Friday, September 26, 2014

VIPEPERUSHI VYASAMBAZWA DODOMA KUWATISHIA WABUNGE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawasaka watu wanaosambaza vipeperushi vya vitisho dhidi ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba, watakaoingia bungeni leo ambapo pia watu hao walichora ukuta wa Jengo la Makao Makuu Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Vipeperushi hivyo ambavyo vimesambazwa katika maeneo mengi ya mji, ikiwemo CCM Makao Makuu, maeneo ya Bunge na Uwanja wa Jamhuri, vilikuwa vikisomeka , ‘Onyo – Dodoma si mahali pa kufuja wezi wa fedha za umma, utakayeingia bungeni kuanzia kesho (leo), yatakayokupata utajuta.”

Pia, katika Jengo la CCM makao makuu na kwenye ukuta wa Uwanja wa Jamhuri, kuliandikwa maneno kwa rangi nyekundu yaliyokuwa yakisomeka `No Katiba Ufisadi’.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema jana alfajiri viliokotwa vipeperushi maeneo mbalimbali mjini Dodoma vyenye ujumbe wa kutishia kuvunjika kwa amani.

Alisema wanaendelea kupokea taarifa za watu wanaodaiwa kuandaa vipeperushi hivyo na wanafanyia kazi ili waweze kuwakamata na kushtakiwa, kulingana na kosa walilolitenda hasa la kutoa vitisho na kuhamasisha uvunjifu wa amani.

“Kila mmoja ajiepushe kujiingiza kwenye kuhamasisha uvunjifu wa amani, kujiingiza katika mikusanyiko isiyo halali na maandamano ambayo yameshapigwa marufuku na Jeshi la Polisi.

Atakayekiuka na kujiingiza katika vitendo hivyo vya kiuhalifu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za Nchi na kwa mamlaka iliyopewa Jeshi la Polisi,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Dunga Omary alisema ni jambo la ajabu kuona kuwa jengo la CCM linaandikwa maneno kama yale wakati Katiba ni ya Watanzania wote.

“Kwa nini CCM wamelengwa kwani Katiba ni ya watanzania hatupaswi kulaumiwa kwa sababu ya Katiba,” alisema na kuongeza kuwa, ushahidi wa mazingira ya kawaida utaona kuwa wale walioshindwa kuandamana wameamua kufanya hivyo na huko ni kufilisika kisiasa.

Kuvamia Polisi Mkoani Mwanza, uongozi wa chama hicho umesema utahakikisha watu wao waliokamatwa na jeshi la polisi, wanatolewa bila masharti, la sivyo watahamasisha wananchi kuvamia kituoni.

Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Chadema mkoani humo, John Nzwalile wakati akizungumzia kujipanga kwao kufanya maandamano nchi nzima.

Alisema maandamano na migomo isiyo na ukomo itaendelea kufanyika ili waweze kufikisha ujumbe wao na kuongeza kuwa, watatumia akili na kudai kuwa maandamano yao yamefanikiwa kwani polisi wameandamana zaidi yao.

Tangu jana asubuhi askari polisi wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali na jiji la Mwanza ili kukabiliana na wafuasi wa chama hicho ambao wangeandama katika maeneo mbalimbali na kuishia kwa mkuu wa mkoa.

Hata hivyo, hakukuwa na maandamano huku kwenye lango kuu la kuingia katika ofisi ya mkuu wa mkoa ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana aliliambia gazeti hili kuwa hadi jana majira ya saa 5.30, hakukuwa na kiongozi yeyote wa Chadema aliyekuwa anashikiliwa na jeshi hilo.

AFANDE AFUMWA NA KIMWANA

Mwenyewe Adai ni Maswala Yake Binafsi Asiulizwe

 
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, juzikati alinaswa akiwa na demu mpya akiwa ni siku moja tu baada ya kufanyika kwa 40 ya aliyekuwa mzazi mwenzake, marehemu mama Tunda.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Septemba 21 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati staa huyo aliyekuwa mmoja wa watoa burudani katika tamasha la Fiesta, alipoonekana akiingia akiwa ameambatana na mrembo mmoja akiwa ameshikana naye kimahaba.


