Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akizungumza na waandishi wa
habari alipokutana nao leo kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya
Uongozi wa Bunge hilo kilichokaa leo kutathmini kazi za kamati 12 za
Bunge hilo lilipofikia pamoja kuridhia baadhi ya maependekezo ya
kuongeza ibara na sura ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati zao.
Wednesday, August 20, 2014
MAMA AMCHANA MWANAWE WA MIEZI MIWILI NA VIWEMBE SEHEMU YA HAJA KUBWA BAADA YA MTOTO KUZALIWA AKIWA HANA
Vitendo vya baadhi ya wananchi kujitibu pasipo kufuata maagizo na njia za kitaalamu vimeendelea kukithiri nchini ambapo hapa jijini Mwanza mama mmoja ameamua kumchanja kwa viwembe mwanae mwenye umri wa wiki mbili baada ya
mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu ya Haja kubwa.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya mama huyo aliyefahamika kwa jina la Anastazia Ngilitu kumchana kwa wembe zaidi ya mara tatu ili kumsaidia mwanae kupata haja kubwa kwa kile kilichodaiwa mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu
ya haja kubwa.
Akiongea kwa uchungu mama huyo mkazi wa Tabora aishie jiini mwanza kwa sasa amesema kuwa alijifungua watoto mapacha watatu ndani ya Mtaro kisha wawili kufariki alipofikswa Hospitali na kusalia mtoto mmoja aliyekutwa na tatizo la Kutokuwa na sehemu ya haja kubwa.
Sambamba na hayo mama huyo amesema kuwa sababu za kumchana na wembe mwanawe ni baada ya kumuona mtoto wake anashindwa kupata haja kubwa hali
iliyopelekea tumbo kujaa na kulia.
Ameongeza kuwa wakati wa kujifungua mtoto huyo walimfanyia upasuaji katika hospitali ya Bugando ila hali ya kuziba ilijirudia tena na kuamua kumchana kwa
kutoakana na kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama za upasuaji hospitali.
Katika hatua nyingine Mama huyo amesema kuwa kwa sasa hali yake ya Maisha siyo nzuri kwani watoto wake wanaishi kwa kunywa maji na kwamba hapo awali alikuwa anafanya kazi ya kufua nguo kwenye nyumba za watu ila kwa sasa hawezi
kutokana na kuwa na mototo mdogo.
Sambamba na hayo mama huyu anasema kuwa licha ya kuolewa na wanaume watatu kwa wakati tofauti na kila mmoja kumnyanyasa kwa kumpiga na mwingine kumdhurumu pesa zaidi amesikitishwa na kitendo cha Mume wake wa sasa hivi kumtaka kufanya mapenzi ikiwa tumbo la uzazi halijakaza hali anayotaja kumsababishia maumivu makali na kutokwa na damu nyingi baada ya mumewe
kumpiga.
Kitendo cha mama huyu kumchana mtoto wake kwa wembe kinatoakana na hofu ya kwenda hospitali kwani anasema hana uwezo wa pesa kwani kwa sasa yeye mwenyewe anasumbuliwa na uvimbe katika titi lake la kushoto na alipoenda Hospitali ya SEKOTURE aliambiwa gharama za upasuaji ni shilingi elfu 30 na
alipokosa alirudi nyumbani na kuendelea kujitibu kwa dawa za kienyeji.
Kwa upande wao baadhi ya kina majirani ambao wamekuwa wakimpa msaada mama huyu mara kwa mara,Wamesema kuwa mama huyu ana maisha magumu kwani mume wake humpiga na kumfukuza mara kwa mara hali inayomfanya aishi kwa kuomba omba na wakati mwingine kulala na watoto wake
bila kula.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mama huyu aliolewa na mume wa kwanza mkazi wa eneo la maji moto mkoani Mara na waliachana baada ya kupigwa na kuchomwa kisu tumboni ikiwa ni pamoja na kupigiliwa msumali wa nchi sita katikati ya mkono
wake wa kushoto ikiwa ni sambamba na kumvuta hereni akimwambia kuwa ni dalili za kuwa malaya hali iliyomsababibishia masikio yake kuvimba.
Mume wa pili aliyemuoa mama huyo inaelezwa kuwa yeye alimdhurumu kiwanja walichouza milioni moja na laki saba kilichokuwa eneo la makaburi Bwiru kisha
kuzichukua na kuaga kwenda kuzifanyia biashara.
