Thursday, August 28, 2014

KURUGENZI WA ZAMANI WA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS), CHARLES EKELEGE ATUPWA JELA MIAKA MITATU KWA KOSA LA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.

Kadhalika, Ekelege anadaiwa kutoa asilimi hiyo ya  punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili  Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage na Kampuni Quality Motors na kulisababishia shirika hilo hasara ya dola hizo.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi  Augustina Mmbando baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na mahakama yake kumuona mshtakiwa bila kuacha shaka ana hatia.

Hakimu alisema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kwamba mshtakiwa kupitia wadhifa wake alifanya maamuzi bila kinyume na sheria za TBS zinazomwelekeza kuwasilisha masuala yote ya kiutendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi.

Alisema kitendo cha kutoa msamaha kwa kampuni hizo bila kuacha shaka moja kwa moja mahakama imeona alitumia madaraka yake vibaya.

“Kwa upande wa  shitaka la pili, kiongozi yeyote katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapokuwa madarakani ni kwa ajili ya maslahi ya taifa, lakini mshtakiwa alikosa uzalendo na kutumia madaraka yake vibaya kuhujumu uchumi” alifafanua hakimu kuhusu ushahidi wa Jamhuri.

 “Mahakama inamuona mshtakiwa ana hatia katika kosa hili la pili la kujumu uchumi … pia mshtakiwa amesababisha watanzania waliompa dhamana kukosa kula keki ya taifa lao kwa kujinufaisha yeye binafsi” alisema hakimu huyo na kuongeza kuwa.

“Katika ushahidi uliotolewa na mshtakiwa alikiri kufanya maamuzi bila kupata baraka na kibali cha Bodi ya Wakurugenzi na kwamba aliidanyanya mahakama” alisema Hakimu Mmbando.

Akifafanua zaidi alisema mshtakiwa alidai kuwa katika kutoa maamuzi pinguzo kwa kampuni hizo alishirikisha menejimenti na kwamba shirika lilikuwa na utaratibu wa kufanya kikao kila siku asubuhi.

Hata hivyo, shahidi wa pili wa utetezi Thomas Mlugulu alishindwa kuieleza mahakama wajumbe waliokuwa wakihudhuria kikao cha cha asubuhi cha shirika kwa kila siku zaidi ya kumtaja Betwel Matemba ambaye alishakufa na hawezi kufika mahakamani.

Alisema ushahidi wa utetezi ulikuwa dhaifu kushindwa kukanusha ushahidi wa Jamhuri ulioweza kuithibitishia mahakama ukweli kuhusu mashitaka yanayomkabili Ekerege.

Hakimu alisema mahakama pia inamtia hatia mshtakiwa kwa shitaka la tatu la kuisababishia serikali hasara ya dola hizo na kuwasababishia watanzania kukosa kula keki ya taifa lao.

Hakimu Mmbando alitoa nafasi kwa mawakili wa pande zote mbili kutoa hoja kabla ya kusoma adhabu.

Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Janeth Machulya, alidai kuwa kulingana na makosa aliyotiwa hatiani mshtakiwa kwamba alipewa dhamana na rais pamoja na watanzania lakini aameshindwa kuwa mzalendo.

“Kwa kuwa mshtakiwa ameshindwa kuwa mzalendo kwa mamlaka aliyopewa na wananchi, tunaomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa vigogo wote wanaopewa madakara na kuyatumia vibaya,” alidai na kuongeza.

“Mheshimiwa kwa kosa la uhujumu uchumi mahakama izingatiee utoaji wa adhabu kulingana na sheria ya kosa hilo inavyoelekeza” alisema Machulya aliyeongoza mashahidi wa Jamhuri katika kesi hiyo na mahakama kumtia hatiani kigogo huyo.
Wakili wa utetezi Majura Magafu alidai kuwa mahakama imuonee huruma mshtakiwa kwa sababu ana familia inamtegemea.

Pia, wakili huyo alidai kuwa mshtakiwa anajutia makosa aliyofanya na kwamba  akipewa nafasi hawezi kurudia.
Hukumu hiyo iliyoanza kusomwa saa 6:20 mchana hadi saa 8:10 hakimu aliahirisha kwa nusu saa kabla ya kusoma adhabu.

Saa 8:49 mahakama iliyoketi chini Hakimu Mmbando ilianza shughuli zake.

Akisoma adhabu hiyo, hakimu alisema Viongozi wote wa serikali wako juu kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa ili kulinda na kuangalia nchi na mali zake, siyo kuongoza kwa matakwa ya kiongozi husika.

