Friday, August 29, 2014

WALAZIMIKA KUTEMBEA ZAIDI YA KILOMETA 4 KATIKA KUTAFUTA MAJI SAFI NA SALAMA.

 Na Baraka lusajo mbeya,
WANANCHI wa  kijiji  cha kyimo  kata   ya  kyimo  wilayani Rungwe mkoani  Mbeya  wamelazimika  kufukia mitalo ambayo ilikuwa imeandaliwa  na idala ya maji wilayani  humo  baada  ya wao  kukosa huduma hiyo kwa  muda mlefu na kulazimika  kutembeya  zaidi ya kilometa {4}  katika  kutafuta  maji  safi na salama 

 
Wakizungumza jana na  wandishi  wa  habari walipotembelea potembelea  kata hiyo mara baada ya kujurishwa uwepo  kwa ukosefu wa  huduma ya maji  kwa muda mlefu walisema kuwa Serikali kupitia benki ya Dunia {WBC} iliwapatia fedha kiasi  cha  Tsh,Mil,299   kwa ajiri ya ujenzi wa tenki  lamaji ambalo lilitegemewa  kujengwa  katika eneo hilo baada ya wao  kuto kuwa  na huduma hiyo kwa  muda mlefu  lakini  wanashangaa baada ya  huduma hiyo kukamilishwa na kuelekezwa  katika  kata ya jilani   ya lufingo  bila wao kunufaika  na huduma hiyo  na kupelekea  kuchukua  uamzi  wa  kufukia  mitalo ambayo ilikuwa imeandaliwa na idala ya  maji   wilayani humo   na huku wakishinikiza  idala hiyo  kuelekeza  maji kwanza kijijini kwao.
Omari Kajange mkazi wa kata hiyo alisema kuwa Mkuu wa mkoa huo Abasi Kandoro ndiye aliyewapa taarifa kuwepo kwa mradi huo na kuwa baada ya kuona mkandarasi amejenga chini ya kiwango walimpatia taarifa na yeye  kumuagiza mkandarasi huyo ajenge upya ndani ya siku 14.

Alisema kuwa mkandarasi huyoaliyejulikana kwa jina moja la Gulamali alikaidi agizo hilo ikiwa amefikisha zaidi ya miezi mitatu bila kujenga Tenki hilo na hakuna hatua iliyochukuliwa na wao wakiendelea kukosa huduma hiyo muhimu kwa kulazimika kutembea zaidi ya kilometa {4} katika kutafuta huduma hiyo. 

Kajange aliongeza kuwa kutokana na Serikali wilayani humo kushindwa kuchukua hatua waliamua kufanya mkutano mkuu uliowatuhumu  viongozi wa kata hiyo kushindwa kuwajibika na kutaka wapatiwe majibu juu ya hatua walizochukua kutokana na   ukosefu wa  huduma hiyo.

Akijibu hoja hizo diwani wa kata hiyo Frankson Mwaitalage alisema kuwa ni kweli jambo hilo lipo lakini lipo chini ya mkuu wa mkoa ambaye tayari ameanza kuchukua hatua juu ya uchakachuaji huo dhidi ya mkandarasi huyo.

Mwaitarage alisema kuwa Sekretalieti ya mkoa ndiyo iliyompa kazi injinia huyo na kuwa serikali ya kijiji ilitakiwa ipeleke lalamiko hilo mkoani kupitia kwa mkuu wa wilaya Chrispin Meela  na si kwangu.

“mimi mnanionea bule suala hili lipo chini ya mkuu wa mkoa,mimi sina mamlaka tulichokifanya ni kuukataa mradi huo maamuzi juu ya injinia huyo yatatolewa na mkuu wa mkoa na maji  yataanza  kupatikana mpaka mpale mladi  utakapo kuwa umekabidhiwa  na serikali kwa wanachi husika na  sivinginevyo ”alisema diwani huyo.

