Friday, September 5, 2014

DUUUUUU

FREEMASON WATOA TAMKO KUHUSU MWISHO WA DUNIA HII..!!



WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet,
sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.


  ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.


  DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali.
Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani. DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene  na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.


  NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa).


  WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.


  MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.

  BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.

  IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia. Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.

  WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba.
Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.

  FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja.
Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni  wakiwa wengi.

 MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita kidogo).
Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea

RAIS KIKWETE AONGOZA UFUNGAJI WA ZOEZI LA MEDANI LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50


Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia madhara ya mapigo ya silaha mbalimbali wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
Sehemu ya askari wakitoka katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakisimama kwa wimbo wa Taifa wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
Askari wa kikosi cha mizinga akichukua taswira meza kuu wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na sehemu ya wapiganaji wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza askari wanawake walioshiriki katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.PICHA NA IKULU

ZAIDI YA WATU 30 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA MKOANI MUSOMA. TAFADHALI PICHA ZINATISHA


 Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.Watu 25 wamepoteza maisha papo hapo na wengika kujeruhiwa vibaya sana.kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndoho kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 25 kupoteza maisha pamoja hapo.wakishuhudia tukio hilo la ajali.



Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.
Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.
 Mabasi hayo yakiwa yamegongana 












Mwenyezi Mungu azilaze roho za maremu wote mahala pema peponi..







Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao ni Waandishi wa Habari mkoani Mara Frolence Focus wa Mwananchi na Pendo Mwakembe wa Raia Tanzania wamenusulika kwenye ajali hiyo wakiwa kwenye basi la Mwanza Coach kutokea Musoma.

Akizungumzia kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba 4 hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mra, Frolence amesema walishangaa kuona abiria waliokuwa wamekaa mbele wakisimama na kurudi nyuma na ghafla akasikia mlio mkubwa.

Akizungumza na Redio kahama fm nje ya chumba cha (ICU) kwa niaba ya Mganga Mkuu, Dakatari Martini Khani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa wamepokea idadi kubwa ya maiti na majeruhi huku idadi kamili ikiwa bado haijafah

 Miili ya Abiria waliokufa ikiwekwa vizuri ili kutambuliwa



 Mahututi wakikimbizwa wodini


wanainchi wakiwa kwenye simanzi
Watu wakitambua miili ya marehemu
Basi la Mwanza coach limepata ajali eneo la sabasaba likiwa njiani kuelekea mwanza na kuua watu zaidi ya 30 na majeruhi wengi,Taarifa kamili inakujia punde kaa nasi.

UKATILI KIASI HIKI

UKATILI WA KUTISHAMAMA ADAIWA KUMSULUBU MTOTO, APEWA KIBANO

HII ni too much! Jalada namba KW/RB/7565/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI lililopo kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe, Dar, linamhusu mama aliyetajwa kwa jina moja la Teddy, mkazi wa Tegeta kwa madai ya kumtumikisha na kumtesa mtoto Magdalena Elisha (10) na kumsababishia majeraha na makovu ya vidonda sehemu mbalimbali mwilini.
Mama anayedaiwa kumsulubu mtoto huyo akilia baada ya kutiwa nguvunu na polisi.
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zilidai kwamba, Teddy alimchukuwa mtoto huyo jijini Arusha kwa lengo la kumsaidia kukaa na mwanaye kwa kuwa familia ya mtoto huyo haina uwezo na ameishia darasa la tatu kwa kukosa vifaa vya shule.
Mtoto Magdalena Elisha anayedaiwa kusulubiwa na mama huyo.
Kwa mujibu wa Teddy, bila kujua kwamba ni kosa kumwajiri mtoto, aliamua kumwadhibu mtoto huyo kutokana na kutomsikiliza bosi wake hasa alipokuwa akionywa kuachana na tabia ambayo haikuwa ikimfurahisha.
Kwa upande wake Magdalena alidai kwamba alikuwa akipokea kipigo kila siku hasa wakati mama huyo alipokuwa akirejea nyumbani kutoka ‘jobu’ na kukuta mwanaye analia.
Sehemu ya majeraha aliyoyapata Magdalena Elisha baada ya kusulubiwa na mama huyo.
“Alikuwa akinipiga kila siku akikuta mtoto (wa miaka miwili) analia. Pia kuna siku alinipiga sana asubuhi, nikaona nikimbilie kwa mjumbe, ndiyo tukaenda kituo cha polisi, tukakutana naye akiwa anatoka polisi kutoa taarifa kuwa nimepotea, mimi naomba nisaidiwe nirudi kwa mama yangu Arusha,” alisema Magdalena na kumfanya bosi wake huyo apewe kibako na vyombo vya sheria.