Akiwa ndani ya uwanja huo, mkali huyo wa mashairi yenye vina kwa muda mwingi alikuwa pamoja na msichana huyo ambaye hakufahamika jina, wakiwa na dalili zote za wapendanao.


Alipoulizwa juu ya suala hilo, Afande Sele alicheka na kumtaka paparazzi wetu kuachana na masuala hayo aliyoyaita binafsi, badala yake asubiri apande jukwaani apate picha za kazi atakayofanya.

HUKUMU YA KESI YA KUBENEA HII HAPA


 Mahakama Kuu ya Tanzania iliyokaa chini ya Majaji Augustine Mwarija, Aloysius Mujulizi na Dr Fauz Twaib imetoa uamuzi wake leo kufuatia maombi ya Saed Kubenea kama ifuatavyo;

1.Kuna mgongano mkubwa kati ya toleo la Kiswahili na Toleo la Kiingereza la kifungu cha 25 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

2. Kwamba pamoja na mgongano huo, Sheria imekusudia kwamba Madaraka ya Bunge Maalum la Katiba yatatekelezwa kupitia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya katiba kama ilivyowasilishwa kwake.

3. Kwamba mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba yana mipaka, na kwamba madaraka yake yanaongozwa na kutekelezwa kupitia Rasimu. Bunge Maalumu la Katiba linaweza kubadili na kuboresha mapendekezo yaliyomo katika Rasimu mradi tu maboresho yasiende kinyume na misingi iliyowekwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya katiba, kama ilivyokuwa pia kwa Tume.

4.Mahakama Kuu haina Mamlaka ya kuamua ni kiwango gani Bunge maalumu la Katiba linaweza kuboresha Rasimu kwani hilo ni suala la kisiasa, ingawa Bunge Maalumu la Katiba linafungwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya katiba.

MAVAZI ALIYOVAA MREMBO HUYU YASABABISHA STEVE NYERERE KUZOMEWA


NYOTA wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki wa Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa ‘kihasarahasara’.Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’akiwa na mrembo huyo.Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20, 2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya Yanga na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji walishinda 2-0. Steve alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani (zinazotumiwa na Yanga).
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo walipozomewa na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa kuwa, demu huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara hadharani.
Mrembo huyo akikatiza mbembezoni mwa uwanja.Baadaye mwandishi wetu alimfuta Steve na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Wale kunizomea ni haki yao ila mimi na mwenzangu tumeona kama wametushangilia.” 
Alipoulizwa uhusiano wake na demu huyo,Steve aligoma kujibu badala yake alikimbilia kwa mwandishi mwingine na kuomba msaada. Mrembo huyo alipotakiwa kuzungumzia tukio hilola kuzomewa na sababu za yeye kuvaa vile, alijibu kwa mkato: “Kuzomea ni haki yao, mimi nawaona kama washamba tu.

HOTEL YA BLUE PEARL DAR YAFUNGWA KWA AIBU

Services at the Blue Pearl hotel in Dar es Salaam’s Ubungo suburb have been affected after the owner of the business allegedly failed to pay rent amounting to about Sh6 billion ($3,800,000).

Yesterday afternoon officials from Majembe Auction Mart arrived at the hotel and started taking out furniture and packing them into a lorry.

Customers were told to vacate the hotel premises because it had been closed down and services were no longer being provided.

The executive director of Majembe Auction Mart, Mr Seth Motto, said his organisation was called into action after the management of Ubungo Plaza Ltd, which is the owner of the building, assigned them to carry out the operation.

BARAZA LA WANAWAKE CHADEMA KUANDAMANA KWA AMANI WIKI IJAYO


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Taifa Chadema, (BAWACHA), Halima Mdee akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  leo juu azma ya baraza hilo la wanawake kufanya maandamano makubwa ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete asipokea rasimu  iliyotengenezwa na bunge maalum la katiba. mwenyekiti huyo alimesema maandamano hayo yamepangwa kufanyika katika wiki ijao hajataja siku gani lengo kubwa la maandamano ni kufikishwa ujumbe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete kuwa rasimu hiyo si ya wananchi huku akisema yatakuwa ya amani tuu

Baadhi ya wakazi wa mji wa dodoma leo wakipita mbele ya uzio wa Ofisi kuu ya CCM Mkoa huku  wakisoma ujumbe ulioandikwa kwenye uzio wa CCM  wenye maandishi yanayosomeka  Ufisadi no Katiba ,ujumbe huo haukujulikana umeandikwa na Watu gani  katika maeneo mbalimbali mjini hapa Dodoma

MCHUNGAJI ALIYEWAHI KUWALISHA NYASI WAUMINI SASA AWANYWESHA PETROLI! 0 <a href='http://imgads.night-hawk.net



Mchungaji wa Afrika Kusini aliyewahi kuwalisha waumini wake majani, sasa anawanywesha petrol.Pastor Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries aliwahi kuandikwa sana na vyombo vya habari duniani kwa kuwaagiza wafuasi wake kula majani kama wanyama kwa madai kuwa binadamu wanaweza kula chochote kilichotoka kwa Mungu.BOFYA KUANGALIA VIDEO>>

NAKALA YA RASIMU MAREKEBISHO LUKUKI


Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba jana ilikabidhi bungeni Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ikiwa na ibara 289 kulinganisha na 271 za Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba.

Rasimu hiyo pia ina sura mpya mbili ambazo ni Mamlaka na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na nyingine inayohusu Ardhi, Maliasili na Mazingira.


Akiwasilisha rasimu hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Andrew Chenge aliliambia Bunge kuwa Ibara 233 za rasimu hiyo zinatokana na Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Chenge, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), alisema ibara 47 za Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimebaki kama zilivyokuwa, 186 zimefanyiwa marekebisho, 28 zimefutwa na 41 ni mpya.


Rasimu hiyo ya Katiba inayopendekezwa imefuta kabisa muundo wa Muungano wa shirikisho ambao ungezaa muundo wa serikali tatu na badala yake imerudisha muundo wa sasa wa serikali mbili.


Chenge alisema kamati za Bunge hilo pamoja na wajumbe walio wengi, waliona kuingiza muundo wa shirikisho ilikuwa ni kukiuka makubaliano ya Muungano yaliyofikiwa mwaka 1964.


Kwa kurejesha muundo wa serikali mbili uliokuwa ukipigiwa chapuo na CCM, Rasimu hiyo imependekeza kuwapo kwa makamu watatu wa rais.


Chenge alisema uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea mwenza atakayekuwa makamu wa kwanza wa rais.


Chini ya muundo huo, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), atakuwa makamu wa pili wa rais ilhali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa makamu wa tatu wa rais.


Chenge alisema mapendekezo hayo yamezingatia ukweli kuwa kuwapo kwa mgombea mwenza anayekuwa makamu wa kwanza wa rais, kutafanya rais na makamu wake kutoka chama kimoja.


Rasimu hiyo inayopendekezwa, imepunguza Tunu za Taifa kutoka saba zilizokuwamo kwenye Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba hadi nne huku mambo ya muungano yakiongezwa kutoka saba hadi 14.

MARK OBAMA NI KAKA YA BARACK KABISA


Raisi wa Marekani Barack Obamma ana kaka yake aitwaye Mark Obama Ndesandjo ambaye ameshare baba mmoja na Rais ya wa marekani,Baba yao alifunga ndoa na mama yake Ndesanjo lakini baadae waliachana na kufunga ndoa na mama yake Barack Obama aliyejulikana kwa jina Ann Dunham hizi ni baadhi ya picha zao zitazame hapa..