wawili hawa wamenusurika katika ajali ya mtumbwi iliyogharimu vifo vya watua zaidi ya 10 baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama ziwa Tanganyika
Akiongea
na mtandao huu katika wodu namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma
alipolazwa bibi harusi huyo alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi sana
baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.
”Sikumbuki
kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika
kujiokoa na kifo,kwakweli mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu
watu wanakufa ila namshukuru mungu kwa kutunusuru na kifo na yote mimi
nimemwachia mungu”alisema bibi harusi huyo
Muhanga
mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa
mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwa imejaza sana watu na mizigo ndiyo
maana ilizidiwa uzito na kuzama baada ya kupigwa na wimbi.
”Safari
ya kwenda kijijini kwetu lazima tupite njia za majini hakuna barabra
kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo mwambao mwa ziwa Tanganyika
kungekuwa na barabara tungepita barabrani”alisema Mhanga huyo
Naye
muuguzi wa wodi namba tano walipolazwa majeruhi hao alisema kuwa
wamejuhi wote waliopo wodini hali zao zinaendelea vizuri na mpaka sasa
wameshapokea jumla ya maiti sita.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed alisema kuwa mpaka sasa
jumla ya watu 27 wameshaokolewa,na miili sita kuopolewa pamoja na
walionusurika 11,lakini bado inahofiwa kuwa kuna miili mingine zaidi
ambao bado haijapatikana kwani mitumbwi hiyo inakadiriwa kuwa ilikuwa na
watu zaidi ya sabini.Waokoaji mbalimbali wakijindaa kwenda katika eneo ilipotokea ajali ya mitumbwi iliyobeba harusi kutoka kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalya kutafuta miili ya marehemu ambayo bado haijapatikana