Tuesday, October 7, 2014

RAIS KENYATTA AKABIDHI MADARAKA KWA ROTO TAYARI KWENDA ICC

Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje. Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.Mahakama hiyo inasama kuwa Kenyatta alihusia katika kupanga na kufadhili ghasia za kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia hizo.
Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama hiyo ya ICC
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo inapaswa kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Kenyatta ameombwa na mahakama hiyo kufika mbele yake ili kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda kwamba serikali ya Kenya imekataa kuwasilisha ushahidi unaohitajika katika kesi ya Kenyatta. 
Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini kauli kutoka kwa pande zote mbili.
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima kabla ya kuondoka nchini kuelekea Hague
Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha kesi dhidi ya Kenyatta baada ya upande wa mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Mashahidi wa upande wa mashitaka wamejiondoa katika kesi hiyo.
Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa kuambatana na Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono.CHANZO BBC SWAHILI

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi wa dini alipowasili katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam kufungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea machapisho toka kwa mwandaaji wa Mkutano wa viongozi wa dini chini ya taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na washiriki wa Mkutano wa  viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na wafanyakazi wa hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam wanaowahudumia washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence. PI

MWANAMKE ALIYEJIBADILI JINSIA YAKE NA KUWA KIUME HUKO KENYA ASHINDA KESI

Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke na kutaka jina lake kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi yake dhidi ya baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.

Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi la serikali.

Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.
'Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo,'' alisema jaji.
Jaji alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu kuwaheshimu wengine kama ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo mengi ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey kuhisi kuwa sawa anapaswa kukubalika kama alivyo na kumyima haki hiyo ya kubadilisha jina lake katika chati chake itakuwa ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwa mteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.

ROSE MUHANDO NDANI YA KASHFA NZITO

MSANII nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kuingia mitini na shilingi milioni moja alizolipwa kwa ajili ya kutumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya Injili ya John Lisu iitwayo Uko Hapa, Jumapili iliyopita.
Msanii nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando.Kwa mujibu wa chanzo makini, Rose alimegewa kiasi hicho cha pesa na Kampuni ya Msama Promotion iliyoandaa uzinduzi huo uliofanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Jumapili iliyopita.
“Rose jamani ana mambo! Mnajua kama amemliza Msama (mkurugenzi wa Msama Promotion) shilingi milioni moja? Alipewa ili atumbuize kwenye uzinduzi wa albamu ya John Lisu lakini akaingia mitini.“Mbaya zaidi kila alipopigiwa simu kuulizwa kwa nini hajafika Dar ile Jumamosi ili Jumapili awepo ukumbini akawa hapokei simu.
Kikaendeela: “Rose ananishangaza sana, sikuwahi kufikiria kama anaweza kufanya hivyo, kikubwa kinachowaumiza wengi ni kutopokea simu na ingekuwa vizuri kama angetoa taarifa mapema kwa kutohudhuria kwake na sisi tungejua cha kufanya mapema,” kilisema chanzo hicho ambacho kipo ndani ya waandaaji hao. 
Chanzo hicho hakikuishia hapo, kiliendelea kuanika kuwa shutuma za aina hiyo zimekuwa zikimuandama sana mwanamuziki huyo kiasi cha kushindwa kuaminika na kudai kuwa hana njaa ya kutokomea na pesa hiyo kwani ni kiasi kidogo sana kwake.
Msanii nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando akizungumza jambo.Risasi Mchanganyiko lilimsaka bosi wa Msama Promotion, Alex Msama ambaye alikiri Rose kutotokea kwenye uzinduzi huo licha ya kulipwa kiasi hicho cha pesa na kilichomuumiza zaidi ni kutopokea simu za wasaidizi wake waliotaka kujua nini kilimpata.
“Aliniangusha sana maana hata yeye nilimtangaza sana kwenye vyombo vya habari kwamba atakuwepo, lakini matokeo yake ikawa kimya, sijui nini kimempata lakini nitatoa tamko siku mbili hizi,” alisema Msama kwa masikitiko makubwa.
Alipopigiwa simu Rose Muhando alikacha kuongelea suala hili

