Wednesday, September 24, 2014

MWANAMKE AMSHUSHIA KIPIGO HAWARA YA MUMEWE BAADA YA FUMANIZI

Kila kukicha kunaibuka vituko vingi duniani, wamo wanaosema huenda ni mwisho wa dunia! Mama mmoja almaarufu kwa jina la Mama la Mama anadaiwa kumbonda hawara wa mumewe baada ya kumwekea mtego wa fumanizi kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti).
Hawara akihaha ndani ya gesti ya White Paris (kimara) mara baada ya fumanizi.
SEKESEKE
Sekeseke hilo kubwa na la aina yake lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Gesti ya White Paris iliyopo eneo la Kimara-Kona jijini Dar na kusababisha umati (inzi) kujazana na kufunga mtaa.
ILIKUWAJE  WANAWAKE KWA WANAWAKE?
Habari zilidai kwamba Mama la Mama alihisi mumewe anachepuka hivyo aliamua kumfuatilia nyendo zake hasa kwenye kipengele cha matumizi ya simu.Ilisemekana kwamba, Mama la Mama alichukua laini ya simu ya mumewe alipokuwa akijiandaa kwenda kazini.
Hawara  akidhibitiwa mara baada ya kunaswa katika mtego wa Mama la mama.
Ilidaiwa kuwa baada ya mumewe kuondoka na simu bila kujua haina laini, Mama la Mama aliiweka laini hiyo kwenye simu yake kisha akapitia namba kadhaa na kuitilia mashaka moja na alipopiga, akawa amepatia.Akamhadaa kwa kubadilisha sauti na kuzungumza kama mumewe.
MWANAMKE AINGIA MKENGE  
Habari zilizidi kunyetisha kuwa baada ya kubadili sauti alifanikiwa kumwingiza mwanamke huyo mkenge lakini hawara huyo akamuuliza kulikoni ‘baby’ sauti imebadilika ndipo akamjibu anaumwa.
Hawara akipokea kichapo hevi kutoka kwa Mama la mama.
Ilielezwa kwamba Mama la Mama alimdanganya hawara huyo kuwa endapo wataonana atapona hivyo akamwambia wakutane gesti hiyo kwa kuwa Mama la Mama ni mkazi wa Kimara, Dar.Ilisemekana kuwa Mama la Mama, huku akijifanya mwanaume alimuomba hawara huyo wakutane gesti kwani alikuwa amekumbuka penzi lake.
Ilidaiwa kwamba, bila kufikiria mara mbili, hawara huyo alikurupuka, akafunga safari kwa kuwa aliahidiwa penzi na fedha za kujikimu.Ilisemekana kwamba baada ya makubaliano Mama la Mama alikwenda kwenye gesti hiyo na kulipia chumba kisha akamsubiri kimwana ambaye alikuwa akitokea eneo la Kigogo, Dar.
Hawara akitoka gesti mara baada ya kuambulia fedheha kuu iliyomsibu.
NDANI YA CHUMBA CHA GESTI
Habari zilitiririka kuwa baada ya kufika kwenye chumba alichoelekezwa ndani ya gesti hiyo alishangaa kukuta aliyemuita ni mwanamke mwenzake ambapo alijikuta akiishiwa nguvu na kupigwa na butwaa.
Wanahabari wetu wakiwa eneo la tukio, walimwona mrembo huyo akiwa amechanganyikiwa na hapo ndipo sekeseke likaanza na kujaza kadamnasa ndani na nje ya gesti.
KIPONDO
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.
Hawara kulia akiwa mapokezi ya gesti hiyo.
HAWARA AKODI CHUMBA KUKWEPA KIPIGO
Baada ya sekeseke zito, hawara huyo aliogopa kutoka nje ya gesti akihofia kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali waliokuwa wamezagaa nje hivyo aliamua kukodi chumba kingine ambapo alizama chumbani kisha kujifungia kwa ndani na kulala.
Akiwa kwenye mishemishe zake bila kutambua lolote, mwanaume aliyesababisha wanawake hao kukutana aliendewa hewani na mkewe na alipoulizwa kama anamfahamu mwanamke aliyeitwa gesti alijibu kuwa aliwahi kuwasiliana naye walipokutana baa kwani ni baamedi.
Umati wa watu ulioshuhudia laivu songombingo hilo.
MTUHUMIWA ANENA
Awali kabla ya kujifungia chumbani, hawara huyo alidai kuwa mume wa Mama la Mama ni mpenzi wake ambapo wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takribani mwezi mmoja.
Alisema kwamba kilichomtokea anamwachia Mungu kwani amedhalilika kupita maelezo.
Hadi gazeti hili linang’oa nanga eneo la tukio Mama la Mama alikuwa ameondoka eneo hilo huku hawara akiendelea kutandika usingizi chumbani.