Mwaitolage alimaliza kwa kusema kuwa atamuagiza mwenyekiti wa kijiji hicho aitishe mkutano mkuu ili mambo yote yawekwe wazi kwa kuwa tatizo hilo la huduma ya  kmaji katika maeneo hayo lipo kwake na muhtasari wa mkutano huo yatapelekwa kwa mkuu wa mkoa kwa ajili ya maamuzi zaidi.

BINTI ASEMA AMECHOKA KUTUMIWA KWENYE BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

ANGALIA PICHA DADA HUYU NA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

Msichana anayetambulika kwa jina moja la Mary (23) anayedai kuchoshwa na kazi ya kubebeshwa madawa ya kulevya.
  Msichana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mary (23), mkazi wa Dar ambaye ni mwenyeji wa Nyegezi, Mwanza, ameangua kilio na kusema; ‘nabebeshwa madawa ya kulevya (unga), nalipwa kiduchu hadi nimechoka’.Awali, gazeti hili lilitonywa na vyanzo vyake juu ya kuwepo kwa ishu hiyo maeneo ya Manzese, Dar ambapo uchunguzi ulifanyika na kumnasa binti huyo ambaye alifunguka kila kitu.
Akizungumza na wanahabari wetu kwa uoga mkubwa, Mary alidai kwamba alichukuliwa kutoka kijijini kwao huko Nyegezi ambapo alipofikishwa Dar, alijikuta akiunganishwa kwenye mtandao wa kuuza ‘unga’. 

“Nililetwa Dar mwaka jana na mwanaume mmoja, aliniahidi kunitafutia kazi, niliishi naye kama mtoto wake.“Zilipita kama wiki mbili tangu aliponileta bila kuniambia nitafanya kazi gani, siku moja ndipo akanipeleka Mitaa ya Magomeni (Dar) na kuniambia nitakuwa nafanya shughuli za kuuza unga huku nikiishi nyumbani kwake na yeye ndiye bosi wangu. 
“Nilishangaa sana kuona ile ndiyo kazi niliyoahidiwa kuja kuifanya Dar. Nilianza kumlilia bosi wangu anirudishe kwetu Mwanza lakini alinigomea, hata pale nilipotafuta kisingizio cha kumwambia nimemkumbuka mama yangu, aliniambia nimtumie nauli aje Dar,” alisema binti huyo akilengwalengwa na machozi.
Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyowahi kunaswa.
 Aliendelea kusimulia kwa majonzi kwamba, siku hadi siku amekuwa akiiona dunia ikimuelemea kwa kuwa amechoka na hayupo radhi kufanya shughuli hiyo, kwani mbali na hatari yake haoni manufaa anayopata. 

Alisema, awali alikuwa akilipwa Sh. 3,000 kila siku kwa kupakia kwenye paketi na alipobadilishiwa kitengo na kuanza kuhesabu kete na kubebeshwa amekuwa akilipwa kiduchu, yaani Sh. 50,000 kwa mwezi. 

“Hii kazi sitaki hata kuisikia, nimeshafanya kwa mwaka mmoja sasa, sijapata faida yoyote kwani nalipwa kiduchu huku nikiishi kwa hofu muda wote hivyo nimechoka.“Kuna kipindi mama yangu alikuja na kufikia kwake, alimnyanyasa na kumnyima nauli ya kurudi Mwanza. Alikuwa ananiambia kama vipi nikajiuze nipate nauli ya mama yangu.
Kamanda Godfrey Nzowa.
 “Sikuwa tayari kufanya hivyo, mama yangu akasaidiwa na jirani akasafirishwa kurudi kijijini Mwanza,” alisema na kuongeza:
“Kuna wakati ananitishia maisha endapo nitatoa siri popote, jambo ambalo limenifanya nikose uhuru na amani ya maisha, ndiyo maana nimeshukuru kukutana na magazeti ya Global Publishers nitue huu mzigo.” 