“Mshtakiwa unastahili kuhukumiwa ili kuwa mfano kwa viongozi wengine wanaochezea keki ya taifa hili kwa manufaa yao binafsi… unakwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kwanza, mwaka mmoja kwa kosa la pili na mmoja mwingine kwa kosa la tatu na ailipe serikali fedha alizoisababisha hasara” alisema Hakimu Mmbando.

Baada ya hukumu kusomwa;
Mshtakiwa alianza kububujikwa na machozi huku watu wanaodaiwa kuwa familia yake wakiangua vilio kwa sauti wakati mpendwa wao akiwa chini ya ulinzi tayari kwenda gerezani kuanza kutumikia kifungo.
Watu mbalimbali waliokuwa katika viunga vya mahakama hiyo walimzunguka mshtakiwa huyo huku kila mmoja akisema lwake’jamani jela ni jela’ wengine ‘tatizo hizo fedha alizoambiwa alipe anazo au alishakula zote’ walisikika wakizunguma.

Mapema Mwaka 2012, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami aliondolewa katika wadhifa huo kutokana na kashfa ya kutoa punguzo la tozo na baadaye Mei 21, mwaka 2012, mshtakiwa alisimamishwa kazi kama Mkurugenzi wa TBS ili kupisha uchunguzi na hatimaye jana kuhumiwa.

Katika kesi ya msingi, Ekelege anadaiwa kuwa kufanya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa kampuni hizo mbili.

Pia, ilidaiwa kuwa Machi 28, mwaka 2008 na Agosti 7, mwaka 2009, katika ofisi za TBS zilizopo wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa nia ovu Ekerege alitumia madaraka yake vibaya.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa punguzo la asilimia 50 ya ada ya utawala kwa kampuni hizo bila idhini ya baraza la utendaji la TBS kinyume cha sheria namba 2 kifungu kidogo cha (3) ya TBS ya mwaka 2005.

Ilidaiwa kuwa kitendo hicho kiliziongezea kampuni hizo faida ya Dola 42,543 za Kimarekani sawa na (kwa wakati huo) Sh. Milioni 68,068,800.

Upande huo wa Jamhuri ulidaiwa shitaka la pili, katika tarehe na mahali pa tukio la kwanza, mshtakiwa alilisababishia shirika kupata hasara ya fedha hizo.
 Charles Ekelege akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo ambapo alihukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kulipa faini ya sh.milioni 68.
 Hapa Ekelege akiwa amekaa nje ya Mahakama hiyo na familia yake  kabla ya kuhukumiwa. 
 Ekelege akiteta jambo na familia yake akiwa Mahakamani hapo.
 Askari polisi akiwa na familia ya Ekelege (wa pili kulia), wakati akitoka kwenye mahakama hiyo.

TOTO ABAKWA NA KUUAWA KINYAMA HUKO SHINYANGA


Mazishi ya mwanafunzi aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga yamefanyika katika makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga.
Mwanafunzi huyo  aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa Agosti 25 mwaka huu saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Akizungumza wakati wa mazishi ya mwili wa marehemu  yaliyofanyika LEO MCHANA naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila alilaani kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto huyo huku akiitaka jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahusika wa mauaji hayo.
“Kifo cha mtoto huyu ni mapenzi ya mungu yaliyosababishwa na wanadamu wabaya,naomba suala la hili lifuatiliwe hatuhitaji siasa katika hili inauma sana kwani vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinatishia amani Shinyanga”,alieleza Nkulila.

 Kwa upande wake Intelijensia mkoa wa Shinyanga Bundala Maige alisema suala la ulinzi kwa watoto ni jamii nzima na kwamba wahalifu wako ndani ya jamii hivyo kuitaka jamii kuwafichua wahalifu hao ili kukomesha vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani Shinyanga.


Naye mwenyekiti wa mtaa wa Masekelo kata ya Masekelo yalikofanyika mazishi ya mtoto huyo bwana Peter Juma Kitundu alisema kifo cha mtoto huyo kinatia simanzi kubwa kwani kimesababishwa na binadamu huku akiiomba serikali kulifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo  na lisiingizwe suala la siasa.

Kwa upande wake mwinjilisti  Emmanuel Donald Kaswalala aliyeendesha ibada ya mazishi alilaani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watotot huku akiiomba jamii kumrudia mwenyezi mungu kwa kuondokana na matendo mabaya.

