Friday, October 3, 2014

MKE AMMWAGIA MAJI YA MOTO MUMEWE



Mwanamke mmoja katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amemfanyia ukatili mume wake kwa kumwagia maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kupikia ugali.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi wilayani hapa, tukio hilo lilitokea juzi, saa 4:30 usiku, katika mtaa wa Nyamakokoto,  mjini Bunda, baada ya kuzuka ugomvi ulitokana na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) kuchelewa kurudi nyumbani.

 Mwanaume huyo amejeruhiwa vibaya mume wake sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyopelekea kulazwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.
 
Akizungumza na NIPASHE juzi, mwanaume huyo alisema sababu ya mke wake kummwagia maji ya moto ni kumuuliza sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani alirudi saa 4:30 usiku.

Alisema siku hiyo alitoka kazini kwake saa 1:00 usiku na kukuta mke wake ambaye amezaa naye watoto wanne akiwa hajarejea nyumbani huku watoto hawajetengewa chakula.
 
Alisema baada ya kukuta hali hiyo aliamua kuchukuwa fedha na kwenda kununua mboga ili aweze kuandaa chakula cha usiku akijua hawezi kurudi muda huo.

Alisema baada ya kufika saa 4:00 usiku wakati watoto wake wameshabandika maji ya kupikia ugali, aliamua kwenda kwa rafiki wa mke wake ili kuuliza alipo mkewe, lakini walisema hawajamuona.

Alisema aliamua kurejea nyumbani na ilipofika saa 4:30 usiku mwanamke huyo alirejea na baada ya kumuuliza kwanini amechelewa kiasi hicho, alichukuwa sufuria la maji ya moto na kumwagia.

“Tangu nimuowe na kufanikiwa kuzaa naye watoto wanne sijawahi kumpiga licha ya kufanya vituko vya mara kwa mara….sasa aliporejea muda wa saa 4:30 na mimi kumuuliza ni kwani amechelewa kiasi hicho na akijua ni mke wa mtu, hapo ndipo alipochukuwa maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kupikia ugali na kunimwagia” alisema.

Mganga wa zamu katika hospitali ya Bunda, Dk. Bakari Ibrahimu, alisema majeruhi huyo amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa kifuani na mikononi na kwamba anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

