VIONGOZI
WA VUGUVUGU LA KATIBA YA WANANCHI, (UKAWA), WAKIONYESHA HATI YA
MAKUBALIANO BAADA YA KUTIA SAINI JUMANNE NOVEMBA 4, 2014 KWENYE OFISI
ZA MAKAO MAKUU YA CUF, BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM. CHINI YA
MAKUBALIANO HAYO, YALIYOHUSISHA VYAMA VINNE, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI
NA NLD, YATAANZA KUTEKELEZWA KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
UNAOTARAJIWA KUFANYIKA BAADAYE MWAKA HUU AMBAPO, UKAWA UTAMSIMAMISHA
MGOMBEA ANAYEKUBALIKA KWENYE ENEO HUSIKA BILA YA KUJALI CHAMA. HATA
HIVYO MWAKILISHI WA NLD HAKUWEPO NA IKAELEZWA KUWA ATASAINI BAADAYE

Sehemu yamakubaliano ya UKAWA yaliyotiwa saini

Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza kuhusu ushirikiano huo

Katibu Mkuu wa UKAWA, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, akizungumza kwa kutumia nyaraka

Baadhi ya
viongozi wa UKAWA, wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano makao makuu ya
CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam, Jumanne Nov 4, 2014

Kutoka
kushoto, Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, Mwenyekiti wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba, na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia,
wakisaini makubaliano hayo ya UKAWA

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, (Kulia), akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo