Tuesday, August 19, 2014

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA JAJI LEWIS MAKAME



 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, National Electoral Commission (NEC) kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame kilichotokea katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.


“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chini ya Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, Mheshimiwa Lewis Makame ambaye amelitumikia Taifa letu katika Utumishi wa Umma kwa uaminifu, uadilifu, bidii na umahiri mkubwa”, amesema kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake.

Katika utumishi wake, Marehemu Jaji Lewis Makame, enzi za uhai wake, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na baadaye Mwenyekiti wa NEC ambayo aliiongoza kwa miaka 17 mfululizo hadi alipostaafu mwaka 2011. Uongozi wake ulichangia sana kuimarisha amani, utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa katika mazingira mapya ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa hapa nchini.

“Ni kwa kutambua kipaji kikubwa cha uongozi alichokuwa nacho Marehemu Jaji Lewis Makame, Taifa letu limepoteza mtu muhimu sana kwani hata baada ya kustaafu kwake alikuwa bado anahitajika sana kutokana na mchango wake wa ushauri katika mambo mengi yanayohusu maendeleo ya nchi yetu”, amesema Rais Kikwete na kuongeza,

“Kutokana na msiba huu mkubwa, nakutumia Salamu za Rambirambi kwa kumpoteza aliyekuwa Kiongozi Mahiri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu kwa kumpoteza Kiongozi na Mhimili Madhubuti. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Jaji Lewis Makame, Amina”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huu.

Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awape moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira Wanafamilia wote, ndugu na jamaa wa Marehemu, ili waweze kuhimili machungu ya kuondokewa na Mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Agosti, 2014

JWTZ YASHEREHEKEA MIAKA 50 KWA KUIJALI JAMIIZAIDI

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdqca7TALcQiK_knq0Xn-NPUMMoeAXXKlQ835GXnumtl2Uvv75eaCn7PxY1GgboiJs7bXlqmLgKIKs3ByKBsuz2zGoXBRkIwVmq7Qr0A-_tBsaY1sP6Mebmaq_LZrS2P5YSI5hU-woaiQy/s1600/pix+2.JPG

 Meshack Ndosikoi Mkurugenzi wa jinsia kutoka wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto ambaye ni mgeni rasmi akifanya ufunguzi wa hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya jesi la wananchi wa Tanzania leo jijini Dar es salaam na kuzindua wiki ya kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na wale wanaishi katiaka mazingira magumu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEincC4xGKMKyebmGdo9GTfwCCdeDNpbkBsEsR2Olx22qvU7C8khxp0UlIt0iO7VA1AY8JF-ajbvy6SP0kUvM7ueM97ndG7_PHl9y8ac4KRlpoa7b8o-NEvAw82dbgkeN75Mxs7Co1TVqx6C/s1600/pix+8.JPG Mkurugenzi Meshack Ndesikio akiw katika picha ya pamoja na maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania katiaka hafla ya kuazimisaha miaka 50 ya jeshi hilo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuHXe4Pt6TUVQ_waGk7jOH-TIYOgABixzVqohmgd73a944IVuwvgb0vQcOQ9S7B9byBAa1LVES-uNXE8a__b3q_Pqv5C1vAfxtyFh0lM4Cz0CadLDejQ1kifaHy09eAtS_Ab56MzLO5yYk/s1600/pix+1.JPG
Mkurugenzi wa ustawi wa jamii wa jeshi la wananchi wa Tanzania Brigedia Jenelari Sarah Wambali akisoma risala kwa mgeni rasmi katiya kusherehekea miaka 50 ya jeshi hilo









https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjAlRGI4mZZYnOXJYsy1HTxve4_wqX__J6_aPYNhSMUeUIBFI8hlfAwe8rc4FZaRz1ScGTv1DbaSsMyVFxUKeO7bCTNoteb81JHxayBtmR5106v1NY1DSSmOmr-X1sHWf5ycZtcO5DFsWt7/s1600/pix+3.JPGMkurugenzi akitoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa watoto wa kitua cha nyumba ya furaha na amani kilichopo Mburahati jijini Dar ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa wiki ya kuhudumia jamii zinazitolewa na jeshi hilo katika kusherehekea miaka 50 ya jeshi la wananchi wa Tanzania

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDN1jP_7Y8svCfrwV44z3hb_0tmQZuPI3JK4j_DKQbZQx9oImSyeUOVR7ynRDd1xAek_ekYKQHAGJwkKtw4o_-WMabXo6RO9NOPwHCKvNAz0V3GlgfJ5ph9POPXzVKdGF7fedIXONhEIas/s1600/pix+4.JPGbBrigedia generali Sarah Wambali akipeana mkono na watoto wa kituo cha watoto yatima cha nyumba ya furaha na amani cha mburahati baada ya kukabidhi msaada wao kituoni hapo

BAADA YA STORY ZA ORIJINO KOMEDI KUVUNJIKA JANA HABARI HII ILIANDIKWA NA MASANJO KUWA WAPO MBIONI KUANZA KAZI

  1.  
     BAADA YA LIKIZO WANAJESHI WANAJIPANGA KUANZA NEW SEASON AT TBC MIKOCHENI!!!
     

PADRI MTANZANIA ARUHUSIWA NA PAPA KUOA


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Moshi. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.


Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo.


Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.


Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.


Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.


Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.


Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”


Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.


“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu.MWANANCHI

MAULID WA KITENGE SASA KUSIKIKIA E-FM



Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akisaini Mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela.
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya Radio hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaama

Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.

Maulidi Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji walio bobea katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.
 

 

Katika kuthibitisha yeye mwenyewe, Maulid Kitenge kupitia akaunti yake ya Twitter hapo jana alitangaza kuondoka rasmi katika radio hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 14. Kupitia Twitter, Kitenge ameandika hivi
 
 

BOMBA LA MAFUTA LA TAZAMA LAPASUKA HUKO GONGO LA MBOTO LEO


Na Father Kidevu Blog.
Bomba la mafuta linalotumika kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar es Salaam Tanzania hadi Nchini Zambia lijulikanalo kama TAZAMA limetobolewa na mafundi waKampuni ya Raddy Fiber Solution Ltd ya jijini Dar es Salaam wakati wakichimba chini ya barabara kupitisha awamu ya pili ya kebo za mkongo wa taifa wa mawasiliano katika eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa kampuni ya Raddy, Rajab Mikumwo amesema mafundi wake walitoboa bomba hilo kwa bahati mbaya majira ya saa nane alasiri leo wakati wakifanya kazi ya kuchimba njia ya kupitisha bomba.
 Sehemu inayoonesha mafuta ya kimiminika baada ya bomba hilo kutobolewa chini. 
 Wakazi wa Gongo la mboto wake kwa waume wakiwa katika pilika za kuchota mafuta hayo machafu ya Diseli.
Mkazi wa Goms akiondoka na dumu lake la mafuta. 
Mafuta hayo yakitiririka katika mtaroni mithili ya maji.Picha Kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

AMKATA KICHWA MDOGO WAKE APATE UTAJIRI!


Marehemu Mathias aliyeuawa kwa kukatwa kichwa na kaka yake wa kuzaliwa,Johnson Damian Mkude.

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamng’ang’ania mfanyabiashara maarufu wa Wilaya ya Mvomero, Johnson Damian Mkude (39) akituhumiwa kumkata kichwa mdogo wake wa kuzaliwa, Mathias kisha kuondoka nacho kwenda kwa mganga kwa kile kilichodaiwa ni kufanyiwa dawa ili awe bilionea, mkasa wote huu hapa. Tukio hilo ambalo kwa sasa ndiyo gumzo mkoani hapa lilijiri usiku wa Agosti 3, mwaka huu katika mashamba ya Kata ya Mlali ambapo ndugu wa marehemu waliokuwa wakimsaka ndugu yao walifanikiwa kuona kiwiliwili Agosti 6, mwaka huu. 


MWILI WAZIKWA KATIKA SHAMBA LA MTU
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kushuhudia kiwiliwili kikiwa kimeharibika vibaya. Ilibidi baba wa marehemu, mzee Damian Mathias Mkude (63) amwombe mmiliki wa shamba hilo lililopo kwenye Kijiji cha Mbalala, Kata ya Mlali kumzika mwanaye hapo ambapo alikubali. 

BABA WA MAREHEMU

Akizungumzia tukio hilo kwa uchungu, baba wa marehemu mzee Mkude alisema:”Mwezi mmoja kabla ya tukio, Johnson alinichonganisha na Mathias, nakiri hadi marehemu anakufa nilikuwa sina uhusiano naye mzuri kutokana na maneno aliyoniambia kaka yake

Ofisa wa polisi akifafanua jambo kwa wananchi eneo la tukio.
 “Lakini nilipomuuliza kuhusu hayo maneno, Mathias alikanusha, nikaamua kuyafanyia uchunguzi. Wakati naendelea na uchunguzi Agosti 3, mwaka huu, majira ya jioni, giza halijaingia niliwaona wanangu (Jonson na Mathias) wamepakizana kwenye bodaboda. 

“Siku hiyohiyo, saa 5 usiku, mke wa Mathias, Revina Evarist akaja kwangu na kunijulisha kwamba mumewe hajarudi nyumbani na si kawaida yake kufika muda huo. Tulipompigia simu hakuwa hewani. Kwa vile nilimuona akiwa na kaka yake, nikampigia yeye lakini simu yake ilizimwa. 

“Ilipofika saa 7 usiku tukaamua kwenda kwa kaka yake, tukamkuta. Nilipomuuliza mdogo wako yuko wapi akasema hajui. Akajiunga na sisi, tukaendelea kumtafuta mdogo wake kwa zaidi ya siku 2 bila mafanikio,” alisema mzee huyo.
Mke wa marehemu, Mathias, Revina Evarist akihuzunika kwa kumpoteza mumewe.

 MAITI ILIVYOONEKANA
Mzee huyo akasema Agosti 6, mwaka huu alipata taarifa kwamba  kuna maiti imeonekana kwenye mashamba ya Mlali.

 “Nilishtuka sana kusikia hivyo, nikamtuma mkwe wangu, mume wa mtoto wangu mkubwa na mtoto wa dada yangu, Gasper Msimbe. Walisafari hadi Kata ya Mlali kushuhudia maiti hiyo. 

“Walipofika waliikuta maiti haina kichwa lakini walimtambua kuwa ni Mathias kwa nguo na viatu. Walinijulisha haraka ambapo nilikwenda eneo la tukio. Nilipofika niliumia sana  kushuhudia mwanangu asiyekuwa na hatia kauawa kikatili huku mwili wake uliokuwa hauna kichwa ukitoa harufu kali kwa kuharibika.”
Revina Evarist akilia kwa uchungu.

 BAADA YA MAZISHI
“Sasa kilichonishangaza ni kwamba, baada ya mazishi kule shambani, zimesikika tetesi kuwa, Johnson ndiye aliyemchinja mdogo wake na kutoweka na kichwa kwa imani za kishirikina ili awe tajiri mkubwa. 


“Nikaambiwa anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi Mzumbe (kabla ya kupelekwa mkoa). Nilikwenda, nikamkuta amewekwa chini ya ulinzi huku akiwa na hirizi alizokamatwa nazo akiwa kwa mganga wa kienyeji eneo la Sangasanga, Mvomero.” 


BABA AOMBA KICHWA CHA MWANAYE
“Pale kituoni, polisi walinitaka nimsalimie lakini nikakataa mpaka arudishe kichwa cha mdogo wake. Tena naliomba jeshi la polisi kumbana Johnson ili kama kweli amechukua kichwa cha mdogo wake akirudishe nikizike hapa nyumbani Kijiji cha Nyandila,” alisema mzee huyo.

Diwani wa Kata  ya Nyandila (Chadema), Peter Joseph Zengwe.

 MKE WA MTUHUMIWA AZUNGUMZIA KUFUNGA NDOA
Uwazi lilifika nyumbani kwa Johnson ambapo mke wa mtuhumiwa, Mchilo Peter (33) alikiri mumewe kuswekwa mahabusu akituhumiwa kumkata kichwa mdogo wake.

 Alipotakiwa kueleza chochote kuhusu tukio hilo, mwanamke huyo alisema kwa mafumbo:

“Huko ni kukosa elimu, kwa nini mganga akudanganye. Kama ni gari mbona yeye hana, mume nimeanza kuishi naye tangu mwaka 2000,  namwambia tufunge ndoa hataki, Jumapili kusali hataki, yuko bize kusaka pesa.


“Siku ya tukio kachukua pesa zote ndani zaidi ya shilingi laki 7. Leo baada ya njaa kuwa kali nimeamua kufungua duka licha ya kupokea vitisho kwamba kuna kundi la watu linataka kuvamia duka kwa lengo la kuchoma moto kama hawatapewa kichwa cha Mathias,” alisema mama huyo.
Alipoulizwa kuhusu mali wanazomiliki, alisema wana nyumba, duka na nguruwe wawili. 



MTUHUMIWA ALIJULIKANAJE?
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata  ya Nyandila (Chadema), Peter Joseph Zengwe, Agosti 15, mwaka huu baada ya mauaji hayo kutokea, vijana wawili, Amos na Mohamed Chali walikamatwa na polisi wakidaiwa kuhusika na mauaji hayo.

Marehemu Mathias enzi za uhai wake.

 “Siku chache baada ya mauaji hayo, Amos na Mohamed Chali walifuja pesa kwa kunywa pombe kupita kiasi ambapo mmoja aliropoka kilabuni kwamba walilipwa fedha nyingi kwa kumuua Mathias.
“Baada ya majigambo hayo, watu wakatoa taarifa polisi na wahusika wakakamatwa na ndiyo waliomtaja Johnson,” alisema diwani huyo. 



MGANGA AINGIA MITINI
Uwazi lilifanikiwa kufika Sangasanga kwa mganga huyo na kuambiwa kuwa alikimbia kwa kutumia mlango wa nyuma baada ya polisi kufika kwa ajili ya kumkamata. 



MATUMIZI YA KICHWA
Habari zilizoenea kwenye kijiji alichokuwa akiishi marehemu Mathias zinadai kwamba, mganga huyo ambaye jina halikujulikana mara moja, alimwambia mtuhumiwa kuwa, angekifanyia dawa kichwa hicho ambapo angekiweka dukani ili kuvuta wateja wengi kwa siku, hivyo ndani ya mwaka mmoja tu angekuwa bilionea.