VITA YA WABUNGE MAMBO YAWEKWA PEUPEEEEE



Mbunge wa CCM kupitia kadi ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Arusha, Catherine Valentine Magige . IMEFICHUKA! Madai ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Geita, Vicky Paschal Kamata kuwatumia meseji za kashfa wabunge wenzake, Lucy Thomas Mayenga (CCM) na Catherine Valentine Magige (UVCCM)Mkoa wa Arusha sasa mambo hadharani.Kwa mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao warembo wako katika vita baridi ikiendeshwa chini kwa chini kwa Cathy (pichani) na Lucy kudai kwamba wamekuwa wakitumiwa meseji zenye kejeli na kashfa nzito kutoka kwa mheshimiwa Vicky.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, licha ya sababu kutokuwa wazi sana, lakini madai ni kwamba wana bifu linalokimbilia mwezi wa nne sasa.
“Unajua si rahisi wao kuweka wazi bifu lao, lakini wenyewe watakuwa wanajua nini kiini, ukifuatilia utagundua kuwa maisha yao yamekuwa ni ya vikundivikundi, akina Lucy wana kundi lao na Vicky ana la kwake,” kilisema chanzo hicho.
Mbunge wa CCM kupitia tiketi ya Umoja wa Vijana, Lucy Thomas MayengaKWA NINI VICKY?
Chanzo kiliendelea kuanika kwamba, baada ya meseji zinazodaiwa kukosa staha kutumwa na asiyejulikana kwenda kwenye simu za mkononi za Cathy na Lucy, waheshimiwa hao hawakupembua sana mchele, moja kwa moja wanadaiwa kumtaja hasimu wao kwenye vyombo vya dola kuwa huenda anahusika na ‘utundu’ huo. 
POLISI WAFUATILIA MINARA YA SIMU
Duru za kipolisi zinadai kuwa kufuatia waheshimiwa hao kumlalamikia Vicky, wana usalama hao walianza kuchunguza mawasiliano yake ambapo walibaini mambo makuu mawili. 
KWANZA, baadhi ya meseji hizo zilionesha kutumwa kwa kupitia mnara wa simu uliopo maeneo ya bunge. PILI, kuna meseji iliwezeshwa kusafiri kwa nguvu ya mnara uliopo eneo linaloitwa Uwanja wa Ndege ambapo inadaiwa Mheshimiwa Vicky ndiko anakoishi.
 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Geita, Vicky Paschal Kamata SERIAL NUMBER
Pia yapo madai kwamba, polisi hao walikwenda kitaalam zaidi na kubaini kwa kutumika namba zilizomo ndani ya simu eneo la kuwekea betri (serial number) ambazo zilionesha kuwa, laini iliyokuwa ikituma meseji za kuudhi kwa waheshimiwa hao pia imekuwa ikutumia na laini ambayo polisi walimjua mhusika, ingawa wasemaji wake wamesita kuthibitisha. 
POLISI NYUMBANI KWA VICKY
Habari zaidi zinadai kuwa, Jumanne iliyopita, polisi mkoani Dodoma walifika nyumbani kwa mheshimiwa Vicky na kufanya uchunguzi kama wanaweza kupata simu yenye laini iliyoripotiwa na akina Mayenga (pichani) kwamba imekuwa ikiwakashifu kwa meseji lakini hawakufanikiwa kukuta chochote. 
Alipotafutwa Vicky ili kujua undani wa meseji hiyo juzi, simu yake haikuwa hewani. Kwa upande wake Lucy ambaye alidai kutumiwa meseji za matusi katika gazeti moja (siyo la Global), naye simu yake iliita bila majibu, huku Cathy akishindwa kupatikana na kulifanya gazeti hili kuzidi kuchimba kwa kina sakata hili ili kupata mbivu na mbichi na kuzianika bila kusitasita.

POLISI ALIYEMFUNGIA MWANAFUNZI GESTI ASHITAKIWA KIJESHI



TAARIFA tulizozipata mchana huu kutoka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, zinasema jeshi la polisi nchini limemkamata na kumfikisha katika mahakama ya kijeshi askari wake Pc.Godlisen anayetuhumiwa kumtumikisha katika vitendo vya ngono mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Okaoni iliyopo wilaya ya Moshi.
Habari zinasema kuwa,askari huyo ambaye septemba 21 mwaka huu alimfungia kwenye nyumba ya kulala wageni mjini moshi mwanafunzi huyo na baadaye wawili hao kupata ajali mbaya ya pikipiki, aliumia kwenye moja ya bega lake na hivyo kushindwa kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi.
Kaimu kamanda wa liposi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita, pamoja na kukiri kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo, alikataa kuweka wazi kama askari huyo amefunguliwa mashitaka ya kijeshi.
Kamanda Koka amewaambia waandishi wa habari leo kuwa, jeshi la polisi linafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na kwamba kama itabainika,askari huyo atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.
Pamoja na jeshi hilo kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari huyo,taarifa kutoka kwa mmoja wa wazazi wa mwanafunzi hiyo zinadai kuwa,kuna juhudi za makusudi zinafanywa na askari wa jeshi hilo kutaka kukwamisha mashitaka ya kijeshi dhidi ya askari huyo.
Taarifa zinadai kuwa,polisi wa kituo kikuu cha polisi mjini moshi,wanajenga ushawishi kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kutaka kulimaliza suala hilo kienyeji huku hali ya mwanafunzi huyo ikielezwa kuwa mbaya kutokana na miguu yake kuvimba.

