Monday, August 25, 2014

THE LEGENDS REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO


 Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye nembo ya TANAPA na Real Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
 Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara fupi. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Elinas Palangyo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devota Mdachi, Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete na Afisa Utalii Antipas Mgungusi.
 Wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid pamoja na wenzi wao wakiwa Hifadhi ya Kilimanjaro.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro
 Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.
 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

KIJANA ACHOMWA MKUKI WAKIGOMBEA SHAMBA

MAPIGANO yakurushiana mishale,mawe na marungu yanayohusishwa na kugombea ardhi, yameibuka kati ya wananchi wa Kijiji cha  Sirorisimba wilaya ya Butiama na Kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda mkoani Mara na kusababisha baadhi ya wananchi kujeruhiwa kwa kuchomwa mishale na kukimbia makazi yao.


Tukio hilo limekuja kufuatia madai ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina ya vijiji vya wilaya hizo mbili huku ukimya wa viongozi wa wilaya ukitajwa kuwa chanzo cha kuibuka kwa mapigano hayo.


Wakiongea na Blog hii baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sirorisimba  wilaya ya Butiama mkoani Mara wamesema mgogoro huo umeanza miaka mingi iliyopita ambapo wananchi kutoka kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda wamekuwa wakivamia wananchi wa kijiji hicho lakini mpaka sasa hakuna hatua zinazochukuliwa na viongozi wa wilaya hiyo.

Walisema uvamizi wa maeneo makubwa uliofanywa hivi karibuni katika eneo hilo umesababisha mapigano makali na kusababisha mtu mmoja kuchomwa Mshale mgongoni na kulazwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.

Mmoja wa majeruhi aliyechomwa mshale kwenye tukio hilo na kulazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Hamisi Nyahanga amesema  alivamiwa kwenye eneo lake la kilimo na wananchi na kuambiwa siku zake za kuishi zimekwisha na kuamua kukimbia ndipo alipopigwa mshale wa mgongo .

KIJANA AFARIKI DUNIA WAKATI AKIFANYA NGONO NA KAHABA

Kijana mmoja Nchini Malawi, Fletcher Jere (26) amefariki Dunia kutokana na kuzidiwa utamu wakati akifanya ngono na kahaba mmoja mjini Blantyre.

 

Gazeti la Daily Times nchini Malawi limeripoti kuwa kijana huyo alinunua kahaba huyo maeneo ya Ndirande katikati ya jiji la Blantyre.


Afisa wa Polisi mjini Blantyre Bi.Edina Ligowe (pichani) amesema kuwa Bw. Jerre alikufa kutokana na kuwa na hisia za juu sana pamoja na kuhisi utamu uliopitiliza wakati akifanya Ngono na Kahaba huyo (sexual excitement and sweetness).
Aidha Afisa huyo amesema kuwa kahaba huyo hatofunguliwa Mashtaka yoyote kwa sababu hakuna kosa alilofanya kwa yeye kuwa mtamu kupitiliza. 
 She committed no crime by being too sweet to the man
 
 


SIR CHANDE: NILIVYOPATA UONGOZI FREEMASON


Hekalu la Freemasons lililopo katika Mtaa wa Sokine jijini Dar es Salaam
Wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.
Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.
Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.
Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.
Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.
Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.
Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.
Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.
Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.
“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.
Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.
Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.
Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.
Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”
Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.
“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.
Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.
Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Kanuni za Freemason zinafundisha nini?
Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.
“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.
Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.
Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki
Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.
“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:
“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.
Chanzo;Mwananchi

WABUNGE WA CCM WAWASHA MOTO HUKO MTERA MKOANI DODOMA



IMG-20140824-WA0005
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi katika kijiji Iringa Mvumi Jimbo la Mtera mkoani Dodoma ambapo Chama cha mapinduzi kimeendelea kuuelimisha umma juu ya masuala ya Maendeleo, utekelezaji wa ilani, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa, bunge la katiba na mambo yanayohusu maendeleo ya katika vijiji na wilaya zetu.
Pia kuwakumbusha juu ya thamani ya muungano wetu na vipengele muhimu vinavyojadiliwa ndani ya katiba.
IMG-20140824-WA0006
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kutema cheche katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0007
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo ukiwasikiliza wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania waliokuwa wanahutubia katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0008
Mbumge wa ji,bo la Sikonge Mh. Said Mkumba akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0010
Wananchi wakisikiliza kwa makini Mbunge wa Chalnze Ridhiwani Kikwete alipokuwa akiwahutubia
IMG-20140824-WA0011
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.
IMG-20140824-WA0012
Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera , Asumpta Mshana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Iringa jimbo la Mtera jana nyuma ni mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde
IMG-20140824-WA0013
Baadhi ya wananchi wakiwa wamekaa kwenye mapaa y nyumba huku wakifuatilia kutano huo.
IMG-20140824-WA0014
Umati wa wananchi aliohudhuria katika mkutano huo.
IMG-20140824-WA0015
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.
IMG-20140824-WA0017
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akipanda jukwaani kuwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma baada ya mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete kuwahutubia.
IMG-20140824-WA0019 IMG-20140824-WA0020
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiendelea kutema cheche mbele ya wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.

