Friday, September 12, 2014

HII MPYAAAAAAAAAAAAA

KWA NINI WAHESHIMIWA WOTE HAWAONYESHI HAYA KAMA HUYU MHE.MWIGULU NCHEMBA??KAVUNJA REKODII..HEBU ANGALIA ALICHOFANYA


Nilifanikiwa kuonana na Mhe.Mwigulu hakuwa na mengi ila nakumbuka tu maana alianza kwa kuniambia hivi:

 Mwigulu Nchemba:

Namshukuru sana Mungu,Nimetimiza Miaka 10 ya NDOA yangu.Pongezi Nyingi sana Kwa Mama Joshua (Mke Wangu),Familia Yangu,Ndugu,Jamaa na Watanzania Wote kwa Maombi Yenu.
Yohana.13.34.Anasema pia jukumu la kulea watoto wetu ni letu wote ndiyo maana kwa mapenzi ya dhati nikiwa nyumbani natamani kumsaidia mke wangu kazi mbalimbali ikiwepo kukaa na watoto,kitu ambacho kwangu kinanipa furaha sana kwani muda mwingi nimebanwa na majukumu ya kitaifa na kimataifa..

 

MFUNGWA MFANYIWA UPASUAJI KUTOA SIMU ALIZOZIFICHA MWILINI MWAKE

Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.

Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.

Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.

OSCAR PISTORIUS APONEA KWENDA JELA


Hatimaye Jaji Thokozile Masipa ametoa maamuzi juu ya kesi iliyokuwa inamkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius na kutupilia mbali madai kuwa aliua kwa kukusudia.

Baada ya muda mrefu na mgumu wa muenendo wa kesi hiyo, jaji huyo ameamuru kuwa Pistorious hana hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili.

Jaji Masipa ameeleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Oscar alimuua mpenzi wake kwa kukusudia baada ya kuwepo ugomvi kati yao.

Hata hivyo, jaji Masipa ameeleza kuwa ameridhishwa na maelezo ya upande wa mashitaka kuwa Oscar Pistorius alikuwa na uwezo wa kutambua mabaya na mema wakati wa tukio hilo.

Huenda mwanariadha huyo akafunguliwa shitaka la kuua bila kukusudia baada ya kuwavuka mashitaka yaliyowasilishwa mahakamani hapo.

Oscar Pistorius alimuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao mwaka 2013. Lakini katika utetezi wake aliiambia mahakama kuwa alimpiga risasi kimakosa akidhani ni mtu aliyevamia katika nyumba yao usiku ule.

PATROBAS PASCHAL: MWENYEKITI MPYA BAVICHA TAIFA


PATROBAS Paschal amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, (Bavicha).

Mwenyekiti huyo alichaguliwa katika uchaguzi uliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kunakoendelea uchaguzi mkuu wa chama hicho Taifa.

Akitangaza matokeo hayo jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi wa vijana, Hashim Issa, alimtangaza Patrobas kuwa mshindi  kwa kura 173..Mwenyekiti mpya wa BAVICHA, Patrobas Paschal

Hata hivyo, uchaguzi huo ulifanyika katika awamu mbili ambako ya kwanza Upendo Peneza alipata kura 68 na Patrobas Paschal 61

Alifafanua kuwa kufanyika kwa uchaguzi wa awamu ya pili ni baada ya mshindi kutopata asilimia 50 ya kura alizopata.

Issa, alisema katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara ilikuwa ikiwaniwa na wagombea 11 ilichukuliwa na Patrick Ole Sosopi aliyepata kura 128 dhidi ya mpinzani wake Jesca Kisikwa aliyepata kura 110.

Alisema kwa upande wa Zanzibar Makamu Mwenyekiti iliyokuwa na wagombea watano, mshindi ni Zeudi Abdallah aliyepata kura 126 dhidi ya Shabani Omary Shabani kura 69.

WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) KANDA YA DODOMA INAKABILIWA NA UFINYU WA ENEO LA KUHIFADHIA MAZAO MSIMU HUU WA UNUNUZI WA MAZAO



 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.

 Wakinamama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.
 Moja ya maghala ya NFRA Kanda ya Dodoma ambayo yamejaa mahindi na Mtama na hivyo kuhitaji maeneo/maghala mengine zaidi ya kuhifadhia mazao.
 Gari iliyobeba mahindi ikipima uzito ili kupeleka mahindi hayo kuhifadhiwa kwenye maghala kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo.
 Baadhi ya Magari ya mizigo yakipakua mahindi na mtama kwenye kituo cha (NFRA) Kanda ya Dodoma.
 Magari yaliyobeba mahindi na mtama yakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakisubiri kuuza mazao hayo kwa wakala huyo wa serikali kama walivyokutwa kituoni hapo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja naC baadhi ya wanachama wa vyama mbalimbali vya ushirika vya kilimo vilivyoleta mazao kuuza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, mapema jana wakati ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mazao kituoni hapo.

