Thursday, October 16, 2014

AJALI YA LORI LA MAFUTA DAR LAANGUKA LAWAKA MOTO WATU WAPOTEZA MAISHA

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema wakimsikiliza miliki wa Nyumba ya kulala wageni United State na bar, Laurent Kasiga  iliyopo Mbagala Rangi tatu, Dar es Salaam ambayo iliteketea kwa moto uliotokana na roli la mafuta lililopinduka na kuwaka moto wakati vijana wakiiba mafuta.
 Mkuu wa Moa akikagua Nyumba hiyo ya kulala wageni iliyokuwa na vyumba 32.
 wananchi wakiangalia athari za moto huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiangalia tenki la lori hilo.
 Lori hilo lilivyoteketea kwa moto uliosababishwa na mshumaa.
Moja ya maduka ya vifaa vya pikipiki lililoteketea 
 
Wafanyabiashara wa mchele waliokuwa na fremu katika eneo hilo wakiwa katika majonzi baada ya mzigo wao kuungua moto na kuharibika kabisa.

Mmoja wa majeruhi katika tukio hilo la moto akisimulia. 
Baadhi ya sehemu za mwili za watu walioungua. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akiwa na mmoja wa wauguzi wa hospitali ya Temeke alipowatembelea waathirika wa ajali hiyo. WATU watatu wamefariki na wengine sita wakiwa katika hali mbaya Hospitali ya Muhimbili kufuatia tukio la moto uliolipuka kwenye gari la kubeba mafuta jana maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam. 

AKizungumza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohammed Mpinga, alisema ajali hiyo haikuleta athari yoyote baada ya gari lile kupata ajali ila athari ilijitokeza baada ya watu kuvamia na kuanza kuiba mafuta na baadaye kujaribu kuiba betri ndipo cheche za moto zilipolipuka na kusababisha kuwaka kwa gari hilo. 

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick, amewataka wananchi kutokuwa na tabia ya kuvamia ama kuiba vitu pindi ajali zitokeapo.
Sadick alisema hayo alipotembelea hospitali ya Muhimbili na Temeke walipolazwa majeruhi hao.

MWANAJESHI ATOA ADHABU KALI KWA RAIA ALIYEVAA NGUO ZA JESHI KARIAKOO


Picha unazoona sio utani wala sinema ni raia wa kawaida akiogelea kwenye dimbwi kwa amri ya mwanajeshi.
Raia huyo alikutana na adhabu kali za mwanajeshi huyo baada ya kukutwa amevaa mavazi halisi ya jeshi la Tanzania maeneo ya Kariakoo Dar es Salaam.
Jamaa huyo alipokamatwa na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha akaamriwa kuvua mavazi hayo na kisha kuaza kutumikia mazoezi ya hatari ..
Haya mavazi raia wanayapenda ila kwenda kutumikia jeshi hawataki ...ahahaaa jamaa alichokipata hawezi kutamani nguo za rangi ya kombat maisha yake yote.

HIZI NDIZO VURUGU KUBWA ILIYOTOKEA KWENYE MECHI BAINA YA SERBIA NA ALBANIA
















MCHUNGAJI AMTOROSHA MKE WA MTU AMBAYE NI MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI

MCHUNGAJI anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji huyo. Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na Janet. 
“Mume alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini nadhani aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo. 
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.
Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel akilizungumzia sakata hilo. Iliidaiwa kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya nchini Burundi wakati yeye ni Mkongo wa Uvira na alionekana kuishi nchini kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na. WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI. 
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa kitendo chake hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa. 
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela.Amani lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile alikuwa kikaoni. 
Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia tena simu ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.