Nyumbani
kwa bondia Francis ‘SMG’ Cheka hakuishi pilika ambazo zinatokana na
kazi ya chupa za plastiki anayofanya bingwa huyo wa zamani wa dunia wa
WBF.
Nje
ya nyumba yake kuna mafurushi kila kona yakiwa na ‘bidhaa’ tofauti
ikiwamo chupa za plastiki, chupa za konyagi, chibuku na plastiki ngumu
(ndoo na madumu) yaliyopasuka.
Cheka anavyookota chupa
“Mimi
ndiyo mwanzilishi wa biashara hii hapa Morogoro, niliianza 2004 baada
ya kuamua kuingia mtaani kuokota na kuziuza mwenyewe, wakati huo kilo
moja niliuza kwa Sh100 na nilikuwa nikizunguka kutwa nzima kutafuta
chupa mtaani,” anasema Cheka.
Anasema wakati anaanza kuokota chupa alikuwa na miaka mitano tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa, lakini hakuwa maarufu.
“Nilikuwa
nina uwezo wa kuzunguka na kuokota hadi kilo 100 kwa siku, japo ilikuwa
kazi ngumu, lakini nilipata fedha nikanunua kiwanja maeneo ya
Kilimahewa na kujenga nyumba kwa kazi ya kuokota chupa.
“Pia
niliweza kujiandalia mapambano peke yangu kwa kazi hii, ambayo
yalinijenga na kunipa umaarufu kwenye ngumi, nimejiandalia mapambano
zaidi ya 15 kwa fedha niliyopata kwa kuokota chupa,” anasema Cheka.
Anasema
vijana wengi wa Morogoro walianza kuokota chupa baada ya kuona Cheka
amejenga nyumba kwa kazi hiyo, hivyo hakuwa na hiyana aliwafundisha kazi
hiyo na wengine aliingia nao mtaani kuokota.
“Nilipoanza
kucheza mapambano ya ubingwa wa Afrika nilisimama kuokota chupa
nikawaachia wengine na mimi kuelekeza nguvu zangu kwenye ngumi, kijiwe
changu nikamweka mtu wa kufanya hiyo kazi na nikawa na nanunua kwa watu
wengine kisha mimi nauza tena.
“Kwa
kipindi chote ambacho nilikuwa nimebanwa na masuala ya ngumi, mradi
wangu huu uliyumba kwani kila niliyemwachia alikuwa na fikra za
kuniibia, ilifikia mahali nikakwama kwani nilikopa fedha benki kuongezea
nguvu kwenye biashara yangu ya makopo hivyo nilipaswa kulipa,” anasema
Cheka.
Anavyookota chupa mtaani
“Watu
wanashangaa mtu kama mimi kuokota chupa, lakini ndiyo kazi inayoniweka
mjini, wiki iliyopita nilikuwa Msamvu (stendi kuu ya Morogoro) nakusanya
chupa kwa bahati nikakutana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alishangaa kuniona naokota Chupa.
Credit:Mwananchi.