Friday, October 10, 2014

AJALI ZA BARABARANI ZAZIDI KUWAMALIZA WATANZANIA








Gari ya Dar Xpress lifanyalo safari zake Kati ya Dar - Rombo likiwa limepata ajali jana jioni eneo la Marangu _Mamba. Watu kadhaa walijeruhiwa
 
 NA HUKO TABORA BASI LA NBS LAPINDUKA BAADA YA KUGONGA PUNDA

 

Habari zilizotufikia  kutoka mkoani Tabora ni kwamba basi la NBS lililokuwa linatoka jijini ,Mwanza kwenda Mpanda,limegonga punda leo asubuhi na kupinduka katika eneo la Nzega Ndogo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia ni kwamba mtu mmoja,ambaye ni kondakta wa basi hilo amefariki dunia na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega.Inaelezwa kuwa majeruhi 12 wako mahututi

 

TUNDU LISU AKERWA NA UONGOZI WA CHADEMA


Mwenyekiti CHADEMA jimbo la kanda ya kati, Tundu Lissu, akihutubia wana CHADEMA na baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida kwenye viwanja vya Peoples mjini Singida.Tundu pamoja na mambo mengine, amewahimiza wananchi kuikataa rasimu ya katiba mpya kwa madai kwamba imechakachuliwa.
Na Nathaniel Limu, Singida
IDADI  ndogo ya wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa jimbo la kanda ya kati, Tundu Lissu, kuzungumza nao, ilimuudhi mgeni huyo rasmi na kutangaza kwamba viongozi wa CHADEMA Manispaa ya Singida, hawana sifa ya uongozi.
Tundu akionyesha kukerwa mno na mahudhurio hayo, alisema wananchi wa mji wa SIngida kwa kipindi cha miaka sita, hawajapata viongozi wanaowastahiki.
“Haya maneno yaliyosemwa na viongozi wa CHADEMA manispaa ya Singida, kwamba wananachi wa mji huu, ni waoga kuhudhuria mikutano ya CHADEMA, ni blaa blaa tupu na hayana ukweli wo wote.
  Ningejua hali ingekuwa hivi, nisingekuja”,alisema kwa masikitiko.
Alisema wananchi wa manispaa ya Singida toka CHADEMA izaliwe, hawajawahi kupata viongozi wenye uwezo bora wa kuongoza, kuhamasisha na kuwaambia ukweli wa mambo yanayoendelea.
DSC00993
Akifafanua zaidi, Tundu alisema wananchi wa manispaa ya Singida, sio waoga kuhudhuria mikutano ya CHADEMA.  Mahudhurio mabovu ya leo, ni matunda ya maandalizi mabovu yaliyofanywa na viongozi wasio na sifa.
Katika hatua nyingine, Tundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Singida mashariki, alitumia muda mwingi kumsifia baba wa taifa hayati Julius Nyerere, kwa kudai kwamba alikuwa ni mtu mwenye akili nyingi na alikuwa mwadilifu na hakuwa  mwizi.
“Mwalimu Julius alikuwa na hekima kweli kweli, lakini hata hivyo alikuwa si Mungu, alikuwa binadamu kama mimi na wewe.  Alikuwa kiongozi safi huwezi kumlingansiha na watoto wake hawa (marais waliomfuata)”,alisema.
DSC00992
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Singida,wakimsikiliza mwenyekiti CHADEMA jimbo la kanda ya kati na mbunge wa jimbo la Singida mashariki, Tundu Lissu, wakati akiwahutubia.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Kuhusu rasimu ya katiba mpya, Tundu alisema rasimu hiyo siyo mpya ni ile ile ya mwaka 1962, isipokuwa imejaa mapambo  mapambo, ili kuwaghilibu wanachi.
“Rasimu ya katiba ingesema rais hana haki ya kumnyang’anya mtu ardhi, rais ni binadamu aliyefanya  makosa kama binadamu wengine, akikosa ashitakiwe. Mawaziri wasitokane na wabunge au iondoe nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya. Hiyo ningesema ni rasmu bora kwa usatawi wa watanzania” na kuongeza;
“Katiba mpya itakuwa ya ovyo kuliko hii ya sasa.  Katiba mpya huko mbele itatupelekea tupigane vita na wazanzibar.Nionavyo mimi ni kwamba Wazanzibar hawataipitisha kabisa, nina hofu na huku bara, bara kumejaa ujinga mwingi, kuna uwezekano mkubwa wa kupitishwa  rasimu hii ya katiba mpya”.

