Friday, November 15, 2013

NGASA AIVISHA MAPENZI KWA SNURA




Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa wamenaswa ‘laivu’ wakiwa kimahaba, Amani lina mkanda kamili.
Ngassa akiwa kimahaba na Snura.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, tukio hilo lililijiri hivi karibuni nyumbani kwa Snura maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.
Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.
Ngassa akimbusu Snura.
“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.
Ili kujiridhisha, Amani lilisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua utata na maswali kwa walioziona.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura na Ngassa kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar wakila bata ndefu.
Baada ya kulishwa ‘niuzi’ hizo, gazeti hili lilimsaka Snura ambapo alipopatikana alitakiwa alimwagiwa habari yote juu ya uhusiano wake tata na Ngassa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Ngassa akimsuka Snura.
“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu.
“Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”
Wakizidi kujiachia kimahaba.
Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.