Kuhusu ndugu Bi Anastazia amesema kuwa wazazi wake wote wamefariki na kwamba aliyebaki ni bibi yake ambaye naye anamtaja kuwa ni mchawi kwani wakati alipoenda Tabora,bibi yake alimwambia ampe mkono wa mtoto ili usiku wa manane
amuamshe kwa kumpiga nao kichwani ili aende kazini.
Anastazia anasema kuwa kutokana na matatizo hayo aliwahi kushauriwa kumtupa mtoto huyo eneo la vichakani soko la sabasaba,ushauri aliopewa na rafiki yake mkazi wa Ilemela aliyemtaja kwa jina moja la Amina ambaye alimwambie mtoto wako hatapona,Jambo ambalo yeye alikataa na kusema kuwa anaogopa mkono wa Sheria.
Tatizo linalomsumbua mama huyo kwa sasa ni chakula na matibabu kwa mwanaye na yeye mwenyewe anayesumbuliwa na uvimbe katika titi la kushoto na kuwaomba wasamalia wema kumsaidia ili aendelee na shughuli zake aondokane na
kuombaomba.
MWONEKANO WA MASIKIO YAKE BAADA YA KUVUTWA HELENI NA MUMEWE WA KWANZA.
PAPA FRANCIS AJITABILIA KIFO
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kwa mara ya kwanza ametabiri hatima ya maisha yake duniani akisema kuwa anaamini Mungu anaweza kumpa muda wa miaka miwili au mitatu ya kuishi.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akitoka ziarani Korea Kusini kurejea Vatican, Papa Francis alisema suala la kuendelea kuishi ni neema ya Mungu.
Suala hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu kutafakari kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua kwa sababu hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu nitakuwa nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba
alisema.Papa Francis (77), pia alizungumzia uwezekano wa kustaafu endapo atahisi kwamba afya yake hairuhusu kuendelea na kazi.
Utamaduni
wa kuachia madaraka ndani ya kanisa hilo linalotajwa kuwa na waumini
wengi duniani uliasisiwa upya mwaka jana na mtangulizi wake, Papa
Benedict XVI aliyeng’atuka kutokana na matatizo ya kiafya.Pamoja na
kwamba Papa Francis hajawahi kuzungumza hadharani kuhusu ni lini pengine
anaweza kufariki dunia, lakini baadhi ya vyanzo vya habari kutoka
Vatican vinasema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwaambia watu wake wa
karibu kuhusu siku zake chache zilizosalia duniani.
Wachambuzi
wa masuala ya kiimani kwa nyakati tofauti walisema huenda kiongozi huyo
ana tatizo la kiafya ambalo halijawekwa wazi.Wakati hayo yakiendelea
taarifa za ndani zinabainisha kwamba kiongozi huyo aliwahi kutolewa pafu
moja baada ya kuathirika wakati akiwa kijana nchini Argentina
MAGAVANA WA BENKI YA PTA KUKUTANA TANZANIA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (katikati)
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dodoma juu ya
mkutano wa 30 utakaofanyika nchini mwishoni wiki hii. Kushoto ni
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA),
Admassu Tadesse na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu
Tadesse (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana
kuhusu mkutano wa miaka 30 ya wanahisa na magavana utakao shirikisha
nchi 18 za Afrika, mkutano huo utafanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Waziri wa Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Steven
Wasira akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (kushoto)
abibadilishana mawazo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na
Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse mara baada ya mkutano na
waandishi wa habari jana mjini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile.
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
19/082014
Bodi
ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa
Afrika (PTA) itakuwa mkutano wa mwaka utakaofanyikia nchini jijini Dar
es salaam tarehe 22 mwezi huu.
Hayo
yamebainishwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari juu ya mkutano huo utakaofanyika mwishoni wiki hii.
“Huu
ni mkutano wa kawaida wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa nchi wanachama
pamoja na Mawaziri wa Fedha, Tanzania ni mwanachama ndio maana mkutano
wa 30 unafanyika hapa” alisema Wasira.
Wasira
amesema kuwa katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo
masuala ya fedha na uchumi, maendeleo ya benki ya PTA na mafanikio yake
kwa nchi washirika.