Na John Banda
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma kuhakikisha inatafuta suluhisho la haraka la changamoto ya maghala na mifumo ya kuhifadhia mazao inayoikabili taasisi hiyo wakati huu wa msimu wa kununua mazao.

Vilevile Dr. Nchimbi ameelekeza ukarabati wa Maghala ya hifadhi ya “National Milling” yaliyopo eneo la Makole ambayo uwezo wake ni kuhifadhi takribani tani elfu 10 kwa ghala uwekewe mkakati ili kusaidia kuleta suluhisho la haraka la ukosefu wa maeneo ya kuhifadhia mazao yanayoendelea kununuliwa hivi sasa.


Alitoa maelekezo hayo jana alipotembelea kituo cha NFRA Dodoma kukagua maendeleo ya zoezi la ununuzi na uhifadhi wa mahindi na Mtama ambapo alijionea maghala yaliyopo kwa ajili ya kuhifadhia mazao yamejaa na foleni kubwa ya magari yaliyoleta mahindi na mtama kutoka kwa wakulima yakiwa yanasubiri kushusha mazao huku changamoto kubwa ikiwa sehemu ya kuyahifadhi mazao hayo.

Meneja wa NFRA Kanda ya Dodoma Ndg. Mambali alisema kuwa kwa sasa NFRA inanunua mahindi na Mtama kutoka kwa walulima, na kwa mwaka huu, NFRA Kanda ya Dodoma imepanga kununua tani elfu 15 na mpaka sasa tani elfu tatu tu ndio zimeshanunuliwa ambapo tani elfu moja ndio zimefanikiwa kuhifadhiwa kwenye maghala hivyo kunahitajika suluhisho la haraka la sehemu ya kuhifadhi mazao ili zoezi la ununuzi lifanyike kama lilivyopangwa.


Katika hatua nyingine Dr. Nchimbi amepongeza NFRA kwa kutoa kipaumbele kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei maalumu tofauti na inavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ambapo bei inayonunua kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kilo moja ya mahindi ni shilingi 530 wakati kwa wafanyabiashara wengine inanunua kwa shilingi 500.

Akiwasilisha ombi la vyama vya ushirika vya wakulima kuongezewa kiwango cha tani wanazoruhusiwa kuuza kwa NFRA, Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima cha Matumaini Kongwa Ndg. Stanley Machakala amemuomba Mkuu wa Mkoa Dodoma kuwasaidia waongezewe tani zaidi za kuiuzia NFRA kwani huko vijijini bado wakulima wamebakiza mahindi mengi yanayohitajika kuuzwa.

Akitoa ufafanuzi juu ya ombi hilo, Dr. Nchimbi ameahidi kuwasaidia vyama hivyo vya ushirika vya wakulima kulifikisha suala hilo ngazi husika na kusimamia hadi watakapoongezewa kiwango cha mahindi na mtama

JAJI WARIOBA APAZA SAUTI "BUNGE LA KATIBA LISITISHWE"


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema ni vyema Bunge Maalumu la Katiba likasitishwa kwani Katiba bora haiwezi kupatikana kwa muda wa wiki mbili.

Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku moja baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kumtaka Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kulisitisha, huku mwenyewe akisema litaendelea na hadi kufikia Oktoba 4 Katiba inayopendekezwa itapatikana.

Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwa haraka waliyokuwanayo wajumbe wa Bunge hilo wakati wanajua kuwa Katiba haiwezi kupatikana kwa muda uliobaki.

Alisema wiki mbili au tatu zilizobaki ni chache mno na kwamba Katiba mpya haiwezi kupatikana, hivyo ni vyema sasa busara ikatumika kulisitisha.

“Mimi sizungumzii kauli ya Ukawa, lakini natoa maoni yangu kwamba sidhani kama watamaliza kwa kipindi hiki kifupi, kuna mambo hawawezi kupata kwa muda huu mfupi.

“Ninachotaka watumie tu busara waliahirishe… sijui haraka yao hii ni ya nini. Kwanini wanashindwa kuelewa kuwa Katiba ni suala la maridhiano?” alihoji Jaji Warioba.

Kwa upande wake, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Augustino Ramadhani, alikataa kuzungumzia chochote juu ya suala hilo, akisema tangu Rais Jakaya Kikwete alizindue Bunge hilo, alijitoa kuzungumzia suala la Katiba.

