Sunday, July 12, 2015

RAIS KIKWETE AMSHUKURU ALLAH KWA MCHAKATO KWENDA SALAMA BILA MPASUKO.



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Katika Mkutano Mkuu uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli amechaguliwa kwa kura 1560 akifuatiwa na Asha-Rose Migiro aliyepata kura 702 huku Balozi Amina Salum Ali akipata kura 349.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Dk. Magufuli amepita kwa kura hizo kutokana na nguvu yake dhidi ya wagombea wengine.
“Hakukuwa na namna hapa kwa kuwa, wajumbe wanaamini katika mazingira haya magumu ya upinzani Dk. Magufuli anaaminika na kukubalika nje kuliko hawa wengine,” anasema mtoa taarifa na kuongeza;
“Baada ya kutemwa Membe (Bernard Membe) kwenye NEC kila mjumbe ambaye alikuwa upande wa Lowassa (Edward Lowassa) alipumua jambo lililomrahisishia Magufuli.”
Mkutano huo umehairishwa mpaka saa nne asubuhi, ambapo ndiyo muda ambao Dk. Magufuli ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na Waziri wa Ujenzi atatangazwa rasmi kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho.
Awali ndani ya ukumbi wa mkutano, kulidawa kuwepo kwa mpango wa wafuasi wa Lowassa kutaka kumpitisha Balozi Amina ili chama hicho kipate changamoto katika ‘kumuuza’ kwa wananchi ikiwa ni kulipiza kisasi kwa kukatwa mtu wao (Lowassa).
Katika Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, majina yaliyopitishwa yalikiwa ni Migiro, Magufuli, Balozi Amina, Membe na January Makamba.
Katika Halmashauri Kuu ya CCM yalipita majina matatu ya Dk. Magufuli, Dk. Migiro na Balozi Amina.



WAKATI CHAMA TAWALA WAKIFANYA UTEUZI, UKAWA WASHIRIKI FUTARI YA PAMOJA


  • Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa akishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Kushoto kwake ni Mbunge wa CUF, Ali Khamis Seif (Mkoani) na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa NLD Zanzibar, Ahmad Hemed.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed (katikati) pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy (kushoto) huku wakishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
Baadhi ya Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutoka kushoto, Naomi Kaihula (Viti Maalum CHADEMA), Salum Baruan (CUF- Lindi Mjini) na Mohamed Habib Mnyaa wakishiriki futari iliyoandaliwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA (Summit) kilichojadili mikakati mbalimbali ya maandalizi ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.(VICTOR)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini),Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni) na Mama Riziki.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Vioingozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini) na Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni).

MZEE KINGUNGE ATOA YAKE YA MOYONI MJINI DODOMA



MWANASIASA mkongwe nchini, mzee Kingunge Ngombale Mwiru, amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutofanya dhihaka ya kumpendekeza kada yoyote kuwa mgombea wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwani kwa kufanya hivyo kitaanguka.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma Jumatano Julai 8, 2015, Kingunge ambaye ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na ndani ya chama hicho alisema “ninatishwa na watu wanaotumia nguvu nyingi kwelikweli kupambana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama, badala ya kuelekeza nguvu hizo kupambana na wapinzani wetu, hii ni hatari.’, alionya
Amesema, CCM ni lazima ifuate katiba yake ili wajumbe wanaotarajiwa kutoa maamuzi watoe maamuzi sahihi na sio kupindisha katiba kwa kuanzisha utaratibu ambao sio utamaduni wa kidemokrasia.
“kuna kiongozi mmoja anasema, kada yeyote wa chama hicho aliyeomba kuteuliwa kuwania urais, endapo jina lake litakatwa hatakuwa na nafasi ya kukata rufaa, hii haijawahi kutokea na wala haipo kwenye katiba yetu.’ Amesema Mzee Kingunge.
"CCM lazima imteue mtu anayekubalika ndani na nje ya chama ili chama kiweze kushinda, kinyume na hapo, hii ni njama ya kukifanya kishindwe kwenye uchaguzi".

Hivi karibuni Katibu wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa hakutakuwa na nafasi ya kada wa chama hicho atakayeenguliwa kwenye mchujo kuweza kukata rufaa, kwani hakuna kanuni inayoelekeza kufanya hivyo.

Hata hivyo Kingunge amepinga kauli hiyo na kusema, inakwenda kinyume cha katiba ya CCM ambayo inaweka bayana kuwa maamuzi ya vikao vya chini yanaweza kukataliwa na vikao vya juu ikiwa ni pamoja na mwanachama ambaye anaona hakutendewa haki kuwa na nafasi ya kupinga uamuzi wa vikao vya chini.