WABUNGE KUGOMBEA UBUNGE NA ELIMU YA DARASA LA SABA.

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Amir Kificho (kulia) akiwaeleza jambo wajumbe wa bunge hilo walipohudhuria kikao cha 32 cha Bunge mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi.

Dodoma.
Pendekezo la Rasimu ya Katiba kuwa wabunge walau wawe na elimu ya kidato cha nne limetupiliwa mbali na wajumbe wa Bunge Maalumu, baada ya Kamati karibu zote kulikataa.


Kamati hizo zimependekeza kigezo cha elimu kuanzia walau kidato cha nne kama sharti muhimu la mtu anayetaka kugombea Ubunge kiondolewe, badala yake mgombea ama ajue tu kusoma na kuandika, au ajue kusoma na kuandika Lugha ya Kiswahili au Kiingereza kama ilivyo kwenye Katiba ya sasa.Mbali na pendekezo hilo, kamati hizo zimegawanyika kuhusu Ibara ya 129 ya Rasimu ya Katiba inayowapa wananchi nguvu ya kumuondoa mbunge wao madarakani kabla ya miaka mitano kumalizika.


Hayo yalijitokeza bungeni Dodoma jana, wakati kamati hizo zikiwasilisha taarifa zake kuhusu Sura ya 9 na 10 ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Akiwasilisha maoni ya Kamati Namba 10, Mjumbe wa kamati hiyo, Dk Dalaly Kafumu alisema suala la kugombea nafasi yoyote ni la kidemokrasia, hivyo haipaswi mtu yeyote kuzuiwa kwa kigezo cha elimu.


“Haki ya kuamua iwapo mgombea anafaa au hafai ni ya wapigakura. Wasizuiwe kikatiba kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua mtu wanayemtaka,”alisema na kuongeza: “Utaratibu huu haupo duniani kote hata nchi zilizo na demokrasia iliyokomaa. Hivyo ibara hiyo isomeke tu ajue kusoma na kuandika na si kiwango cha elimu kama sifa ya msingi.”


Mapendekezo hayo yaliungwa mkono na Kamati Namba 8 kupitia kwa Mjumbe wake, Juma Alawi aliyesema kuweka kiwango cha elimu kwa wagombea ubunge ni ubaguzi.


Kuondolewa kwa kigezo cha elimu ya kidato cha nne pia kumeungwa mkono na kamati namba 10, 4, 12, 9 na 12 za Bunge hilo zilizowasilisha taarifa zake jana asubuhi.


Kamati namba 12 ndiyo iliyokwenda mbali zaidi na kudai kuwa ibara hiyo itasababisha ubaguzi kulingana na elimu wakati kiwango cha chini cha elimu kwa Tanzania Bara ni darasa la saba na Zanzibar ni darasa la 10.


Hata hivyo, ni Kamati Namba 2 tu inayoongozwa na Shamsi Vuai Nahodha iliyokubali pendekezo la Rasimu la kutaka kuwapo kigezo cha elimu. Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo, Vuai alitaka ibara hiyo ifanyiwe marekebisho na kufuta maneno “anajua kusoma na kuandika Kiingereza na Kiswahili” na badala yake isomeke, “ana elimu isiyopungua kidato cha nne”.


Wakati kamati karibu zote zikikubaliana kuhusu kuondoa kigezo cha elimu katika kuwania ubunge, zimetofautiana kuhusu Ibara ya 129 ya inayowapa wananchi nguvu ya kumuondoa mbunge wao asiyewajibika kwao.


