Friday, October 17, 2014

MTANZANIA AWAUA WATOTO WAKE WAWILI KATIKA HALI YA KUSTAJABISHA HUKO AUSTRALIA

Raia wa Tanzania anayeishi katika jiji la Melbourne, Australia, Charles Amon Mihayo, 36, aliwanunulia binti zake Savannah, 4, na Indianna, 3, gauni za dance ya ballerina, akawaangalia wakidansi, kisha akawaua wote wawili kwa kuwakaba. 

Baada ya kuwaua mabinti hao, Mihayo aliwapigia simu polisi kuwataarifu, kisha aliiogesha miili ya marehemu, na wakati akiivalisha nguo miili hiyo, aliwaambia polisi waliofika na kugonga mlango, wasubiri kidogo.

Alipofungua mlango, polisi walimuuliza, kwanini amewaua watoto wake. Mihayo alijibu kuwa hakuna “good reason for what he did but it made sense to him at the time” [hakuwa na sababu ya maana ya kuwaua, lakini aliona ni kitu cha busara wakati anafanya mauaji hayo.]
savannah indianna Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Savannah,4, na Indianna, 3, enzi za uhai wao

Mtuhumiwa alisema kuwa hakupanga kuwaua binti zake, lakini hiyo haijalishi sasa maana maji yameshamwakiga; na kwamba hakutakiwa kufanya vitendo hivyo lakini ndio imeshatokea.


Dakika tisa baada ya Mihayo mwenyewe kuwapigia simu polisi na kuripoti kuwaua wanae, mama wa watoto hao aliwapigia simu ya dharura polisi kuwataarifu kuwa kuna kitu kimewatokea wanae waliokuwa wameenda kumtembelea baba yao.
Ripoti ya polisi inasema siku moja kabla ya tukio, Mihayo alimtumia text-message mama wa wanae, ambaye ndiye aliyekuwa akiishi na watoto hao, kumuomba awapeleke watoto wakamtembelee ili awaone mara ya mwisho.

Kabla ya kukutana, Mihayo aliwanunulia watoto hao gauni na viatu. Mama na watoto walipofika nyumbani kwa Mihayo, apartment ambayo amepangisha kutoka kwa bibi wa wanae, Mihayo alimuuliza mzazi mwenza ana muda kiasi gani na wanae, kisha akawaingiza ndani.
charles mihayo Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Charles Mihayo ndani ya gari la polisi, akificha sura yake kutoka kwa wapiga picha

Mama na bibi waliwasikia watoto wakicheza, kabla ya mmoja wa watoto hao kutoka barazani akiwa amevaa gauni ya maua na viatu vyeupe alivyonunuliwa na baba yao.

Mtoto huyo alianza kudansi kabla ya baba yake kumuita arudi ndani, ili ajitayarishe kumuonyesha mama kitu kingine dakika kumi baadae.
Baadae kidogo, mama na bibi waliona watoto wamekuwa kimya. Mama aligonga mlango, Mihayo akamwambia asubiri kidogo. Mama huyo akagonga tena. Mihayo akafoka “utajua watakapofika hapa!” Akimaanisha polisi. Mama alikimbilia kwenye sebule ya mama yake na kuwapigia simu polisi. Polisi, ambao tayari walishapigiwa simu na Mihayo mwenyewe, walipogonga mlango, Mihayo aliwajibu “I’m just finishing up.”
savannah indianna mom Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Marehemu Savannah na Indianna, wakiwa na mama yao

Alipofungua mlango, huku akifuta mikono yake na taulo, aliwaambia polisi: “tayari nimemaliza…Nimeshawaua” [It's done, I've killed them.]
Mihayo, ambaye alikiri kuwaua watoto hao kwa kuwakaba baadae aliwaambia polisi kuwa alikuwa amefurahia mama watoto kuwaleta wanae, ili aseme “goodbye” kwao kwa mara ya mwisho. Mihayo aliwaeleza kuwa aliwavalisha wanae gauni za ballerina na mabinti wakaanza kudansi. “Walienda nje kumuonyesha mama yao nguo zao mpya” alisema Mihayo. Alisema kuwa watoto waliporudi ndani, alirekodi video na simu yake watoto hao wakidansi nyimbo ya “Let it Go” kutoka kwenye movie “Frozen.”
Mihayo alisema baada ya nyimbo kwisha, watoto hao walianza kucheza mchezo wa “hide and seek”(unafanana na kombolela.) Hapo ndipo alipoweka mto nyusoni mwa watoto wote wawili, na kuwabana mpaka walipoacha kuhangaika na kupumua.
charles mihayo 0 Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Picha ya kuchorwa ya Charles Mihayo akiwa mahakamani. 

Camera haziruhusiwi mahakamani
Baada ya watoto hao kupoteza maisha, Mihayo aliwapigia simu polisi, na kuwapeleka watoto hao bafuni na kuanza kuwaogesha na kuwavalisha nguo.
Mihayo hakutoa sababu za mauaji hayo zaidi ya kusema wapelelezi hawawezi kuelewa “what he has been through” na kwamba kutoa sababu ya mauaji haitabadilisha chochote.

Mihayo anashikiliwa mahabusu, akisubili kutokea mahakama kuu kukabiliana na tuhuma siku za usoni.

TANZANIA YAKUBALI KUWA MSULUHISHI MGOGORO WA KISIASA SUDAN KUSINI


·        Ni kweli ngazi ya vyama tawala na mikutano ya upatanishi
kufanyika Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s Liberation  Movement (SPLM), mgogoro ambao umesababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa usuluhishi huo utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Kikwete amesema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo  imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Kikwete ametangaza jitihada hizo za upatanishi za Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Rais Kikwete amewaambia wananchi kuwa Tanzania imekubali kuwasaidia ndugu zao wa Sudan Kusini kwa nia ya kutimiza wajibu wake wa kimataifa na kwa kuongozwa na kaulimbiu ya Oktoba Mwaka 1959 ambayo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliitoa wakati nchi ya Tanganyika bado ikidai uhuru wake kutoka kwa Wakoloni wa Kiingereza.

Rais Kikwete ameikariri kaulimbiu hiyo maarufu: “Sisi Watu wa Tanganyika tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambako hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau.”

Rais Kikwete amesema kuwa Mwenge wa Uhuru unabeba falsafa kubwa ndani yake kuhusu “nchi yetu na uhusiano wake na watu wengine duniani hasa wanyonge, wenye dhiki na wasiokuwa na amani. Dhamira hii ya Mwalimu na nchi yetu ilitimizwa Desemba 9, 1961, siku Tanganyika ilipopata Uhuru ambako Bendera ya Taifa huru la Tanganyika na Mwenge wa Uhuru vilipandishwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro na Mwenge kuwashwa.”

“Toka wakati huo mpaka sasa, Mwenge wa Uhuru umeendelea kumulika nchi nzima ukipita katika mitaa, vijiji, shehia na majimbo, wilaya na mikoa ukieneza ujumbe wa udugu, umoja, upendo, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

 Kwa kuzingatia ujumbe uliobebwa na Mwenge wa Uhuru, nchi yetu na sisi Watanzania tumejitolea kwa hali na mali kusaidia ndugu zetu Barani Afrika waliokuwa wanatawaliwa kujikomboa kutoka kwenye makucha ya wakoloni na wabaguzi wa rangi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu.  Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”

Mwisho.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

AIBU KWAKO LUNDENGA, MCHEZO HUU SI HALALI


Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo. Utata huo uliibuka saa chache mara baada ya shindano hilo kufanyika Oktoba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji. 

