Monday, August 11, 2014

MAKAMANDA WA MATAWI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM KATA YA KIMANGA WALIVYOSIMIKWA

Dotto Mwaibale
VIJANA nchini wametakiwa kuwa makini kwa kutumiwa na wanasiasa ili kuvuruga amani na usalama wa nchi uliodumu kwa muda mrefu.

Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Khamis Juma Sadifa wakati wa hafla ya kuwasimika makamanda tisa wa umoja huo wa matawi katika Kata ya Kimanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

"Ninyi vijana ndio walengwa wakubwa kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani na usalama wa nchi hivyo kuweni makini katika jambo hilo kwani tunachokihitaji ni amani na usalama wa nchi kwa watu wote na itikadi za vyama vyetu" alisema Sadifa

Sadifa alisema hata nchi hii ikitokea kuongozwa na chama kingine lakini bila ya kuwa na amani ni kazi bure hivyo ni vema kila mmoja wetu akatambua kuwa hana budi kuilinda amani iliyopo na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine Sadifa alitoa baraka zake kwa Kamanda wa Vijana wa CCM wa Kata ya Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, Scollastica Kevela kuendelea na utendaji kazi wake wa kuinua uhai wa chama katika kata yake kwa kuwatembea vijana na wanachama ili kujua changamoto zinazo wakabili.

"Nakuomba kamanda wangu Kevela endelea kufanya kazi yako ni kuimarisha chama katika matawi kwa kukukutana na vijana na si kukiuka sheria ya kuanza kufanya kampeni kama inavyodaiwa" Sadifa alitoa onyo.

Sadifa aliongeza kuwa kazi kubwa ya ukamanda wa vijana ni kuwakutanisha vijana na kusikia changamoto walizonazo na kuziwakilisha ngaji ya juu kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.

Kwa upande wake Kevela alisema kazi ya kuwainua vijana kiuchumi ndio kipaumbele chake cha kwanza na atahakikisha anafanya hivyo kupitia vikoba ambako yeye ni Makamu wa Rais wa chama hicho nchini.

Alisema amekuwa akifanya ziara katika matawi mbalimbali kwenye kata yake ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kuimarisha chama hangamoto zinazowakabili vijana hao.


Katika hafla hiyo Sadifa alitoa vifaa vya michezo jezi na mipira kwa vilabu mbalimbali vya matawi katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wa ofisi ya CCM katika eneo hilo ambapo zaidi ya sh. 500,000 zilipatikana.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa, akielekea meza kuu tayari kwa shughuli ya kusimika makamanda hao.
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Kimanga, Scollastica Kevela (katikati), akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kusimikwa kwa makamanda tisa wa vijana wa matawi katika Kata ya Kimanga Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Ilala, Alfred Tukiko.Wanachama tisa wa Matawi Kata ya Kimanga wakila kiapo baada ya kusimikwa.

HIZI NI SABABU ZA ANDRE JOHNSON KUKATA UUME WAKE

Sasa basi emetoa sababu zake akisema alikuwa na akili timamu alipokuwa anafanya hivyo.
 Johnsonaliishangaza jamii ya wanamuziki wa kizazi kipya, kufuatia kitendo chake cha kukata uume wake Kaskazini mwa Hollywood mwezi Aprili. Madaktari walishindwa kunguanisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya mwili wake.
Tangu hapo alikimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.
Lakini aliamua wiki hii kujieleza kwa nini alichukua hatua hiyo na kuambia kituo cha televisheni cha E! nchini marekani''Ndio nilikuwa nimetumia dawa za kulevya , lakini nilikuwa najifahamu.''
'mimi sio mwanadamu'

Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha masaibu yangu. Suluhu langu kwa masaiibu yangu ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu, 'mini ni mungu''.......''vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi. Mimi siko hapa ardhini kama mwanadamu bali mungu ''
Matamshi yake Johnson, yanaonekana kama ya mtu anayekabiliwa na matatizo ya kiakili, lakini Johnson anasisitiza kuwa yuko timamu , yeye sio kichaa.
Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini daktari alimwambia hana matatizo.
''Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo sikutaka kuongea sana kuhusu swala hilo. ''
"sikutaka kujiua ,'' alisema Johnson.''
"hilo ndilo jibu langu kwa kitendo nilichokifanya. Leo nafurahi niko hai, na hilo ndilo jambo muhimu zaidi, hata bila ya uume wangu. ''
chanzo:bbc

VIDEO QUEEN WA TZ ATOWEKA GEREZANI NCHINI CHINA

Video Queen wa Bongo anayeshikiliwa na jeshi la polisi nchini China kwa msala wa madai ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ anadaiwa kutokuwepo gerezani.



Video Queen wa Bongo, Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Kwa mujibu wa ‘mtu wetu’ aliyeambatana na rafiki zake Jack kwenda kumuona gerezani, Macau, Hong Kong nchini humo, walijikuta wakipigwa na butwaa kuambiwa hakuna mtu kama huyo gerezani hapo hivyo kuibua hofu kuwa huenda amenyongwa. 

