyo, UKAWA haijatangaza mgombea wa Vunjo. Licha ya Mbatia, yupo mtia nia mwingine kutoka CHADEMA, John Mrema, ambaye naye ameshatangaza kugombea ubunge huo, akisubiri uamuzi wa mwisho wa UKAWA.

Lakini Mrema amekuwa anamshambulia Mbatia kwa kuwa ndiye amekuwa anafanya mikutano ya mara kwa mara.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Tanzania Daima hivi karibuni, Mbatia, malalamiko ya Mrema hayana msingi wowote, na kwamba hatajibizana naye.

“Siko tayari kujibizana na mtu. Kuna kazi kubwa mbele yetu. Tuelekeze nguvu zetu kuwatumikia Wana Vunjo. Mkutano wa Septemba ndio unaomtesa. Nyinyi ni mashahidi. Tangu Septemba 6, sijafanya mkutano wowote. Kulalamika kwake ni sawa na kulalamikia kivuli. Kivuli chake kinamuhukumu. Mimi siko tayari kumjibu,” alisema Mbatia.

Kati ya 1995 na 2005, Mrema akiwa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na baadaye TLP, aliwahi kuthubutu kutimua viongozi wenzake kwa mtindo huo.

Miongoni mwao ni aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wake, Harold Jaffu na Thomas Ngawaiya, ambao aliwaitia Kamati ya Utendaji na kuwashitaki kwa kuwashitukiza, baada ya kugundua wamepunguza utii wao kwake.

Kabla ya hapo, alijaribu kufukuza Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi, akiishitaki kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu kwamba kamati hiyo ilikuwa haimsaidii kufanya kazi. Kati ya wajumbe 22 wa kamati hiyo, aliungwa mkono na wajumbe saba tu.

Kamati Kuu, ikiongozwa na Mabere Marando, ilikataa kufukuzwa na Mrema, na baadhi yao (Ndimara Tegambwage na Profesa Mwesiga Baregu) wakamshauri ajiuluzu akagoma; kukazuka mtafaruku mkubwa ulioenea kwa njia na sura mbalimbali, na hatimaye ukasambaratisha chama hicho.

Aliwahi pia kuthubutu kuwafukuza Balozi Paul Ndobho na Steven Wassira aliokuwa nao NCCR-Mageuzi, akiwatuhumu kwamba walikuwa wanafanya njama za kumwengua asigombee urais, walipokuwa wanamshawishi aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba (sasa hayati) ajiunge na NCCR-Mageuzi.

Baadaye Mrema alikimbilia TLP mwaka 1999, na kwa staili hii, alifukuza viongozi wote wa Mkoa wa Kagera wa chama chake, siku alipokwenda kumzika aliyekuwa mbunge pekee wa chama hicho wakati huo, Phares Kabuye, wa Biharamulo Magharibi.

Sababu ya kuwafukuza ni kwamba waliunga mkono hoja ya upinzani kuweka mgombea mmoja wa CHADEMA dhidi ya CCM katika uchaguzi mdogo.

Wajuzi wa siasa za Vunjo ndani ya TLP wanasema Makundi ndiye alikuwa kisiki muhimu katika ngome ya kisiasa ya Mrema jimboni; na kwamba kwa kuthubutu kumvua uanachama ni sawa na Mrema kuhatarisha ubunge wake, mithili ya mtu anayekata tawi alilokalia.

MISS TZ 2014 AKIMBILIA KANISANI KUTOA SADAKA YA SHUKURANI


Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu aliopotangazwa mshindi.
Ziba masikio, fanya yako! Wakati watu wakichonga juu ya sakata la madai ya kuwa na mtoto na utata juu ya umri wake, Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu anadaiwa kukimbilia kanisani. Habari za uhakika zilidai kwamba, baada ya kutwaa taji hilo hivi karibuni na kuibua sintofahamu, mrembo huyo alikimbilia kwenye Kanisa la Ufunuo kwa Nabii Yaspi Bendera lilipo Yombo-Buza jijini Dar kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoto yake ya kuwa Miss Tanzania.

Ilidaiwa kwamba, Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke kwa leseni ya CCM, Abbas Zuberi Mtemvu, akiongozana na mama yake, walikwenda kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wema aliomtendea Mungu.