AGEUKA KUWA KICHAA KWA KUVAMIWA NA MAJIPU BAADA YA KUPIGIWA SIMU NA WATU WASIO FAHAMIKA

Na Baraka lusajo, Mbeya.
Binti mmoja mkazi wa  kijiji cha Ntete  kata ya lufingo wilayani Rungwe mkoani  mbeya Nelu  mwakasuri   ameingia katika wakati mgumu  baada ya  kupigiwa simu  na mtu /watu wasio fahamika na kugeuka kuwa  kichaa  kwa  ghafla.
 Akisimulia   kwa masikitiko makubwa   mama  mzazi wa binti huo  Eda  Nsiani alisema tukio  hilo la kuskisikitisha lilitokea   majila ya  sanane ya   usiku wakati  binti yake akiwa amelala   chumbani  kwake na mtoto wake  mwenye  umri wa mwezi mmoja na kushangaa  baada  ya  binti  yake  kuanza  kupiga makelele  ya kuomba msaada  akisema’’  Nisaidieni  nisaidieni   mwenzenu  nimepigiwa  simu sasa hivi  na mtu au  watu wasio fahamika lakini  sikio limeanza kuniuma kwa ghafla na  nahisi  kichwa changu  kung’oka nisaidieni tafadhar’’ alisema  mama mzazi,
 Alisema  baada  kufika  chumbani   kwake  nilikuta  binti  yangu akijitupa huku na kule ambapo  baada ya hali hiyo kuzidi kuchukua  sula mpya  niamua  kuchukua  hatua  ya  kuwaita  watumishi wa mungu   ambao walifika  muda  mfupi   na kuanza  kufanya maombi  usiku  mzima  lakini  pamoja na kufanyiwa  maombi   kote  bado hali iliendelea  kuwa  mbaya kupita  kiasi  kwani ilipo timu majila  ya  asubuhi niliamu kumwachia huru, lakini  cha kushangaza  nilikuta  akinza kukimbilia barabarani  na huku  akisema  anatafutwa  na  ndugu zake  kuzimu na kusema   ukichana  na kukimbilia  barabarani  mda  mwingine  anakuwa akichukua  kisu akitaka  kujiua  mwenyewe  na kupelekea  kumfungia ndani wakati  wote akiwa amefungwa  na kamba.
   Alisema   baada ya kukumbwa  na hali  hiyo     baada ya muda mfupi alianza  kuvamiwa na majipu  ya ajabu  kuzunguka  mkono wake wa  kushoto   ambao mpaka sasa  umevimba   vibaya kutokana na kuvamiwa na majipu hayo.
 Kwa  upande  wa wakazi wa maeneo hayo  walisikitishwa  na hali hiyo na  ukizingatia  kuwa  ni  tukio la  kwanza  kujitokeza kijijini hapa  na  kuwaomba  watumishi wa mungu kutoka  sehemu mbalimbali kufika  katika  eneo hilo kwa  lengo  kumuona  mgonjwa  mwadhirika  wa tukio hilo  ikiwa ni pamoja  na kumfanyia  maombi ili waweze kurudi katika  hali yake  ya kawaida. 



WAHAMIAJI HARAMU KUMI NA WATOTO 3 WAKAMATWA KAHAMA


picha wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji wilaya ya kahama baada ya kukamatwa kituo cha basi
Afisa wa uhamiaji akichukuwa maelezo kwa muhamiaji haramut tengemea Benjamini ofisi za uhamiaji
IRene mkazi wa ngara ambaye moja wa tanzania ambaye anajiushisha na kukaa na wahamiaji haramu na mtoto khadija 8 miaka ambaye ni Raia wa Burundi anayefanya naye kazi kwake.
Baadhi ya wahamiaji wakiwa chini ya ulinzi katika ofisi za uhamiaji kahama baada ya kukamatwa.
Mtoto khadija akiwa na mtoto wa Ireni stephen ambaye amembeba kwa ajili ya kumlea mtoto huyo.
Irene akiwa na watoto wake wawili na mfanyakazi wake wa watoto wake khadija ofisi ya uhamiaji kahama kwa mahojiano.
Irene akiwa na afisa wa kike ofisi za uhamiaji kahama na watoto wake baada ya kukamatwa kituo cha mabasi.
Irene akihojiwa na kamishina wa uhamiaji Zakaria Misana ofisi kwake kwa kosa la kukaa na mtoto wa miaka 8 kumfanyisha kazi kinyume na sheria. 
kamishina wa uhamiaji zakari misana akiongea na waandishi wa habari ambao wapo picha juu ya wahamiaji haramu ofisini kwake .
Wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji kwa kosa la kuingia nchini bila kibali
Afisa wa uhamiaji akifanya mahojiano na moja wa wahamiaji haramu ofisi za uhamiaji .


