Thursday, October 9, 2014

AFARIKI DUNIA AKISHINDANA KUNYWA POMBE HARAMU TOKA MALAWI



NA BARAKA LUSAJO, MBEYA
KIJANA mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Wajibu Astofu (16) mkazi wa kijiji cha Lupata kata ya Ipoma katika Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe Mbeya amepoteza maisha baada ya kushindana kunywa pombe haramu za viroba toka nchini Malawi zilizopigwa marufuku kuingizwa na kusambazwa nchini.
 
Akizungumza jana na waandishi wa habari mwenyekiti wa kijiji hicho Pius Dibile alisema kuwa kijana huyo aliweka mashindano na mwenzake ya kunywa pakiti kumi na moja pome hizo za viroba vyenye alcol 35 na kuwa atakayemaliza angepata zawadi.
Alisema kijana huyo ndiye alikuwa wa kwanza kuanza mashindano hayo na kufanikiwa kumaliza pakiti zote kumi na moja na ndipo alipoanza kuishiwa nguvu na kujipigapiga na kupelekea serikali ya kijiji na baadhi wa wanakijiji kufika eneo hilo na kufikia hatua ya kumkimbiza katika hospitali ya misheni ya Itete iliyokaribu na eneo hilo.
Dibile alisema kuwa alipofika katika hospitali hiyo madaktari wa zamu walijaribu kuokoa maisha yake kwa kumuwekea mashine ya kumsaidia kupumua lakini hali ikazidi kuwa mbaya na hatimaye akakata roho na kuwa viroba hivyo vilimkausha maji mwilini na kushindwa kupumua.

Aliongeza kuwa Serikali ya Kijiji hicho kiliitisha kikao cha dharula na kutaka kumuajibisha aliyedhamini mashindano hayo kwa kununua pombe hizo zilizopelekea umauti wa kijana Astofu na kuwa walikuwa wamechelewa kwa kuwa alikimbilia kusikojulikana na jitihada za kumpata zinaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chripin Meela aliwataka wananchi kutii agizo la Serikali na kwamba wao walipopiga marufuku waliona madhara ya pombe hizo kwa watumiaji ambapo bado wafanyabiashara wasio waaminifu wanaingizo pombe hizo na kuzisambazo kwa njia za panya na kusababisha maafa kwa wananchi.

 
Meela aliitaka serikali ya kijiji kumtafuta kijana huyo aliyedhamini mashindano ya pombe hizo na kumkamata ili afunguliwe kesi ya mauaji ili sheria ifuate mkondo wake na iwe fundisho kwa wengine na kuwa wananchi watoe ushirikiano pindi wawaonapo wafanyabiashara hao wanaposafirisha biashara hizo.


WATATU WANUSURIKA BAADA YA GARI LA VINYWAJI KUPINDUKAAJALINI LUGALO, DAR


Kioo cha lori cha  mbele kikiwa kimepasuka.…
Kioo cha lori cha  mbele kikiwa kimepasuka.
Makreti ya soda yalivyoanguka.
Baadhi ya kreti za soda zikiwa zimezagaa eneo la ajali.Mmoja wa wahusika akitoka kuzima na kuuchomoa ufunguo wa gari lililopata ajali.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akilinda usalama eneo hilo.
Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo husika.Watu wakishuhudia ajali hiyo.
Chupa zikiwa zimeanguka kwenye mtaro.
Gari  jingine la  Coca Cola likiwa tayari kubeba mzigo wa ajali.
Gari maalum likijitayarisha kulivuta gari lililopata ajali.
Sehemu ya foleni inayosababishwa na gari hilo.
WATU watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya Coca Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu,  mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia ghafla mbele ya gari hilo  kubwa lililokuwa limebeba vinywaji na  ndipo gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu.

MREMBO HUYU APONZWA NA PENZI LA MGANGA..AFUKUZWA NYUMBANI KWAO!

 



Ulozi? Mrembo aliyejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23), anadaiwa kufukuzwa nyumbani kwao kufuatia kuchanganywa na penzi la mganga wa kienyeji ambaye pia ni ustadhi aliyejulikana kwa jina moja la Zein. Mrembo anayejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23) anayedaiwa kufukuzwa nyumbani. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kutimuliwa kwao, binti huyo ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake walezi maeneo ya Kariakoo jijini Dar alisimulia kwamba alifukuzwa kwao kwa sababu hakulala nyumbani siku moja wiki iliyopita na aliporudi wazazi wake walezi wakamtaka arudi alipotoka.
“Baada ya kufukuzwa sikuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kuja kwa mpenzi wangu (Zein) maana ninampenda na siku si nyingi atanioa.
Mganga wa kienyeji ambaye pia ni ustadhi anayejulikana kwa jina moja la Zein. “Mama na wajomba wameshakubaliana na uamuzi wangu isipokuwa baba tu,” alisema binti huyo.
Alipotafutwa mganga huyo mwenye maskani yake Magomeni-Mwembechai, Dar, alisema kwamba ni kweli yupo na binti huyo na lengo lake ni kumuoa.

