Thursday, September 11, 2014

MPINZANI WA WILLIAM LUKUVI AWA MAKAMU MWENYEKITI WA BAVICHA

 kwa mtindo huu Lukuvi lazima ajipange

Patrick Ole Sosopi
YULE kijana anayetarajia kutoa upinzani mkali kwa William Lukuvi endapo chama chake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kitamsimamisha kuwania ubunge Jimbo la Isimani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Patrick Ole Sosopi amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bara wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema(BAVICHA). Mbali na kuwa mbunge wa Jimbo la Isimani kwa awamu ya tatu sasa, William Lukuvi ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (sera na uratibu wa bunge). Katika uchaguzi huo wa BAVICHA uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Patrobasi Katambi na Zeudi Abdalla alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar. 

Kuchaguliwa kwa Sosopi kushika nafasi hiyo nyeti ndani ya chama hicho kumeelezwa na baadhi ya wafuatiliaji wa siasa za mkoa wa Iringa kwamba kunamuongezea nguvu kisiasa. 
Patrick Ole Sosopi ambaye ni baba wa mke mmoja na mwenye mtoto mmoja, ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa, jimbo la Ismani. 
Ana umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na Utawala (rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO). Kwa sasa kazi zake ni kufuga ng'ombe. 
Historia yake ya uongozi ilianzia akiwa shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu cha RUCO ambapo alikuwa waziri wa Fedha kwenye serikali ya wanafunzi 2011/2012. 
Alijiunga rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii yake ya kimasai na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili. 
Aliaminiwa na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na kushauriana na familia yake na vijana mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, aligombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA Bara na ameshinda. 
Ingawa ni mojawapo wa wasomi wachache kwenye jamii yao ya kimasai, ni mtu ambaye usomi wake haujamfanya asahau mila na tamaduni za kimasai. Chakula chake, mavazi yake, desturi yake ya maisha ya kila siku ni desturi za kwao na zenye kuhuwisha Utanzania.

MWANAMKE AFUNGIWA BAFUNI MIAKA MITATU BAADA YA KUZAA MTOTO WA KIKE!



Mwanamke mwenye umri wa miaka 25, raia wa India ameokolewa na polisi baada ya kufungiwa bafuni na mumewe kwa muda wa miaka mitatu akiteswa kwa sababu tu alijifungua mtoto wa kike!
Pamoja na mateso ya kunyimwa chakula mara kadhaa, mwanamke huyo alizuiwa kumuona mwanae huyo kwa kipindi chote cha miaka mitatu
 Kwa mujibu wa gazeti la International Business Times, Afisa wa polisi aliyetajwa kwa jina la Seema Kumar ameeleza kuwa mwanamke huyo alikutwa akiwa amedhoofu na baada ya kutolewa nje hakuwa na uwezo wa kufungua macho vizuri katika sehemu ya mwanga kutokana na giza alilolizoea kwa kipindi cha miaka mitatu bafuni.

Seema amesema mwanamke huyo aliwaeleza polisi kuwa hata wakwe zake (wazazi wa mumewe) walimchukia na hii ilichochewa zaidi na kiasi kidogo cha mahari aliyotoa ili kufunga ndoa ya mumewe huyo na kwamba siku zote walikuwa wakimtaka aongeze kiasi hicho.

Kwa utaratibu wa baadhi ya makabila ya kihindi mwanamke ndiye anaelipa mahari.

Uchunguzi wa polisi umebaini kuwa tangu mwanamke huyo afunge ndoa na Prabhat Kumar Singh mwaka 2010 amekuwa akiteswa mara kwa mara na mumewe huyo huku wakwe zake wakimtaka kuongeza mahari na kumsakama kwa kujifungua mtoto wa kike.

WASAGAJI WAFUNGA NDOA BAADA YA KUISHI PAMOJA MIAKA 72


Zaidi ya miongo sabini baada ya kuanza uhusiano wa kimapenzi, Vivian Boyack na Alice "Nonie" Dubes wamefunga ndoa. Boyack, 91, na Dubes, 90, walifunga ndoa rasmi Jumamosi iliyopita, limeripoti gazeti la Quad City Times. 

