Monday, September 8, 2014

MSHITAKIWA WA UGAIDI AONYESHA ALIVYOLAWITIWA NA POLISI MAHAKAMANI


MMOJA wa watuhumiwa wa ugaidi katika kesi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), amevunja ukimya mahakamani baada ya kuonyesha suruali ilivyolowa kwenye makalio akisema ni madhara ya kulawitiwa na kuingizwa miti na polisi.
Mshtakiwa huyo, Salum Ally Salum, aliamua kufanya hivyo jana ili kuithibitishia mahakama kile walichodai ni unyama waliotendewa na polisi wakati wakihojiwa.

“Mheshimiwa hakimu, angalia (anageuka na kuinua suruali katika eneo la makalio), haya ndiyo madhara niliyopata kwa kuingiliwa nyuma na kuingizwa jiti,” alidai.

Baada ya mshtakiwa huyo kuzungumza, Hakimu Hellen Riwa alimshauri kutoa taarifa kwa uongozi wa Magereza ili aweze kupata matibabu ya haraka kwani akiendelea kukaahivyo anaweza kupata madhara makubwa.

MBUNGE WA NZEGA AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA MWAKANI.


1Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya serikali za Mitaa na Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangallah akiwasili katika hoteli ya Hyyat Kilimanjaro kwenye mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ambapo leo ametangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao 2015, Dk. Khamis Kigwangallah ameongozana na mke wake Dr. BayoumAwadh na watoto wake Sheila ambaye ni mkubwa Hawa na HK Junior
Mbunge wa Nzega CCM Dr. Hamis Kigwangalla,  akitangaza rasmi nia yake ya kugombea Urais kupitia tiketi ya CCM mwakani 2015
 amesema kutokea kuuza karanga na biggee mtaani mpaka kuwa Doctor Mbunge na Kiongozi wa CCM Taifa na kufikia na ndoto ya kutegemea kugombea Urais ina maana moja tu kwamba sera za CCM zina tija kwa Taifa na wananchi wake na yeye ni mfano wa kwanza mkubwa wa kuaminiwa kwamba sera hizo zinajali usawa kwa wananchi kwani pamoja na kupitia yote aliyopitia bado anaweza kutuhubutu kugombea Urais wa Tanzania kwa kukubaliwa na kuruhusiwa kikatiba na chama chake CCM na kuruhusiwa kisheria na Sheria za Jamhuri ya Tanzania.










MSICHANA ANAYEDAI KUBAKWA NA MUME WA FLORA MBASHA AELEZA MAHAKAMANI JINSI ALIVYOBAKWA


Na Francisca Emmanuel.
SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya ubakaji inayomkabili mume wa mwimbaji wa muziki wa injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) ameieleza mahakama jinsi alivyobakwa akiwa kwenye gari na nyumbani kwao. 
Shahidi huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni shemeji wa Mbasha, alidai mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago kuwa Mei 23 mwaka huu, Mbasha alimbaka kwa mara ya kwanza wakati mkewe Flora akiwa hayupo.
Alidai siku hiyo, Flora na mumewe walitoka kwenda kufuatilia CD za video zao za nyimbo huku mtoto wao (jina tunalo) akiwa shuleni.
Alidai alishangaa kuona ghafla Mbasha alirudi nyumbani peke yake na kumlazimisha kufanya mapenzi kisha alimtukana na kumtishia kumdhuru endapo atatoa siri.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, shahidi huyo aliendelea kudai kwamba Mei 25 mwaka huu, siku ya Jumapili walikwenda kanisani na waliporudi Mbasha alilalamika kuwa ana njaa hivyo alimpa fedha kununua chipsi.
Alidai baada ya kula, Mbasha alimwambia waondoke nyumbani kwenda kumtafuta Flora ambaye hakuwepo nyumbani siku hiyo.

“Tulipanda gari aina ya Toyota Ipsum, wakati tupo njiani aliniambia nikae kiti cha mbele pamoja naye kwani nilikuwa nimekaa kiti cha nyuma. Nilikubali kukaa katika kiti hicho ndipo aliniambia kuwa ananipenda hivyo tufanye mapenzi kwani nimeshazoea,” alidai shahidi.
 
Aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kukubali kukaa katika kiti cha mbele, Mbasha alipandisha vioo vya gari na kulaza kiti alichokuwa amekalia mtoto huyo na kuanza kumvua sketi yake na nguo za ndani.

Pamoja na hayo alimkaba shingo na kumziba mdomo kwa khanga ili asipige kelele na kumbaka kwa mara nyingine.

Shahidi huyo alieleza kwamba baada ya kitendo hicho kuisha, Mbasha alishuka kwenye gari na kumuacha dada huyo akiwa ndani ya gari na aliporudi alimtaka waendelee kufanya mapenzi kitendo ambacho mtoto huyo alikataa.

Hata hivyo, alidai baadaye alimtafuta Flora kwa simu na alipopokea hakumwambia kilichotokea hadi alipofika Sinza kwa dada zake ambako walimweleza Flora kwa njia ya simu kitendo alichofanyiwa na mumewe, huku akiwa haamini kilichotokea.

Alidai walitoka pamoja na dada zake kwenda kuripoti katika kituo cha Polisi cha Sinza na polisi waliokuwepo kituoni hapo waliwaamuru kutoa taarifa hizo katika kituo cha polisi ambacho tukio la ubakaji limetokea.

Hivyo walirudi hadi kituo cha Polisi cha Tabata na kutoa taarifa.

Kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu cha sheria za mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kinaeleza kuwa mashauri yote ya ubakaji yanatakiwa kusikilizwa katika mahakama ya siri.

Wakili Katuga aliiomba mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo katika mahakama ya siri kwa kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18 na hairuhusiwi mtu yeyote asiyehusika kusikiliza mashauri hayo. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 12 mwaka huu.

Mbasha anashitakiwa kwa mashitaka mawili ambayo Mei 23 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala, alimbaka mtoto wa miaka 17 nyumbani kwake. Pia alidaiwa Mei 25 mwaka huu, alimbaka tena mtoto huyo ndani ya gari kinyume na sheria.