Monday, January 18, 2016

TEKNOLOGIA YAZIDI KUSONGA MBELE KATIKA KILIMO


Wakati Tanzania ikijivunia kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, juhudi nyingi zinafanyika ili kuona msemo huu haupitwi na wakati na kuendelea kumfanya mkulima kunufaika na kile anachokifanya. Wataalamu na watafiti wanajitahidi kila kukicha kubuni kila njia kufanya kilimo cha Tanzania kinainuka kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ili kufikia viwango vya kimataifa kama zilivyo nchi nyingine.

Rijk zwaan ikiwa ni kampuni ya uzalishaji mbegu za mboga mboga nchini, wameamua kutumia njia za kisasa kuwafundisha wakulima jinsi ya kutumia mbegu za kisasa kwa njia ya mitandao ya kijamii ya Whats App na Facebook ambapo wamekuwa wakiwahimiza wakulima kutumia kilimo cha green house ili kuepukana na hasara zingine ambazo zingeweza kuepukika kwa kutumia kilimo hicho. Na kwakutumia njia hiyo imewarahisishia wakulima kushare uzoefu na mtaalamu kila wakati wanapohitaji msaada.

Kwa njia ya mitandao ya jamii tumefanikiwa sana, kwani kwa sasa teknolokia imekwenda mbali sana kitu ambacho kinatusaidia sisi kukutana na wakulima hata kabla ya kuonana nao ana kwa ana, na tumekuwa tukijivunia ubunifu huu kwani tumeona mwitikio wa wakulima kupasahana habari kuhusu shirika letu na bidhaa zetu wao kwa wao. Alisema Bwana Abel Kuley, meneja uzalishaji na maendeleo wa Rijk zwaan
Baadhi ya mbegu zilizooteshwa tayari kwa kupelekwa shambani 


Wakati tunaanza kuuza mbegu, tulianza na wakulima ambao wana ardhi lakini hawajui kitu cha kufanya hivyo tulianza kuwaeleza faida ya kilimo cha mbogamboga na namna ya kulima kilimo bora hivyo wale walioanza walianza kidogo kidogo lakini kila aliyeanza hakuna aliyejilaumu kuwa alifanya makosa kuingia katika kilimo hiki kwa kuwa wengi walijutia kwa nini hawakuijua siri hii tangu awali. Aliongeza Bwana Abel


Naye Bwana Hearald Peeters Mkurugenzi Mtendaji wa Rijk zwaak alisema wao wanatoa huduma ya mbegu za kisasa za mbogamboga kwa wakulima wadogo wadogo na wakubwa pia. Lakini tumekubali kufanya shughuli hii sisi wenyewe  kwa kuwafikia wakulima moja kwa moja kwani tunajua kuwa wateja wetu wametofautiana maeneo yao ya kilimo kwa maana ya hali ya hewa, udongo, pamoja na magonjwa ya mimea kutokana na eneo husika, hivyo hatutaki kuwauzia wakulima mbegu kana kwamba wote wanatoka sehemu moja. Alisema 
Hearald Peeters akiwa katika shamba la nyanya ndani ya Rijk Zwaan

Kila wakati tunapopata mteja mpya huwa tunamuuzia mbegu zetu lakini huwa hatumuachi hivyo hivyo kwani huwa tunamfundisha mfumo mzima wa jinsi ya kuzilima na kuzihudumia mpaka atakapovuna. Hata hivyo huwa hatumuuachii mkulima kuuza mwenyewe hivyo huwa tunatafuta masoko kwa ajilli yake japo wakulima wetu huwa wanapata wateja kabla hata hawajavuna, hivyo huwa tunapenda kumuhudumia mteja wetu na kumuacha akiwa na furaha na kwa mtindo huu wamekuwa wakipashana habari na kuongeza kasi ya kutumia mbegu zetu na kwa kufanya hivi wakulima wengi wamekuwa wataalamu wa kilimo hiki kwani huwa wanajifunza kwa vitendo kwa kusaidiana na wataalamu wa Rijk zwaan. Alisema Bwana Hearald


Hata hivyo Rijk zwaani wanawasihi wateja wao kuwa hakuna kampuni ya usambazaji wa mbegu waliyoingia nayo mkataba kwa kuuza mbegu zao kwakuwa wao wanatoa huduma ya uuzaji wao wenyewe ili kuhakikisha mkulima anapata mbegu halisi kutoka kwao