MCHUNGAJI AACHA MKE NA KUOA DOGODOGO


MCHUNGAJI Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20 tu ‘dogodogo’, Risasi Jumamosi limetonywa.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC akimuoa 'dogodogo', Pamela Didas.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC akimuoa ‘dogodogo’, Pamela Didas.
Kwa mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi wa Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29, mwaka huu.
Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akipiga picha na mke mpya wakati wa harusi.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akipiga picha na mke mpya wakati wa harusi.
Chanzo chetu ndani ya kanisa hilo kilidai kwamba, mchungaji huyo aliwaambia waumini wake aliamua kumuoa Pamela kwa vile ndoa yake ya mwanzo aliifunga akiwa  Muislam na alifungishwa na shehe (hakumtaja jina).
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiwa mke mpya.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiwa mke mpya.
Habari zaidi zinasema kuwa, mchungaji huyo baada ya kutua nchini, Jumapili moja akiwa kanisani kwake aliwatangazia waumini wake, hasa wanaume kwamba kama wana wake ambao walichukuana wakati wa ‘ujinga’ na wamekaa nao kwa miaka mitatu au zaidi na hawana tabia ya Kimungu, mkorofi na mchokozi na hawajafunga nao ndoa, wawaache ili Mungu awape wake wema.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi Jumamosi, juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiongoza maombi kanisani.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiongoza maombi kanisani.
Baadhi ya waumini walioweza kuzungumza na Risasi Jumamosi walionesha kushtushwa na kitendo cha mchungaji wao kumuoa Pamela lakini hawakuwa tayari kusema neno!
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.”
Baadaye alimtumia ujumbe  mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.”
Mchungaji Peter Rashid Abubakari.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari.
Pia Risasi Jumamosi lilizungumza na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho Tanzania ili kuwasikia wanasemaje kuhusu kitendo cha mtumishi huyo kufunga ndoa nyingine.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao magazetini, baadhi ya wachungaji hao walimpongeza Mchungaji Peter kwamba, aliona alikokuwa na anakokwenda ndiyo maana aliamua kuchukua uamuzi huo.

JK APOKEA KATIBA INAYOPENDEKEZWA MJINI DODOMA LEO


 Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi  katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakiwa wameinua juu  Katiba inayopendekezwa katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014 Kulia ni

Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akifuatiwa na Makamu wake Mhe samia Suluhu Hassan

WAKUTWA WAKILIMA SHAMBA WAKIWA UCHI WA MMNYAMA

Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watu wanne wa familia moja kwa tuhuma ya kukutwa wakilima uchi wa mnyama shambani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina. Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu Venansi Kimario alisema tukio hilo limetokea septemba 2 majira ya saa 12 asubuhi katika kijiji cha Bushikwamala kata ya Kalemela wilayani Busega Mkoani Simiyu. Kimario alisema kuwa watu hao walikamatwa na jeshi la polisi alfajirihuko Bushigwamhala wakiwa wanalima kwenye shamba lao na walipohojiwa walidai kuwa walielekezwa na babu yao kipindi cha uhai wake kuwa wakilima uchi watapata mavuno mengi. Kamanda Kimario aliwataja waliokamatwa kuwa ni Makoye Kagoje (42), na mke wake Neema Kigwela (31) pamoja na watoto wao, mmoja wa kiume (15) na wa kike (12) majina yamehifadhiwa. Aidha Kimario alisema watu hao pamoja na watoto wao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa wakifanya vitendo vya ushirikina. Babu yao alishafariki mwaka jana na aliwaambia kuwa wakilima wapo uchi watapata mavuno mengi, hivyo waliamua kufanya hivyo kutokana na wosia wa babu yao 
Alisema baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wem aliliweza kufika katika eneo hilo na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kulima bila nguo. Hata hivyo Kimario amewataka watu wasijishirikishe kwenye vitendo vya ushirikina na siyo kwamba ukilima uchi utapata mazao mengi tofauti na kufuata kanuni za kilimo bora, viongozi wa madhehebu ya dini na viongozi wa serikali tuwaelimishe watu waachane na imani za kishikina.

MTOTO MIAKA 9 AKUTWA AMEJINYONGA JIJINI DAR.

Baba mzazi wa marehemu Focus Saimon (9).Focus aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, amedaiwa kufanya tukio hilo Jumamosi iliyopita kwa kufunga gauni la mdogo wake shingoni na kujitundika kwenye komeo hilo mpaka kukata roho. 
Katika hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda, Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa sebule yao.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa siku ya tukio, Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo wake, Irene Steve (5).
Mama mzazi wa Focus Saimoni (kushoto) akihuzunika kumpoteza mwanaye.“Alipofika alichukua ufunguo kwa mama mwenye nyumba na kuingia ndani, akanywa chai. Baada ya muda, mdogo wake (Irene) alirudi na kumkuta tayari ananing’inia kwenye komeo la mlango,” kilisema chanzo.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia. 
Mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria (kushoto) akiwa na mama mzazi wa Focus Saimoni.“Nilimwambia Focus usinitanie mbona hauzungumzi na mimi, nilipomwangalia vizuri ndipo nikaona ana damu mdomoni, nikakimbia kwa mama mdogo anayeishi jirani na kumueleza,’’ alisema Irene. 
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria alisema naye hakuamini tukio hilo.“Aliponiambia Focus kaning’inia mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.“Ila mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine. 
Mdogo wa marehemu Focus Saimoni, Irene. 
Akizidi kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema alishangaa wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi aliukuta mwili umeshushwa chini. “Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna aliyenijibu,’’ alisema Catherine.Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo. 
Marehemu Focus Saimoni (9) enzi za uhai wake.’’Tukio hili lina shaka ndani yake, mtoto wa miaka 9 anawezaje kujinyonga, kwa stress zipi? Kwa kweli inasikitisha sana, jeshi la polisi lina wajibu wa kuchunguza ukweli wa kifo cha mtoto huyo,” alisema mama huyo.Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio hilo na kuwauliza wazazi kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.