Sunday, August 10, 2014
HADITHI YA KUNUSURIKA NA KIFO KWA DK SLAA NA MNYIKA
Madiwani walioasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamerejea na kudai walirubuniwa na makada watano wa CCM kuhama kwenye chama hicho ili wawatumie kuwaua, Dk. Willbrod Slaa na John Mnyika.
Madiwani hao ni Sebastian Mzuka wa kata ya Ngokolo na Zacharia Martin wa kata ya Masekelo wote kutoka Shinganya mjini ambao wamewataja makada hao kuwa ni Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Wengine ni Naibu waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC, chama tawala, Nape Nnauye, na Habibu Mchange (aliyefukuzwa Chadema).
Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika ofisi za chama hicho, madiwani hao walisema kuwa, mauaji hayo yalipangwa kutekelezwa kwa kiasi cha Sh. milioni 180.
Diwani Mzuka alisema wamefika kwenye ofisi hizo ili kueleza kinachoendelea kudhoofisha chama na kuomba toba baada ya kuhama.
Alisema mara baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuvuliwa madaraka Chadema, Mchange alipewa kazi (dili) na CCM kutafuta viongozi na madiwani wa Chadema lengo likiwa ni kukidhoofisha.
Alisema Mchange aliwafuata Shinyanga kuzungumza nao kuhusu suala hilo.
Alisema Januari 27, mwaka huu alipewa kazi ya kulipua helkopta iliyokuwa ikitumiwa na Katibu Mkuu Chadema, Dk. Slaa, Mbunge wa Ubungo, Mnyika na Mwenyekiti wa kanda ya Mashariki katika ziara ya Kanda ya Ziwa.
“Aliniambia kuwa Masele ana dili la shilingi milioni 180, baada ya ujumbe huo nilipokea simu ya waziri huyo ambaye aliniambia nikifanikisha nitalipwa fedha hizo,” alisema.
Alisema kuwa Masele alimtaka aeleze helikopta hiyo itatua wapi, muda gani na kama kweli wahusika wamo ndani yake kisha ulipuaji ufanywe na watu walioandaliwa.
Alisema alijiandaa na kufuatilia ila hofu ya kimungu ilimuingia akahofia taifa litapokeaje tukio la kifo cha Dk. Slaa na yeye akihusika.
“Nilimweleza Masele lakini alimpigia simu mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna Rose Nyamubi, ambaye alimshauri kuwa sio vyema tukio hilo likafanyika wilayani kwake, baadaye nilikutanishwa na katibu mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda pamoja na mtu mmoja wa usalama, ” alisema.
Aidha, alisema aliwashauri badala ya kulipua watumie mabango na kurubuni vijana kuhujumu ziara ya Dk. Slaa ambapo walifanikisha hilo.
Alisema baadaye walikutana tena na Nape, Nchemba na kuombwa wawashawishi madiwani na viongozi wengine wahamie CCM kwa ahadi ya kupewa ukatibu wa Wilaya kwenye wilaya watakazoamua.
Alisema baadaye madiwani hao walienda Mwanza mjini ambapo huko walikutana na Nape ambaye alieleza kusikitishwa kitendo cha Chadema kumvua uwanachama Zitto.
KUONDOKA CHADEMA
Alisema Februari 26, mwaka huu waliondoka rasmi Chadema ambapo Nape alifika huko na kukutana naye hoteli ya Kalena ambapo katika mazungumzo alimhakikishia maisha mazuri pamoja na uongozi.
“Usiku ulipofika gari la mwenyekiti wa mkoa wa Mwanza iliwachukua na kuwapeleka uwanja wa ndege na kusafiri kuja Dar es Salaam kukutana na Nchemba ambaye naye aliwataka waelekee Dodoma na baadaye Kalenga,” alisema.
