Tuesday, November 11, 2014

HALI YA RAIS KIKWETE YAZIDI KUIMARIKA NA ARUHUSIWA KUFANYA KAZI NDOGONDOGO



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasiliana na baadhi ya wananchi waliokuwa wakimjulia hali kupitia simu yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms) leo Jumatatu.Rais Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore Maryland nchini Marekani anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mara kwa mara na afya yake inaendelea kuimarika(picha na Freddy Maro)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na wananchi tokea mwishoni mwa wiki.

Tangu alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) Jumamosi iliyopita kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia nafuu ya haraka.

Rais Kikwete bado anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia SMS Rais Kikwete waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu anakusudia kujibu SMS zote ambazo ametumiwa.

Aidha, Rais Kikwete jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania kwa mara ya kwanza tokea afanyiwe upasuaji. Rais alizungumza na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.

Wakati huo huo, madaktari wanaondelea kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa bandeji kwenye sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali yake inaendelea vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Novemba,2014
 

unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea na kazi ndogo ndogo wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore Maryland nchini Marekani leo
 

MIRAJI KIKWETE AKANUSHA KUMILIKI KAMUNI YA SIMBA TRUST

Mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Miraji Kikwete usiku wa Nov 11 2014 ameeleza kuhusu ishu inayosambazwa kwamba anamiliki kampuni ya Simba Trust iliyopo Australia akishirikiana na dada yake.Kufuatia tuhuma hizo Miraji alipost maandishi akikanusha hiyo ishu akisisitiza kwa eleweke hivi ningekuwa napokea milioni 100 kwa siku wallahi ningeshukuru kwa mola ila siwezi kuchukua fedha kinyume na haki ninayo stahili’
‘Katika jambo lililonishangaza ni hizi tuhuma za kuwa ninamiliki kampuni ya Simba trust ya Australia mimi na dada yangu Salama, naona sasas mmeishiwa hoja na kuanza kuzusha mambo, sijawahi kufika Australia na sina kampuni ninayomiliki na dada yangu, lakushangaza kwanini PAP wanilipe pesa bila sababu maalum’
‘Sina pesa nyingi kiasi hicho, kidogo ninachokipata ni kwa jasho langu, sijawahi na sitodiriki kupokea pesa ambazo si haki yangu kupata, acheni kupandikiza chuki zisizo na ukweli wowote, atakaethibitisha basi na aonyeshe hilo kwa vielelezo na ushahidi, chuki hazijengi, kweli umeishiwa hoja na mambo ya msingi ya kujadili’