Rais
wa Marekani Barack Obama amejikuta katika wakati mgumu baada ya kadi
yake ya muamana (credit card) kukataliwa katika mojawapo ya migahawa
iliyopo jijini New York.Obama amekiri kukutana na mkasa huo alipokuwa
akizunguma na waandishi wa habari baada ya kusaini agizo la rais
litakalotumika kama sheria ya matumizi ya kadi za muamana ambayo
itasaidia katika kuzuia wizi wa kadi hizo ambao umekithiri nchini humo.
Akizungumzia
mkasa wa kukataliwa kadi yake, Obama amesema alifika katika mgahawa
mmoja na baada ya kuhudumiwa vitafunwa, mara baada ya kadi kuingizwa
katika mashine iligoma kufanya muamana, ndipo alipohisi kuwa kuna namna
kadi hizo ‘zinachakachuliwa’, hivyo akalazimika kutumia kadi ya mkewe
Michelle Obama kufanya muamana huo.
Tatizo la
wizi wa kadi za muamana limeathiri watu takribani milioni 100 kwa mwaka
jana, ambapo kusainiwa kwa agizo hilo la rais wa Marekani kutasaidia
katika kuhakikisha usalama wa huduma za muamana na pia kuanzishwa kwa
huduma ya dharura mtandaoni itakayowahudumia watumiaji waliopoteza kadi
zao.
Marekani
ni moja ya nchi zinazotoa huduma za kadi ya muamana ambapo mtumiaji wa
huduma hiyo anakuwa na uwezo wa kupata huduma za malipo ya baada kwa
manunuzi ya bidhaa na huduma mbali mbali.