Aliongeza kuwa Dodoma walienda nyumbani kwa Kinana ambaye huko waliwakuta Masele, Nchemba na Mchange ambapo wakati wote Katibu Mkuu alisifu kitendo chao cha kuondoka Chadema.
Alisema katika mazungumzo makada hao walimwambia Nchange asichoke kwa kazi anayofanya.
ACT YATAJWA
Mzuka alisema makada hao walikubaliana mgogoro ndani ya Chadema lazima uboreshwe na kuahidi kugharamia fedha za kwenda mikoani na pia wakasema kuna chama kitasajiliwa.
Pia alisema makada hao walisema watahakikisha Msajili wa vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi anakipatia usajili wa kudumu kwa gharama yoyote chama cha ACT ili CCM ipate ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Alisema katika mazungumzo hayo, Kinana alisema ACT imeanzishwa kwa lengo maalum la kuipa CCM ushindi kwa kuwa hata huko duniani, ushindi wa chama tawala unatokana na usajili wa vyama vipya.
WABUNGE WANNE KUHUJUMIWA
Makada hao walikubaliana katika uchaguzi ujao mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, asirudi bungeni kwa sababu ameitia hasara serikali kuhusu hoja zake dhidi ya katiba.
“Katika jimbo la Lissu, ACT itafadhiliwa kusaidia kutoa mgombea CCM ambapo itagawa kura za jimbo,” alisema.
Diwani huyo alitaja wabunge wengine ambao wapo kwenye mtego huo kuwa ni mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema ambaye imeelezwa amesababisha kushuka kwa utalii.
Wengine ni mbunge wa Iringa mjini Mchugaji Peter Msigwa na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi.
Kwa upande wa Lissu alisema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Diwani akijiuzulu anatakiwa aandike barua rasmi kwa mwenyekiti wa Halmashauri na kuambatanisha na kiapo.
“Hawa hawakufanya hivyo kwa hiyo bado ni madiwani wa halmashauri ya mji wa Shinyanga,na uthibitisho kuwa hawajajiuzulu ni kuwa siku 90 zimepita bila kutangazwa uchaguzi, “ alisema.
MBUZI WASABABISHA VIFO OMKOANI LINDI
WATU wanane wamekufa papo hapo, wengine tisa wakijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Nyangao mkoani Lindi baada ya gari aina ya Land Rover, mali ya Halmashauri ya Mji Masasi kupata ajali katika kijiji cha Mtama wilaya ya Lindi Vijijini mkoani hapa.
Gari hilo lenye namba za usajili STL 1615, lilikuwa linatokea Lindi ambako maofisa wa Halmashauri ya Masasi walikuwa wanashiriki katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Ngongo, nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Kutokea kwa ajali hiyo kulithibitishwa jana na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga aliyesema ilitokea juzi majira ya saa 11.30 jioni katika kijiji cha Mtama.
Aliwataja waliokufa kuwa ni Issa Salumu (33), Malik Selemani (24), Juma Ausi (21), Rajab Khalfan (17), Said Mchora (24) na Fadhili Mchalasi (26) ambapo watu wawili hadi sasa hawajafahamika majina yao, na amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.
Marehemu wote ni wakazi wa kijiji cha Mtama. Kwa mujibu wa Kamanda Mzinga, waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ni dereva wa gari hilo, Kessy Mwaijande (40).
Pia wamo madiwani watano wa Halmashauri ya Mji Masasi ambao ni Habiba Amlima, Maimuna Chiputa, Exaveria Mhagama, Asha Abbas na Blandina Nakajumo.
Wengine ni Abraham Mohammed, Shaabani Issa Kitemwe na Ally Adam, wote wakazi wa kijiji cha Mtama.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa majira ya jioni kwenye eneo hilo la tukio, waliliona gari hilo likiwa kwenye mwendo kasi, mazingira ambayo yalisababisha dereva wa gari hilo aliyekuwa akijaribu kukwepa mbuzi waliokuwa barabarani kushindwa kumiliki gari hilo na hatimaye kuacha njia na kuwagonga watu waliokuwa pembezoni mwa barabara hiyo, waliokuwa wakifanya biashara ndogo.