“Watu wanaendelea kumsema  mtoto wa mwenzao huku yeye anamshukuru Mungu kwa sababu hata kabla hajatwaa taji hilo alikuwa akisali hapa hivyo Mungu amepokea maombi yake na si vinginevyo kama watu wanavyomsimanga,” alisema   muumini mmoja wa kanisa hilo.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nabii Yaspi ili kupata uhakika wa mrembo huyo kutinga kanisani kwake ambapo alikiri ni kweli alikwenda kanisani kwake na ameshampigia maombi kwa Mungu hivyo atanyakua Taji la Miss World mwaka huu.

Nabii Yaspi Bendera wa Kanisa la Ufunuo lilipo Yombo-Buza jijini Dar.

Sitti alishiriki shindano hilo tangu ngazi ya vitongoji na kutwaa Taji la Miss Temeke kabla ya kuibuka kidedea kwenye Miss Tanzania linalofukuta ambapo kesho (Jumanne), mkurugenzi wa shindano hilo, Hashim Lundenga anatarajiwa kutoa tamko rasmi.

HII NDIYO NYAMA ALIYOKULA MWATHIRIKA WA KWANZA WA EBOLA

Nyama wa wanyama wa msituni ndio inaaminika kuwa chanzo cha mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa janga kwa mataifa kadhaa ya Afrika Magharibi na kwa ulimwengu wote.
Familia ya Mwathiriwa wa kwanza wa Ugonjwa huo iliwinda Popo ambao huwa na virusi vya Ebola.
Lakini katika baadhi ya wanyama hawa huwa wamebeba magonjwa hatari.
Kama Popo huwa wamebeba virusi aina tofauti ambavyo ni hatari kwa mwili wa binadamu huku baadhi ya Popo wanaokula matunda wakiwa na virusi vya Ebola.
Nyama ya wanyamapori ambayo huchomwa au kupikwa huwa haina athari sana mwilini
Kinyesi cha wanyama hao kilicho na virusi hivyo kinaweza kuwaathri wanyama wengine kama vile Nyani na Sokwe.
Kwa wanyama hao kama kwa binadamu virusi hivyo vinaweza kuwa hatari.
Lakini Popo wanaweza wasiathirike sana.
Kwa hivyo inakuwa rahisi kwao kubeba virusi hivyo bila ya kuathirika kwa vyovyote.
Raia wengi wa Afrika Magharibi hula nyama ya wanyama wa msituni
Je ulaji wa nyama ya wanyama wa msituni inaweza kuwa ndio chanzo cha janga la Ebola ambalo limekumba hasa kanda ya Afriak Magharibi?
Kitovu cha janga hilo kimesemekana kuwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili kutoka kijiji cha Gueckedou Kusini Mashariki mwa Guinea, eneo ambalo nyama Popo ambayo huwindwa na kuliwa mara kwa mara.
Mtoto huyo aliyesemekana kuitwa, Child Zero, alifariki tarehe sita Disemba mwaka 2013.
Hata hivyo haijulikani ambavyo virusi hivyo vinaathiri mwili wa binadamu, kulingana na Profesa Jonathan Ball,mtaalamu wa virusi katika chuo kikuu cha Nottingham.
Nyama hiyo huuzwa katika masoko mengi katika eneo hilo
Anasema inawezekana virusi hivyo hupitia kwa wanyama kama Nyani lakini ushahidi unaonyesha kuwa virusi hivyo pia vinaweza kupitia kwa Popo.
Hata hivyo anasema ni vigumu kwa virusi kutoka kwa mnyama hadi kwa binadamu.
Anasema mwanzo virusi vinaingia kwa seli za mwili ambapo vinazaana kwa kuugusana na damu mwilini.
Zaidi ya Popo 100,000 huliwa nchini Ghana kila mwaka
Familia ya mtoto huyo,ilisema kuwa iliwinda aina mbili ya Popo ambayo huwa na virusi vya Ebola.
Nyama ya msituni inaweza kutoka kwa Nyani, Popo wanaokula matunda na wakati mwingine hata kutoka kwa Panya na Nyoka.
Kutoka katika maeneo mengine nyama hii huwa ni mlo muhimu kwa jamii lakini kwa wengine hula tu kama njia ya kufurahisha nafsi zao.
Nchini DRC watu hula milioni ya tani za nyama ya wanyama wa msituni kwa mujibu wa shirika la utafiti la (Centre of International Forestry Research,) kila mwaka.
Popo wanaokula Marunda wanaaminika kubeba virusi vya Ebola lakini huwa wahaonyeshi dalili za kuambukizwa virusi hivyo
Sio nchini DRC pekee ambako nyama ya wanyama wa msituni huliwa bali pia nchini Ghana.
Lakini cha kushangaza ni kwamba hapajakuwa na hata kisa kimoja cha maambukizi ya Ebola nchini Ghana.
via>>BBC

