WENGI WAABADILI MTAZAMO WA URAIA
Vijana wengi
wamekuwa walalamikaji wa mambo na wala si watendaji wa mambo wanayolalamikia,
wakati huohuo vijana ndio nguvu kazi katika maendeleo ya jamii lakini si
washiriki wa kuleta maendeleo hayo.
Hayo yalisemwa na Kefar Mbogela ambaye ni mratibu msaidizi
wa mradi wa Fahamu Ongea Sikiliza (FOS) ambao upo chini ya taasisi ya Restless
Development nchini. Ambapo alisema lengo ni kutengeneza jamii bora ya vijana na
kufanya vijana kuwa vioongozi bora katika jamii na wanakuwa wafanya maamuzi
katika jamii.
Mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa unalenga kuwahamasisha,
kuwaelimisha na kuwafanya vijana kushiriki katika shughuli za kiraia na hasa
katika mchakato wa uchaguzi mkuu Tanzania. “Mraadi huu unawataka vijana wajitokeze
kushiriki kwa wingi kujiandikisha, kupiga kura na kugombea kwani ni haki ya
kila mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea kwani kijana huyo ana sifa za kupiga kura na kugombea pia. Alisema
Kefar
Akiongea kwa hamasa alisema kuwa vijana wengi wamekuwa
hawashiriki katika shughuli za kimaendeleo kitu ambacho kimewafanya vijana hao
kujinyima haki ya kimaendeleo kwa kutoshiriki kwao. “matatizo ya vijana
wanayajua vijana wenyewe na mengi
yanaweza kutatuliwa na vijana wenyewe iwapo vijana wataashiriki kikamilifu
katika nafasi za kuleta maendeleo kwani wao ndio nguvu kazi inayotegemewa
katika kuleta maendeleo kuliko makundi mengine ya watu.
Pia alisema ni vyema vijana wakawajibika kuyatimiza majukumu
yao wenyewe badala ya kuendelea kuilaumu serikali huku wakiwa hawajitokezi
katika shughuli za kiserikali wakidhani ya kuwa ni jukumu la serikali kufanya
majukumu kwa ajiri ya vijana kitu ambacho ni kujidanganya na kuendelea
kujicheleweshea maendeleo.
Wakati wa mafunzo hayo vijana walielezwa umuhimu wa vijana
kushiriki katika kupanga maendeleo
kuanzia katika ngazi ya mtaa mpaka serikali kiujumla ili kuondoa dhana
ya kuwaona vijana ni watu wasiofaa katika jamii kama ilivyo hivi sasa. Hivyo
aliwasihi vijana hao kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa kujiandikisha
na kupiga kura kwa kuchagua viongozi sahihi.
Nae Bwana Abdul Lukanza ambaye ni afisa uhusiano wa vijana
alieleza umuhimu wa nafasi ya vijana katika demokrasia kitu ambacho kiliamsha
hisia za vijana wengi na kufanya maswali mengi kujitokeza miongoni mwa vijana
hao.
Hata hivyo kitendo hicho kilitoa fursa kwa Bwana Abdul kuelezea sifa na faida za
demokrasia na kuwasihi vijana hao kufikisha elimu waliyoipata kwa vijana
wengine ili Kuongeza uwezo na motisha kwa vijana kushiri katika mchakato wakujiandikisha,
kupiga kura na kugombea nyadhifa mbalimbali, Kukuza ufahamu wa viongozi katika
kazi na ni majukumu yao kuwasaidia wananchi kushiriki kikamilifu katika chaguzi
zijazo.
Mafunzo hayo ambayo yalishirikisha vijana zaidi ya 50 kutoka
mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Shinyanga yalifanyika mkoani Kilimanjaro,
yaliwaacha vijana kuwa na hamu kubwa ya kwenda kutoa elimu hiyo baada ya
kutambua kuwa vijana ndio chachu ya maendeleo.
“Elimu hii niliyoipata nitakwenda kuwapa vijana wenzangu ili
nao fahamu zao ziweze kufumguka kama ambavyo ilivyo kwangu” alisema Salim
Muhamed kutoka Manyara.
Wakati huohuo Lilian kutoka Tanga alisema kuwa elimu
aliyoipata imemfungu ufahamu mkubwa na kumwezesha kutambua kuwa vijana wengi ni
waongeji lakini si watendaji kitu ambacho mwisho wa siku wamebaki kuwa
walalamikaji. “ Elimu hii ni lazima iwafikie vijana maana nimegundua kwamba
watu wengi wanataka kufanyiwa mambo na si kufanya wenyewe ili kujikwamua
kimaendeleo” AlisemaLilan
Restless ni taasisi ya maendeo ya vijana ambayo ilianzishwa
mwaka 1985 nchini Uingereza kama SPW (Student Partnerships Worldwide) ambapo
kwa tanzania shirika hili lilianza mwaka 1993 mjini Moshi mkoani Kirimanjaro na
mwaka 1998 lilihamishia makao yake makuu mkoani Iringa ambapo lilikuwa likikusudia
kutoa elimu ya afya ili kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi ambako ndiko
makao makuu ya Restless yapo mpaka sasa.
Mradi huu wa OFS unatekelezwa katika mikoa kumi na nane (18) ya
Tanzania Bara ambayo imechaguliwa kwa
vigezo maalumu vya uwakilishi wa kikanda. Mikoa hiyo ni; Mwanza,Kigoma,Manyara,
Kilimanjaro,Dar es Salaam, Arusha,Mbeya, Iringa, Dodoma,Shinyanga, Mtwara,
Lindi, Simiyu,Morogoro,Geita, Kagera, Tanga na Ruvuma.Katika mikoa yote hii wapo vijana wakujitolea wanaotoa hamasa na mafunzo kwa mitandao ya vijana
iliyoundwa na vijana wenyewe ili kutoa elimu ya uraia kote nchini.
Mbali na mradi huu pia Restdi wa lessDevelopmnt wanafanya
mradi wa Mwanamke tunu, Vijana tung'are kazini, Dance for life na mingine mingi kwa ajili ya vijana nchini
Raha ya
ngoma uingie ucheze hivi ndivyo waswahili husema wakiwa wanamaanisha huwezi
kukisemea kitu ikiwa hukijui na wala hujashiriki. Kwa mantiki hii vijana
wanatakiwa kushiriki katika michakato ya kuleta maendeleo ya nchi tukianzia
katika kuchagua viongozi