Na Mohab Dominick
KAHAMA
August 26, 2014.
Wahamiaji haramu kumi na watoto watatu wamekamatwa wilayani kahama mkoani shinyanga wakiwa wakielekea mkoani tabora kwenye mashamba ya tumbaku kwa ajili ya kilimo.

Haya aliyesema hayo jana kamishana wa Uhamiaji Wilaya ya Kahama Zakari misana wakati akizungumza na redio kyela fm ofisini kwake ambapo alisema kuwa wahamiaji hao walikamatwa katika kituo cha mabasi wakati wakimsubiri mwenyeji wao ili kuwapeleka mkoani tabora.

Alisema kuwa wahamiaji hao ambao ni Rai wa nchi jamhuri ya Burundi waliangizwa na mkazi moja wa Tabora ambaye aliyejulikana kwa jina moja la shabani,ambapo baada ya kukamatwa na kupata taarifa ndipo wenyeji wao walipokimbia kutojulikana.

Misana aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Emily Havyarinana(33),Habimana paschal(45),masabo Tadei( 34),Bahati leopoo( 42),Niondeze John(24),Emmanuel mathayo( 21),Tegemea Benjamini( 23) mkazi wa chivu ,joseph Elias (12), ,Laneck wilford (17),Estar John (18) raia wa Burundi pamoja na Irene stephe(20)raia wa Tanzania mkazi wa ngara.

Aidha Misana alisema kuwa walikuwa wanakwenda Mkoani Tabora katika kijiji cha Isakamleme kwa ajili ya shughuli za kuvuna mahindi, kuchambua Tumbaku pamoja na kuvuna mpunga.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Irene Staphano ameajili mtoto mwenye umri wa miaka(8) aliyejulikana kwa jina moja la Khadija mkazi wa Burundi jambo ambalo ni kosa kuajili mtoto mdogo ambapo ni kinyume cha sheria ya jamhuri ya Muungano waTanzania.

Misana alisema miezi kama hii katika mikoa ya mipakani kumekuwa na tatizo la wahamiaji haramu wanaokimbilia mikoa ya kagera,Tabora pamoja na shinyanga, ambapo wilaya ya kahama imejipanga vyema katika kamati ya ulinzi ili kudhibiti jambo hilo.

Misana aliwataka watendaji wa kata na vijiji vilivyopo mipakani kushirikiana na wananchi kudhibiti matatizo ya wahamiaji hao ambapo amesema kuwa atakayebainika kuishi na raia ambaye sio raia ya Tanznia atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Ambapo alisema kuwa wahamiaji hao watachukuliwa hatua za kisheria baada ya kuingia nchini bila kibali hivyo watafikishwa mahakamani wilayani humo ili kujibu kesi inayowakabili.

YULE MCHAWI ANAYEMEZA MAPANGA, ALIYEKATAZWA KUINGIA DUBAI




Rolf Buchholz, Mjerumani anaetajwa kuwa mtu mwenye vipuli vingi zaidi usoni akiwa amejitoboa zaidi ya mara 100 usoni amekataliwa kuingia Dubai kutokana na sababu za kiusalama.
Rolf alikuwa amejipanga kufanya onesho la sarakasi na kikundi chake nchini humo ambapo huonesha michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘kumeza mapanga’.


KIJANA AVUA NGUO BAADA YA KUFIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO!

KIJANA Ben Boleyn aliamua kuvua nguo baada ya kufika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini chenye joto la kati ya sentigrade 10 hadi 12.
 
 
Ben Boleyn akiwa kilele cha Mlima Kilimanjaro.
 Ben alifanya hivyo baada ya kuwekeana dau la shilingi 500 na mwenzake miongoni mwa aliopanda nao mlima huo.
 
 
Ben akivua nguo baada ya kuwekeana dau na mwenzake.
 Kijana huyo mwenye miaka 18 alipanda mlima huo katika kuchangisha fedha kusaidia watoto wa kituo cha kulea watoto cha Acorns Children's Hospice kilichopo jijini Worcester nchini England.
 Kwa kupanda mlima huo, Ben alikusanya pauni 600 ila baada ya kuvua nguo zake na kuweka picha yake mitandaoni alichangisha fedha nyingi zaidi.
 
