Tuesday, August 12, 2014

MAJAMBAZI YAUWA MUME NA MKE NA KUJERUHI MTOTO




Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamiana kuwaua mume na mke na kumjeruhi mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyeachwa na mama yake aliyeuliwa katika tukio lililotokea kijiji cha Murvyagira wilayani Ngara mkoani Kagera Ijumaa ya Agost 08,2014.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu amesema majambazi hao walivamia nyumbani kwao majira ya saa 3 usiku ambapo walitumia panga na jembe kuwaua baba na mama yake na kisha kuwapora Maharage gunia moja, Radio, Gunia la Karanga, Mabati na Fedha vitu ambavyo hadi sasa thamani yake haijajulikana, huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.
Aidha baadhi ya wananchi walioongea na Blog hii, wameomba juhudi ya kuimarishwa hali ya usalama na ulinzi wilayani Ngara izidishwe hasa wakati huu ambako matukio ya mauaji yamezidi kujitokeza.
Mwili wa mwanaume ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa kwa kukatwa Mapanga na watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi.

Mwili wa mwanamke ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa na majambazi hao. Mama huyo ameacha Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyejeruhiwa na watu hao wanaodhaniwa ni majambazi.

SHAHIDI AELEZA JINSI MGANGA MANYAUNYAU ALIVYOWATAPELI MIL. 29.6



Dar es Salaam, Shahidi wa pili katika kesi ya kujipatia Sh29.6 milioni kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mganga wa jadi, Dunia Salumu (37) ‘Manyaunyau’ amedai kuwa walilazimika kuuza kiwanja na nyumba ya urithi kutafuta fedha za kununua mabeberu saba na mafuta ya ngamia ili kumpa mganga huyo kama masharti ya kumfufua ndugu yao aliyefariki dunia.
Manyaunyau alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Desemba mwaka 2013 akikabiliwa na shtaka la kujipatia fedha hizo kutoka kwa Tecla Modest.
Akiongozwa na Mwendesha Mashtaka, Nassoro Katuda shahidi huyo, Diana Steven (26) alidai kuwa baada ya kumaliza matanga ya mjomba wake, Saimon Modest aliyefariki mwaka 2008, wakiwa nyumbani Mchikichini, Dar es Salaam walisikia sauti ya mtu ikisema kuwa ‘mimi sijafa’.
Wakati Diana akiendelea kutoa ushahidi huo mrefu, Hakimu Wilberforce Luhwago, alimkatisha akieleza kuwa ameisikiliza kesi hiyo kwa muda mrefu na kuna nyingine za kusikiliza, hivyo itaendelea Agosti 13, mwaka huu.

Ushahidi wenyewe

Alisema siku tatu baada ya mazishi ya mjomba wake, ndugu yao aitwaye Hamisi akiwa na Manyaunyau walifika nyumbani kutoa pole na walipofika Manyaunyau alidai kuwa marehemu hajafa, bali ameuawa na kaka yake na amechukuliwa na Mpemba kwa ajili ya kwenda kuuza duka.

“Mimi na mama zangu wawili tulishtushwa na kuhoji, mtu aliyekufa anaweza akawa hai?” alisema Diana katika ushahidi wake uliochukua saa nane.

“Baada ya hapo alituambia siku iliyofuata twende ofisini kwake (Manyaunyau), Mburahati, tukiwa na Sh100,000. Mama zangu walisema hawana, lakini ndugu yetu mmoja aitwaye Bright Steven alikwenda kwenye ATM na kuchukua Sh80,000 na safari ikafanikiwa,” alidai.

Diana alisema baada ya kupeleka fedha hizo, Manyaunyau aliwapangia kwenda siku nyingine, akiwataka kurudi wakiwa na kitambaa cheusi na walipokipeleka alisema alikichukua na kukifunika kikaanza kutoa sauti ya mtu mzima ikisema: “Karibuni sana wajukuu zangu na maelezo yote mtapewa na mwenyeji wenu.”

Alisema Manyaunyau pia aliwataka wapeleke chupa sita za mafuta ya ngamia wakiyakosa wampelekee Sh1.8 milioni. Alisema walimpelekea fedha hizo walizozipata kwa kuuza sehemu ya kiwanja walichorithi kwa mama yao.

“Siku tuliyopeleka hiyo hela pia tulipeleka mtama, jogoo mwekundu na tulipelekwa katika pori lililopo Kibamba na kila tulipokuwa tukienda kule Kibamba tulikuwa tunakodi teksi kwa Sh40,000,” alidai Diana.

Alidai kuwa kabla ya kufika katika pori hilo, Manyaunyau aliwaagizia soda wakanywa na baada ya kumaliza aliwaambia wapige makofi huku wakisema hodi hodi mkubwa!

“Tuliingia katika pori hilo saa 2: 00 usiku, tukaona mwanga kama radi imepiga na tukaona kitu cheupe kama mtu kafunikwa sanda... ile tuliyoipeleka kwa Manyaunyau siku chache kabla ya kwenda katika pori hilo.

“Alituambia mtu wenu ndiyo huyo ila msimfunue kwa sababu ni mchafu, akasema inatakiwa hela ya kununua mafungu mawili ya dawa ya kumsafishia.

Sisi hatukuelewa, ndipo alipotuambia siku iliyofuata twende ofisini kwake atufafanulie. Tulipofika alituambia anataka mbuzi saba madume na Sh2 milioni na kwenda naye tena Kibamba.

“Tukiwa porini hapo tulisikia sauti ya babu ikisema marehemu wenu ameshikiliwa na wachawi, wanataka damu ya mbuzi saba, hivyo tulirudi nyumbani na kwenda kuuza tena kiwanja kilekile kwa mtu mwingine na kupata Sh4.9 milioni na kuzipeleka kwa Manyaunyau kununulia mbuzi hao,” shahidi alidai na kuongeza kuwa ‘babu’ alizidi kuongeza madai, mara hii akisema anataka nguo, mkeka na chakula nyumbani kwa Manyaunyau.

“Baada ya kauli ya babu, tulipeleka chakula kwa Manyaunyau na hapo alituambia tujiandae kwa safari ya Majohe na huko tulikwenda mimi na mama zangu wawili na mke wa Manyaunyau na tulipofika tuliongea tena na ‘babu’ na kutuambia tutafute Sh2 milioni nyingine kwa ajili ya kumkomboa ndugu yetu.”

Waliporudi kutoka Majohe, alidai kuwa walikwenda kukopa kwa riba na Manyaunyau alisema fedha hizo wazifunge katika kitambaa cheusi na kuziweka katika ndoo na kuzipeleka katika Msitu wa Majohe.

“Tulipofika Majohe tulipiga makofi na kuziweka zile pesa na siku iliyofuata Manyaunyau alituambia tutoe Sh3.5 milioni kwa ajili ya kukanyagia na sisi tulizipelekea hukohuko Majohe.”

Alidai kuwa siku iliyofuata walikwenda ofisini kwa Manyaunyau na kuambiwa kuwa wapeleke chakula nyumbani kwake baada ya hapo waende kumwangalia mchawi aliyemchukua ndugu yao huko Kibamba eneo la makaburi.

“Tulipofika eneo hilo la makaburi alitokea mtu mrefu sana akiwa ameshikilia mkia na akapiga magoti na hapo hapo alitokea tena mtu mnene na kusema hamuwezi kumuona ndugu yenu kwa sasa.”

Diana alidai kuwa baada ya kuambiwa hivyo, ilisikika sauti ya ‘babu’ ikisema watafute Sh5 milioni nyingine.

“Tulivyosikia hiyo sauti ya ‘babu’ akisema tutafute ndugu zangu walisema hawana hiyo hela na sauti ya babu iliendelea kusema kuwa nyie leteni tu hiyo hela marehemu akija atailipa,” alieleza.
-www.udakuspecially.com

MJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA APIGWA NA VIJANA WANAODAIWA KUWA MASHABIKI WA CHADEMA

 mjumbe-201
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta, akimjulia hali, mjumbe wa bunge hilo, kupitia kundi la wateule 201, Thomas Magnus Mgoli katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako amelazwa kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwenye mgahawa wa Lydia. PICHA: SELEMANI MPOCHI

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Thomas Markus Mgoli amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kushambuliwa kwa kipigo na watu wasiojulikana.