Mapendekezo ya Tume ya Jaji Warioba yalitaka wananchi wawe na haki ya kumuondoa mbunge, endapo ataunga mkono sera zinazokwenda kinyume na masilahi ya wapigakura wake au iwapo atashindwa kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero zao au ataacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka jimbo lake kwa miezi sita bila sababu.


Kamati Namba 12 iliafiki wananchi kupata nguvu hiyo ya kumuondoa mbunge endapo tu atakuwa ameunga mkono sera ambazo zinakwenda kinyume na masilahi ya taifa na si ya wapiga kura waliomchagua.



“Kimsingi hakuna namna bora ya kumtathmini mbunge kuwa ameshindwa kutekeleza na kutetea hoja na kero za wapigakura,” alisema Jaffo kwa niaba ya kamati.


Kamati namba 8, 2, 10, 4 na 9 zilipendekeza ibara hiyo ifutwe isipokuwa kamati namba 9 iliyoenda mbali zaidi na kupendekeza kutungwa kwa sheria ya kumdhibiti mbunge anayeshindwa kutekeleza majukumu yake.


Hata hivyo, baadhi ya wajumbe walio wachache katika kamati zao walipendekeza ibara hiyo ibaki kama ilivyo kwenye Rasimu. Maoni ya kamati mbalimbali za walio wachache waliounga mkono kubaki kwa ibara hiyo yalisomwa na Dk Tulia Ackson na Elizabeth Minde ambao wote ni wanasheria kitaaluma.


Wakati huo huo, suala la kuwapo au kutokuwapo kwa Mahakama ya Kadhi katika Katiba Mpya jana liliibuka tena Bungeni baada ya wajumbe walio wachache kutaka liingizwe kwenye Katiba.

MAINDA AONYESHWA MUME WAKE NA MUNGU KWENYE MAONO


Na Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo ambaye amejikita kumtumikia Bwana kwenye wokovu, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kamwe hawezi kuainisha sifa za mwanaume anayehitaji aolewe naye kama ilivyo kwa mastaa wengine kwa kuwa jukumu hilo ni la Mungu.

Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema japo umri wake unaruhusu kuolewa hawezi kuweka wazi sifa za mwanaume anayehitaji awe wake kwa kuwa huenda sifa anazozihitaji Mungu hajampangia kuolewa na mtu wa aina hiyo.

“Kwenye maono naona kabisa mume wangu yupo karibu ambaye Mungu ameniandikia, sasa siwezi kusema nahitaji mwanaume mwenye sifa zipi sababu nikisema nahitaji awe hivi kumbe Mungu hajanipangia huyo,” alisema Mainda.

KUNDI LA BOKO HARAMU SASA LAMKUFURU MWENYEZI MUNGU, YAUA RAIA KISHA NDUGU NA JAMAA WALIOFIWA KUTOIZIKA MAITI.


Wapiganaji wa Boko Haram wamesababisha maafa Kaskazini ya Nigeria ngome yao ya vita

Taarifa za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja ya miji ambayo ilitekwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria

Seneta mmoja wa eneo hilo,Ahmed Zanna, aliambia BBC kwamba wakazi hawaruhusiwi kuwazika jamaa wao waliouawa na wapiganaji hao.

Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji huo ambao Boko Haram imeuteka.
Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.

Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa.

Seneta huyo ameitaka serikali ya Nigeria kupeleka wanajeshi mjini Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo ili kuulinda dhidi ya wapiganaji hao.

Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na wapiganaji hao.

Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000 wameachwa bila makao kufuatia mapigano katika mji wa Bama.

Bwana Zanna anasema kuwa barabara za mji huo zimejaa miili ya watu na Boko Harama imewakataza wakazi kuwazika jamaa wao. ''Kwa hivyo hali ni mbaya na inaendelea kuzorota,'' asema bwana ZANNA

Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji mkuu Maiduguri.

Bwana Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa ikiwa Boko Haram wataushambulia mji wa Maidiguri ambao una watu zaidi ya milioni mbili.BBC

PICHA SI NZURI. MWANAMKE AUAWA KIKATIRI MOROGORO

Wiki iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra pichani. Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata kuchanwa na viwembe.
Mwezi wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.

Kiukweli aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni, mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana akavimba  na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania maisha yake.