Katika kile kinachozidi kumtia hofu ni pale alipoambiwa siku chache zijazo ataanza kusafirisha unga nchi mbalimbali na kupata utajiri mnono jambo ambalo hataki kulisikia, kwa kuwa anaogopa kuozea jela hivyo kikubwa anachohitaji ni msaada wa nauli ya kurudi kwao Mwanza akamsaidie mama yake ambaye ni mzee na ni mgonjwa.

MASKINI ZITTO KABWE

Azidi Kuchoreshwa na Diva Baada ya Zitto Kumakana Diva.


Kuwa uyaone mengi sio maghorofa bali ni vituko vya binaadam katika hii dunia just imagine Zitto anavyoabika sasa hivi daaah, hivi kweli kuna mwanaume aliekuwa mahabani na Diva naye akasema nina girlfriend?? baada ya Zitto kumkana Drama Queen kwamba hatoki naye sasa drama queen amtolea za uso na kutoa moja ya email aliotumiwa na zitto mmmh Diva,Diva,Diva huendani na jina lako

Email Kutoka kwa Zitoo Kwenda Kwa Diva:

KIJANA AFARIKI KWA KULA VIJIKO VIWILI VYA WALI





  Wakazi wa kijiji  cha mpunguiti  kata  ya  luteba wilayani  Rungwe mkoani mbeya  wamelazimika  kuitisha mkutano wa  kimila baada ya mwanachi  mewezao    Dulo mwangwego  miaka   {26} kufariki dunia  ghafla  baada   kula wali vijiko  viwili.
 Wakiiongea   kwa masikitiko  makubwa wanachi hao kupitia katika  mkutano wa  hadhara ulio anza  majila ya saa  kumi na moja  ya alfajili  ambapo waliseesema    wameamua  kuchukua hatua ya kuitisha mkutano wa huo baada  ya   kijana  huyo kufariki  dunia  katika mazingra ya  kutatanisha kwa  kula wali vijiko  viwili.

  Hata  hivyo taarifa za awari kutoka  kwa wananchi  hao zimeeleza kuwa   katika siku za  hivi karibuni   vijana wawili walienda   kufanya kazi   ya kumsaidia  kulima  mwanakijiji mwenzao  Jimu  mwakibwaga kama   kibarua  lakini   baada ya   ya  vijana hao kuonekana  kufanya  kazi viziri  bosi wao Jimu mwakibwaga  aliamua kuwapatia   kilo  nne za  mchele   ambao  waliondoka  nao hadi katika  makazi  yao, lakini   hata  hivyo kijana huyo baada ya kujaribu  kula  vijiko  viwili alijikuta   akianza  kunyong’onyea mwili wake kwa ghafla   kwa  kanza kutokwa na  damu katika sehemu  za puani  ikiwa ni  pamoja  na kutokwa  na damu katika  sehemu  ya haja  kubwa , ambapo   kutokana na hali   hiyo  kuzidi kuchukua nafasi yake aliamua  kuwaita  majilani zake ambao  walimkimbiza katika Hospitali  teule ya  Halmashauri ya Busokelo  itete kwa  matibabu zaidi.
 Hata   hivyo kipindi  hiki  kilifanikiwa  kuhojiana  na  baadhi  ya   ndugu  wa marehemu  juu ya  kisa  hicho  ambapo wamesema  chanzo  cha tukio  hilo   kimekuja  kufuatia  kula  wali ambao alipewa na   mwanakijiji  mwenzake baada ya kumualika kumsaidia  kufanya kazi ya kulima  shamba  ambapo  baada ya kufika  nyumbani  kwake , alipikiwa  chakula  hicho  vizuri  lakini  baada   ya  kujaribu  kula  vijiko  viwili alijikuta akinza kujigalagaza  huku na kule   kwa kutokwa na damu katika sehemu za puani  na  haja  kubwa na ndogo   hali ambayo ilipelekea   kumfikisha  hospitali  ambako aliweza kupoteza  uhai wa maisha  yake wakati  akiendelea na matibabu.
   Kwa upande wake  chifu  wa maeneo hayo  ASajile  Mwambage  alisema hatua  hiyo imekuja  baada ya  kuwepo kwa  maslalamiko kwa  wananchi wake juu ya kifo  cha ndugu yao na kutaka  kuitishwa kwa mkutano wa kimila wakitaka  kujua  hatima  ya kifo  cha  kijana   wao na  ukizingatia  kuwa  hilo  ni  tukio  la pili kujitokeza katika maeneo hayo ambapo  katika siku  za hivi karibuni   mwanakijiji mwenzao   Jueli mwanjwango alifariki  katika mazingra ya  kutanisha  baada ya  kudaiwa  kuchapwa na fimbo  na jilani   yake kutokana   ugonvi wa mifugo.

  Hata   hivyo mkutano huo ulianza  mnamo  majila ya  saa kumi na   moja  ya  alfajili  na kumalizika majila ya  saa mbili za alfaji  na huku  ukiwa na lengo la kutomeza   vifo vya ajabu katika maeneo  hayo.

SHAHIDI AFUNGUKA ALIVYOFANYISHWA MAPENZI NA MGANGA WA JADI


Shahidi wa pili katika kesi ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mganga wa kienyeji, Yahaya Michael (34) ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jinsi alivyoingiliwa kimwili na mganga huyo kwa madai kwamba atampatia dawa ya kupata mtoto.

Mwanahamisi Omary (26) alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma kuwa alimfahamu mganga huyo baada ya kusumbuliwa na tumbo la uzazi kwa muda mrefu.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Felista Mosha, Mwanahamisi alidai alikuwa akitibiwa ugonjwa huo bila ya kutoa taarifa kwa mumewe Edrick Elinezer. Alidai alitibiwa kwa miezi sita bila ya mafanikio.

Shahidi huyo alidai Aprili, mwaka huu, Michael alimwambia kuwa ana majini hivyo hawezi kupata mtoto na kumpatia dawa kwa ajili ya kunywa na kuoga.

Alidai mganga huyo alikuwa akimtibu nyumbani kwake lakini baadaye alihamishia ofisi yake katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Kigogo Luhanga na kudai kuwa mganga huyo alikuwa akipaka dawa katika uume wake na kumuingilia kimwili huku akiwa hajitambui kwa madai kwamba atamsaidia kupata mtoto.

Aliendelea kudai kwamba baada ya kutokuwa na mawasiliano kwa muda mrefu na mumewe, alipata taarifa kuwa mume wake alipigiwa simu na mganga huyo na kumtaka apeleke gari lake Toyota Rav4 lenye namba za usajili T 139 BSG maeneo ya Jangwani kwa kuwa majini ya mkewe yanataka mtoto.

Awali, Hakimu Juma alisema wadhamini wa mshitakiwa wanatakiwa kumtafuta mshitakiwa huyo na kumfikisha Mahakamani hapo, aliwatahadharisha wasipofanya hivyo kwa wakati watalipa faini ya Sh milioni sita kwa kila mmoja.

Michael alidaiwa Aprili 29, mwaka jana, maeneo ya Jangwani Wilaya ya Ilala, alijipatia gari aina ya Toyota Rav4 T 139 BSG lenye thamani ya Sh milioni 12 mali ya  Eliezer kwa njia ya udanganyifu. Kesi hiyo itasikilizwa  tena Septemba 18, mwaka huu.