“Kama umefuatilia nilishajitoa tangu siku Rais Kikwete anazindua Bunge la Katiba, nilijitoa kabisa, sitaki kabisa kuzungumzia Katiba tena,” alisema Jaji Ramadhani.

Alipotakiwa kueleza sababu za yeye kujitoa kuzungumzia Katiba, alisema: “Ni uamuzi wangu.”

CHEYO NA UKAWA

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),  John Cheyo, alisema Bunge hilo haliwezi kusitishwa wala kuongozwa kwa matakwa ya watu waliopo barabarani.

Akizungumza wakati akichangia majadiliano ya jumla ya mchakato wa Katiba mpya, alisema makubaliano yaliyofikiwa baina ya TCD na Rais Kikwete, ni kuhakikisha Bunge hilo linapata Katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi.

Cheyo alisema kuwa Bunge hilo linaendelea na kazi yake kwa mujibu wa sheria.

Alisema maandamano yanayotarajiwa kufanywa na vijana wa vyama vinavyounda Ukawa, hayatasaidia lolote.

Alielezwa kushangazwa kwake na matamko ya Ukawa na kueleza kuwa ukweli wa kile kilichojadiliwa upo kwenye video ambayo inaonyesha kila mmoja alivyochangia majadiliano hayo.

“Katiba itakayodumu ni ile ya maridhiano, lakini katika maridhiano haina maana kwamba wanaokaa kuzungumza lazima wang’ang’anie upande wao.

“Wanaokaa kuzungumza maana yake wanatafuta ni vitu gani ambavyo wanaweza kuvizungumza, na ni vitu gani ambavyo vinaweza hata kuwekwa pembeni kwa sasa, lakini baadaye vikaja kushughulikiwa kwa mazingira ya wakati huo, hili tumejifunza tulipokuwa tunazungumza na Mheshimiwa Rais juu ya mchakato wa Katiba na Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Mheshimiwa Rais amekuwa ni mfano mzuri wa kukubali kushauriana, na kama Katiba tunavyoizungumza hapaswi hata kukubali, lakini amejiweka chini akakaa kitako na viongozi wa TCD na viongozi wanaojiita Ukawa,” alisema Cheyo.

Aliongeza kuwa katika mkutano wa kwanza uliochukua muda wa saa nne, majadiliano yalikuwa ni namna gani Katiba itapatikana na Uchaguzi Mkuu utafanyikaje na si vinginevyo.

Moja ya mambo yaliyokubalika ni Bunge la Katiba lipate Katiba inayopendekezwa na wananchi kama ilivyokusudiwa.

“Pia tulikubaliana kwa hali halisi ya muda tulionao haiwezekani mchakato mzima ukamalizika, na maana ya kumalizika mchakato ni kura ya maoni ya wananchi na ndio wenye Katiba,” alisema.

Cheyo alisema katika makubaliano hayo, viongozi wote waliafikiana kuwa awamu ya Bunge Maalumu imalize kazi yake kama ilivyokuwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

“Bunge hili haliendeshwi kwa amri ya mtu aliyepo barabarani, linaendeshwa kwa mujibu wa sheria ambayo inasema uhai wa Bunge ni Oktoba 4, mwaka huu, wote tulikubaliana,” alisisitiza Cheyo.

Alisema si rahisi Rais akurupuke na kuliahirisha Bunge hilo kwa shinikizo lolote kwa sababu sheria imeweka wazi ukomo wake.

Aliwataka viongozi wa Ukawa kukubaliana na tamko alilolitoa mbele ya vyombo vya habari, ambalo lilipatikana baada ya makubaliano.

Aidha aliwataka wajumbe wenzake kujiamini na kwamba ripoti itakayotolewa na Kamati ya Uandishi ndiyo itakuwa Katiba inayopendekezwa.

“Na kwa sababu yoyote ile, huko nje kuna anayeamini vingine, anaweza kuamini Serikali tatu, na haipo, mimi sitaki, anaamini Kadhi na haipo hiyo ni shauri yako…,” alisema Cheyo.

TEC YAWASHANGAA UKAWA

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severine Niwemugizi, alisema Ukawa walikuwa na kikao cha maridhiano na Rais Kikwete, hivyo walikuwa na nafasi ya kumtaka asitishe Bunge.

Alisema badala yake walitoka kwenye kikao hicho na kuanza kulalamikia wananchi huku wakiwaambia waandamane ikiwa Rais Kikwete atashindwa kusitisha shughuli hizo.