UZEMBE WA WANACHADEMA NDIO USHINDI WA CCM DKT SLAA


Na Mathias Canal
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza mikutano yake ya nchi nzima kama ilivyotangazwa na katibu mkuu wa chama hicho Dkt Wilbroad Slaa, hivi karibuni alipozungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Chadema kimeridhia kufanya mikutano nchi nzima ambapo katika mkoa wa Iringa mkutano huo ulianza jana katika viwanja vya Mlandege kwa kuhutubiwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Prof Abdalla Safari
Akizungumza na mamia ya watu waliojitokeza katika mkutano huo ambao imeelezwa kuwa haujawahi kutokea mkutano kuwa na wimbi la watu kama hao, amesema kuwa ukombozi wa nchi ya Tanzania umetokana na damu ya watanzania hivyo hakukuwa na sababu ya watanzania kuishi maisha ya umasikini kama ilivyo kwa nchi kama hii yenye rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na misitu, madini na ardhi ya kutosha.
Safari alisema kuwa wananchi wa Botswana wanafaidika na madini ya nchi yao kwa serikali kukusanya 70% ya madini huku nchi kama Tanzania ikichukua 5% ya madini, hivyo ni dhahiri kuwa Uwezo duni wa kufikiri kwa viongozi wa Tanzania ndio sababu ya umasikini wa Watanzania na utajiri wa wananchi wachache (Mafisadi).
"Pia nawaahidi kwamba UKAWA tumeridhia kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi kuanzia ngazi ya serikali za mtaa hadi Taifa, lakini kubwa zaidi tunataraji kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa katiba kukusanya maoni ya wananchi" Alisema Safari
Hata hivyo Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt Wilbroad Slaa amesema kuwa kuna daftari la mkazi linapita mtaani hivyo wananchi wanapaswa kujiandikisha kwa wingi ili wawe na uwezo wa kupiga kura sambamba na kujitokeza kuwania nafasi za uongozi wa serikali za mitaa.
"Mnapaswa kutambua kuwa siku 21 kabla ya kupiga kura ni muda wa kujiandikisha hivyo kila mmoja ajiandikishe na kuhamasisha wengine, nachukua nafasi hii kuwakumbusha kuwa uzembe wa wanachadema ndio ushindi wa CCM" Alisema Slaa.
Slaa alisema kuwa CCM imeshindwa kutoa elimu bure kwa watanzania kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu tangu waingie madarakani hivyo wasitegemee kufanikiwa kwa kipindi kifupi kilichosalia.
Naye mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mch Peter Msigwa alijibu mapigo ya Katibu mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana alipozuru Mkoani Iringa hivi karibuni, alisema katibu huyo alitumia muda mwingi katika mkutano wake kumzungumzia badala ya kuzungumzia maendeleo ya nchi.
"Nilishinda kwa ushindi mnono mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu hivyo nawaomba msikubali kupotoshwa na propaganda ya kwamba nilishinda baada ya CCM kujichanganya, tuna mambo mengi ya kuzungumza lakini tutaendelea kuonana mara kwa mara kwani muda wetu hautoshi, wapo waliosema mimi na Chiku Abwao tuna ugomvi hivyo ni rahisi kukomboa Jimbo la Iringa Mjini, hilo lisahaulike naamini mmemsikia wenyewe Chiku alichokisema"
Msigwa alisema kuwa kuhusu mfuko wa jimbo ameanza kupita kila Kata ili kutoa ufafanuzi kwa kina kwa kile kilichofanyika hatimaye watanzania kutopotoshwa na baadhi ya wanasiasa.
Kwa upande wake Salumu Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zanzibar amesema kuwa, Chadema kinaamini katika vijana ndio maana wengi wao ni viongozi na ufanisi wa hoja unaonekana.
Mwalimu alitumia nafasi hiyo pia kumuomba ruhusa Katibu mkuu wa chama hicho ili kurejea tena mkoani Iringa kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha na kujitokeza katika kuwania nafasi za serikali za mtaa.
Viongozi wengine waliohudhuria katika mkutano huo ni pamoja na Patrick Ole Sosopi Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa sambamba na Chiku Abwao Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa.