Friday, November 7, 2014

WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI YA BASI


Watu 37 wamejeruhiwa mara baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Mbeya kwenda Dar es salaam kupasuka tairi na kupinduka katika eneo la Meta wakati dereva akifanya jitihada za kuikwepa baiskeli katikati ya barabara, Chimala, Mbarali mbeya. Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Happy Nation lenye namba za usajili T. 281 ARR Scania lililokuwa likendeshwa na dereva aliyefamika kwa jina moja la Shabani.Taarifa iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi inasema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea mkoani Dar es Salaam. Amesema ajali hiyo imetokea leo Nov 7 majira ya asubuhi baada ya kupasuka tairi la mbele kushoto hali ambayo ilisababisha kuacha njia na kupinduka. 

Amesema mara baada ya kupasuka tairi dereva alishindwa kuimudu nahasa kutokana na eneo lenyewe kuwa na kona kali hivyo aliamua kuligongesha kwenye ukingo wa barabara nakusabisha hali hiyo.
Aidha Msangi amesema kuwa kati ya majeruhi hao 29 ni wanaume na wengine 8 nakwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo. 
Amesema kuwa majuruhi Sita kati ya wote hali zao ni mbaya na tayari wamefikishwa katika hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi wakati majeruhi wengine 10 wakiwa wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya Chimala.
Akithibitisha kupokea kkwa majeruhi hao Muuguzi katika chumba cha msaada wa haraka hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt Orivia Masoi amesema kuwa wamepokea majeruhi sita ambapo wanne wamelazwa wodini na wawili tayari wameruhusiwa. 
Aidha mmoja wa majeruhi Nicolaus Fungo ambaye amelelazwa wodi namba moja kwa ajili ya matibu hao amesema majeraha makubwa maeneo ya mbavuni na kwamba hali yake inaendelea vizuri mara baada ya kuaptiwa matibabu.

KONYAGI FEKI ZAKAMATWA..



  Baadhi ya maofisa usalama wakiangalia mzigo uliokamatwa wa konyagi feki  ukipandishwa katika gari kwa ajili ya kuelekea kituo cha polisi buguruni Dar es salaam jana 
Baadhi ya vibarua waliokodiwa kwa ajili ya kupakia Konyagi ili wapeleke kituo cha polisi Buguruni wakifanya kazi ya kujaza katika marobota ili waweke katika gari baada ya konyagi hiyo feki kukamatwa Dar es salaam jana kwenye moja ya Godawn maeneo ya vingunguti karibu na kituo cha mchicha watumiwa walikamatwa na kupelekwa polisi
Baadhi ya watuhumiwa wa Konyagi feki wakifanya kazi ya  kupakia kwenye mabox konyagi hizo ambapo walikamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa kituo cha polisi buguruni kwa uchunguzi zaidi
Baadhi ya watumiwa wakiwa chini ya ulinzi ambapo jana waliswekwa lumande na kulala ndani ya kituo cha polisi buguruni baada ya kukamatwa wakipack konyagi feki maeneo ya vingunguti Dar es salaam jana
MMOJA YA WATUHUMIWA AMBAYE ALIJITAMBULISHA KUWA YEYE NI MMILIKI WA KONYAGI FEKI AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA JANA

Baadhi ya watumiwa waliokutwa katika godwon lenye konyagi feki wakiendelea na kazi ya kupakia katika mabox watumiwa hawo walikamatwa na kulala lumande katika kituo cha polisi buguruni Dar es salaam jana kwa uchunguzi zaidi