“Inashangaza kuona Ukawa wanalalamika nje ya kikao wakati walikuwa na nafasi kubwa ya kumwambia Rais Kikwete asitishe Bunge mara baada ya kumalizika kwa kikao chao, badala yake wameamua kuja kwa wananchi na kuanza kulalamika.

“Kwani katika hicho kikao hawakuwa na makubaliano? Na kama ni hivyo kwanini walikubali kutumia Katiba ya mwaka 1977 kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani?” alihoji.

Alisema katika kikao hicho Ukawa na Rais Kikwete waliingia makubaliano ya kusitisha mchakato wa Bunge hadi mwaka 2016 ikiwa Rais ajaye atakubali kuendelea nao.

“Nimewashangaa sana wajumbe wa Ukawa, kwa sababu walikuwa na nafasi kubwa ya kuwasilisha malalamiko yao kwa Rais na kuingia makubaliano ya kusitishwa kwa shughuli hizo, lakini baada ya hapo wanakuja kwa wananchi na kuanza kulalamika huku wakidai kuitisha maandamano, kwani hawakuwa na nafasi ya kumwambia rais malalamiko yao,” alisema.

MBOWE

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alisema hakuna sababu ya kuharakisha mchakato huo na kuwa hata ikibidi baada ya miaka 100, Katiba bora itapatikana.

Alisema jambo muhimu ni Katiba kukidhi mahitaji ya Watanzania na izingatie maoni yao.

“Hatuwezi kuvumilia kuona uchakachuaji wa fedha, unyanyasaji, na ukatili. Yanayoendelea kwenye Bunge la Katiba ni unyama na wizi,” alisema Mbowe.

Taarifa hii imeandaliwa na Elizabeth Hombo, Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam na na Rachel Mrisho, Dodoma.

WAKATI KENYA KUKIIBUKA MUNGU-MTU ANAYEABUDIWA HUKO TANZANIA WALIA NA KANISA LA AJABU LENYE NABII AJIITAE ELIYA



Kituo cha TV cha K24 kiliripoti juu ya uwepo wa Mungu nchini Kenya ambae ibada zinafanyika nyumbani huku yeye mwenyewe akisema "Mimi ni Mungu, nimekuja kuvunja mambo yote yaliyoandikwa"
 Wakati hayo yakitokea Kenya hapa Tanzania kanisa lingine la ajabu limegunduliwa ambapo linafanya ibada zake kwa utofauti mkubwa na makanisa yaliyozoeleka na wengi.

Kanisa hilo ambalo linajulikana kwa jina la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam linafanya ibada zake Jumanne badala ya Jumapili wakiamini ndivyo Neno la Mungu linavyotaka.
Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hilo ni kupinga jina la Biblia Takatifu. Muumini mgeni anayefika kwenye kanisa hilo hulazimika kukabidhi Biblia yake kwa uongozi ambapo wao hutoa ‘kava’ ya nje yenye jina la Biblia na kuweka kava nyeupe yenye maandishi ya Kitabu Cha Bwana.
Kama vile hayo hayatoshi, kanisa hilo linaamini siku za mwezi ni 28 na si 29, 30 au 31. Wanasema Mungu alipanga hivyo na ndiyo maana  aliwapa hata wanawake mzunguko wa siku 28 kuingia katika hedhi.

“Kinachotuingiza kwenye majira halisi ya Mungu ni kufuta tarehe 29, 30 na 31 za Julius Kaisari katika kila mwezi wa kalenda ya Gregori kwa mamlaka ya Mungu wa Majeshi ili kuondoa uovu ulioambatana na tarehe hizo za ziada kwenye miezi 12 ya mwaka,” alisema muumini mmoja kanisani hapo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo lilichapisha kitabu ambacho kinaonesha kuwa mwanzo wa mwaka si Januari bali ni Machi (wao huita Abib au Aviv). Na mwisho wa mwaka si Desemba, bali ni Februari (wao huita Adari).


Kwa ugunduzi wao huo, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo hawafanyi ibada ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu Desemba 25, yaani Krismasi kama madhehebu mengine ya Kikristo kwa vile wanaamini Yesu alizaliwa Februari 28.

Aidha,kiongozi mmoja alijitambulisha kwa jina la Daudi alimtaja kiongozi mkuu wa kanisa hilo kuwa ni Mchungaji Elia wa Pili Mungu wa Majeshi Mtume na Nabii wa kizazi cha nne na akabainisha kuwa, awali alikuwa akifanya kazi Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kama  mhandisi.
“Aliacha kazi ya uhandisi na kuanza kumtumikia Mungu wa kweli kuanzia mwaka 2003, kazi  ambayo amekuwa akiifanya hadi sasa ambapo kanisa limesimama na kuenea Tanzania nzima na duniani,” alisema Daudi.