 
Ben baada ya kuvua nguo.
 Ben ambaye hujitolea katika kituo hicho alipanda futi 19,341 za Mlima Kilimanjaro kwa siku 9 akiwa na wenzake 7.
 Ben ambaye ni mwenyeji wa Kingswinford, England alisema: Kila mtu alifurahia kitendo nilichokifanya katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kuchukua picha zangu
 
 Wazazi wangu walipigwa na mshangao mwanzoni, ila walipoona watu wanazidi kuchangia kwa wingi walinielewa maana nilifanya kitu tofauti."

HALIMA MDEE AMWAGA MACHOZI HADHARANI BAADA YA KUPEWA FOMU YA KUWANIA UENYEKITI WA BAVICHA



Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.Mbunge huyo anaungana na Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao na wanachama wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda ambao nao wamesharejesha fomu kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Suzan Lyimo.Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Agosti 30 na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu.
Wanawake zaidi ya 30 kutoka Kinondoni, Kawe, Pwani na Ubungo jana saa 5.20 asubuhi, walifika katika ofisi za Bawacha jijini Dar es Salaam kumchukulia fomu Mdee wanayedai kuwa ndiye anayestahiki kuliongoza baraza hilo kutokana na msimamo wake wa uongozi wa kutotaka kuyumbishwa.

“Tumekaa na kutafakari ili kumpata mwanamke atakayeweza kuliongoza baraza hili kwa kututoa hapa tulipo na kutupeleka mbele zaidi, tumeona Halima Mdee anatufaa zaidi ndiyo maana tumeamua kuja kumchukulia fomu,” alisema Felister Njau, Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kawe.
Huku akishangiliwa na wenzake alisema, “Tunakwenda kumtafuta sehemu yoyote alipo ili tukamkabidhi hii fomu na tutamwomba akubali ombi letu.”
Msafara wa wanawake hao wakiwa na fomu yao mkononi ukiongozwa na Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Kunduchi, Elefedina Mali ulikwenda makao makuu ya chama hicho ambako walimkuta Mdee na kumkabidhi fomu hiyo.
Aliwashukuru na kuwaomba wamvumilie kwani anahitaji muda wa kulitafakari ombi hilo.

Huku akibubujikwa na machozi, Mdee (pichani) alisema; “Nimewaelewa naombeni nikajitafakari kwanza, nitawaeleza nitakachoamua.” Wanawake hao pia walichangishana fedha Sh53,000 walizomkabidhi Mdee kwa ajili ya kurejeshea fomu hiyo.

MADAKTARI WANASWA WAKIMTOA MIMBA MWANAFUNZI

 
Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
 

IMEBUMA kwao! Madaktari wawili, Hamis Chacha na Shengena wa zahanati moja iliyopo Yombo Buza jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu baada ya polisi kuwaibukia na kuwaweka chini ya ulinzi kwa madai ya  kufanya jaribio la kumchoropoa mimba msichana mmoja aliyedaiwa kuwa ni denti wa chuo f’lani cha digrii za juu, Dar.

Tukio hilo la aina yake lilijiri Agostii 25, mwaka huukatika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, Operesheni Fichua Maovu  ‘OFM’ ya Global Publishers  ikiwa katika pitapita zake ilinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi madaktari hao.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
 
Vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa na madakta hao katika zoezi la utoaji wa mimba.
 
Daktari Shengena alipoona kamera ya OFM alitaka kukimbia licha ya kuwepo kwa askari ndani ambapo walitumia nguvu za ziada kuwadhibiti vyema na kuingizwa ndani ya chumba alichokuwemo mwenzake ambaye naye alinaswa akiwa na vifaa vilivyodaiwa ni vya kuchomolea mimba akiwa amevificha kwenye mfuko wa rambo.
 
Madaktari wakiwa chini ya ulinzi wa makamanda wa OFM.
 
Baada ya maafande kuwaweka chini ya ulinzi, madaktari hao walizua kituko kufuatia kuzitupa chini shilingi 40,000 walizopewa na denti huyo kama malipo ya kazi hiyo wakidhani ni za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘Takukuru’.
 
kiasi cha fedha cha Shillingi arobaini elfu walicholipwa madaktari kwa ajili ya kufanikisha zoezi la utoji mimba.
 