WAJUKUU WAZAMA KABURINI KUZUIA MAZISHI YA BIBI YAO

WAJUKUU wa marehemu Sabina Ngalu (77) wameibua kutuko makaburini kufuatia kuzama ndani ya kaburi la marehemu huyo na kugoma kutoka wakidai kwamba mpaka walipwe shilingi laki moja (100,000), Uwazi lina mkanda mzima.
Wajukuu wa bibi huyo wakiwa kaburini. Tukio hilo la aina yake lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji cha Nyamwanza Kata ya Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili eneo la mazishi kwenye shamba lake ukitokea Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme la mjini Sengerema. 
Sababu za wajukuu hao kung’ang’ania ndani ya kaburi hilo walitaka wapewe ng’ombe mmoja au pesa hizo taslimu kwa mjibu wa mila na desturi za kabila la Kisukuma jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya wanandugu waliodai mila hizo zilipitwa na wakati. 
Kufuatia wajukuu hao kuendelea kugomea ndani ya kaburi, kaka wa marehemu, Enosi Ngalu alikwenda kukata fimbo na kuwashukia kisha kuwacharaza viboko wote huku nao wakisisitiza hawatoki mpamka ‘kieleweke’.
Padri na wananchi wakiwa makaburini. Baadhi ya wajukuu walioonja joto la jiwe ya kuchapwa viboko ni Andrea Mabula, Sabina Bukuru, Johari Bukuru, Asha Bukuru, Faida Bukuru, Yuves Petro, Semeni na kiongozi wao, Enos Ntilaga. 
Kitendo cha wajukuu hao kuendelea kugoma kutoka kaburini kilimchefua Padri Nicodemus Mayalla ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Yesu Kristo Mfalme, Sengerema ambaye aliamua kuondoka eneo la maziko huku akiwataarifu polisi kuhusiana na vurugu hizo. 
Kufuatia hali hiyo, mmoja wa waombolezaji alizama mfukoni na kutoa kiasi hicho cha pesa na kuwapa ndipo walipokubali kutoka dani ya kaburi hilo ili mazishi yaendelee. 
Ili kuonesha alikerwa na kitendo hicho, Padri Mayalla ambaye kwa wakati huo alikuwa amewekwa chini na baadhi ya ndugu wakimsihi kutosusia mazishi hayo, aligoma kurejea kaburini kuongoza ibada ya mazishi.
Jeneza lenye mwili wa bibi huyo likishushwa kaburini. Baada ya vuta nikuvute, hatimaye Padri Mayalla alikubali kuendelea na ibada lakini aliwataka wajukuu hao kurudisha pesa waliyochukua na kuwaomba radhi wana mtaa huo na ndipo yeye aweze kurudi kaburini. 
Wajukuu hao waliitwa mbele ya padri huyo na mbele ya wana mtaa, wakaomba samahani ikiwa ni pamoja na kurudisha kitita hicho cha pesa paroko huyo naye akarejea kaburini na kuongoza ibada ya mazishi. 
Hata hivyo, wakati ibada ikiendelea polisi zaidi ya wanne kutoka Kituo cha Polisi Sengerema wakiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) na mabomu ya machozi walifika eneo la tukio ili kuhakikisha amani na utulivu vinatawala. 
Polisi akiwa eneo la tukio. Cha kushangaza, saa baada ya kutoka makaburini, wajukuu hao waliwahi nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Mlimani, Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema na kuanzisha timbwili jingine kwa kuficha chakula na vyombo vya kupakulia wakidai warudishiwe pesa yao waliyoirejesha makaburini kwa shinikizo la baba paroko. 
Baada ya timbwili hilo kukolea, mmoja wa wafiwa alizama mfukoni na kutoa shilingi laki moja na kuwakabidhi wajukuu hao ambao walirudisha chakula jikoni na taratibu za waombolezaji kupata chakula ziliendelea.

MWIZI AUAWA MBEYA BAADA YA KUVUNJA DUKA NA KISHA KUIBA

Mtu mmoja mkazi wa Itewe wilaya ya Mbeya Vijijini aliyefahamika kwa jina la Jacob Kimaila (31) ameuawa baada ya kupigwa na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi kutokana na tuhuma za kuvunja duka, salon na kuiba.
Mtuhumiwa alifariki mnamo tarehe 05.10.2014 majira ya saa 09:30 asubuhi huko katika kituo cha afya Inyala, kata ya Inyala, tarafa ya Tembela, wilaya ya Mbeya vijijini, mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa, chanzo cha kifo chake ni  kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na kupigwa na wananchi siku ya tarehe 04.10.2014 majira ya asubuhi.
Jitihada za kuwatafuta waliohusika katika tukio hili zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika kituo cha afya Inyala alipokuwa anapatiwa matibabu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wawafikishe katika mamlaka husika watuhumiwa wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali kwa hatua zaidi za kisheria.

MOYO WA BINADAMU NA UTUMBO WAPATIKANA KATIKA OFISI YA MKUU WA SHULE IPELO. RUNGWE

Wananchi  wa kijiji cha  Ipelo    kata ya  kandete  wilayani rungwe  mkoani mbeya wamelazika kujichangisha  fedha kwa  lengo la kumtafuta mganga wa  kienyeji  baada  ya watoto wao kufariki   dunia kila   mda wa miezi {3}  katika  mazingra  ya  kutatanisha.

    Wakizungumza  na kipindi hiki wakati wa   maandamano ya  utoaji  wa  madawa  katika shule  ya  masingi   Ipelo  wananchi   hao wamesema hatua  hiyo imekuja kufuatia  vifo  vya ajabu kujitokeza  kijiji hapo  kwa watoto  wao ambao wamekuwa wakifariki kila  baada ya  miezi mtatu   na  wote  kutokomea mahali pasipo fahamika.baada ya mganga huyo kutoa vitu vya ajabu katika shule hiyo ambapo alitoa  utumbo wa binadamu ndani ya  Rambo pamoja na  moyo wa ngombe ndani ya kichupa ukiwa unahema.        Majabu.
 Hata  hivyo  imeelezwa  kuwa  mpaka sasa  watoto  wanne  walifariki  dunia  katika  mazingira  ya  kutatanisha  na kwamba  hali  hiyo  huwa  inajitokeza kwa wanafunzi  wa  darasa  la nne ambao  mpaka sasa  wamegoma kwenda  shule wakiogopa   vifo hivyo.
Aidha wakazi wa kijiji hicho wameomba msaada kwa serikali  na  watumishi wa mungu  kwa  ujumla kuwasaidia janga hilo ambalo  limeonekana kuwa  kelo  kwa     kwao.
  Sambamba na hayo  ikumbukukwe  kuwa   vitu  hivyo  viliweza  kutolewa  na mganga  huyo   vikiwa   vimefukiwa na   mtu au watu katika  ofisi ya  mkuu  wa shule  na  vikisadikiwa kuwa ndiyo chanzo  cha matatizo   hayo.
 Kwa  upande wa  viongozi wa  mitaa  hiyo  wamesema  hawawezi kuzungumza chochote  juu ya suala hilo  kutokana  na kwamba  serikali haiamiini  masuala ya  kishirikina  na kwamba mganga huyo ameitwa  na wananchi  husika  bila  wao kushirikishwa chochote.

UGONJWA MWINGINE WAIBUKA NCHI JIRANI YA UGANDA

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tahadhari ya kusafiri nchini Uganda baada ya kuthibitishwa kuwa daktari mmoja amefariki kutokana na ugonjwa hatari wa Marburg unaosambazwa na popo.Kwa sasa Shirika hilo kwa ushirikiano na mamlaka za afya za Uganda wamemzuilia ndugu mmoja wa marehemu kwa hofu kuwa huenda naye aliambukizwa. Watu wengine zaidi ya 80, wakiwemo matabibu 38 waliokutana na mwenzao huyo siku kumi kabla ya kifo chake nao pia wanachunguzwa.

Kwa mujibu wa WHO na mamlaka za afya za Uganda, matokeo ya uchunguzi katika maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Virusi kufuatia kifo cha tabibu huyo tarehe 28 Septemba yanathibitisha kwamba alifariki kutokana na homa hiyo hatari ya Marburg. Waziri wa Afya wa Uganda, Erioda Tumwesigye, alisema kuwa wizara yake inathibitisha daktari huyo aliyekuwa mtaalamu wa vipimo vya mionzi, alikufa kwa Marburg.
Marehemu alikuwa tabibu katika Hospitali Kuu ya Wilaya ya Mpigi na alianza kuugua tarehe 17 Septemba akihudumu katika hospitali ya Mengo jijini Kampala, ambako alikuwa ameajiriwa mwezi mmoja uliopita. Inahofiwa kwamba katika kipindi cha wiki mbili kabla ya kifo chake alikutana na watu wengi wakiwemo matabibu wenzake pamoja na kwamba ni jamaa zake waliomzika.
Kutokana na hilo, mwakilishi wa WHO nchini Uganda, Dokta Wondimagegnehu Alemu, alitahadharisha watu watu wanaoingia nchini Uganda, hasa katika wilaya ya Mpigi iliyo jirani na jiji la Kampala na pia Kasese alikozikwa marehemu. "Tunatoa tahadhari ya usafiri nchini Uganda baada ya kutambua kwamba mtu mmoja amefariki kutokana Marburg," alisema mwakilishi huyo ya WHO. 
Watu 80 wawekwa kwenye karantini.
Wizara ya afya ya Uganda pamoja na mashirika na taasisi nyengine husika zimechukua hatua za dharura mkiwemo kuwabaini na kuwatenga zaidi ya watu wapatao 80 waliokutana na mtu huyo aliyefariki kutokana na ugonjwa huo hatari wa Marburg.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, watu hao watachunguzwa katika kipindi cha siku 21, ambazo ndiyo muda wa ishara za ugonjwa huo kujitokeza na kubainika na "yule atakayeonesha dalili hizo atasafirishwa moja kwa moja hadi kituo cha kitaifa cha kushughulikia magonjwa hatari," alisema Daktari Jane Aceng, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Afya nchini Uganda, akiongeza kwamba wanafanya kila jitihada kuona kwamba wanamfuatilia kila mtu na "kuudhibiti ugonjwa huo mara moja kabla haujasambaa".
Popo husababisha Marburg 
Ugonjwa wa Marburg ni homa hatari inayonasibishwa na ugonjwa wa Ebola kwani virusi vya magonjwa hayo ni ya jamii moja ijulikanayo kama filoviridae.
Mnyama aina ya popo, ambao ni jamii ya mamalia wanaoruka na wanaoishi kwa kula matunda, ndiyo wanaosemekana kusambaza kirusi cha Marburg na maambukizi baina ya binadamu hutokana na kugusana kwa vidonda au majimaji yoyote kutoka kwa mgonjwa kama vile damu, mate, matapishi, kinyesi au mkojo wa aliyeambukizwa.
Jamii nyingi za watu wa Uganda, Kongo na eneo la kati ya Afrika, hula nyama ya popo kama kitoweo au hasusa ya kusindikizia ulevi.
Miongini mwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na mtu kuwa na homa ya ghafla ya kiwango cha juu cha joto, maumivu ya kichwa, kutapika damu, maumivu ya viungo na misuli pamoja na kuvuja damu kutoka sehemu kadhaa kama vile machoni, puani, meno, masikioni, njia ya haja kubwa na hata kwenye ngozi. Aidha mtu aliyekumbwa na ugonjwa huo huharisha sana.
Kwa bahati mbaya, kama ilivyo kwa Ebola, ugonjwa huo nao haujapatiwa dawa maalum ya kuutibu wala chanjo dhidi yake. Wagonjwa hupewa tu dawa za kutuliza ishara husika.
Wataalamu wanaelezea kuwa viwango vya uwezekano wa mtu kufariki kutokana na ugonjwa huo ni kati ya asilimia 24 hadi 88, huku wakisisitiza njia za kujilinda na mgonjwa aliyekwishaathirika kuepuka kukutana kwa majimaji ya miili, damu, kinyesi au mate.