Thomas ambaye ni mjumbe wa bunge hilo kutoka kundi la 201 akiwakilisha Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), amelazwa wodi namba
18 ya daraja la kwanza, akipatiwa matibabu.

Akizungumza kwa tabu kutokana na kusumbuliwa na maumivu makali yanayotokana na kipigo hicho, mjumbe huyo alidai alivamiwa na watu hao wakati akitoka kununua bia kwenye baa iliyopo eneo la Area A, karibu na shule ya msingi Chamwino.

“Around saa 2 kwenda saa 3 usiku, nilikuwa kwenye maeneo ninayoishi, nikaingia kwenye baa ambako ni kawaida yangu huwa nakwenda kununua vinywaji na kurudi ndani, nikakutana vijana ambao huwa siku zote wanajitambulisha kwangu kuwa ni wanasiasa," alidai na kuongeza kuwa:

" Wakanihoji uhalali wangu wa kuwepo Dodoma kuendelea na bunge maalum la katiba, nilipokuwa naendelea kujieleza ndipo waliponivamia na kuanza kunipiga wakisema mimi ni kibaraka na hawatakubali tuendelee na haya tunayoyafanya.”

Alisema hakuna haja ya kuuana wala kuumizana ila ni vizuri ifike mahali, tukubali kwa kutokubaliana na tujenge misingi ya kukubaliana.

“Nina amini hivyo kwa sababu si mara ya kwanza nimewakuta pale baa, jana ilikuwa ni zaidi ya siku ya sita kukutana nao na kila siku
wamekuwa wakitengeneza mijadala na tunajadiliana. Namkumbuka aliyenipiga lakini hao wengine watatu siwajui kabisa, ”alisema mjumbe huyo.

SITTA AZUNGUMZA


 
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, akizungumza baada ya kumtembelea mjumbe huyo hospitalini hapo, alisema amenusurika kifo kwa kuwa alikuwa anaishi karibu na baa hiyo.

“Inabidi nitoe tahadhari kwa wajumbe wote kuanzia sasa kuhusu usalama wao, siyo utamaduni wetu kupigana na wale ambao wana njama zao za kukwamisha bunge la katiba tuko hapa kisheria, ijione tu kwamba wao ndiyoo wana haki na sisi pia tuna haki,”alisema Sitta.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanahojiwa watu watatu kwa mahojiano zaidi.

Misime alisema Mgoli aliripoti tukio hilo jana usiku akidai kuwa alikuwa baa na wenzake watatu wakaanza kubishana kuhusiana na mvutano unaondelea bungeni na baada ya kushindwa kuelewana, walianza kumshambulia kwa kipigo.

“Hadi sasa tunashikilia watatu tunawahoji ili kupata ukweli wa tukio hilo, siwezi kuwataja kwa sasa sipo ofisini,” alisema Kamanda huyo.



Alipotakiwa na NIPASHE kama tukio hilo linatokana na masuala ya kiasa, alisisitiza kuwa: “ Ninachojua tunawashikilia watuhumiwa watatu haijalishi ni wafuasi wa chama gani.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Mzee Nassor amethibitisha kupokelewa kwa majeruhi huo na kusema kuwa amefanyiwa vipimo na kuanza kupatiwa matibabu chini ya jopo la madaktari wa hospitali hiyo.

Imeandikwa na Godfrey Mushi; Salome Kitomari na Editha Majura, Dodoma.

MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI WA MISHIPA YA FAHAMU, UBONGO KUTOKA MISRI KUTOA HUDUMA BURE MUHIMBILI

MADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, masikio na viungo kutoka nchini Misri wako nchini. Wamekuja kufanya kampeni maalumu ya afya, upasuaji na huduma mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI).

Chini ya kampeni hiyo, wagonjwa walioidhinishwa kufanyiwa upasuaji katika maeneo hayo, watapatiwa huduma na madaktari hao hadi Jumatatu ijayo.

Walianza kutoa huduma jana. Huduma ya upasuaji kwa madaktari hao, imeandaliwa na Shirika la Kimataifa linalojihusisha na utoaji wa misaada na huduma kwa jamii ya Al-Rahma International na African Relief Committee of Kuwait kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Othman Kiloloma alisema Tanzania ina upungufu mkubwa wa madaktari bingwa wa maeneo hayo, hususani ubongo na mishipa ya fahamu, ambapo kwa sasa wako watano.