Vile
vile Wasira amesema kuwa PTA ni benki ya Kiafrika na inafanyakazi nzuri
ambapo inaonesha inakua kwa zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka kwa miaka
kadhaa hadi sasa na imekuwa na mizania ya Dola za Kimarekani mil. 2.8
ikiwa miongoni mwa benki za maendeleo zinazofanya vizuri katika bara la
Afrika.
Aidha,
Wasira ameongeza kuwa mkutano huo utatanguliwa na semina ya
wafanyabiashara itakayofanyika Agosti 21 siku moja kabla ya mkutano mkuu
wa Magavana hao ambapo Serikali itawakilishwa na Naibu Waziri wa Fedha
Mwigulu Nchemba.
Kwa
upande wake Rais na Mtendaji Mkuu wa benki ya PTA Admassu Tadesse
amesema kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele na ni mwanachama hai
ambapo imekuwa mfano mzuri kwa nchi wanachama kwa kutoa michango
mbalimbali kwa wakati.
Zaidi
ya hayo, Tadesse amesema kuwa benki hiyo mwaka huu inaadhimisha miaka
30 tangu kuanzishwa kwake, Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa
mkutano wa mwaka huu ili washerehekee na Watanzania.
Tadesse
amesisitiza kuwa Benki ya PTA inatoa huduma zake kwa nchi wanachama
ikiwa na lengo la kuwa tasisi ya kifedha inayoongoza Mashariki na Kusini
mwa Afrika katika utoaji wa huduma za kibenki.
Benki
ya PTA ilianzishwa mwaka 1985 ambapo hadi sasa ina jumla ya wanachama
22 ikiwemo nchi 18 ambazo ni Burundi, Comoros, Djibouti Congo, Kenya na
Malawi.
Nchi
nyinine ni Misri, Eritrea, Ethiopia, Mauritania, Rwanda, Seychelles,
Somalia, Sudan, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania
Aidha, PTA inashirikiana na nchi nyingine nje ya bara la Afrika ambazo ni Belarus na China.
Washirika
wengine ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Kampuni ya Bima ya
Mauritia iitwayo Eagle na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mauritius.
Mkutano
wa mwaka huu unafanyikia Tanzania ikiwa ni utaratibu wa benkiya PTA
kufanya mikutano ya mwaka kwa mzunguko ambapo washiriki watakuwa
Mawaziri wa Fedha, Magavana wa nchi wanachama, sekta binafsi, Mabalozi
wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini na Wawakilishi wa Mashirika ya
kimataifa.
MRADI WA KUZUIA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE WAZINDULIWA JIJINI MBEYA
Naibu
Meya wa Jiji la Mbeya Chifoda Yesaya Fungo akizindua Mradi wa kuzuia
ukatili wa kijinsia kwa wanawake katika ukumbi wa Halmashauri jiji Mbeya
|
Mrtibu wa MBEPAU Jane Lawa akitoa maelezo mafupi jinsi mradi huo utakavyofanya kazi kwa kushirikiana wadau mbalimbali katika jamii |
Mratibu wa NGOS Victor Kabuye akifafanua zaidi jinsi mradi huo utakavyofanya kazi karibu na jamii |
Baadhi ya wageni waalikwa katika uzinduzi wa mradi huo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi |
MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA AKITOA NENO LA SHUKRANI
|
PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA KUZINDULIWA KWA MRADI HUO Picha na Mbeya yetu |
RASIMU YA KATIBA MPYA YA JAJI JOSEPH WALIOBA YACHANWA CHANWA DODOMA
Mwenyekiti wa Kamati Namba Tano ya Bunge la Katiba, Hamad Rashid akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana. Kulia ni makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Assumpta Mshana. Picha na Emmanuel Herman
Dodoma. Kuna kila dalili kwamba mabadiliko mengi yaliyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba yakigusa miundo ya taasisi nyeti za umma yatawekwa kando na huenda Bunge Maalumu likatoa Katiba isiyokuwa na mabadiliko makubwa kama ilivyotarajiwa.
Gazeti hili limebaini kuwa kamati nyingi za Bunge hilo zimebadili mapendekezo mengi hasa yanayowagusa viongozi na taasisi nyeti kama Bunge, tofauti na ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.
Miongoni mwa mambo ambayo yamependekezwa kurejeshwa kama yalivyokuwa ni muundo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo kwa mujibu taarifa kutoka kwenye kamati mbalimbali, ni kuendelea na muundo wa sasa unaowajumuisha wabunge kutoka Zanzibar.