WABUNGE WALIVYOJIACHIA JANA BUNGENI

1
2Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba wakishangilia leo mjini Dodoma mara baada ya matokeo ya upigaji kura kuonyesha kuwa Theluthi mbili ya Zanzibar imepatikana.
3Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Anne Makinda akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
4Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, mhe. John Shibuda akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
5Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. John Cheyo akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
6Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Pandu Ameir Kificho akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
7Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Selemani Nchambi akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
8Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
10 (1)Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia alikuwa ni mjumbe wa Buge Maalum la Katiba, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
11Aliyekuwa Makamu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza bunge hilo mjini Dodoma wakati wa ufungaji wa bunge hilo leo 2 Septemba, 2014.
13Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akitoa akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
15Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiwashukuru wajumbe na Watanzania kabla ya kuvunja bunge hilo rsmi leo 2 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
17 (1)Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakitoa maneno ya shukurani kwa wajumbe na Watanzania kabla ya kuvunja bunge hilo rsmi leo 2 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

MKE, MUME WAVUANA NGUO WAKIZICHAPA HADHARANI



Hii ni aibu kubwa! Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu, Kigogo-Luhanga jijini Dar wamenaswa wakiangusha bonge la timbwili barabarani na kusababisha umati wa watu kujikusanya eneo hilo kujionea ‘sinema’ ya bure.Timbwili zito likianza kati ya njemba mmoja anayefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata. Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata kilaji. 
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.
 PICHA ZAIDI>>
Mke akimlia 'taimingi' kumbwaga mume wake kwa mweleka.
MUME ATOKA KIDOGO
Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo wa usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi akute msosi uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’.
Mara Puuuuu...!! wote chini “Sasa akiwa pale baa, alizidi kunogewa na masaa yalizidi kupotea ndipo Zeno alirudi nyumbani na kukuta mlango umeegeshwa na mkewe hayupo huku akisikia harufu kali ya kitu kuungua na kumfanya apige chafya.
“Alipokaa sawa alibaini kuwa maini aliyoleta yalikuwa yameungua na kuwa kama mkaa hali iliyompandisha hasira na kuanza kumsaka mkewe,” kilidai chanzo hicho.
Mume (Bw Zeno) akimburuta mkewe kwa ghadhabu. AMUIBUKIA BAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, Zeno akiwa katika sakasaka yake ndipo alipombamba mkewe kwenye baa hiyo akimalizia ‘kunyonya’ kilevi kikali. ZACHAPWA 
Bila kuuliza, Zeno alimkunja mkewe na kumtoa nje huku akimpa makofi ndipo Mwajuma akaona kama anaonewa hivyo akamvizia mumewe na kumchota mtama ambapo wote walikwenda chini kutokana na kuwa katika hali ya kuzidiwa na kilaji.
Wote wakichukua uamuzi wa kuzima timbwili hilo. LAHAMIA NJE YA BAA
Timbwili hilo liliendelea nje ya baa hiyo ambapo vijana wawili wa mtaani hapo waliofahamika kwa majina ya Haidani na Kulwa walihofia yangeweza kutokea machafuko zaidi wakakimbilia kwa mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Shukuru lakini walimkuta mke wa mjumbe ambaye aliwaambia mumewe alikuwa kazini.
Mke(Bi Mwajuma Mtata) akijaribu kuzuia kupigwa picha na kamera za wanahabari. WARUDI NYUMBANI
Wapenzi hao baada ya kugaragazana vya kutosha ikiwa ni pamoja na kuvuana nguo, mwanaume alianza kumburuza mkewe na kurudi nyumbani kwao ambapo walipofika eneo la Kwamkoma walianza kutifuana tena kabla ya kuamuliwa na wasamaria wema.
Jirani akihoji kulikoni mpaka iwe hivi... ETI WAMEYAMALIZA!
Taarifa tulizozipata wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni juzi, Jumatano, wawili hao walikuwa tayari wameshayamaliza na wanaishi raha mustarehe baada ya kuombana msamaha.