WADAU WAISUBIRI KWA HAMU CD YAKE INAYOTARAJIWA KUTOKA MWEZI DECEMBER MWAKA HUU
Wapenzi wa muziki wa nyimbo za kikristo haswa wale wapendao
kusikiliza na kuangalia waimbaji wanaoimba live yaani uimbaji bila ya mshindo
nyuma wikiendi hii walipata burudani ya kutosha kutoka kwa mwanadada Sarah
Ndosi, aliyefanya live recording katika ukumbi wa kanisa la VCCT mbezi jijini
Dar.
Sarah aliyeonekana kuwa ni mzoefu wa uimbaji huo alizikonga
nyoyo za mashabiki wake waliofika kushuhudia tukio zima alipo imba nyimbo sita
(6) mfurulizo na kuwafanya watu kusimama na kushangilia huku wengine wakishikwa
na mshangao wa aina ya muziki ambao mwanadada huyo aliimba.
“Kiukweli dada huyu anastahili tuzo tena ya heshima maana
nyimbo anazoimba si za hapa, anaimba nyimbo za mbele (akimaanisha nyimbo zenye
hadhi ya kimataifa) na atasaidia nyimbo za kitanzania kujulikana mbele
(akimaanisha nje ya tanzania)yaani wanamuziki wangekuwa wanaimba viwango hivi wanamuziki wakibongo
(wanamuziki wakitanzania) wangekuwa mbali sana” alisikika shuhuda
aliyejitambulisha kwa jina la Prezzor Fredy Chavala, The king
Hata hivyo watu wengi walipigwa na mshangao pale ambapo
mwanadada huyo aliiimba Accapela ya aina yake ambayo kwa hakika iliwafanya watu
kuinua mikono yao kuonyesha kwamba wamemkubali na kufurahia burudani waliyokuwa
wakiipata ukumbini hapo.
“Aisee Sarah anaimba, hata sikutegemea kama angeimba hivi,
mi nilikuja kuhakikisha kama kilichosemwa kuwa ni live ni kweli na kama kweli
itakuwaje kwani ni wachache sana wanaweza kufanya hivi na kwa ubora unaotakiwa
lakini Sarah ameweza” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mama
Junior
Mwanadada Sarah ambaye alionyesha kipaji chake kwa kuanza
kuimba kwa kurudisha mikogo ya enzi zile za kuimba kwa kupiga mabiti
akiwaongoza waimbaji waliokuwa wakimsaidia katika uitikiaji kilinakshi tamasha
hilo.
Sanjali na hilo Sarah alitoa zawadi kwa wanafunzi walioibuka
kidedea katika shindano la Student Talent Vestival lililoshirikisha wanafunzi
wa shule za secondary za jijini Dar es salaam ambaposhule 15 zilishiriki katika
mashindano hayo na mwanadada Ester alishinda kwa upande wa wadada na Samwel
Wilfred mwanafunzi wa Tambaza alishinda kwa upande wa wanaume wakati kikundi
kutoka Jangwani kilishinda katika mchuano wa makundi bora.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa ameamua kufanya mashindano
hayo ili kuibua vipaji vilivyojificha mashuleni na kupata waimbaji wapya ambao
watakuja na radha mpya katika muziki wa Injili ili kuleta changamoto katika
tasnia ya muziki wa injili.
“watoto hawa wapo vizuri sana yaani wanajua kuimba kiukweli,
wakipata waalimu wazuri wakuwaongoza katika uimbaji wao wanaweza wakaondoa
majina ya baadhi wa waimbaji ambao tayari wanafahamika” alisema Sarah
Hata hivyo Sarah amesema kuwa mashindano hayo ya kutafuta
vipaji mashuleni ni endelevu ambapo amesema kuwa yatakuwa yakifanyika kila
mwaka ikiwa mwaka huundio ilikuwa mwanzo wake. Pia amewataka wanafunzi
mashuleni kuweka juhudi katika masoyo yao ili kutowakatisha tama waalimu na
wazazi katika kuwasapoti katika vipaji vyao. Hakuacha kuwasihi wazazi na waalimu
kuwapa nguvu watoto ikiwa wanavipaji kwani hata yeye uimbaji wake aliuanzia
akiwa shuleni na ndio imemfanya akafika hapo alipo katika uimbaji.
Sarah Ndosi amesema CD zake zitakuwa tayari sokoni ifikapo
mwezi December mwisoni , hivyo amewaomba watu wote kumuunga mkono katika kazi
yake hiyo ambapo amesema CD hizo zitauzwa kwa
Tsh 10000 kila moja.