Uchunguzi wetu gerezani hapo ulibaini kwamba tofauti na hofu ya rafiki zake, kuna uwezekano Jack amehamishiwa gereza lingine lililopo nje kidogo ya Mji wa Macau.Chanzo chetu hicho kilidai kwamba habari za ndani zilieleza kwamba Jack amehamishwa gereza hivyo kwa maelezo zaidi watu wanaokwenda kumtembelea waende kwenye ofisi za gereza hilo alilokuwa awali watapewa maelekezo wapi alipo mtu wao.

 
Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ akiwa Chini ya ulinzi mkali China.“Unajua watu wanaokwenda kumtembelea Jack gerezani ni Watanzania walioko huku China kwa shughuli maalum hasa za sanaa, kama vile sarakasi au maigizo, wengine wote wanaogopa, wanajua wanaweza kukamatwa. 
“Tulipokwenda na mazagazaga yetu tuliambiwa Jack amehamishwa gereza na inaonekana aliomba mwenyewe ila hatujui ni kwa nini alifanya hivyo,” kilisema chanzo hicho.Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, John Haule alitoa taarifa na kutaja jumla ya watuhumiwa waliokamatwa kwa kesi za madawa ya kulevya ambapo alisema kuwa kuna Watanzania wengi wapo kwenye magereza mbalimbali China. 

“Katika magereza ya China hadi Februari (mwaka huu) tulipewa taarifa kwamba wapo Watanzania 177 magerezani na kati ya hao 15 wamehukumiwa kunyongwa kutokana na baishara hiyo ya madawa ya kulevya,” ilisema taarifa hiyo ya katibu mkuu. 

Jack alikamatwa Macau, Hong Kong, mwaka jana hivyo kesi yake inaendelea kuunguruma. Tofauti na Beijing ambao huwa wananyonga watu wanaojishughulisha na unga, Hong Kong ni kifungo cha miaka kadhaa tu.


 

KAKOBE AFUNGUKA KUHUSU HELKOPTA YA GWAJIMA

 
 
Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja.Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili
kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’

‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’ – Kakobe
Kuhusu Askofu Kakobe kununua Helikopta yake, amesema >>> ‘mimi sio mtu wa mashindano na pia kila mtu anakwenda sawa kutokana na ono aliloitiwa, haya sio mambo ya kushindana… hicho ndicho kinacholeta shida mara kwa mara, Gwajima ana Helikopta ni kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu, mimi nina chakwangu ni kwa utukufu wa Mungu, hakuna haja ya kuigana

WEREMA SI MVUMILIVU WA MANENO: ATAKA KUTWANGANA NA BI SOPHIA SIMBA BUNGENI







Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba nusura wapigane baada ya kupishana kauli wakati wa mjadala wa ndani ya Kamati Namba Sita inayoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira.

Habari kutoka ndani ya kamati hiyo inayofanyia vikao vyake katika moja ya kumbi za Dodoma Hoteli zinasema, mvutano huo ulitokea Alhamisi iliyopita na kusababisha Wassira kusitisha kwa muda kikao hicho, kisha kwenda kuwasuluhisha.


Jana, Wassira licha ya kukiri kutokea kwa mvutano huo, alikanusha taarifa kwamba aliahirisha kikao hicho kwa ajili ya kuwasuluhisha.


“Kupishana katika masuala haya makubwa ni jambo la kawaida, hivyo mimi sidhani kama ni jambo linalopaswa kwenda mpaka kwenye magazeti maana kila wakati hutokea tofauti hizi na ndiyo maana sisi wenyeviti tupo ili kusimamia mijadala,” alisema Wassira na kuongeza:

 
“Lakini kwamba eti hilo jambo lilisababisha kikao kuahirishwa au kusitishwa hapana, kikao kiliendelea na kazi yake baada ya hilo lililoleta na ubishani kumalizwa”.


Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema mvutano huo ulitokea wakati kamati hiyo ilipokuwa ikijadili Sura ya Nne na Tano, hususan suala la uraia wa nchi mbili. Sura ya tano ndiyo inayozungumzia masuala ya uraia.


“Sophia Simba yeye anataka uraia wa nchi mbili wakati Werema alikuwa akisema hilo jambo haliwezekani kutokea kwa sasa,” kilisema chanzo chetu.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, mvutano huo uliendelea baina ya viongozi hao na ndipo Jaji Werema aliposimama katika mchango wake na kuhoji elimu ya Simba, hivyo kuamsha hasira za waziri huyo ambaye pia alijibu mapigo. 

 
“AG alipopewa nafasi ya kuzungumzia baada ya mabishano ya muda alihoji shule (elimu) ya Simba kwamba amesoma shule gani akimaanisha kwamba ni mgumu kuelewa, kwa hiyo waziri alikasirika na yeye alianza kujibu mapigo,” kiliongeza chanzo hicho.


Baada ya kutokea mvutano huo, baadhi ya wajumbe waliingilia kati kusitisha mzozo huo, ndipo Mwenyekiti Wassira alipositisha kikao hicho kwa muda kisha kuwasuluhisha wahusika.


