Wednesday, October 29, 2014

AJALI MBAYA ILIYOTOKEA ARUSHA LEO WATANZANIA ZAIDI YA 15 WAPOTEZA MAISHA

ANGALIA PICHA

Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili zitawajia punde. 








ROSE MUHANDO ADAIWA KUBWIA UNGA!


Nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando. Kwa mujibu wa vyanzo, Rose anadaiwa kutumia unga kiasi kwamba, baada ya matumizi hujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile la kujitafutia mkate wake wa kila siku na ndiyo maana amekuwa akikwaa skendo za kupokea fedha za shoo halafu hatokei tu! 
HUKU mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia madawa ya kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa kutokea kwenye matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano linateremka nayo. 
WATOA MADAI
Hivi karibuni, akina mama watatu walifika kwenye Ofisi za Global Publisheers na kumtolea madai Rose kuhusu tuhuma zanazomwandama kwamba amekuwa akiingia mitini na fedha za watu wanaomwita kwenye matamasha ya nyimbo za Injili.


“Sisi tunavyojua, Rose anatumia madawa, wengine wanasema unga wengine wanasema sijui nini huko. Sasa akishatumia hayo madawa huwa yanamfanya awe kama amelewa na kushindwa kufanya lolote.

“Huwa anafika hatua anashinda kitandani amelala tu na hawezi kutoka, ndiyo maana mtu anaweza kumpa pesa asitokee kuimba kwa sababu anashindwa kutoka ndani kwake.

MWANAMKE ATUMBUKIA CHOONI WAKATI AKIFANYA MAPENZI NA HAWALA, HUKU MUMEWE AKIWA MAUTUTI CHUMBAN



Picha hii haiendani na picha tukio lakini picha hii pia wananchi walikuwa wakifanya uokoaji baada ya kijana mmoja kudumbikia chooni na kufa papo hapo. 
Na.Gabriel Mbwille, Mbozi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la TIENA MWAZEMBE mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji Hangomba kata ya Bara wilayani Mbozi mkoani Mbeya amenusurika kufa baada ya kutumbukia chooni wakati akifanya mapenzi huku mumewe akiwa maututi chumbani.

Habari za uhakika kutoka kijiji hapo zinadai kuwa mwanamke huyo licha ya kuwa mke wa mtu alikuwa anafanya ngono chooni na WASI MGALA wakati mumewe akiwa ndani anaumwa na kwamba alidumbukia choo baada ya banzi alilokuwa amekanyaga kukatika wakati wanafanya tendo hilo

hatahivyo baada ya mwanamke huyo kutumbukia ndani ta choo mwanamke aliyekuwa nae chooni humo wakifanya tendo hilo alikimbia na kumuacha wanamke huyo akipiga mayowe ndani ya choo kitu kilichowafanya wanakijiji wafurike na kumuokoa mwanamke huyo
SAIKI GODFREY KAROTI amesikitishwa na kitendo hicho kuwa ni udharirishaji kwake 

JAMAA ALIYEKUWA AKIWABAKA VIKONGWE ATIWA MBARONI HUKO KISARAWE PWANI




JESHI la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Michael William maarufu (Michael dada), mkazi wa Kiluvya, wilayani Kisarawe anayetuhumiwa kuhusika na matukio ya ubakaji wa vikongwe mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei alisema jeshi hilo lilikuwa likimsaka mtuhumiwa huyo kwa kipindi kirefu kutokana na kudaiwa kutenda makosa mbalimbali ya ubakaji wa vikongwe na wanawake na kutokomea kusikojulikana.

Alisema, William alitiwa mbaroni juzi baada ya kudaiwa kuhusika katika tukio la wizi wa mifugo lililotokea wiki mbili zilizopita huko Kiluvya.
Pia kamanda Matei alisema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika katika matukio ya ubakaji zaidi ya 10 ambapo kabla ya kufanya vitendo hivyo alikuwa akiwatishia wahusika kwa mapanga.
“Huyu kijana anayejiita Michael dada ni maarufu kwa matukio ya ubakaji na alilisumbua jeshi letu mara kadhaa kwa kunasua mitego aliyowekewa leo tumelazimika kumleta mbele yenu waandishi ili mumuone ni mdogo lakini ametusumbua sana,” alisema.SOMA ZAIDI>>
William alikiri mbele ya waandishi wa habari kuwa miaka ya hivi karibuni aliwahi kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha kosa ambalo lilimsababishia kuhukumiwa miaka 30 jela
Matei alisema kabla kifungo hicho hakijamalizika mwaka 2011 na 2012, William alikata rufaa na kutolewa ili kuendelea na taratibu nyingine na tangu hapo hakuonekana hadi polisi walipofanikiwa kumkamata kwa kosa la wizi wa mifugo.
Hata hivyo William alikana kuhusika na tuhuma zinazomkabili na kudai yeye sio Michael dada kama anavyoitwa bali ni Michael William na tuhuma za ubakaji ni za kusingiziwa.

KITU KINACHOSADIKIWA KUWA BOMU CHAKUTWA JIJINI DAR


Picha ya kitu kinachosadikika kuwa ni bomu kimegundulika maeneo ya Kijitonyama,  jijini Dar.

Gari la uchafu likiwa linaenda kuchukua  uchafu eneo la tukio.

Wananchi wakiwa eneo ambalo kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kimeonekana.

Askari polisi wakiwa eneo la tukio.