VIONGOZI CHADEMA DODOMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI WAACHIWA KWA DHAMANA



Mkuu wa kitengo cha sheria CHADEMA, Tundu Lisu, (Katikati), akiongozana na washtakiwa kwenye kesi ya kukusanyika isivyo halali wakati wakitoka mahakama ya wilaya ya Dodoma Jumanne Septemba 23, 2014. Lisu ambaye alikuwa akiwatete washtakiwa hao ambao baadhi yao ni viongozi wa chama hicho mkoani Dodoma, alisema, walishtakiwa kwa kosa la kukusanyika isivyo halali hapo Septemba 18, mwaka  huu,wiki iliyopita na waliachiwa huru kwa dhamana.
Lisu akiongozana na washtakiwa wakati wakitoka mahakani hapo, Jumanne Septemba 23, 2014
Mkuu wa kitengo cha sheria CHADEMA, Tundu Lisu, (Katikati), akiongozana na washtakiwa kwenye kesi ya kukusanyika isivyo halali wakati wakitoka mahakama ya wilaya ya Dodoma Jumanne Septemba 23, 2014. Lisu ambaye alikuwa akiwatete washtakiwa hao ambao baadhi yao ni viongozi wa chama hicho mkoani Dodoma, alisema, walishtakiwa kwa kosa la kukusanyika isivyo halali hapo Septemba 18, mwaka  huu,wiki iliyopita na waliachiwa huru kwa dhamana.
Lisu akiongozana na washtakiwa wakati wakitoka mahakani hapo, Jumanne Septemba 23, 2014

SIRI YA MANCHESTER KUFUNGWA GOLI 5 NA LEICESTER UNITED

KIPIGO CHA GOLI 5-3 ILICHOAMBULIA MANCHESTER UNITED SIRI YAFICHUKA

Siri ya kipigo kizito ilichokipata klabu ya Manchester United kutoka kwa klabu iliyopanda daraja msimu huu ya Leicester City imefichuka.
Taarifa zilizozagaa nchini Uingereza zinadai kuwa wachezaji na viongozi wa klabu ya Leicester City walifanyiwa maombi maalumu kutoka kwa mmoja kati ya viongozi wa dini ya Kibudha waliokuwepo uwanjani King Power Stadium kwaajili ya kazi hiyo maalumu. 
Wachezaji wa timu hiyo walifanyiwa maombi maalumu na kupewa mikono ya baraka ambayo inaaminika ndio iliyowasaidia kuupata ushindi huo wa kihistoria dhidi ya Manchester United kutoka kwa makasisi hao wa dini ya Kibudha waliofanya kazi hiyo kwenye dimba la King Power Stadium.

AMKODISHA MPENZI WAKE KWA MTU YEYOTE ILI APATE PESA YA KUNUNUA IPHONE 6


Mwanafunzi wa Chuo kikuu kimoja cha China ambaye jina lake halikutambulika kwa haraka ameamua kufanya ‘uchizi’ ili mradi tu aipate pesa ya kununua aina mpya ya iPhone iliyoingia sokoni, iPhone6.
 
Kijana huyo wa alionekana akiwa nje ya chuo kikuu cha Songijiang akiwa na bango kubwa lililoandikwa kwa kichina na kutafsiriwa ‘Girlfriend Sharing’.
 
 Katika tangazo hilo kijana huyo anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi wake kwa mtu yeyote atakayeweza kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha kutosha kuinunua iPhone 6 yenye screen kubwa.
 
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama Twitter.
 
Tangazo hilo limeambatana na picha za mpenzi wake na amewatoa hofu wateja wanaosita kuingia nae mkataba kuwa hata mpenzi wake ameridhia na yuko tayari kudate na mtu yeyote atakaejitokeza.
 
Muda wa kuwa na msichana huyo baada ya kumkodi umebainishwa kutokana na malipo yatakayofanywa na mteja. Viwango ni vya saa 1 (10 yuan), siku 1 (50 yuan) au mwezi mmoja (500 yuan).
 
Hata hivyo, wapenzi hawa sio wa kwanza kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya kampuni ya Apple. Mwaka jana katika uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa Shaghai waliwaweka sokoni watoto wao watatu ili wapate pesa ya kununua computer na simu za iphones lakini walikamatwa na kufunguliwa mashitaka.
 
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
 
Siyo hayo tu, hivi karibuni mwanaume mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa iPhone 6 kama mahari ya dada yake hata kabla aina hiyo ya simu haijazinduliwa Bahrain.

