Saturday, November 22, 2014

MAHAKAMA YAKANA KUANDIKA BARUA KUZUIA MJADALA WA TEGETA ESCROW BUNGENI

Wakati Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakichachamaa wakisema hawatakubali Bunge hilo kuingiliwa na mhimili wa Mahakama, Mahakama hiyo imejiweka kando na tuhuma hizo.
http://3.bp.blogspot.com/-_8KNOoetHc0/UZSaUgDsCUI/AAAAAAAACGo/qJUBJ9N4eVg/s1600/wabunge6.JPG
Sakata hilo lililotawala kikao cha Bunge hilo jana lilitokana na madai yaliyoibuliwa juzi na wabunge wa kupinzani unaoundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi.

Wabunge hao Tundu Lissu (Chadema), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Habib Mnyaa (CUF) waliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kuwa wamepata taarifa za uhakika kuwa Mahakama imeandika barua ikiritaarifu Bunge lisijadili kashfa ya uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.

Wabunge hao, walisema kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili wa Bunge na kwamba lengo lake ni kutaka kukwamisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili wahusika wasichukuliwe hatua.

Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi, alipotakiwa kuthibitisha kama Mahakama imeandika barua hiyo kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge kuzuia suala hilo lisijadiliwe kwa kuwa kiko mahakamani, alisema yeye na wasajili wenzake hawana taarifa kuhusu kuandikwa kwa barua hiyo.

“Labda unieleze hiyo barua imeandikwa na nani na lini, kama ni Jaji au Msajili nitajie jina lake ili iwe rahisi kufuatilia, lakini hadi sasa nimepekua kwenye kumbukumbu zetu sijaona barua hiyo,” alisema Msumi.

Aliahidi kwamba jana angewasiliana na wenzake wa Mahakma ya Rufani kama kuna barua imeandikwa kutoka mahakama hiyo kwenda bungeni.

Hadi sasa hakuna mamlaka yoyote ya serikali iliyothibitisha rasmi kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge.
Juzi Naibu Spika,Job Ndugai, alisema kuwa ofisi ya Spika haijapokea barua hiyo.

Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akizungumza bungeni jana kuhusiana na madai hayo, hakuthibitisha wala kukanusha kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda bungeni kuzuia mjadala huo, zaidi ya kusisitiza itumike busara ili kuepusha mihimili hiyo kuingiliana katika majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Chanzo: Nipashe

A-Z KUHUSU BILIONEA ALIYEKUFA AKIWA NDANI YA GARI BUKOBA!


Tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari. Tukio hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18, mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia, kabla ya kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST lenye namba za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na kimada wake aliyetajwa kwa jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini Bukoba.

KIFO cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo hadharani juu ya kila kitu kilichotokea
Mwili wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Bukoba kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa siku ya leo. 

Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki Klabu ya Linas, alidaiwa kunywa pombe kali aina ya Whisky Bond pasipo kula vizuri huku akisumbuliwa na tatizo la presha hivyo wakati akifanya yake ndani ya gari, ghafla presha ilipanda, akaanza kutapatapa.
Msafara wa magari ukitoka kuchukua mwili wa marehemu hospitali kuelekea nyumbani kwake.
“Si unajua tena jamaa umri umeenda kidogo na anasumbuliwa na presha, sasa inawezekana na kinywaji alichokunywa ndiyo kilitibua zaidi. Pombe ukiwa hujala huku una tatizo la presha madhara yake ndiyo haya,” kilisema chanzo chetu.
Mke wa marehemu akiwa haamini kama mumewe amefariki.

 
Baada ya hali yake kubadilika ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake badala ya kukimbia kama ambavyo wengine hufanya, yeye alifanya juhudi kubwa kujaribu kuokoa jahazi kwa kupiga simu kwa marafiki wa marehemu, lakini kabla hawajafika, mtu mmoja alitokea na kumsaidia marehemu kumpeleka katika kituo cha Afya cha CLCT-Ndolage.

Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki kabla hajafika hospitali.
“Wakati wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio sana kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
Binti aliyekuwa na marehemu.

Chanzo kilidai kuwa, baadhi ya marafiki wa marehemu waliingiwa hofu na mrembo huyo na kuwa na wasiwasi wakihoji chinichini kwamba pengine alimpa marehemu kitu kibaya. 
“Marafiki wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo, walikuwa wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye madhara,” kilisema chanzo chetu.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.


Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu maeneo ya Kyakairabwa, kata ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona aibu kuzungumzia kifo chake hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa marehemu alikuwa mtu anayeheshimika katika jamii.
Jeneza la marehemu, Leonard Mtensa.

 “Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
Ili kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na kifo chake,  daktari mmoja mtaalamu wa magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida. “Wako watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine wanakuwa na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa. 
“Halafu pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya presha, akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali kubadilika) wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya vyakula anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu. 
Mfano wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.

“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,” alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana mjini humo.