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Leonard Thomas amegundua kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar.

Akizungumza na GPL Lenard alisema: "Nilikuwa naenda kuchoma moto taka ndipo nikaona kitu kama chuma kizito kama bomba ila kikanishangaza kiko kipekee nikiwa bado na shangaa mwenzagu akaja kuniambia kuwa ni bomu ndipo nikawajulisha polisi.

Polisi walifika eneo la tukio na kuweka ulinzi wakati wakisubiri wataalamu wa mabomu wafike.

MFANYABIASHARA AJILIPUA BAADA YA KUSABABISHA AJALI

busi
SAKATA la Mkurugenzi wa Kampuni ya Kitalii ya DAGT, Timoth Mroki, kujiua kwa kujilipua kwa risasi, limeibua mambo mapya kutokana na kuelezwa kuwa wivu wa kimapenzi.
 
Habari zilizopatikana jijini Arusha, zinasema kuwa Mroki (36), alikuwa na vimada wawili ambao ni wake za watu na kuwa kabla ya kujilipua kwa risasi na kupoteza maisha, alitoa taarifa kwa wanawake hao (majina yanahifadhiwa).
 
Imeelezwa kuwa Mroki alikuwa akitoka na wanawake hao kila mmoja kwa muda wake, lakini baadaye siri hiyo ilianza kuvuja na hatimaye vimada kufahamiana, ikiwa ni pamoja na mkewe kuanza kupenyezewa taarifa hizo.
 
Mroki, ambaye pia ni Meneja wa Operesheni na Masoko wa Kampuni ya Tanzania Bush Camp, alijiua kwa kujipiga risasi Oktoba 25, mwaka huu, saa 1:00, baada ya kubaini kuwa vimada wake hao wamefahamiana.
 
Habari kutoka kwa mtu wa karibu zimesema kuwa, vimada hao baada ya kufahamiana, walikutana na kufanya mazungumzo kisha kupiga picha pamoja na kumrushia kupitia simu ya mkononi.
 
Kugundulika kwa siri hiyo, kulizusha taharuki kwa Mroki, hivyo kusababisha kuyumba kwa uhusiano baina yake na vimada hao, akiwemo mmoja ambaye pia ni mshirika wake kibiashara.
 
“Hawa wanawake wana siri nzito kuhusiana na kifo hiki kwa sababu kabla ya kufanya uamuzi, aliwasiliana nao…kikubwa awali walikuwa hawafahamiani ila baadaye walikutana na kuungana kuwa kitu kimoja.
 
“Haifahamiki ni kwa vipi walijenga urafiki, ila watu wa karibu wanasema walijipanga kumkomoa ili afilisike kwa kuwa kila mmoja alikuwa na malengo yake,” alisema mtoa habari wetu.
 
Kuungana kwa wanawake hao kumlichanganya Mroki, ambaye tayari uhusiano wake nyumbani pia ulianza kuwa tete baada ya mkewe kuhisi kuna mambo yanafanyika kinyume cha utaratibu.
 
Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa miongoni mwa wanawake hao, yupo aliyejenga uswahiba na mke wa marehemu huku uhusiano wa kimapenzi ukifichwa chini ya mwamvuli wa biashara.
 
Chanzo chetu kimesema kuwa, kutokana na ukaribu huo, familia hizo zimekuwa na kawaida ya kutembeleana, ikiwa ni pamoja na watoto kukaa kwa siku kadhaa nyumbani kwa kimada mmoja.
 
Imeelezwa kuwa kutokana na kugundulika kwa siri hiyo, Mroki alichukua uamuzi wa kujimaliza ili kukwepa aibu mbele ya familia.
 
“Kugonga gari si sababu ya Mroki kujiua, ni kutokana na kutingwa na mambo mengi kichwani, hasa baada ya siri ya kimapenzi kuanza kubainika,” aliongeza mmoja wa rafiki wa marehemu.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema Mroki alijiua kwa kujipiga risasi kifuani kwa kutumia bastola aina ya KEL –TEC yenye namba HCB21.
 
Katika taarifa yake, Kamanda Sabas alisema kabla ya tukio hilo, Mroki alikuwa na gari namba T222CMX, aina ya Isuzu Double Cabin, iliyokuwa ikitokea Mbauda kwenda katikati ya jiji.
 
Hata hivyo, taarifa hiyo iliongeza kuwa kutokana na msongamano wa magari, Mroki alitanua barabara kukwepa foleni huku akiwa katika mwendo kasi.
 
Alipofika maeneo ya Shams, aligongana na gari la mizigo, mali ya Kampuni ya Gupta, lenye namba T548 BRL.
 
Taarifa ilisema pamoja na kusababisha ajali hiyo, Mroki aliendelea na safari yake ndipo madereva wa bodaboda walipoamua kumfukuza na kumkamata eneo la kona ya Nairobi Ngarenaro.
 
Mroki aliporejea eneo la tukio na kuulizwa sababu za kusababisha ajali na kuendelea na safari, alitoa bastola na kufyatua risasi mbili hewani na ya tatu kumpiga kifuani.

TANZANIA YAKATAA RASMI NDOA ZA JINSIA MOJA KWENYE AGENDA ZA MAENDELEO YA MILENIA


001
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.

SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.

“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy.

Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.

002
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.

Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo. Amesema kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.

Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga. Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
003
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.

“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
004
Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za kutimiza malengo ya milenia.
005
Mdau akichangia mada yake.
006
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.

008
009