“Licha ya upungufu wa madaktari wa maeneo hayo lakini waliopo wako MOI jambo ambalo husababisha kutofikiwa kwa wagonjwa wengi na ambao wana mahitaji ya haraka hususani wale walioko maeneo ya pembezoni,” alisema Dk Kiloloma.

Aliongeza kuwa wataalamu wengi, bado wako masomoni nchini Misri na Afrika Kusini.

Alisema kwa viwango vinavyotakiwa, daktari bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo, hutakiwa kuwaona wagonjwa 6,000 lakini kutokana na uhaba wa madaktari daktari mmoja hujikuta akiona wagonjwa milioni 11 hadi 12.

Akizungumza Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Profesa Mohammed el Begermy alisema wamekuja nchini kwa lengo la kuokoa wagonjwa wa masikio, ambao wengine wamejikuta wakishindwa kusikia.

Alisema wana uwezo wa kufanya upasuaji, utakaowezesha mgonjwa kusikia tena, kwani asilimia 60 ya wagonjwa wasiosikia hukutana na hali hiyo kutokana na kushindwa kufikiwa na huduma stahiki, huku watoto wengine wakishindwa kutamka maneno kwa kushindwa kusikia.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu, Profesa Hussein Moharram alisema eneo hilo ni la kipekee ambalo huchukua muda mrefu kusomea na linahitaji kutoa huduma kubwa na za dharura.

“Kupata mtaalamu wa eneo hili, inahitajika kusoma takribani miaka 10 hadi 15 na kutokana na wanaosomea taaluma hiyo kutafuta njia ya mkato, hivyo husababisha wataalamu wa eneo hilo kuwa wachache kwani hata upasuaji wake huchukua muda mrefu kuanzia saa sita,” alisema.

Alisema kuwepo katika kampeni hiyo, kutasaidia kushirikiana na wataalamu wa Tanzania, kuongeza uzoefu na kuharakisha huduma kwa wagonjwa.

BAADA YA SHAHIDI KUSHUHUDIA KUPONYWA UKIMWI KWA NABII MAHELA MAMIA WAHAMIA KWENDA KUPONYWA

Nabii Samwel Mahela  wa Kanisa la Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikocheni A (katikati mwenye suti), akitoa huduma ya maombezi katika kanisa hilo.
 
 
MSANII wa Filamu aliyejitambulisha kwa jina moja la Jane amedai amepona ukimwi baada ya kuombewa katika Kanisa la Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikochezi A.
Akizungumza mbele ya waumini wa kanila hilo Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii wakati akitoa ushuhuda wa kupona ugonjwa huo alisema ana mshukuru mwenyezi mungu na Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Nabii Samweli Mahela kwa kumuombea na kupona.
"Nampashukurani zangu mungu kwa kuniponya kupitia mtumishi wake Nabii Mahela nimeteseka sana na ugonjwa huu aleluya sasa nimepona"alisema Jane na kushangiliwa na waumini wa kanisa hilo.
Jane alisema alianza kuugua ugonjwa huu zaidi ya miaka 10 iliyopita na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali bila kupata nafuu mpaka alipoambiwa na mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliyemtaja kwa jina la Onesmo kuwa kuna watu wanapona baada ya kuombewa katika kanisa hilo na Nabii Mahela.
"Baada ya kuambiwa kuhusu uponyaji huo nilifika kanisani hapa na kuonana na Nabii Mahela ambaye alinifanyia maombi mfululizo na kuona hali yangu ikibadilika na sasa afya yangu imeimarika" alisema Jane.
Akizungumza  kuhusu suala hilo Nabii Mahela alisema mbele za mungu hakuna lisilo wezekana kama ilivyowezekana kwa Jane kwa kuwa aliamini atapona kwa maombi na kweli amepata nafuu jambo la kumshukuru mungu.
"Biblia inasema kila aaminie atapona kwa jina la kristo na ndivyo ilivyotokea kwa Jane" alisema Nabii Mahela.