Mshtuko! Siku chache baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu ameibua mshangao wa aina yake kutokana na utata wa umri wake, Ijumaa limesheheni data. 
Mara baada ya mrembo kutangazwa mshindi, habari za chini kwa chini zilidai kwamba Sitti alijinasibu kuwa ana umri wa miaka 18 na elimu ya (digrii mbili) (masters), mambo ambayo yaliwashtua wengi na kuanza kuhoji uhalali wa umri huo ukilinganisha na kiwango chake cha elimu.
“Mh! Haiwezekani, kama ana miaka kumi na nane atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili?” Alihoji mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akipozi. ELIMU YA BONGO IKOJE?
Kwa mfumo wa elimu nchini ulivyo, mtoto huanza darasa la kwanza akiwa na kati ya miaka mitano hadi saba, jambo ambalo haliingii akilini kwa Sitti kwani hesabu zinakataa hata kwa mtu asiyesomea mahesabu. 
Ukiachilia mbali shule ya awali (nursery) ambayo huchukua kati ya miaka miwili hadi mitatu, ukihesabu miaka saba ya elimu ya msingi (primary), miaka minne ya sekondari (ordinary level), miaka miwili ya kidato cha tano na sita (advanced level) na miaka mitatu ya shahada kwanza (bachelor degree), jumla ni miaka 16. 
Mlimbwende, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu. Pia kuna madai kwamba ametumia mwaka mmoja kusomea shahada ya pili (masters) huku kukiwa na muda ambao kwa kawaida huwa unapotea baada ya kumaliza kidato cha nne kwenda cha tano na baada ya kumaliza kidato cha sita kwenda chuo kikuu. 
INA MAANA ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MIAKA MIWILI?
Kwa mantiki hiyo, kama kweli Sitti ana umri wa miaka 18, basi atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo ni msamiati mpya kwa jamii ya Kibongo.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akifurahia jambo na marafiki zake wa mamtoni. BABA MZAZI ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata na tafrani inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hadi kufikia hatua ya watu kutukanana, gazeti hili lilimtafuta baba mzazi wa Sitti ambaye ni Mbunge wa Temeke, Dar kwa leseni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu alipopatikana alifunguka:
“Umri wake ni kama alivyosema mwenyewe siku ile (miaka 18), kama mnataka kujiridhisha nendeni hata huko Miss Tanzania mtaoneshwa passport (hati ya kusafiria) yake…,” alisema mzazi huyo huku akiomba aachwe kwanza ashughulikie wananchi wa jimboni kwake. 
Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akiwa na baba yake, Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu. TUMUAMINI MZAZI?
Hata kama tukiamini maelezo ya mzazi, maana yake ni kwamba mrembo huyo alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo linazidi kuongeza utata katika sakata hilo. 
AKATAA KUHITIMU MASTERS
Alipobanwa zaidi kuhusu taarifa zinazosema kuwa mwanaye amehitimu masters, mzazi huyo alikanusha na kudai kwamba mwanaye amehitimu bachelor degree(shahada).
“Kuhusu masters mnakosea, mwanangu hana masters, ana bachelor, nilimshauri achukue masters lakini akaomba nimuache ashiriki kwanza mashindano ya u-miss ndiyo aje aendelee baadaye,” alisema mheshimiwa huyo.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu wakati wa kutwaa taji
NI AIBU NYINGINE KWA LUNDENGA?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, suala la warembo kudanganya umri limekuwa ni sugu hivyo kuleta tafsiri ya aibu kwa muandaaji wa mshindano hayo, Hashim Lundenga akidaiwa kupigwa changa la macho pindi anapowapokea katika mchakato wa awali.
Pasipoti ya kusafiria ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu. “Hii ni aibu nyingine kwa Lundenga kwani haiwezekani mtu akaingia akasema ana miaka kumi na nane halafu awe na elimu kama hiyo, anashindwaje kulibaini hilo mapema?” Alihoji mdau mkubwa wa urembo nchini akikumbushia kisa cha Wema Isaac Sepetu, Miss Tanzania 2006/07 ambaye naye alidanganya umri akasema ana miaka 18 wakati alikuwa na kumi na saba.
Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu. MSIKIE LUNDENGA SASA
Alipotafutwa Lundenga ili kuzungumzia suala hilo, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“I can’t answer that question (Siwezi kujibu swali hilo)…siwezi.”
SITTI ANASTAHILI KUWA NA UMRI GANI?
Ukiachilia mbali muonekano, baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa ukifuata utaratibu wa mfumo wa elimu Bongo, Sitti alipaswa angalau awe na umri wa miaka 23, hata kama madai ya kurushwa madarasa ni sahihi.

KAMATI KUU YA CHADEMA YAKUTANA NA WANACHAMA WALIOWEKA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE UCHAGUZI MKUU 2015


 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiingia katika ukumbi wa mkutano wakati wa Kikao cha Kamatii Kuu ya Chama hicho kilipokutana na Wanachama waliotia nia ya kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiingia katika ukumbi wa mkutano wakati wa Kikao cha Kamatii Kuu ya Chama hicho kilipokutana na Wanachama waliotia nia ya kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Joseph Haule 'Prof. J' (wa kwanza kushoto)akiwa katika Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema pamoja na wajumbe wengine wakimkaribisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Viongozi Wakuu wa Chadema wakiomba dua kabla ya kuanza Kikao.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Salum Mwalimu.
Salum Mwalim akifafanua jambo wakati wa Kikao hicho.
 Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar,  Said Issa Mohamed akizungumza katika Kikao hicho.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika akizungumza katika kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Prof. Abdalah Safari.
Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza katika wakati wa Kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho ilipokutana na Wanachama waliotia nia ya kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Wabunge wa Chadema wakiwa katika kikao cha Kamati Kuu.
  
Baadhi ya viongozi wa Chadema.
Mustafa Muro akiwa katika Kikao hicho.
Wanachama wa Chadema.
Wanachama wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Chadema.

Wanachama wa chama hicho.
Mwanamuziki wa kizazi kimpya Prof. J akiwa ni miongoni mwa watia nia.
Msanii wa bendi ya M4C akitumbuiza.