Walipotafutwa jana kwa nyakati tofauti kuzungumzia mzozo wao, Werema na Simba hawakuwa tayari kubainisha kilichotokea.


Werema alitaka aachwe apumzike na kwamba mambo ya kamati yaachwe kwenye kamati.


“Jamani hamtuachi hata tupumzike Jumapili yote hii? Tafadhali bwana niache nipumzike, hayo mambo kama ni ya kamati, yaachwe kwenye kamati,” alisema Werema na kukata simu.


Simba baada ya kuulizwa alisema: “Heeeee hayo makubwa… I have no comment (sina cha kusema”), kisha alikata simu.


Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema ofisi yake haikuwa imepata taarifa kuhusu mzozo huo na kwamba angefuatilia ili aweze kufahamu kuhusu kilichojiri.
“Nina maofisa wa kutosha katika kila kamati, sasa nashangaa kwamba jambo kubwa kama hilo litokee halafu nisipate taarifa, lakini ngoja nifuatilie lakini kwa sasa sina taarifa yoyote,” alisema Hamad.
 

Werema
Juni mwaka huu, Jaji Werema alitaka kumtia adabu Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila bungeni Dodoma baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuahirisha kikao cha Bunge, ikiwa ni muda mfupi baada ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni.
 

Jaji Werema alichukia baada ya Kafulila kumwita mwizi, akijibu mapigo baada ya mbunge huyo kuitwa tumbili na mwanasheria huyo.


Hali hiyo ilijitokeza baada ya kutofautiana kauli kuhusu mgogoro wa fedha za akaunti ya Escrow kulipwa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.MWANANCHI

AMWAGIWA UJI WA MOTO KWA KUTEMBEA NA BOSI WAKE


MSICHANA mmoja mkazi wa eneo la Minga katika Manispaa ya Singida (muuza duka), amenusurika kifo baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri yake na kumsababishia maumivu makali kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa Singida, wodi namba mbili ya wanawake, Anna Sprian ameifahamishakuwa binti huyo amejeruhiwa sehemu za sikio la upande wa kulia na mgongoni, ambapo amesema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri kutokana na matibabu anayoyapata hospitalini hapo.
Mhudumu
Akizungumza  Agosti 10, 2014 kwa tabu, binti huyo Jackline Lasway (23), maarufu kwa jina la Pendo, amesema majeraha ya moto katika sehemu ya sikio la upande wa kulia na mgongoni.
Singida 1
Majeruhi, Jackline Lasway, akiwa amelazwa katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya mkoa wa Singida, baada ya kujeruhiwa kwa kumwagiwa uji wa moto wakati akiwa dukani kwa bosi wake katika Manispaa ya Singida
Pendo amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Jumamosi Agosti 9, 2014 saa nane mchana wakati akiwa dukani kwa bosi wake aliyemtaja kwa jina la, Charles Kamnde.
Amesema akiwa anaendelea na kazi zake za kuuza bidhaa mbalimbali dukani hapo, gafla alitokea mke wa bosi wake akiwa na chupa yenye uji wa moto na kuwa alimmwagia usoni ambapo baada ya kumwagiwa uji huo alitaka kujiokoa ili usimmwagikie usoni na ndipo ulimuunguza kwenye sikio la kulia na mgongoni na kuwa baada ya mke wa bosi wake kumkosa uso alitoa kisu kutaka kumchoma kifuani.
“Mimi sikuwa na ugomvi naye wala sijui chanzo cha yeye kufika dukani na kunifanyia vile jana, maana kama ni kazi mimi ninafanya kulingana na maelekezo kutoka kwa bosi wangu Chale lakini sijui kilichomfanya afikirie kunifanyia huu unyama” alisema.
Aidha, amesema katika purukushani za kujiokoa kuwa asichomwe kisu hicho, alifanikiwa kumkamata mkono mwanamke huyo na kupiga kelele za kuomba msaada ambapo watu walifika na kumwokoa baada ya muda mchache ambapo alichukuliwa na bosi wake hadi Kituo cha Polisi mjini Singida na kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na kupelekwa katika hospitali hiyo ambako amelazwa huku akiwa ma majeraha mwilini.
Kwa upande wake, mmiliki wa duka hilo Chale Kamnde alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hayuko tayari kulizungumzia kwani maelezo aliyotoa binti huyo yanajitosheleza.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na baadhi ya majirani wa familia hiyo, wameonyesha masikitiko yao juu ya tukio hilo na hatua ya mwananmke huyo kummwagia uji msichana huyo huku wakihusisha tukio hilo na wivu wa kimapenzi baina ya mfanyakazi huyo na mume wa mtuhumiwa.
“Kama aliona kama kuna sehemu kamkosea angemuonya au kama ameshindwa kueleweka basi angemshitaki hata polisi kwani kitu alichokifanya hakiendani na haki za binadamu kwakuwa ni kumdhalilisha huyu msichana ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato chake na familia yake.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo