Tuesday, September 23, 2014

WANANCHI WATAKA KUFANYA MAANDAMANO BAADA YA OFISI YAO KUWEKWA KWENYE KILABU CHA POMBE, RUNGWE,

WANANCHI wa Kata ya Kawetele Tarafa ya Tukuyu mjini wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wanatarajia  kufanya maandamano  ya amani hadi kwenye ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kupinga hatua ya ofisi yao kuwekwa kwenye kirabu cha pombe.
Wakizungumza jana na  Yetu rungwe  blog kwa nyakati tofauti wamedai kitendo cha ofisi ya serikali kuwa katikati ya kirabu cha pombe na kumbi za starehe kimeshusha hadhi ya mji wa Tukuyu ambao ndiyo makao makuu ya wilaya hiyo.
Walida kuwa asilimia ishirini ya wananchi wa kata hiyo ni walokole hivyo wanakosa kupata huduma za kiofisi kutokana na mazingira mabaya ya kiofisi yalivyo hivyo hulazimika kupata huduma za kiofisi kwenye kata za mbali kinyume na taratibu.
Wananchi hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini walisema madai yao yakuomba ofisi kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Veronika Kessy yamegonga mwamba na kudai kuwa wamepanga kufanya maandamano ya amani wakitaka kupatiwa ofisi.
Afisa mtendaji wa Kata hiyo Niklaus Kosama alikiri kuwepo na hali hiyo na kudai kuwa yeye ameletwa kufanya kazi katika kata hiyo  na hana mamlaka ya kupinga ofisi kuwepo mahali hapo.
Anyimike Mwasakilali diwani wa Kata hiyo mbali na kukiri kuwepo kwa hali hiyo pia alidai kuwa alipeleka maombi ya kupatiwa ofisi kwa mwenyekiti wa Halmashauri na mkurugenzi wa halmashauri hiyo  lakini alikuwa akipigwa dana dana
Alisema afisa utumishi wilayani humo alimueleza kuwa amempa barua ya kuhama mtumishi anayeishi nyumba no,RDC/RHB/BLD/08 kuwa mwezi wa 11 mwaka huu mtumishi huyo atahama na nyumba hiyo itafanyika kuwa ofisi ya kata.
 Yetu rungwe  ilimulika   hadi  kwenye nyumba hiyo kujiridhisha kana kwamba ni kweli mtumishi huyo wa Idara ya maji kama kapewa barua ya kuhama,ambapo alikanusha kuwa hajawahi kupewa barua ya kuhama na wala hata kwa mdomo.

Alfredy Mwakipiki mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo kwa upande wake alisema anachokijua ni kuwa wananchi wa kata hiyo walifanya harambee ya kutaka fedha kwa ajili ya ununuzi wa uwanja na wao watawasapoti pindi watakapo jenga hadi mtambaa wa panya.
Alisema Halmashauri ya Rungwe magharibi inakata 20 na imekuwa ikishindwa kujenga kwa wakati ofisi za kata kutokana na bajeti ndogo,hivyo suala la ofisi katika kata hiyo litapewa kipawa mbele pindi wapatapo bajeti.  








































DEREVA WA BODABODA AUWAWA NA KISHA KUPORWA PIKIPIKI MJINI DODOMA


 Tukio hili limetokea eneo la Bonanza kata ya Chamwino, Dodoma mjini. Kwa shuhuda wetu aliyekuwa eneo la tukio  amesema kuwa dereva wa bodaboda amekutwa amefariki  baada ya kuuliwa na watu wasiojulikana  na kisha watu hao kutoweka  bodaboda aliyokuwa akiendesha marehemu huyo. Dereva huyo wa bodaboda  amechomwa kisu maeneo ya tumboni na shingoni katika mwili wake na katika eneo la tukio kumekutwa visu viwili amavyo vinasadikika kutumiwa katika uharifu huo kando kidogo ya barabara na sehemu ulipokuwa mwili wa marehemu.(Picha na Alex wa Pamoja Blog)
 Hiki ni mojawapo ya kisu kinachosadikiwaa kutumika katika kufanya mauaji hayo ya dereva wa Bodaboda na kisha watu hao kutoweka na pikipiki.

AJITOLEA KUONYESHA MWILI WAKE HADHARANI KUWAFUNDISHA WANAWAKE WANAOTUMIA DAWA ZA KUONGEZA MAKALIO

Naitwa naomi, kweli niliposikia kuhusu dawa za kukuza makalio nilienda kuzinunua haraka na kupaka na Kuchoma Sindano Pia ili Kukuza Makalio yawe kama ya Nick Minaj, Mwanzoni nilifurahi kwa kuwa niliona kama vile yanakuwa kweli lakini sasa hivi nimeanza kupata mashimo mashimo pia yanauma sana mpaka yanakuwa mekundu, ukweli yamekuwa mzigo kwangu  Hata sijui Nifanyaje Jamani
Atoa onyo kali kwa wanawake wakitanzania kujikubali vile walivyozaliwa kwani kwake sasa ni mateso 

RAPPER WITNESS APOTEZA MAPACHA KWA UJAUZITO WAKE KUHARIBIKA


Rapper wa kike Witness amepata bahati mbaya baada ya ujauzito wake wa miezi nane na nusu kuharibika.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Witness ameeleza kuwa alikuwa anatarajia mapacha na alikuwa katika hatua za mwisho lakini ghafla ikatokea hali hiyo ambayo hadi sasa inafanyiwa uchunguzi na madaktari kubaini chanzo.


“Kuna mambo ambayo niliambiwa kwamba endapo ningekuwa sina mazoezi au ningekuwa siko strong ina maanisha kwamba na mimi mwenyewe ningekuwa hatarini.” Amesema Witness.