Katika maelezo yake, Jaji Warioba alisema moja ya kero za muungano katika eneo la Bunge ni malalamiko kwamba wabunge kutoka Zanzibar wamekuwa wakishiriki katika Bunge la Muungano na kushiriki kujadili mambo yanayohusu Tanzania Bara.
Kupitia mfumo wa Serikali tatu, Rasimu ilikuwa na mapendekezo ya kuwapo kwa Bunge la Muungano lenye wabunge 75, lakini mapendekezo hayo pia yamefutwa katika kamati karibu zote na kurejesha mfumo wa sasa pamoja na uwapo wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati Namba Tano, Hamad Rashid Mohamed alisema jana kuwa suala la muundo wa Bunge lilisababisha mvutano mkubwa katika kamati yake na baadhi ya wajumbe walikuwa wakihoji uwakilishi mkubwa wa wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Muungano hata kwa mambo ya Tanzania Bara.
Hata hivyo, alitetea hali hiyo akisema uwapo wa wabunge kutoka Zanzibar ni moja ya masharti yaliyowekwa na Katiba. “Hata Katiba ya sasa imeweka sharti la idadi ya wabunge wa Zanzibar, hilo nalo ni sharti la Katiba huwezi kuliondoa, kama unataka kuliondoa unapotunga Katiba maana yake ni lazima uvunje muungano.”
Alisema mwaka 1964 mambo yote ya Tanganyika yaliingizwa kwenye Serikali ya Muungano... “Kwa hiyo ni lazima ukafumue Muungano, useme haya ni ya Tanganyika na haya ni ya Muungano,” alisema.
Hamad alisema katika hadidu ya rejea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikatazwa kugusa mambo ya Muungano. “Hivi wabunge 70 wanaokuja kutoka Zanzibar wakazungumzia mambo ya Bara, hivi kuna dhambi gani, sioni kosa kabisa.” Mwenyekiti huyo alisema kamati yake imebaini kwamba Rasimu ya Warioba ina upungufu mwingi kwani hata baadhi ya kero zilizotajwa zilishafanyiwa kazi na Serikali.
Hoja ya ushiriki wa Wazanzibari katika masuala ya Tanzania Bara iliripotiwa kuibuka katika Kamati Namba Moja ambako mmoja wa wajumbe, Ally Keissy alinikuliwa akihoji sababu za wajumbe wa Zanzibar kushiriki mambo ambayo wao siyo sehemu yake.
Mambo mengine
Mbali na muundo wa Bunge, kamati nyingi pia zimefuta mapendekezo kadhaa yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba ambayo ni pamoja na wabunge kutokuwa mawaziri, ukomo wa ubunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano mitano, wabunge kuwajibishwa na wananchi, kupunguzwa kwa madaraka na kinga ya rais.
Katika Kamati Namba Tano, Hamad alisema suala la wananchi kumuondoa mbunge lilikataliwa. “Hivi ni kigezo gani ambacho kinaonyesha mbunge hakuweza kuwaletea wananchi maendeleo. Nini utatumia cha kupima ufanisi wa huyu mbunge?”
Alisema kuliweka jambo hilo katika Katiba ni kuleta matatizo na kwamba wameliacha suala hilo mikononi mwa vyama vya siasa kuangalia kama mbunge anafanya kazi ya ilani zao au la.
Mgawanyiko mpya
Habari zaidi zinasema kuwekwa kando kwa mapendekezo mengi yaliyolenga kurekebisha mifumo ya uongozi na utawala, kumesababisha mgawanyiko hasa miongoni mwa wajumbe watetezi wa muungano wa serikali mbili, ambao awali, waliahidiwa kwamba muundo huo usingekuwa na sura yake ya sasa, bali ungeboreshwa.
Mmoja wa wabunge wa CCM alisema jana kwamba: “Tutawapa wapinzani sifa maana umma utaamini kwamba bila wao hakuna kinachoweza kubadilika, sasa kama tunarejesha kila kitu ambacho kiko kwenye Katiba tuliyonayo kuna maana gani ya kuwa na mchakato?”
Mmoja wa wenyeviti wa kamati za Bunge Maalumu naye alisema kinachoendelea ndani ya kamati nyingi ni kufuta mapendekezo ya Rasimu na kuleta mapendekezo mapya ambayo ni sawa na yaliyomo kwenye Katiba ya sasa.
“Ndani ya chama (CCM) tuliamua kupinga mapendekezo ya serikali tatu baada ya kuahidiwa kwamba tutakuja na muundo wa serikali mbili zilizoboreshwa, lakini hata hizo hatuzioni. Kwa hiyo wananchi wataamini kwamba kilichosemwa na Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi), ni cha kweli,” alisema mwenyekiti huyo.
Utata wa akidi
Mwenyekiti wa Kamati Namba Tatu, Dk Francis Michael aliamua kuahirisha kikao jana saa tano asubuhi kutokana na kile alichokiita kuwa ni kuwapa muda wajumbe waende kusoma zaidi sura ya tisa ambayo inahusu muundo wa Bunge.
Hata hivyo, habari ambazo zilikuwa zimelifikia gazeti hili mapema zinasema kuahirishwa kwa kikao hicho kulitokana na akidi kutotimia, taarifa ambazo Dk Michael alizikanusha kwa kuonyesha idadi ya wajumbe ambao walikuwa wamesaini karatasi ya mahudhurio.
Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo alikiri kwamba hadi ilipotimu saa 4:00 asubuhi jana kamati yake ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa wajumbe wanne, hivyo waliwapigia simu na kubaini kwamba walikuwa katika shughuli nyingine ikiwamo kumpokea Rais Jakaya Kikwete.
“Baadhi ya wajumbe ni mawaziri kwa hiyo baada ya kukamilisha majukumu yao walifika na saa tano hivi akidi ilikuwa imetimia,” alisema Dk Michael.MWANANCHI
RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAHANI MSIBA WA MAREHEMU JAJI MAKAME
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti
wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis
Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki katika Hospitali ya AMI
Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.
Mama Salma Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti
wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis
Makame, Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki katika Hospitali ya
AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa walipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti
wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis
Makame, Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki katika Hospitali ya
AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam Agosti 19, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto wa marehemu pamoja na Jaji
Mstaafu Mark Bomani alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti
wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis
Makame Masaki, jijini Dar es salaam aliyefariki katika Hospitali ya
AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.
CCM YAKUBALI YAISHE, YAKUBALI KUAHIRISHA BUNGE MAALUM LA KATIBA
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinasema kwamba kikao cha dharura cha CCM kilichofanyika jana kimetaka Bunge la Katiba (BMK) liahirishwe. Hii ni baada ya kujiridhisha kwamba akidi ya 2/3 kutoka Zanzibar haitatimia, hivyo ni bora kuahirisha bunge hilo kuliko kuteketeza fedha za watanzania ambazo zingetumika kubosesha huduma za jamii zilizo taabani kama vile maji, afya, miundombinu na elimu.
Chanzo:Mtanzania
CHADEMA YAKANUSHA KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANGOSI
Baadhi
ya viongozi wa Chadema kutoka kushoto ni Ofisa Habari, Tumaini Makene,
Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika, Ofisa Mwandamizi Mafunzo na
Uendeshaji, Mohamed Mtoi, na mwenye gwanda ni Katibu Mtendaji, Ofisi ya
Katibu Mkuu, Victor Kimesera. Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Chadema. Jengo la makao makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni, Dar.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekana shutuma zilizoelekezewa kwao kuwa wanahusika na kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi. Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Mhe. John Mnyika, ameeleza kuwa hawahusiki na mauaji hayo bali ni propaganda zinazoenezwa ili kuwasahaulisha wananchi juu ya suala la katiba linaloendelea. Mnyika alieleza kuwa wanaoeneza habari hizo ni wale ambao wanataka kuizuia Chadema na Ukawa kwa ujumla kuendelea na harakati za kupigania katiba ya wananchi ikiwemo kufanyika maandamano ya kitaifa iwapo Rais Kikwete hataingilia kati kulisimamisha zoezi la katiba mpya.
WATU 16 WADAIWA KUFARIKI KATIKA AJALI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA
Baadhi ya miili ya marehemu.
Watu
zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa
baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji cha
Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali
hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la
Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea
Mbeya kwenda Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline
lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia
Mpanda.Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani Sikonge.Pia
inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James
Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo a
kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya
kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi( Day-worker)
Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi
yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda
-Mwanza na AM Dreamline lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.
Jitihada
za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.
Subscribe to:
Posts (Atom)