Hata hivyo, mmoja wa mashuhuda hao, Ahmad Mbonde aliiambia HabariLeo Jumapili kuwa, kama si kuwakwepa mbuzi, dereva wa gari hilo asingesababisha ajali.
Kutokana na tukio hilo, Kamanda Mzinga amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kunusuru maisha ya watu wanaoendelea kupoteza maisha na huku wengine wakibaki na ulemavu, mazingira ambayo hupunguza nguvu kazi ya
NYUMBA ZA RWAKATARE ZABOMOLEWA CHINI YA ULINZI MKALI
Katapila likibomoa moja ya nyumba nne zinazomilikiwa na Mchungaji Getrude Rwakatare katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam jana.
WIZARA
ya Ardhi, Nyumba na Makazi jana imebomoa nyumba nne zilizojengwa ndani
ya kiwanja namba 314 zilichopo eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam
zinazomilikiwa na Mchungaji Getrude Rwakatare kwa tuhuma kuwa alivamia
eneo hilo.
Kazi
hiyo ya ubomoaji, ilitekelezwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi na
iliendeshwa kwa pamoja na maofisa wa Ardhi kutoka wizarani na Manispaa
ya Kinondoni, waliodai wamepewa agizo hilo na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Alphayo Kidata.
Mhandisi
wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya alidai wamepewa agizo na Katibu
huyo, kuvunja nyumba ndani ya kiwanja hicho, baada ya kubainika kuwa
eneo hilo siyo mali ya Rwakatare, hivyo hastahili kujenga mahali hapo.
Mhandisi
Mkuya alidai pamoja kutokuwa mmiliki halali wa eneo hilo, nyumba hizo
pia zimejengwa bila utaratibu, ikiwemo kupata kibali cha ujenzi kutoka
katika manispaa hiyo, suala linaloashiria kuwa kulikuwa na kitu
kimejificha.
“Sisi
kama manispaa tumekuja kutekeleza agizo la kubomoa kutoka kwa Katibu
Mkuu, kinachoonyesha ni kuwa aliyejenga eneo hili alivamia eneo la mtu
mwingine huku akijua wazi ni kinyume cha utaratibu” alidai Mkuya.
Alidai
matatizo ya uvamizi wa viwanja, yamekuwa ni jambo la kawaida hasa
katika Manispaa ya Kinondoni na kwamba wanaendelea kuyashughulikia kwa
lengo la kuyapatia ufumbuzi wa haraka.
Awali,
kazi hiyo ya ubomoaji ilitanguliwa na ‘vuta nikuvute’ baina ya
mwanasheria aliyedai kuwa anamwakilisha Rwakatare, Emmanumuel Muganyizi
na Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya kuhusu suala la
kubomolewa kwa nyumba hizo, zinazodaiwa kujengwa ndani ya kipindi
kisichozidi miezi miwili na kupauliwa kwa vigae.
Huku
akiwa na nyaraka mbalimbali za kesi, alidai kesi bado ipo katika
Mahakama ya Kinondoni. Muganyizi alisema anashangazwa na uamuzi huo
uliochukuliwa kwa madai kuwa suala hilo, halijapatiwa ufumbuzi wa
kisheria na Mahakama.
“Ninaamini
hiki kinachoendelea hapa ni sawa na uvunjifu wa amani, kesi bado ipo
mahakamani inapaswa iachwe iishe ndiyo uamuzi ufanyike. Kwa hili
mnalofanya sasa siyo sawa kabisa,” alisema Muganyizi.
Mwanasheria
huyo wa Rwakatare, awali aliingia katika mzozo na waandishi, akidai
kushangazwa na kitendo chao cha kutaka kuandika habari hiyo.
Alidai
habari hiyo haina manufaa kwa jamii, kwa kuwa inahusu madai ya mtu na
mtu. Kwa upande wake, mtu anayedai kuwa mmiliki wa kiwanja hicho,
aliyekuwepo wakati kazi ya uboaji ikiendelea, Janeth Kiwia, alidai
kiwanja chake kilivamiwa na kuanza kujengwa mwishoni mwa mwaka jana
wakati akiwa safarini kwa watoto wake nje ya nchi.
Alidai
kabla ya kuvamia eneo hilo, kulikuwa na nyumba ya vyumba vinne,
aliyokuwa akiijenga taratibu, ambayo hata hivyo ilibomolewa na msingi
wake kutumika kujenga moja ya nyumba hizo.
“Tayari
kulikuwa na nyumba iliyokuwa imefikia usawa wa rinta, lakini cha
kushangaza walipovamia waliibomoa na kujenga ya kwao, namshukuru Mungu
kwa kuwa haki imetendeka baada ya kuhangaika huku na kule kutafuta haki
yangu,” alidai Janeth.
Alidai
kitendo hicho, kimemfanya kujenga imani na Serikali kuwa inatenda haki,
bila kujali kuwa aliyekuwa akiporwa na mnyonge, huku akiitaka
kuwasafisha baadhi ya watendaji waliopo ndani ya wizara hiyo,
wanaoshirikiana na watu wabaya kutaka kupora haki za watu.
“Nilikuwa
sitarajii kama ningefanikiwa tena kupata kiwanja changu, namshukuru
Mungu haki imetendeka bila hata mimi kutoa Shilingi moja, naomba tusife
moyo na Serikali yetu kwa kuwa inafanya kazi,” alisisitiza Janeth.
Mwanasheria
aliyekuwa akisimamia kesi ya Janeth, Howard Msechu kutoka Kampuni ya
uwakili ya Homac, alidai mteja wake ndiye mmiliki halali wa kiwanja
hicho.
HUYU NAE NI MWANAMKE
Mwanamama Power Black Nyati 'Jike Jeuri' akifanya vitu vyake ndani ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
'Jike Jeuri' akipiga 'push - up' ndani ya Uwanja wa Taifa.
'Jike Jeuri' akiwatoa jasho mabaunsa wawili walioshindwa kupeleka kidole chake chini.
Baada
ya kuwatoa 'knock out' mabaunsa wawili, ilibidi aongezeke mwingine wawe
watatu lakini bado walishindwa kupeleka kidole cha Jike Jeuri' chini.
HAWA NDIO MA LORE MODEL WA WATOTO WA JAMII YETU
Kwa mtindo huu huwezi kuwa kioo cha jamii, kwa skendo hii ni lazima utumie jahazi kujisafisha
Mtangazani
Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim
Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa
kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.
Kibonde
anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari
aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki
walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi
nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata
taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki kutumia
gari lililogongwa kumfukuzia.
Walifanikiwa
kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na
kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali.
Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye
hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde
arudi eneo la tukio.
Kibonde
aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani
ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia
gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliopo ndani
ya Gari hiyo.
Mara
Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki
mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo
inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na
kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni! Aligoma
kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini
ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka
sasa.
Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao
Kuna watoto na vijana wanaokuwa wanatamani sana kuwa kama Kibonde kwa vile wanavyomsikia na kumtazama lakini kwa mtindo huu kaka unawaipoteza jamii. Japo kuwa ni kweli kwamba hakuna mwanadamu asiyefanya kosa lakini hili lisingefika hapa kama Kibonde angetii maelezo mpaka anaamua kuwa kituko namna hii.
Si lazima kila afanyacho upendaye ni lazima na wewe uyafanye kila kitu twajifunza kwa wakubwa lakini mkubwa akifanya ujinga mwachie wewe chukua lile lililozuri nenda nalo
kuna wat
Subscribe to:
Posts (Atom)