KESI YA KIFO CHA KANUMBA SASA KUSIKILIZWA BALAZANI ELIZABERTH MICHAEL HALI TETE



Staa wa sinema za Kibongo, Lulu Elizabeth Michael, 'Lulu".
 
WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba watu wengi wana kiu ya kujua kinachoendelea katika kesi hiyo ambapo ilidaiwa kwamba imehamishwa eneo la wazi (open) na kusikilizwa kimyakimya katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, huku usikilizwaji wa kesi hiyo ukiwa tofauti kama ilivyozoeleka.
Kwa mujibu wa shushushu wetu anayependa kufuatilia maisha ya mastaa wa tasnia tofautitofauti Bongo ndani ya mahakama hiyo, chombo hicho cha kusimamia sheria kimeamua kubadili aina ya usikilizaji wa kesi hiyo.
Wakili maarufu Bongo anayemtetea 'Lulu', Peter Kibatala.
 
YAHAMISHIWA BARAZA LA KESI ZA MAUAJI
Habari zilieleza kwamba, kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa kwenye kikao cha baraza la kusikiliza kesi za mauaji kwenye mahakama hiyo, kwa lugha ya kigeni kinaitwa High Court Murder Session.
“Kama ukienda pale mahakamani ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, huwezi kufanikiwa kupata chochote kwa sababu ipo kwenye baraza la kusikiliza kesi za mauaji yaani High Court Murder Session ambalo huwa linasikiliza kesi kimyakimya tofauti na kesi nyingine zinazosikilizwa kwenye kizimba,” kilisema chanzo chetu hicho.

ETI LULU HAJUI KINACHOENDELEA
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba wakati hayo yakiendelea kortini hapo, aliyekuwa mwandani wa Kanumba aliyekuwa naye chumbani siku ya kifo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hajui chochote kinachoendelea na wala hajaitwa mahakamani.
“Tangu imeanza kusikilizwa hakuna siku Lulu ameitwa na sidhani kama anajua kinachoendelea.
“Labda anayejua kinachoendelea ni mama Kanumba (Flora Mtegoa) ambaye hupenda kuulizia kuhusu hatima ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.
WAKILI KIBATALA ANASEMAJE?
Baada ya kujikusanyia data hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta wakili maarufu Bongo anayemtetea Lulu, Peter Kibatala ili kupata ufafanuzi wa aina hiyo ya usikilizwaji wa kesi ya mteja wake ambapo alifichua siri hiyo juu ya kesi ya kifo cha Kanumba.
Wakili Kibatala alikiri kwamba kesi ya kifo cha Kanumba ambayo Lulu ni mshitakiwa wa kwanza akituhumiwa kuua bila kukusudia, imebadilishwa aina ya uitwaji huku akigoma kuingia kiundani kwani bado kesi hiyo ni mbichi na hairuhusiwi kwa wakili kuzungumza nje ya mahakama.

Aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ enzi za uhai wake.
“Ni kweli inaitwa hivyo, huyo aliyekueleza hajakosea na tunategemea mwezi huu wa nane kikao cha baraza hilo la usikilizaji kitaendelea lakini nisingependa kuongea sana kwani mimi siyo msemaji wa Lulu bali ni wakili na si maadili ya kazi yangu kuzungumza nje ya mahakama. Hata Lulu haruhusiwi kuzungumza chochote nje ya mahakama,” alisema Kibatala aliyewahi kuwa wakili wa mwigizaji Kajala Masanja na mwanahip-hop, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.

TUMGEUKIE LULU
Mwanahabari wetu alipomtafuta Lulu ili kujua kama anajua chochote juu ya kesi hiyo, mkali huyo wa sinema za Kibongo aligoma kuzungumza chochote kama aliyoelekezwa na wakili wake, Kibatala.

TUJIKUMBUSHE
Kanumba aliyewatoa mastaa wengi wa filamu unaowaona kwa sasa, alifariki dunia April 7, 2012 nyumbani kwake, Vatican-Sinza jijini Dar. Kifo cha Kanumba kilidaiwa kwamba kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.