"Sherehe hii ilikuwa ifanyike siku nyingi sana," amesema mchungaji Linda Hunsaker wakati akIfungisha ndoa hiyo iliyohudhuriwa na marafiki wachache na baadhi ya wanafamilia wa maharusi.

Wawili hao walikutana katika mji waliokulia wa Yale, Iowa, nchini Marekani. Baadaye walihamia mji wa Davenport mwaka 1947, Boyack akifanya kazi ya ualimu, huku Dubes akifanya shughuli za kihasibu.Dubes amesema wameishi maisha mazuri pamoja, katika miaka yote hiyo na wameweza kutembelea majimbo yote 50 ya Marekani, na ya Canada, na pia kutembelea Uingereza mara mbili.

MRISHO NGASA KIZIMBANI


Mshambuliaji nyota wa Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Mrisho Khalfan Ngassa.
 
 
MSHAMBULIAJI nyota wa Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Mrisho Khalfan Ngassa, amefunguliwa kesi ya madai ya talaka namba 30/2014, katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na mkewe Latifa Abdul Fundi.
Ngassa amefunguliwa kesi hiyo akidaiwa kumtelekeza na kumnyima matunzo ya ndoa mke wake tangu Juni mwaka 2011, migogoro ilipoanzia.
Kesi hiyo iliyoanza kuunguruma Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata), Kitengo cha Mashauri ya Ndoa, mambo yalikwenda ndivyo sivyo kufuatia Ngassa kutotoa ushirikiano katika baraza hilo.
Baada ya baraza hilo kushindwa kesi hiyo, liliihamishia mahakamani hapo ambapo juzi (Jumatatu), mchezaji huyo na mkewe walitakiwa kupanda kizimbani mbele ya hakimu waliyepangiwa, Timothy Lyon, lakini Ngassa alishindwa kutokea kutokana na majukumu aliyokuwanayo kwenye timu ya taifa iliyokuwa nchini Burundi.
Kufuatia udhuru huo, Hakimu Lyon aliiahirisha kesi hiyo mpaka Septemba 30, mwaka huu ambapo Ngassa na Latifa wanatakiwa kupanda kizimbani katika shauri hilo.
Katika kesi hiyo, Latifa anamdai, Ngassa talaka pamoja na mgawanyo wa mali walizochuma wakiwa katika ndoa yao ikiwemo nyumba mbili, moja iliyopo Yombo na nyingine Tegeta Basihaya jijini Dar es Salaam.
Kiwanja kimoja kilichopo Tegeta Basihaya jijini, gari aina ya Toyota Cresta, vitanda viwili, kabati dogo la vipodozi, seti ya masofa, meza, pasi ya umeme, majiko mawili ya kupikia, televisheni, redio kaseti, brenda na draya.
Pamoja na mali hizo, Latifa anamdai Ngassa ampe pesa taslimu shilingi laki mbili na nusu (250,000/) kila mwezi, tangu Juni 2011, mpaka siku ya hukumu ambazo ni kwa ajili ya matunzo tangu alipositisha kumhudumia.
Jalada la kesi hiyo liliambatanishwa na cheti cha ndoa kinachoonyesha wawili hao walifunga ndoa Mei Mosi, mwaka 2009, mashahidi wakiwa Imani Madega na Saidy Rashid.

MSICHANA ANAYEDAI KUBAKWA NA MUME WA FLORA MBASHA AELEZA MAHAKAMANI JINSI ALIVYOBAKWA

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya ubakaji inayomkabili mume wa mwimbaji wa muziki wa injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) ameieleza mahakama jinsi alivyobakwa akiwa kwenye gari na nyumbani kwao. 
Shahidi huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni shemeji wa Mbasha, alidai mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago kuwa Mei 23 mwaka huu, Mbasha alimbaka kwa mara ya kwanza wakati mkewe Flora akiwa hayupo.
Alidai siku hiyo, Flora na mumewe walitoka kwenda kufuatilia CD za video zao za nyimbo huku mtoto wao (jina tunalo) akiwa shuleni.
Alidai alishangaa kuona ghafla Mbasha alirudi nyumbani peke yake na kumlazimisha kufanya mapenzi kisha alimtukana na kumtishia kumdhuru endapo atatoa siri.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, shahidi huyo aliendelea kudai kwamba Mei 25 mwaka huu, siku ya Jumapili walikwenda kanisani na waliporudi Mbasha alilalamika kuwa ana njaa hivyo alimpa fedha kununua chipsi.
Alidai baada ya kula, Mbasha alimwambia waondoke nyumbani kwenda kumtafuta Flora ambaye hakuwepo nyumbani siku hiyo.