JUKATA WAMBEBESHA LAWAMA SITTA, WASEMA KATIBA MPYA NI NDOTO KUPATIKANA


 Kaimu mwenyekiti wa Uukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda akizungumza na wanandishi wa habari leo Agosti 27, 2014 juu ya mwenendo wa bunge la katiba.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Wakati mchakato wa katiba Tanzania ukiwa ni kama kitendawili kisicho na majibu sahihi kutokana na mchakato huo kuvurugika na kukosa mwelekeo, nao Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) wazidi kumtupia lawama zote za kuvurugika bunge hilo mwenyekiti wa bunge hilo mheshimiwa Samweli Sitta na kudai kuwa ndiye aneyeuvuruga mchakato huo baada ya kugeuza Bunge hilo kama kikao cha Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda amesema kuwa JUKATA wamekuwa wakifuatilia mchakato huu wa bunge ka katiba kwa wiki mbili hizi na kubaini mapungufu makubwa sana ambayo yanatokea jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa mwenyeikiti wa bunge hilo hana nia wala dhamira ya kulipatia taifa katiba mpya ya watanzania.

Wanahabari mbalimbali wakiwa wanamsikiliza kiongozi huyo wakati wa mkutano Bw Mwakadenga amesema kuwa swala la mahudhurio ya wabunge wanaoshiriki katika kamati mbalimbali za bunge hilo yamekuwa madogo sana na yasiyo ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na wabunge wengi kutokuhudhuria katika kamati hizo pamoja na kusaini kulipwa posho za siku jambo ambalo amesema kuwa ni wizi mpya kwa
watanzania,
 “Kwanza bunge la katiba linaonyesha kuwa wajumbe 441 wamehidhuria lakini uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hawa ni wale wote ambao wamewahi kufika na kusaini kwenye kitabu cha mahudhurio wengine wao takribani 100 tuligundua kuwa hawapo bungeni wakiwemo mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati”amesema Mwakagenda.

Ameongeza kuwa mambo mengine ambayo yanalifanya bunge hilo kuvurugika ni pamoja na kukosekana kwa muafaka na maridhiano ya kitaifa, matumizi mabaya fedha ikiwa ni pamoja na Wajumbe kulipwa bila kuhudhuria bungeni, kukosekana kwa theluthi mbili toka Zanzibar ili kupitisha katiba,pamoja na uondoaji wa vifungu muhimu kwenye rasimu mambo ambayo amesema kuwa mwenyekiti Samweli Sitta ameyafumbia macho na kijifanya kama hayaoni huku akiwa anajua wazi kuwa anauzika mchakato huo.

“Huyu mzee hatujamwelewa kabisa, sisi tumekaa tumezungumza naye tukamuuliza atueleze swala la theluthi mbili hawa wajumbe watapatikana wapi hajatupa jibu la kuridhisha na ukimwona ni kama mtu ambaye
ameshachanganyikiwa, anapambana na kila anayekuja mbele yake, iwe mwandishi, mwanaharakati, mbunge, yeye amekaa kujihami tu, sasa hali hii sio nzuri kwa mchakato muhimu kama huu”alisema kiongozi huyo wa JUKATA.
Katika hatua nyingine JUKATA wamemwomba raisi Kikwete kiusimamisha mchakato huu wa katiba hadi kipindi kingine kutokana na kuonekana wazi kuwa hauwezekani na kusema Tanzania imekuwa na michakato mingi ambayo sisi kama taifa hatuwezi kuiendesha kwa wakati mmoja na kupata katiba bora, “Kusema ukweli taifa sasa lina michakati mingi sana mfano mchakato wa vitambulisho vya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari la kudumu la kupiga kura na michakato mingine mikubwa, hii haitaki usome sana ndo uelewe ni kutumia busara tu kwamba huu mchakato wa katiba hautawezekana tena, sisi tunamwomba mheshimiwa Rais Kikwete awasikilize watanzania na kuusimamisha mchakato huu wa katiba ili tujipange upya kuanza
tena.
Mchakato wa katiba umekuwa ukiendelea jijini Dodoma bila ya mariano na wajumbe waliotoka wa UKAWA huku kukiwa na taarifa kuwa rais amekubali kukutana nao wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuunasua mchakato huu.