Wakizungumza na waandishi wetu baada ya kuulizwa nini kilikuwa kikiendelea chumbani humo, Dokta Chacha alidai kuwa mgonjwa huyo ana tatizo kwenye kizazi hivyo alikuwa akitaka kusafishwa na si kutoa mimba maelezo yalikosolewa na denti huyo aliyedai kuwa alikwendwa kwa mapatano ya kumchoma mimba ili akaendelee na masomo chuoni.
 
Binti (denti) aliyekusudiwa kutolewa mimba.
 Akijibu kuhusu kwa nini alivificha vifaa va kutolea mimba kwenye mfuko, Dokta Chacha alijiumauma na kusema denti huyo alifuata taratibu zote kama wagonjwa wengine, lakini alishindwa kuonesha risiti au cheti cha kumsajili mgonjwa huyo kwa ajili ya matibabu.
 
Zahanati iliyotumiwa na madaktari hao katika jaribio la utoaji mimba.
 Kichekesho kingine kilikuwa wakati OFM na wanausalama wakitoka nje ya zahanati hiyo na watuhumiwa na kukuta kwenye maeneo mengine kukiwa kweupe na kusemekana kuwa, madaktari na manesi walioshuhudia wenzao wakitaitiwa walitoka nduki kwa kuogopa ushahidi.

Mwishowe watuhumiwa hao walifikishwa katika Kituo cha Kidogo cha Polisi Buza na kufunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. BUZ/RB/32/2014 kabla ya baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na sakata hilo.

BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LIMEFUNGULIWA JANA JIJINI DAR ES SALAAM


1Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya.
2Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
3Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo4Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie  (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo Wilbert Kaahwa6Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Jumaa Saadala akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam7Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

KIJANA APIGWA HADI KUFA BAADA YA KUIBA SIMU MBEYA



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwakilalo (25) mkazi wa Block T alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mbeya baada ya kupigwa na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kuiba simu.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 02:15 usiku huko katika maeneo ya Block T, jiji na mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa marehemu alikamatwa na kuanza kupigwa na wananchi hao na badae alipelekwa na kufungiwa katika ofisi za mtendaji ambapo alitoroka na ndipo wananchi hao walimuona na kumkimbiza na kuanza kumpiga hali iliyopelekea kumvunja mkono wake wa kushoto na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya. Juhudi za kuwatafuta waliohusika katika tukio hilo zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wawafikishe watuhumiwa wanaowakamata kwa makosa/tuhuma mbalimbali katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.

CHINA YAUNGANA NA TANZANIA KUTOKOMEZA UHALIFU


pic no 1
Na. Tamimu Adam – Jeshi la Polisi
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imekabidhiwa msaada wa vifaa vyenye thamani zaidi ya milioni mia moja kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya matumzi ya ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya ndani na ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Tanzania.Msaada huo, ulitokana na Ziara ya Naibu Waziri wa Usalama wa raia wa Jamhuri ya watu China aliyoifanya hapa nchini mwezi mei mwaka jana ambapo aliahidi misaada mbalimbali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Polisi.Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing kwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Pereira Silima ni pamoja na Kompyuta Thelasini (30), Viti tisini na mbili (92), Meza hamsini (50) na PA System kwa ajili ya kumbi mbili za mikutano.

Aidha, Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing alikabidhi Pikipiki hamsini (50)   kwa Jeshi la Polisi ambazo zilipokelewa rasmi na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima. Pikipiki hizo zilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China kwa niaba ya jumuiya ya wafanyabiashara wa kichina walipo Afrika wakati wa ziara yake aliyoifanya hapa nchini mwezi juni mwaka huu.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Pereira Silima baada ya kupokea vifaa hivyo, alimshukuru Balozi huyo wa China na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Pamoja na Wafanyabiashara wa Kichina waliopo Afrika kwa msaada walioutoa kwa Serikali ya Tanzania, na kueleza kuwa vifaa hivyo vyote vitakuwa ni chachu katika kuzuia, kupambana na kukabiliana na uhalifu hapa nchini.
Naye, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki alisema kuwa mbinu za kutenda uhalifu hubadilika mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya kiteknolojia, na katika kukabiliana na mabadiliko hayo Jeshi la Polisi liko kwenye utekelezaji wa Maboresho yaliyojikita katika mihimili mikuu mitatu ambayo ni kulifanya Jeshi kuwa kisasa, lenye weledi na linaloshirikiana na wananchi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu, hivyo vifaa vilivyokabidhiwa vitalisaidia Jeshi la Polisi katika mpango huo unaolenga kuzuia uhalifu.