Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushangaza, wananchi wa Mbezi Msakuzi Wlaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walisusa na kuondoka makaburini kwa kile kilichodaiwa kuwa maiti ya Michael Kisanto (pichani) waliyotarajia kuizika iliwekwa ndani ya jeneza kimaajabu.
Mazishi ya Michael Krisanto yakiendelea.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Makaburi ya Makamba Msakuzi, Mbezi jijini Dar es Salaam ambapo wananchi hao waligundua
kuwa maiti ya kijana huyo iliweka ndani ya jeneza kinyume na utaratibu
uliozoeleka yaani kichwa chake kilielekezwa sehemu ya miguu na miguu
ilielekezwa sehemu ya kichwa.
Msafara wa kuelekea makaburini kwa ajili ya mazishi ya Michael Krisanto.
\Kama
hiyo haitoshi, maiti hiyo badala ya kuviringishwa sanda nyeupe,
ilitumika sanda nyeusi kitu kilicholeta tafsiri tofauti miongoni mwa
waombolezaji.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, kabla jeneza lenye mwili kutumbukizwa kwenye kaburi kulitokea mvutano mkubwa baina ya wanandugu na waombolezaji.
Waombolezaji wakizozana juu ya utaratibu wa mazishi ya Michael Krisanto.
Imeelezwa kuwa, waombolezaji hao waliwataka wanandugu wafuate taratibu zilizozoeleka katika jamii wakati wa kuzika.Hata hivyo, ndugu wa marehemu hawakuwasikiliza na kudai kwamba walikuwa wanafuata mila na tamaduni za kabila lao (jina la kabila linahifadhiwa kwa sababu maalum).
Mwili wa marehemu, Michael Krisanto ukishushwa kaburini.
Wanandugu hao wakaamua kushusha jeneza lenye mwili kaburini na walipoanza kuzika waombelezaji walikuja juu na kulitoa jeneza kaburini hali iliyosababisha kutokea kwa vurugu kubwa.
Wanandugu wa marehemu, Michael Krisanto wakiweka mishumaa pembezoni mwa kaburi la ndugu yao.
“Vurugu
hizo zilisababisha wanawake waliokuwa makaburini kutimua mbio na
wanaume wakasusa na kuwaacha wanandugu waendelee kumzika ndugu yao,” alisema shuhuda wa tukio hilo kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.
Marehemu Michael Krisanto(kulia) enzi za uhai wake.
Habari zinasema kuwa, kutokana na utata huo, hata mchungaji aliyepaswa kuendesha ibada ya mazishi aliondoka bila kutoa huduma ya kiroho. Mmoja wa wanandugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Victor, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo hakuweza kusema chochote badala yake alikuwa akibubujikwa na machozi.