Nae Enock Nanyaro mkulima wa kikundi cha parokia ya familiaTakatifu, Njiro mkoani Arusha amesema tangu aanze kutumia mbegu za Rijki zwaan hajawahi kujuta kwani mafunzo aliyoyapata baada ya kununua mbegu zao yalimfanya kuvuna mazao mengi kuliko miaka yote aliyowahi kulima.
“Nawashukuru sana watu wa kampuni ya……. Maana wao ndiowaliotupeleka Rijk zwaan na kutukutanisha na wazalishaji wa mbegu hizi ambazo ndio nazitumia mpaka leo hii.  Sikuwhi kuwaza kuwa ipo siku moja nitakuwa mtaalamu wa kilimo cha kisasa lakini sasa Rijk zwaan wamenifikisha hapa nilipo leo alisema Bwana Enock



Enock Nanyaro akionyesha mmea uliooteshwa miaka miwili nyuma na bado unazaa matunda bora na yenye afya ikiwa ni mmoja ya mmea wa mfano ambao huutumia kuwaonyesha wakulima wenzake ambao humtembelea ikiwa yeye huita ni maajabu ya mbegu za Rikjzwaan. 


Renalda mlay wa Shant Town mjini Moshi Kirimanjaro, alikiri kuwa hakuwa na ndoto ya kuwa na shamba nyumbani kwake kutokana na eneo alilonalo, lakini mafunzo aliyoyapata kupitia Rijki zwaan aligundua ya kuwa anaweza akalima mboga mboga katika eneo alilonalo nyumbani na akapata faida kitu ambacho anakifanya sasa.

“Mimi nalima pilipili na nyanya kwenye green house nyumbani kwangu na ninapata faida mpaka watu wananishangaa. Nimeifanya hii ni ajira yangu baada ya kuacha kazi ya benki kwani kiwango cha pesa ninachozalisha kwa hili shamba ni zaidi ya mishahara ya baadhi ya watu wanayopata makazini.” Bi Renalda alisema

“Nikianza kueleza uzuri wa mbegu hizi unaweza ukaacha kazi na kuwa mkulima, kwani ukinunua mbegu za hii kampuni na kuziweka shambani hakuna hata moja ambayo haitaota,na uzaaji wake ni maajabu sana.” Alisema Bwana Deo Ryoba wa Moshono, Arusha
Bwana Ole Ngao yeye ni afisa kilimo wilayani simanjiro alisema kuwa wakulima wasilaumu kuhusu uzalishaji duni wa mbegu za kisasa tofauti na vile zinavyosifiwa isipo kuwa wanapasa kuilaumu serikali kwani ndio iliyoshindwa kutoa elimu ya kilimo kwa wananchi wake. Pia alisema kuwa wananchi wengi hawazingatii kile wanachoshauliwa na wataalamu wa kilimo kuhusu kilimo cha kisasa.

“zipo teknolojia nyingi sana ambazo zinatumika sasa katika kilimo, hali ya hewa na mabadiriko katika udongo yanayotokana na matumizi yamda mrefu kwa  kilimo yanamlazimu mkulima kuenenda na sayansi na teknolojia ili kupta faida katika kilimo” alisema Ole
 Hili ni jambo la kujifunza kuwa elimu kwa mkulima yaweza kutolewa hata kwa mitandao ya kijamii. Ipo  haja ya mkulima kubadiri mfumo katika kilimo kwani kwa hali ya sasa teknolojia inatumika kila mahali.

Pia serikali yetu ni lazima iunge mkono teknolojia ya kisasa katika kilimo kwani kumuhubilia mkulima kuhusu mabadiriko ya hali ya hewa bila kumwambia njia sahihi ya kuikabili ni kazi bure.
Hivyo basi ipo haja ya serikali kuitazama sera kwa jicho la tatu ili kuondoa zile sharia zinazowabana watafiti wa kilimo katika kukuza teknolojia katika kilimo Tanzania.

Rijk zwaani ni kampuni ya utafiti na uzalishaji mbegu za mbogamboga iliyopo Usa mkoani Arusha, iliyoanzishwa mwaka 2008  na nia ya kuanzishwa kwa kampuni hii ni kuboresha begu za mbogamboga ili kukuza kipato kwa mkulima wa kawaida kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kilimo hapa nchini ikiwa ni SEVIA, AVRDC, TAHA na wakulima wenyewe.

Kwa kuhakikisha wanafikia malengo yao wamekuwa wakifanya mafunzo kwa vikundi vya wakulima pamoja na kushiriki katika maonyesho ya wakulima yanayofanyika kila mwaka hapa nchini na hata kushiriki maonyesho kama hayo yanayoandaliwa na baadhi ya wadau wa kilimo nchini.

Hearald Peeters akifafanua teknolojia mpya ya kilimo kifaacho kwa watu wasio na ardhi kwa waandishi wa habari walipotembelea Rijk zwaan Arusha