Ameeleza kuwa hali hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita lakini yeye na mchumba wake Ochu waliamua kukaa kimya kwa muda hadi leo walipoamua kuiweka wazi.

Akiongelea afya yake, member huyo wa zamani wa WAKILISHA ameeleza kuwa hivi sasa anaendelea vizuri.

Tunampa pole kwa tatizo hilo lililomkuta na tunamuombea awe na afya njema kama zamani.

PATRICK NGOWI NA DK MENGI WAIBUKA NA TUZO ZA WAFANYABIASHARA BORA AFRIKA

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, ameibuka mshindi wa tuzo mbili kwenye fainali ya shindano la kuwania Tuzo ya Mwaka ya Mfanyabiashara Bora Afrika (AABLA) kundi la Afrika Mashariki.

Sherehe za kutoa tuzo hizo zilifanyika jijini Nairobi, Kenya Jumamosi iliyopita.


Dk. Mengi alitunukiwa Tuzo ya Mfanyabiashara Bora Afrika kwa mwaka 2014, kutoka kundi la Afrika Mashariki. Majaji wa shindano hilo pia waliamua kumtunuku Tuzo ya Maisha ya Mafanikio kwa kuongoza katika suala la uwajibikaji kwa jamii.


Dk. Mengi ambaye pia liingia kwenye kurasa za gazeti maarufu la Forbes Africa la Julai mwaka huu wa 2014, amekuwa akichangia sehemu kubwa ya muda na rasilimali zake kwa ajili ya kufadhili kazi zinazogusa maisha ya jamii.


Kwa upande wa Tuzo ya Kijana Mfanyabiashara Kiongozi wa Mwaka, tuzo hiyo ilienda kwa Patrick Ngowi, CEO wa Helvetic Solar anayeongoza kampuni inayokua kwa kasi kwenye mtandao wa nishati mbadala katika ukanda wa Afrika Mashariki.


Anaongoza wafanyakazi zaidi ya 300, akichangia kwenye ukuaji na maendeleo yanayolenga mipango ya kibiashara katika taifa la Tanzania na ukanda mzima wa eneo hili.

PRODUCER MAN WALTER APATA MKE


 


Producer Man Maji Man Water ambalo jina lake kamili ni John Vomo Shariza Siku ya Jumamosi tarehe 21 Septemba 2014 katika kanisa la KLPT Kigamboni jijini Dar es salaam alifunga ndoa na mke wake aliyejulikana kwa jina Matilda Jimmy Igoti katika ukumbi wa Karimjee Hall jijini Dar es salaam,Zitazame picha za kilichojiri kwenye hafla hiyo 


 
 
 
 
 




 
 
 


 
 
 
 
 


KIJANA AFUMANIWA NA MWANAFUNZI WA KIUME GESTI

Njemba aliyekutwa na denti akipanda kwenye difenda.
“Mwanzo tulifikiri anakuja na vijana hao kama marafiki zake wa kawaida lakini tukaingiwa na wasiwasi baada ya kugundua kuwa alikuwa akilala nao kwa kuwabadilisha,” alisema meneja huyo.
Alidai kwamba Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 usiku, kijana huyo alitinga tena kwenye gesti hiyo lakini alikuwa peke yake na kupewa chumba kama kawaida.
“Wahudumu waliniambia kuwa jamaa amefika tena na amechukua chumba cha juu lakini safari hii alifika peke yake, ilinishangaza sana kusikia kaja peke yake kwani siyo kawaida yake so sikuamini,” alieleza meneja huyo.
Alidai kwamba asubuhi ya Jumatatu, mishale ya saa 4:00, wahudumu walisikia miguno ndani ya chumba alicholala njemba huyo ndipo wakakifunga kwa nje kisha kuita polisi na vijana wa OFM ambao walifika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’.
Meneja huyo alisema kuwa hafahamu njemba huyo alimuingiza kijana huyo muda gani kwani walimuwekea mtego siku nyingi akawa anachezwa na machale.
Hata hivyo, Jiji la Dar huwa halina dogo kwani wakazi wa eneo hilo walijazana kwenye gesti hiyo kutaka kumpiga jamaa huyo lakini polisi walifanikiwa kuwatorosha eneo hilo na kuwampeleka Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar.
Hadi OFM inang’oa nanga kituoni hapo, njemba huyo na kijana aliyekutwa naye walikuwa wakiendelea kuhojiwa. Kujua kilichojiri usikose kufuatilia magazeti ya Global.

WAMAREKANI WAFUNGA NDOA MLIMA KILIMANJARO

Managing Director of Zara Tours Company Zainab Ansell who organized the tour of the newly expected couple is seen here happy with the couple in Mount Kilimanjaro.
Choir of St. Clara from Moshi was there to deliver Christians wedding songs during the holly wedding service in Mount Kilimanjaro.
Pastor Aloyce Mbugi (right) from TAG Arusha Victory Christian Centre reading a word of God during the holly wedding service in Mount Kilimanjaro. Left is Mr. Isaya Mwashala who was an interpreter.
The newly expected couple sitting together with their Patron Ansigar Mtandika and Matron Neema Njau.

This is how it started…narrates Kara Lee: “Sometimes back during the last Christmas in Minnesota, United States of America we had an engagement event with my hubby Richard Miller and committed ourselves that the wedding event must be done on the roof top of Africa and this is none other than Kilimanjaro Mountain”.

Thereafter, the duo started planning for this historic and unique event by raising money for their trip to Tanzania and in particular Kilimanjaro Mountain. They also informed their relatives about their plan to have their wedding in Mount Kilimanjaro of which they got a green light from them.