“Tulipanda gari aina ya Toyota Ipsum, wakati tupo njiani aliniambia nikae kiti cha mbele pamoja naye kwani nilikuwa nimekaa kiti cha nyuma. Nilikubali kukaa katika kiti hicho ndipo aliniambia kuwa ananipenda hivyo tufanye mapenzi kwani nimeshazoea,” alidai shahidi.
 
Aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kukubali kukaa katika kiti cha mbele, Mbasha alipandisha vioo vya gari na kulaza kiti alichokuwa amekalia mtoto huyo na kuanza kumvua sketi yake na nguo za ndani.

Pamoja na hayo alimkaba shingo na kumziba mdomo kwa khanga ili asipige kelele na kumbaka kwa mara nyingine.

Shahidi huyo alieleza kwamba baada ya kitendo hicho kuisha, Mbasha alishuka kwenye gari na kumuacha dada huyo akiwa ndani ya gari na aliporudi alimtaka waendelee kufanya mapenzi kitendo ambacho mtoto huyo alikataa.

Hata hivyo, alidai baadaye alimtafuta Flora kwa simu na alipopokea hakumwambia kilichotokea hadi alipofika Sinza kwa dada zake ambako walimweleza Flora kwa njia ya simu kitendo alichofanyiwa na mumewe, huku akiwa haamini kilichotokea.

Alidai walitoka pamoja na dada zake kwenda kuripoti katika kituo cha Polisi cha Sinza na polisi waliokuwepo kituoni hapo waliwaamuru kutoa taarifa hizo katika kituo cha polisi ambacho tukio la ubakaji limetokea.

Hivyo walirudi hadi kituo cha Polisi cha Tabata na kutoa taarifa.

Kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu cha sheria za mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kinaeleza kuwa mashauri yote ya ubakaji yanatakiwa kusikilizwa katika mahakama ya siri.

Wakili Katuga aliiomba mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo katika mahakama ya siri kwa kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18 na hairuhusiwi mtu yeyote asiyehusika kusikiliza mashauri hayo. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 12 yaani kesho mwaka huu.
 


Mbasha anashitakiwa kwa mashitaka mawili ambayo Mei 23 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala, alimbaka mtoto wa miaka 17 nyumbani kwake. Pia alidaiwa Mei 25 mwaka huu, alimbaka tena mtoto huyo ndani ya gari kinyume na sheria.

MAMA AMTOA MWANAE MACHO BAADA YA KUKATAA KUMUABUDU SHETANI

Mahakama nchini Mexico imewafunga jela miaka 30 kila mmoja ndugu wa familia moja kwa kosa la kushirikiana kumtoa macho kwa kutumia kijiko mtoto wao mwenye umri wa miaka mitano baada ya kukataa kumuabudu shetani.Mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Fernando Caleb Alavarado Rios aliamrishwa kufumba macho mbele ya mama yake mzazi, mama yake mdogo, babu yake na wajomba zake wakati ambapo walikuwa wanamuomba shetani ajitokeze ili awasaidie kuepukana na janga la tetemeko la ardhi!



Lakini kijana huyo alikuwa anaogopa kwa jinsi utaratibu wa ibada hiyo ya kishetani iliyovyokuwa inaendeshwa hivyo akakataa kabisa kufanya hivyo.
Katika hali isiyo ya kawaida, mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Maria del Carmen Garcia Rios alimkamata kwa nguvu na kuwataka wenzake wamsaidie kumtoa macho. Mama yake mdogo alishirikiana na mama yake na wakatekeleza kitendo hicho cha kinyama.
Mama yake Fernando
Kwa mujibu wa UK Daily Mail watu hao walikamatwa baada ya jirani yao kusikia makelele na kujaribu kufanya uchunguzi kujua kinachoendelea.
“Tuliweza kusikia makele na tulikuwa tunapiga hodi kwa nguvu kwenye mlango wao lakini hakuna mtu aliyetujibu, baadae polisi wa patrol alikuwa anapita na wanawake waliokuwa na sisi walikimbia barabarani na kumuita, walikuja polisi wengi na walitumia nguvu kuingia ndani.” Alieleza jirani huyo aitwae Joaquin Arguello.
Polisi aliyejitambulisha mahakamani hapo kwa jina la Benet Curiet aliyefika kwenye eneo la tukio alieleza kuwa baada ya kufika pale alikuta damu zikiwa zimetapaka, aliwahoji watu hao na mama yake alijitambulisha vizuri na kukiri kuwa yeye na mdogo wake ndio waliosaidiana kumtoa macho mtoto huyo baada ya kukataa maagizo yao wakati wa ibada ya shetani.
Jana (September 10) ilikuwa ni miaka miwili tangu lilipotokea tukio hilo May 2012, na mahakama imewahukumu wote waliokuwa katika ibada hiyo kifungo cha miaka 30 jela.
Mtoto Fernando hivi sasa hana uwezo wa kuona na madaktari wamempa miwani maalum na yuko katika uangalizi wa serikali.
Chanzo: UK Daily Mail

MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUSITISHWA TANZANIA


Rais Jakaya Kikwete
Kumekuwa na maoni tofauti kufuatia hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania.
Katika kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Viongozi wa vyama vya siasa nchini humo wamekubaliana kuwa kura hiyo ya maoni ambayo ilikuwa ifanyike kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kinafanyika baada ya uchaguzi huo
Umoja wa wabunge wa kambi ya upinzani Tanzania UKAWA hivi karibuni walisusia bunge la Katiba na kutoka nje kwa kile walichodai kutekelezwa kwa baadhi ya madai ya msingi.
Akizungumza na BBC Deusi Kibamba Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini Tanzania anasema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kusitisha vikao vya bunge la katiba hata kabla ya muda uliopendekezwa wa Oktobar 4 mwaka huu.
Amesema kuwa iwapo wabunge hao wataendelea na vikao hivyo wao pamoja na baadhi ya wananchi wanatarajia kufanya maandamano hadi mjini Dodoma na kufunga milango ya ukumbi wa bunge.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii Robert Mkosamali anasema pamoja na kwamba fedha nyingi zimekwisha tumika hadi sasa kinachpaswa kuangaliwa si gharama hizo bali ni kuangalia ubora wa katiba inayotafutwa hata kama yaweza kutafutwa kwa muda mrefu na wka gharama kubwa.
Mkosamali amesema hata nchi zilizopata Katiba zilichukua muda mrefu na gharama kubwa akitolea mfano nchi ya Kenya.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA BARAZA LA HABARO TANZANIA (MCT), IKULU



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea baadhi ya machapisho ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kutoka kwa Rais wa Baraza hilo, Jaji Thomas Mihayo, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kaimu Katibu Mtendaji na Meneja Nyaraka na Machapisho wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) John Mirenyi baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 11, 2014. Picha na OMR

DIVA AZIDI KUMNG'ANG'ANIA ZITTO KABWE NA KUDAI NI MUME WAKE


Mtangazajiwa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.

Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari  kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.

“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: 

“Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”

Diva alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir.

Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.

Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.

-mail ilisomeka  hivi:
Unanikosea sana ujue unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa kiongozi kwa sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.

“Ungekuwa unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara tatu sasa. Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea sanasana.”
  
Swali la mwandishi:
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.

Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.

Kufuatia Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya mke kwa Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi wake, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na mtangazaji huyo.

Wengi walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.

“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.

Naye Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah Monroe.
“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.


Kufuatia madai hayo, kwa muda wa siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa njia ya simu lakini bila mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa alipo, walisema wanachojua ana shughuli zake nchini Zambia.

UKAWA WAMVAA RAIS KIKWETE TENA


 
       SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA  kulisitisha bunge Maalum la katiba na kupisha Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977, 
           Nao Umoja huo wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4,kwani kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za Wananchi,
              Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili maazimio kati ya  viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.

           Ambapo naye katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo kuendelea hadi  Oktoba 4 mwaka huu, kwani huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na  yeye Rais Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya,
               “Mimi namshangaa jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania zipotee bure kiasi hichi pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga hesabu za Wajumbe wote waliokuwa Bungeni kwenye Vikao vya Bunge garama yake ya posho ni zaidi ya Bilioni 3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi katiba haitopatikana sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana ukweli huko wazi kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge hilo ili fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija”alisema Dokta Slaa,
   Dokta Slaa alizidi kusema anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma za watanzania kwani anakubalina na watu mia sita kutoka kwenye bunge hilo  laa Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania Zaidi ya Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.
           “Huyo ni Rais gani huyo ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma watazania wanaoteseka tena hata kula  mlo moja kwa siku ni kazi,yeye anakubaliana na wajumbe mia sita kuteketeza pesa za Wananchi,hivi kweli ndio kiongozi huyu,kwasababu kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha za Chache kwa ajili ya manufaa kwa wananchi wake”alizidi kusema Dokta Slaa.
        Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi waliyofikia ya kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la katiba litakapohalishwa basi wakubaliane kamaandishi ili  Rais ajaye basi aendelee na mchakato huu asiupuuze,
        “Sisi ukawa tunakubalina na kwa moyo wate maanuzi tulitofikia katika mkutano na Rais Kikwete,na tunasema wazi tumekubaliana kuhailisha mchakato huu basi tunataka tukubaliane kimaandishi kabisa ili Rais ajaye baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa kusikia eti Rais anayekuja ahamue kwa maamuzi yake hatutati kusikia ujinga huo”alisema Mbatia
         Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge hilo Maalum la katiba aliongeza kusema wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba endapo Bunge hilo la katiba litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu hawatakubali kuongozwa na mwenyekiti wa sasa ambaye anaongoza Samwel Sitta na kuzidi kusema  Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge hilo kutokana na kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.
          Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.
         “Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa Serika alifanyie ukaguzi wa kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao vyake hivyo kutawaliwa na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe mmoja kwa siku ametengewa bajeti ya chai ya shilingi Eflu kumi  kwa siku tena chai ya asubuhi na jioni na hata vipaza sauti pia, vyote hivi ni matokeo ya Ufisadi ndio maana tunamtaka alifanyie ukaguzi wa kimahesabu”alisema profesa Lipumba.
   Kuhusu kama Endapo Rais Jakaya asipofanyia merekebisho katiba iliyopo?
    Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema endepo kama Rais Kikwete asipofanyia marekebisho katiba iliyopo basi atakuwa amefanya usaliti kubwa na  ajue ataliweka taifa kwenye machafuko makubwa sana kwani Umoja huo hautokubaliana na yeye.

       Katika Hatua nyingene Umoja huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho ya haraka Daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania ambao hawajapata Fursa hiyo.

MWANAFUNZIA HATARI KWA UTAPELI JIJINI DAR

Denti wa darasa la tano anayetambulika kwa jina moja la Irene (11) aliyenaswa akiwatapeli raia.
 Nyuma ya tukio la denti wa darasa la tano kwenye shule moja ya msingi iliyopo Mbezi-Shamba, Dar, aliyejitambulisha kwa jina moja la Irene (11) la kunaswa akifanya utapeli kwa kuwaibia raia, mazito yameibuka.Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo ya Posta Mpya, Dar, denti huyo alikuwa akisimama nyakati za asubuhi akivalia sare za shule huku akiombaomba kwa madai kuwa hana nauli ya kuvukia katika kivuko cha Kigamboni kwenda shule anayosoma. 

Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, mtoto huyo alikuwa akisimama mbele  ya Kituo cha Daladala cha Posta mpya akijifanya ombaomba kwa madai kwamba hana  nauli.Ilisemekana kwamba siku nyingine mtoto huyo alikuwa akionekana akiuza simu kwa bei chee na alipohojiwa alikokuwa akizitoa alidai ameziokota.
Mwandishi  Gabriel Ng'osha (kushoto) akipata undani wa habari katika tukio hilo. 
 Dereva mmoja, Juma Hamis anayeegesha gari lake eneo hilo (Posta Mpya) alisema kuwa tabia ya mtoto huyo ilikuwa ni ya muda mrefu kwani alianzia Kariakoo, Dar akitapeli na kuiba madukani ambapo watu walimstukia hivyo akaamua kuhamia Posta. 

“Mara kadhaa amenusurika kupigwa akidaiwa kuchomoa simu za watu kwenye mikoba ndani ya daladala.“Kukamatwa kwa Irene, watu wa maofisini na kwenye daladala wameshukuru kwani anafahamika na ni tishio kwa utapeli na ndiyo waliomchoma kwa polisi akadakwa baada ya kukutwa akijidai ni ombaomba,” alisema dereva huyo.
Ofisa wa Polisi kutoka 'Central Police' Posta akifafanua jambo kuhusiana na mkasa huo.
 Jader Sapi, anayefanya kazi katika ofisi moja zilizo ndani ya jengo la IPS, alisema mtoto huyo aliwahi kuingia ofisini kwao na alipotoka, wafanyakazi wawili walilalamika kupotea kwa simu zao, kitu kilichowafanya wajue ni yeye. 

Mama mmoja aliyeshuhudia Irene akichukuliwa na askari, alisema ameshawahi kumpa fedha mara kadhaa denti huyo, akiamini alivyomweleza kuwa hakuna na wazazi na hivyo hana nauli ya kumpeleka shuleni. 

Akizungumza na gazeti hili akiwa mikononi mwa polisi kwenye Kituo Kikuu, Irene alisema ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi (jina kapuni) iliyopo Mbezi-Shamba na siyo kama alivyokuwa akidanganya kuwa anasoma Kigamboni, Dar.
Wananchi wakishuhudia laivu tukio hilo lililotokea maeneo ya Posta mpya, Dar es Salaam.
 Pia alikiri kwamba amekuwa akidanganya kuwa hana wazazi wakati ukweli ni kwamba wazazi wake wapo.“Ni shetani tu aliniingia nikawadanganya raia,’’ alisema Irene. 

Baada ya kushuhudia tukio hilo, wanahabari wetu walimsaka mkuu wa shule anayosoma mtoto huyo, Yusuph Zenny ambaye alikiri kumfahamu Irene na kudai kuwa tayari taarifa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Dar zilimfikia. 

Alitobosa siri kuwa ameshapata malalamiko mara kadhaa kuhusiana na binti huyo na kwamba amekuwa akifanya uchunguzi ili kupata ukweli. 

Hata hivyo, alisema anawasiliana na wazazi ili kulifuatilia sakata hilo hivyo kuwaomba wanahabari wetu wampe muda atatoa majibu au hatua itakayochukuliwa hukuIrene akiwa bado mikononi mwa polisi kwenye dawati la jinsia.

IPTL YAMDAI ZITTO KABWE FIDIA YA SH. BILIONI 500


Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakimtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe awalipe fidia ya Sh bilioni 500 kutokana na kutoa kashfa dhidi yao.

IPTL, Kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo mawili, Harbinder Seth wamefungua kesi dhidi ya Zitto, Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na Kampuni ya Flint Graphics.
Washitakiwa wengine wameshitakiwa kwasababu  makala yenye maneno ya kashfa na kuwachafua, iliyochapishwa Agosti 13 mwaka huu katika ukurasa wa 7 na 14 wa gazeti lao, ikiwa na kichwa cha habari  cha “Fedha za IPTL ni Mali ya Umma” na Kampuni ya Flint Graphics kwa kuchapisha gazeti hilo.
Aidha, wanaiomba Mahakama iamuru makala hayo, yalikuwa ya upotoshaji na kuwachafua kwa kudhamiria,  pia wadaiwa waombe radhi kwa kuchapisha habari ya kuomba msamaha kwenye kurasa za mbele katika matoleo mawili mfululizo ya gazeti hilo. 

Wadaiwa hao waliiomba Mahakama, itoe zuio kwa wadaiwa, watumishi wao, wafanyakazi, washirika, wawakilishi au watu wengine wanaofanya kazi chini ya wadaiwa,  kuchapisha au kuandika makala yoyote ya kuwachafua.

UKAWA WAMVAA RAIS KIKWETE TENA


 
       SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA  kulisitisha bunge Maalum la katiba na kupisha Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977, 
           Nao Umoja huo wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4,kwani kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za Wananchi,
              Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili maazimio kati ya  viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.

           Ambapo naye katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo kuendelea hadi  Oktoba 4 mwaka huu, kwani huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na  yeye Rais Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya,
               “Mimi namshangaa jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania zipotee bure kiasi hichi pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga hesabu za Wajumbe wote waliokuwa Bungeni kwenye Vikao vya Bunge garama yake ya posho ni zaidi ya Bilioni 3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi katiba haitopatikana sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana ukweli huko wazi kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge hilo ili fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija”alisema Dokta Slaa,
   Dokta Slaa alizidi kusema anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma za watanzania kwani anakubalina na watu mia sita kutoka kwenye bunge hilo  laa Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania Zaidi ya Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.
           “Huyo ni Rais gani huyo ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma watazania wanaoteseka tena hata kula  mlo moja kwa siku ni kazi,yeye anakubaliana na wajumbe mia sita kuteketeza pesa za Wananchi,hivi kweli ndio kiongozi huyu,kwasababu kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha za Chache kwa ajili ya manufaa kwa wananchi wake”alizidi kusema Dokta Slaa.
        Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi waliyofikia ya kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la katiba litakapohalishwa basi wakubaliane kamaandishi ili  Rais ajaye basi aendelee na mchakato huu asiupuuze,
        “Sisi ukawa tunakubalina na kwa moyo wate maanuzi tulitofikia katika mkutano na Rais Kikwete,na tunasema wazi tumekubaliana kuhailisha mchakato huu basi tunataka tukubaliane kimaandishi kabisa ili Rais ajaye baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa kusikia eti Rais anayekuja ahamue kwa maamuzi yake hatutati kusikia ujinga huo”alisema Mbatia
         Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge hilo Maalum la katiba aliongeza kusema wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba endapo Bunge hilo la katiba litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu hawatakubali kuongozwa na mwenyekiti wa sasa ambaye anaongoza Samwel Sitta na kuzidi kusema  Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge hilo kutokana na kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.
          Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.
         “Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa Serika alifanyie ukaguzi wa kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao vyake hivyo kutawaliwa na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe mmoja kwa siku ametengewa bajeti ya chai ya shilingi Eflu kumi  kwa siku tena chai ya asubuhi na jioni na hata vipaza sauti pia, vyote hivi ni matokeo ya Ufisadi ndio maana tunamtaka alifanyie ukaguzi wa kimahesabu”alisema profesa Lipumba.
   Kuhusu kama Endapo Rais Jakaya asipofanyia merekebisho katiba iliyopo?
    Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema endepo kama Rais Kikwete asipofanyia marekebisho katiba iliyopo basi atakuwa amefanya usaliti kubwa na  ajue ataliweka taifa kwenye machafuko makubwa sana kwani Umoja huo hautokubaliana na yeye.

       Katika Hatua nyingene Umoja huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho ya haraka Daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania ambao hawajapata Fursa hiyo.

MTANZANIA APEWA CHEO BET


Kabla ya kuanza kukupa info kuhusu huyu Mtanzania nataka nikukumbushe headlines chache za Watanzania walioingia kwenye headlines za kimataifa hivi karibuni.
Ni CloudsTV International kufungua ofisi Kingston Jamaica ambayo itahudumia ukanda wa Caribbean, Diamond Platnumz kuchaguliwa kushiriki tuzo za MTV Europe, AzamTV kuanza kufanya kazi Uganda kwa kuhudumia mamilioni kupitia king’amuzi chake na power bank za Puku zinazomilikiwa na Mtanzania aishie Marekani.
Sasa hivi vichwa hivyo vya habari vitaongezewa hii kubwa nyingine baada ya Mtanzania Kay Madati kuchaguliwa kuwa makamu wa Rais katika kituo kikubwa cha Television nchini Marekani BET.

Taarifa iliyoandikwa na Mtandao maarufu wa Forbes imesema amechaguliwa ‘Kay Madati as Executive Vice President and Chief Digital Officer. Madati, a Tanzanian citizen who has lived in Africa, the United Kingdom, and the United States’
Nilikua sifahamu kama Madati ambae ni raia wa Tanzania aliyeishi UK, Marekani na Afrika, aliwahi kuwa makamu wa Rais CNN Worldwide… aliwahi pia kufanya kazi na BMW Amerika kaskazini, Octagon Worldwide lakini pia amefanya kazi na Facebook.
‘Madati was most recently the Head of Entertainment and Media on the Global Marketing Solutions team at Facebook Inc‘
Sehemu ya kazi ya Madati BET itakua ni kuziongoza timu za BET kwenye maswala ya digital ‘will oversee BET Digital, the interactive arm of BET Networks whose platforms include BET.com, which encompasses entertainment, music, culture, and news; BET Mobile, which provides apps, ringtones, games and video content for wireless devices; Centric.tv, the online home for the Centric cable channel; and BET Video On Demand, one of the largest VOD services providing African-American content‘

ALIYEDAIWA KUUAWA KWA KIPIGO CHA POLISI, UKWELI WAJULIKANA


Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Liberatus Damiani Temu (55) anayedaiwa kufariki kiutata.
 KIFO cha mfanyabiashara aliyeshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam, Liberatus Damiani Temu (55) kilichodaiwa kilitokana na kipigo kutoka kwa askari wa kituo hicho sasa ukweli umejulikana.Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa utata wa tukio hilo ulianzia mbali kwani Mei, mwaka huu, marehemu alimgonga na gari mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Hamis Magoma na kujeruhiwa vibaya.

Mke wa marehemu, Naomi Liberatus (katikati) akihuzunika kwa kumpoteza mwenzake.
 Baada ya kusababisha ajali hiyo, ilidaiwa marehemu Liberatus alifuatilia masuala ya bima ili aweze kumlipa aliyemgonga ambaye pia anatajwa kuwa mteja mzuri katika Baa ya Meku iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu.
Naomi Liberatus akiwa amezimia wakati wa mazishi.
Chanzo kinasema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, hali ya Magoma iliendelea kuwa mbaya hadi Agosti 22, mwaka huu saa tano usiku marehemu alipokamatwa na kufikishwa kituoni hapo akidaiwa kumjeruhi Magoma kwenye ajali.
Padri akiiombea roho ya marehemu ya marehemu (Liberatus Damiani Temu).
Mke wa marehemu, Naomi Liberatus aliyezimia mara mbili wakati wa mazishi, alisema mumewe ambaye kwa kipindi chote tangu apate ajali hiyo, alikuwa hafanyi shughuli yoyote, alikataliwa kupewa dhamana kwa madai kuwa majeruhi (Magoma) alikuwa na hali mbaya.
Mwili wa marehemu Liberatus Damiani Temu ukichukuliwa kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
Kuhusu hatua nyingine ilidaiwa kuwa marehemu akiwa mahabusu aligonga kichwa chake kwa nguvu ukutani, hali iliyosababisha wenzake kupiga kelele za kuomba msaada na kwamba baada ya askari kufika na kukuta hali ilivyo, walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu ambako alifariki dunia.
Marehemu Liberatus Damiani Temu enzi za uhai wake.
 “Watu wanasemasema tu kwamba Liberatus aliuawa na askari, si kweli. Kwa nini tumuue? Kwa kosa lipi? Sisi tulimshikilia kwa sababu hali ya majeruhi aliyemgonga ilikuwa mbaya, hivyo kumweka mahabusu marehemu ilikuwa kwa ajili ya usalama wake pia.