TIZAMA SWAGA ZA SENETA WA KENYA MBUNGE KIJANA

UH 2
Mike Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye vituko ambae alipata umaarufu sana toka akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake kivyakevyake, alikua mbunge kijana ambae anaingia na hereni bungeni, blingbling kibao kama cheni na pete kama anavyoonekana ametupia kwenye hii picha hapa juu akiwa sasa ni Seneta wa jiji la Nairobi.Sasa juzi kati Rais Uhuru Kenyatta alikwenda The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya ICC kwa hiyo Wakenya wenzake wanaopinga huo uamuzi wa ICC na kuona ni usumbufu wakajilipia nauli zao ili kwenda kumsupport ambapo Seneta huyu ni mmoja wa waliojilipia na kulipia wengine pia.

Pamoja na Sonko kwenda huko akiwa na dukuduku la kukerwa na maamuzi ya Mahakama hiyo akiitaka imuache Rais wao wa Kenya afanye kazi, aliamua kuvaa tshirt yenye maandishi ya Kiswahili ‘ikiwatusi’ Wazungu kama anavyoonekana kwenye hii picha hapa chini.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana Seneta wa jiji la Nairobi Mike Sonko akiwa amewasili mahakamani ICC na kikosi chake kisha wakafanya maandamano mafupi kabla ya kumpa support Rais Uhuru kwa kuimba wimbo wa taifa na nyimbo za kizalendo wakati kesi ya Uhuru ikiwa inaendelea Mahakani.
Uh 1
Tayari Rais Uhuru Kenyatta amerejea Kenya jana asubuhi na kupokewa na maelfu ya Wakenya ambao hawakupendezwa na kilichofanywa na Mahakama hiyo.

Muda mfupi tu baada ya kuwasili jana Rais Kenyatta alipiga vijembe Mahakama hiyo kwa kusema ‘Walikua wanafikiria kwamba tutakataa kwenda mi nikawaambiwa ile kitu itakataa kuja huko ni Urais wa Wakenya, tumeenda tumekaa huko masaa matatu hatujaambiwa chochote… hatukufungua mdomo sasa hata nashindwa kujua nilikwenda kufanya nini’
‘Ile kitu hawajafahamu kwa vichwa vyao ni kwamba kama nchi ya Kenya tumetoka safari ndefu, na wasifikiri ya kwamba hatujui ni mahali gani tulifanya makosa, sisi tunawaambia hapana….. tuko na suluhu ya shida zetu’
Sonko 2
UH 3
UH 4

FAMILIA YA MWALIMU NYERERE YADAI PICHA ILIYOPO KWENYE NOTI YA SH. 1000 HAIFANANI NAYE, WATAKA NOTI HIYO IFUTE



Familia ya baba wa taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere imeuomba uongozi wa benki kuu ya Tanzania kuiondoa katika  mzunguko wa fedha noti ya shilingi elfu moja yenye picha ya Baba kwa maelezo kuwa picha ambayo imetumika katika noti hiyo haifanani kabisa na kiongozi huyo na kwamba kuendelea kutumika ni sawa na kumdhalilisha muasisi huyo wa taifa la Tanzania.
MADARAKA NYERERE.
Akizungumza kwa niaba ya familia na ukoo wa Baba wa taifa wakati wa kupokea mradi wa kuboresha makumbusho ya Mwalimu Nyerere na kuzindua onesho la noti na sarafu ambazo zimetumika katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 1967 hadi sasa zenye picha na sahihi ya Baba wa taifa, mmoja wa watoto wa Baba wa taifa Bw Madaraka Nyerere, amesema picha iliyopo katika noti hiyo ya shilingi elfu moja haifanani na sura ya kiongozi huyo hivyo kuomba benki hiyo kuangalia uwezekano wa kuiondoka katika mzunguko.
Naye kaimu gavana wa benki kuu ya Tanzania Bw Juma Reli, pamoja na kutoa ahadi ya ukarabati nyumba ya kwanza ya Baba wa taifa ambayo aliitumia kabla ya kujengewa na TANU amesema kuwa benki hiyo imejitolea kuboresha makumbusho hayo ili kuhifadhia kumbukumbu zenye histori ya baba wa taifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wao mkurugenzi mkuu wa shirika la makumbusho ya taifa Profesa Audax  Mabula na mkuu wa wilaya ya Butiama Bi Angelina  Mabula, wameishukuru benki kuu ya Tanzania kwa kutambua umuhimu wa kuboresha makumbusho hayo katika kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere ili kulinda historia za kiongozi huyo.

WATU 7 WAUAWA KINYAMA KWA KUCHOMWA MOTO


Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma
 Watu saba wameuwawa vibaya kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kwa kuhusishwa na imani za kishirikina,huku nyumba ishirini zikichomwa moto katika kijiji cha Murufyiti,wiliaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto na kubomolewa katika kijiji cha Murufyiti wilayani kKasulu mkoani Kigoma
 Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma,Japhari Muhamed amesema,tukio hilo lilifanyika juzi majira ya saa nne usiku baada ya M/kiti wa kijiji hicho aitwaye Evarist Ruhaya akishirikiana na mganga wa jadi,Faustino Ruchagula kupiga mbiu ya hatari ili kukusanya watu na kufanya unyama huo.
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto na kubomolewa katika kijiji cha Murufyiti wilayani kKasulu mkoani Kigoma
 ....amesema watu waliouwawa ni ,John Muvuma (68),Elizabeth Kaje (55),Dyaba Kitwe (55),Vincent Ntiyaba (42),Helman Ntabiloye (78),Redamta Mdogo (60) na Ramadhani Kalaliza (70) wote wakiwa ni wakazi wa kjiji hicho cha Murufyiti,pia nyumba18 zilichomwa moto na zingine mbili kubomolewa na kutimiza idadi ya nyumba20
 ....kamanda Mohamed amesema,tayari watu13 akiwemo mwenyekiti wa kijiji wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea kuhakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani.
Hii ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto na kubomolewa katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma
 .....nae mtendaji wa kijiji hicho Ogeni Gaspa amesema kabla ya wauaji kuanza alipiga simu kwa OCD ili polisi waje kutuliza ghasia lakini gari hazikuwepo kituoni hivyo hali iliyopelekea Polisi kufika eneo la tukio kwa kuchelewa na kukuta mtu wa mwisho akiuwawa.
....kwa upande wa mtoto mmoja wa marehemu,aliejitambulisha kwa jina la Josiphat John amesema:-wakati tukio hilo linaendelea kwa wazazi wangu nilishindwa kutoka nyumbanikwangu kwa hofu ya kudhulika lakini ilipofika alfajiri nilikwenda kuangalia miili ya wazazi wangu ndipo nilipokuta imeteketezwa na moto...

ICC YAZIDI KUMPAISHA RAIS KENYATTA, APOKEWA KWA SHANGWE NAIROBI



Makundi ya watu wanaoshangilia, yamempokea Rais Uhuru Kenyatta ambaye amerejea Kenya baada ya kuhudhuria Mahakama ya Kimataifa ICC, iliyopo The Hague.
Bwana Kenyatta alihudhuria shauri mahakamani siku ya Jumatano, na kuwa rais wa kwanza aliyepo madarakani kufika katika mahakama ya ICC.
Anakanusha mashtaka dhidi yake ya uhalifu dhidi ya ubinaadam kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zilizosababisha vifo vya watu 1,200 na wengine 600,000 kupoteza makazi.
Rais Kenyatta alipokelewa Nairobi kwa gwaride la heshima na ngoma.
Picha: Bw Kenyatta akiwa na mmoja wa mawakili wake wa utetezi ICC.