...Waumini wakisali ndani ya kanisa hilo la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde.

Aliongeza kuwa, Mungu alimwambia nia ya kumteua afanye kazi za kiroho ni kuvunja misingi mibovu ya kumuabudu na kuiweka inayofaa.
Mchungaji huyo ambaye alikuwa akiongea kwa niaba ya kiongozi mkuu, alisema kanisa hilo limekuwa na maagizo ya kweli ambayo  Mungu aliagiza yafanyike.
Kiongozi huyo akizungumzia namna ya kujiunga na kanisa hilo alisema kuwa, sharti la kwanza ni mtu kubadili jina lake la awali na kupewa lingine ambalo ni matakwa ya Mungu kisha kubatizwa upya.
Alisema kanisa hilo halikubaliani na mambo ya dunia kama vile kuwa na Siku ya Kifua Kikuu, Siku ya Ukoma, Siku ya Ukimwi na kadhalika kwa vile kufanya hivyo ni kwenda kinyume na ufalme wa Mungu.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanaoishi jirani na kanisa hilo walipohojiwa kuhusiana na nyumba hiyo ya ibada walisema wana wasiwasi na nguvu za kishirikina ndiyo zinaratibu mwenendo wao.

 
Muonekano wa kanisa hilo kwa nje.

“Huwezi kuchana ‘kava’ la Biblia na kukataa jina la Biblia Takatifu kwa sababu kufanya hivyo ni kama uchawi ambao kwa Mungu haufui dafu,” alisema muumini mmoja ambaye alikataa kutaja jina.
Waumini wa makanisa mengine husema  “Hawa wanaosema namba za mwezi mwisho tarehe 28 ni mambo ya Freemason. Sisi tunaona hivyo,” alisema muumini mmoja ambaye naye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Hivi karibuni gazeti hili liliibua kanisa lingine liitwalo Brotherhood of the Cross and Star la jijini Dar ambalo waumini wake husujudu na kuingia kanisani wakiwa pekupeku huku mabikira wakipewa kipaumbele cha kupelekwa nchini Nigeria, makao makuu ya kanisa hilo.

MREMA ATAKA RAIS KIKWETE AONGEZEWE MUDA WA KUONGOZA



BUNGE wa Vunjo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Augustine Mrema (TLP), amesema kuna haja Rais Jakaya Kikwete aongezewe muda wa kuongoza nchi.

Alisema kama Rais Kikwete ataongezewa muda, atapata muda wa kukamilisha mchakato wa Katiba ambao ndiye aliyeuanzisha.

Mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao kati ya Rais Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kilichofanyika mwanzoni mwa wiki Ikulu ndogo ya Kilimani mjini Dodoma, aliiambia MTANZANIA kwamba Mrema aliyasema hayo alipokuwa akichangia wakati wa kikao hicho.

“Wakati mjadala unaendelea, Mrema alipendekeza Rais Kikwete aongezewe muda wa mwaka mmoja au miwili ili afanikiwe kukamilisha mchakato huu wa Katiba.

“Alipotoa pendekezo hilo, kuna mjumbe mmoja akamuuliza, ‘sasa Mrema unataka muda uongezwe ili na wewe upate muda wa kupambana na Mbatia (James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) anayekusumbua kule Vunjo au?’

“Huyo mjumbe alipouliza hivyo, Mrema akadakia na kusema, ‘hapo hapo’,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa .

Chanzo hicho kilisema kuwa Mrema aliendelea kumsihi Rais Kikwete amzuie Mbatia asiende Vunjo kwa kuwa anapokuwa huko anatumia jina lake, kwamba amemtuma kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Mbatia alipozungumza na MTANZANIA kwa simu jana juu ya malalamiko hayo, alisema hawezi kuendelea kujibizana na Mrema kwa kuwa ni mkubwa wake.

“Mimi sikulelewa katika mazingira ya kujibizana na wakubwa zangu ila ninachosema ni kwamba, wakati wa mkutano wangu wa hadhara niliohutubia Vunjo wiki iliyopita, wenyeviti 11 wa serikali za vijiji walioshinda kupitia TLP, wenyeviti 32 wa vitongoni ambao ni wa TLP, msaidizi wa Mrema pamoja na wanachama wapya 1,564, walihamia NCCR-Mageuzi,” alisema Mbatia.

Naye Mrema alipozungumza na MTANZANIA kwa simu, alikiri kutaka Rais Kikwete aongezewe muda na kumwomba amzuie Mbatia kwenda Vunjo akidai kuwa anatumia jina la rais kumsema vibaya kwa wananchi.