ALIYECHUKUA SHERIA MKONONI KWA KUMPIGA RUNGU TUMBONI MKE WAKE NA KUMUUA NAYE AGEUZIWA KIBAO NA WANANCHI

WATU wenye hasira wamempiga hadi kumuua mwanamume, aliyemuua mke wake kwa kumpiga rungu tumboni.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, David Misime, alisema tukio hilo la Septemba 20, mwaka huu katika Kijiji cha Mzogole wilayani Mpwapwa, ambapo mtu mmoja, Mwajuma Chomola (48) aliuawa kwa kupigwa na rungu tumboni upande wa kushoto na mume wake, Richard Kodi (55).

Hata hivyo, alisema Kodi naye aliuawa Septemba 21, mwaka huu baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi. Alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.

Aliuawa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo, amekufa baada ya kupigwa na mtu huyo.

Misime alisema uchunguzi wa awali, unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.

Kamanda huyo alisema Kodi alimuua mkewe huyo, aliyekuwa akiishi naye baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe, iliyokuwa kijijini hapo, akidhani kuwa alikuwa ameenda kwenye masuala mengine.

TAPELI WA AJIRA HUYU HAPA


 Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.Tapeli anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter. Tukio hilo lilitokea Septemba 19 mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Kimara baada ya tapeli huyo kumlaghai dada mmoja aitwaye Wema Raymond wakutane hapo kwa ajili ya vipimo vya ukimwi vilivyotakiwa kuambatanishwa katika fomu ya kuomba nafasi ya kazi ambayo awali dada huyo alidai kupatiwa na tapeli huyo. 
Akizungumza na waandishi wetu, Wema alisema alimfahamu tapeli huyo kupitia kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Rebecca, ambaye naye awali alipigiwa simu na mtu huyohuyo akimtaka kimapenzi. 
Wema alisema kuwa rafiki yake alimkatalia tapeli huyo, lakini siku chache baadaye alimpigia tena akimwambia kulikuwa na nafasi ya kazi katika Chuo cha Ardhi hivyo anamhitaji yeye kwa ajili ya nafasi hiyo. 
“Kwa sababu Rebecca ana kazi yake tayari aliamua kunitaarifu mimi kwa kuwa anajua natafuta kazi,” alisema Wema.Alisema alikutana na jamaa huyo ndani ya Chuo cha Ardhi na kupatiwa fomu aliyoelekezwa kujaza kisha akatakiwa kutoa shilingi 280,000 kama malipo ya fomu hiyo na gharama za mafunzo ya siku tatu ya vitendo kuhusu kazi, fedha ambazo hakuwa nazo kwa muda huo na kulazimika kumuomba rafiki yake Rebecca amsaidie.
Wema Raymond aliyetapeliwa na tapeli huyo anayefahamika kwa jina la Baraka au 'Muba'. “Baada ya kumaliza mazungumzo pale chuoni akanisindikiza hadi nje, lakini cha kushangaza pale mlangoni nikamuona anampatia mmoja wa walinzi hela, nikamuuliza kwa nini aliwapa hela, akasema eti watu wengi wanaitaka nafasi ile wakiwemo walinzi hao, hivyo alikuwa akiwapoza wasimsemee kwa kunitafutia mimi kazi isije akafukuzwa kazi,” alisimulia Wema na kuongeza kuwa alitakiwa kesho yake kupima VVU ili vipimo hivyo viambatanishwe kwenye barua yake ya maombi. 
Katika Kituo cha Afya Kimara, alikutana tena na tapeli wake, aliyeonekana kuwasalimia madaktari na manesi kana kwamba wanajuana kisha akaingia kwa dokta na kuzungumza naye.Baada ya muda tapeli huyo alitoka nje kisha akamwambie Wema aingie kwa daktari kwa ajili ya kujaziwa fomu hizo kienyeji bila kupimwa maambukizi ya ukimwi. “Nikiwa ndani machale yalinicheza, ikibidi nimuulize yule daktari kama anajuana na yule jamaa, daktari akasema kwamba hawafahamiani hata kidogo jambo lililonishtua. “Nikamnong’oneza kuwa nahisi kutapeliwa, akaniambia nikakae naye nikijifanya namuongelesha huku yeye akizunguka kwa mlango wa nyuma na kuwaita mapolisi.
Kamanda Suleiman Kova. “Katika upekuzi alikutwa na zile pesa zangu za jana zikiwa kwenye simu yake na shilingi 90,000 akiwa nazo mfukoni huku akionekana kutumia simu yenye jina la Martha Peter ambalo mwenyewe alikiri kuwa alikuwa akinitapeli.” 
“Polisi walichukua maelezo yangu na kufungua jalada RB/4969/2014 KUJIPATIA PESA KIUDANGANYIFU kisha wakaniambia nifike kesho yake,” alisema Wema na kuongeza kuwa siku ya pili alipofika kituoni hapo aliwakuta watu wengine waliodai kutapeliwa na jamaa huyo kwa majina tofauti na walipopiga hesabu fedha alizowatapeli kwa pamoja zilifikia sh.1,435,000.