MTOTO AMCHARANGA MAPANGA MZAZI WAKE MKOANI MBEYA


MKAZI wa kijiji cha Ndala, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Andondile Mwasamlagila (50) amenusulika kufa baada ya kucharangwa na mapanga na mtoto wake, Yuda Mwasamlagila kutokana na ulevi wa kupindukia.

Wakizungumza na blog hii, wanafamilia walisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 11 mwaka huu majira ya jioni ambapo mzee huyo akiwa amejituliza katika makazi yake, akivamiwa na kushambuliwa na mapanga na mtoto huyo.

Walidai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa mzazi huyo wakati akishambuliwa na kwamba waliposogea karibu walikuta akiwa hajitambui huku akiwa na majeraha kwenye shingo na sehemu za kichwa.

Kwa mujibu wa wanafamilia hao, walimkimbiza katika kitu cha afya cha Mwakaleli kwa ajili ya matibabu na kwamba sasa anaendelea vizuri.
Kwamba, wakati majeruhi akipatiwa matibabu, wanakijiji waliamua kwenda kumsaka mtoto wake aliyesababisha tukio hilo ambapo walimkamata akiwa amejificha kwenye shimo huku akiwa amelewa.
Kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Iddy Suleiman alikiri kupokea majeruhi huyo, akisema bado anaendelea na matibabu.

WANAWAKE 600 WAISHIIO ENEO LISILO NA WANAUME NCHINI BRAZIL WAOMBA KUPELEKEWA WANAUME



                               HUU NDIYO MJI WANAOISHI WANAWAKE HAO.
Zaidi ya wanawake  600 wanaotengeneza jumuia ya wakazi katika eneo la women Noiva do Cordeiro kusini mwa  Brazil ambao wengi wao wana umri kati ya miaka 20 na 35 wanaomba kupelekewa wanaume kutokana na eneo hilo wanaloishi kutokuwa na wanaume. 
Mji huo ambao idadi ya wakaaji wake wote ni wanawake umeomba angalau mwanaume mmoja kwenda kuishi katika eneo hilo ingawa atatakiwa kuishi kulingana na sheria za kike zinazotawala eneo hilo.

Ingawa baadhi ya wanawake hao wameolewa na wanafamilia lakini waume zao hufanya kazi nje ya eneo hilo na wanatakiwa kurudi mwisho wa juma tu (Weekend)

Hata hivyo watoto wa kiume wanapozaliwa na kufikisha miaka 18 wanatakiwa kuondoka na hakuna mwanaume yeyote anayetakiwa kuishi katika mji huo ambao upo umbali wa Mile 60 mashariki mwa Belo Horizonte.

Historia ya eneo hilo inarejea miaka ya  1890 ambapo msichana mmoja na familia yake walitengwa kutoka kanisa la Kikatoliki baada ya kushutumiwa kuwa mzinifu.

Taratibu wanawake wengi ambao walikuwa hawajaolewa pamoja na familia zao walianza kujiunga na jamii hiyo na miongo kadhaa baadae wanaume walifanya majaribio kadha ya kuingia katika eneo hilo hali amabayo ilipelekea jamii hiyo ya wanawake kuanzisha sera ya hakuna mwanaume "'no male' policy."

Mmoja wa wanawake hao aliyefahamika kwa jina la Nelma Fernandes mwenye maiaka 23, anakili kwamba ni vigumu kwa msichana anayejulikana katika hilo eneo na ni mrembo kuacha kuchumbiwa ikiwa mwanaume atamuona ila tatizo ni ukosefu wa wanaume hao.

Anasema "mwanaume pekee ambao wasichana hutana nao ni wale ambao wameoa au wana uhusiano wa kindugu,Wote ni binamu.Nimembusu mwanaume muda mrefu sana uliopita."

Anaongeza kusema kuwa "Wote tunandoto ya kupenda na kuolewa lakni tunapenda kuishi hapa na hatutaki kwenda mjini kutafuta wanaume."