Thursday, November 20, 2014

IPTL NI MWIBA KWA CCM


IPTL mwiba CCM
KUNA kila dalili za Baraza la Mawaziri la Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuvunjika tena baada ya ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu kashfa ya uchotwaji fedha zaidi ya sh. bilioni 200, kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zilizohifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kubainisha kuwa fedha hizo zilitolewa kinyume na taratibu.

Kashfa hii nzito ni mfululizo wa nyingi zilizotokea chini ya utawala wa Rais Kikwete na hivyo kusababisha mawaziri kadhaa kuachia ngazi akiwemo aliyekuwa Waziri wake Mkuu, Edward Lowassa aliyejiuzulu Februari 7, mwaka 2008, kufuatia kashfa ya zabuni tata kwa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.
Vigogo wa serikali wanaotajwa kuhusika katika kashfa hii ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospiter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Beno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Wadadisi wa kisiasa wanabashiri kwamba kashfa hii huenda ikiwa mwiba wa kuking’oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, ikiwa vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vitadumu katika muungano wao na kuwaeleimisha wananchi madhara ya ufisadi huo.
Kashfa kama hii iliwahi kuking’oa chama tawala cha KANU cha nchini Kenya mwaka 2002, ambapo kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mmiliki wa Kampuni ya PAP inayodai kuinunua Kampuni ya IPTL, Habinder Singh Sethi, anatajwa kuhusika katika kashfa kubwa ya ufisadi nchini Kenya ya Goldenberg, uliogharimu takribani dola milioni 600.
Ufisadi huo pia ulihusisha mahakama, watendaji, viongozi na wanasiasa wakubwa nchini humo, ikiwemo familia ya aliyekuwa Rais wa wakati huo, Daniel Arap Moi, ambapo katika uchaguzi mkuu wa 2002, vyama vya upinzani kupitia muungano wao wa National Alliance of Rainbow Coalition (NARC) chini ya mgombea wake Mwai Kibaki, kwa kutumia kashfa hiyo, vilifanikiwa kuking’oa Chama tawala cha KANU.
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG ambayo imekabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa ajili ya kuipitia na kuwahoji watuhumiwa, fedha za Escrow sh. bilioni 306 ni matokeo ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kulipishwa capacity charge zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa.
Ripoti hiyo, inasema kwamba Tanesco walipaswa kurejeshewa sh. bilioni 321 zilizolipwa zaidi kwa IPTL kati ya mwaka 2002 hadi 2012. Kwa maana hiyo, Escrow ni fedha za umma. Hii ni kinyume na kauli zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Rais Kikwete wakiwemo Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Nishati na Madini kwamba fedha hizo ni za mmiliki wa Kampuni ya IPTL.
Kwa mara kadhaa, Waziri Muhongo amenukuriwa na vyombo vya habari akitamba na kuwabeza wabunge waliosimama kidete kuhakikisha fedha za Escrow zinarejeshwa, akidai kwamba ushahidi waliowasilisha bungeni kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kuonesha kwamba fedha hizo ni za umma, ni vipeperushi feki kwani yeye anao ushahidi wa makaratasi ya kujaza gari zima la tani moja kuthibitisha kuwa fedha hizo sio za umma.
Waziri Muhongo na Katibu wake, Maswi wamekuwa wakiwatuhumu wabunge David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) na Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) kwamba wamehongwa na aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco, Nimrod Mkono kushupalia sakata hilo ili kukwamisha bajeti ya wizara hiyo ya 2014/2015.
Kashfa ya Escrow imeghubikwa na utata ambapo Harbinder Sing Sethi, anadai alinunua asilimia 70 ya hisa za Mechmar kwa kiasi cha sh. milioni 500 ($300,000) ndani ya wiki tatu tu tangu hisa hizo kuuzwa kwa kampuni moja ya Visiwa vya Uingereza vya Virgin kwa sh. milioni sita.
Lakini barua ya TRA Mkoa wa Ilala, iliyosainiwa na Meneja, Paschal Kabunduguru, yenye kumbukumbu nambari TRA/DR/ILA/RE/175 ya tarehe 15/11/2013, inaonyesha kuwa kampuni ya Mechmar ya Malaysia iliuza hisa zake asilimia 70 katika kampuni ya IPTL kwa kampuni ya Piper Links investment limited mnamo tarehe 9/9/2013 kwa thamani ya sh. 6,000,000 (milioni sita).
Nyaraka za malipo ya kodi kwa mujibu wa barua hiyo inaonyesha Mechmar walilipa kodi ya ongezeko la mtaji sh. 596,000 na kodi ya stempu ya sh. 180,000 mnamo tarehe 6 Disemba 2013 katika Benki ya CRDB Tawi la Waterfront.
Katika hali inayotia mashaka, kampuni ya Piper Links nayo, kwa mujibu wa nyaraka toka TRA, ikauza hisa zake kwa Kampuni ya Pan Africa Power Solutions mnamo tarehe 30 Oktoba, 2013, takribani wiki tatu tangu kununuliwa kwa hisa hizo toka kwa Mechmar.
Kwa mujibu wa barua ya TRA, kodi iliyolipwa ni ya ongezeko la mtaji sh. 47,940,000 na ushuru wa stempu sh. 4,800,000.
Malipo ya kodi hiyo yalilipwa siku ile ile ambayo Mechmar walilipa yaani Disemba 6, 2013, jambo linalozidi kuzua utata mkubwa kuhusu mhamala huo.
Pengine kinachotia shaka zaidi ni kwamba nyaraka zote mbili toka TRA ziliandikwa siku moja, na zote zina kumbukumbu namba zinazofanana licha ya ukweli kwamba zilikuwa zinakwenda kwa makampuni mawili tofauti, moja ikiwa Malayasia, na nyingine ikiwa visiwa vya Uingereza vya Virgin.
Pia nyaraka hizi toka TRA, zinapingana na kauli ya Sethi ambaye amenukuliwa na vyombo kadhaa vya habari akidai kwamba alinunua hisa asilimia sabini za Mechmar mwaka 2010, toka kampuni ya Piper Link—mwaka mmoja kabla ya PAP kuanzishwa.
Wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanasema kwa mujibu wa Sheria ya kodi ya Mapato ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marekebisho katika Sheria ya Fedha ya mwaka 2012, mauzo yeyote ya hisa au mali ambazo zipo Tanzania mauzo yake lazima yathibitishwe na Wizara husika baada ya kodi zote kulipwa.
Nyaraka hizi zinaonesha kuwa mauzo ya IPTL kutoka Mechmar kwenda PiperLink na kutoka PiperLink kwenda PAP yote yamelipiwa kodi siku moja tena baada ya malipo ya fedha za Escrow kwenda PAP Disemba 5, 2013.
Kwa kuzingatia nyaraka hizo, ni dhahiri kuwa mpaka kampuni ya PAP ilipokuwa inalipwa fedha za Escrow hawakuwa na umiliki wa hisa za IPTL. Hata amri ya mahakama ilipotolewa kuwa PAP wapewe mali za IPTL, kampuni hiyo haikuwa na umiliki wa wowote wa IPTL.
Pia katika hati za kuhamisha hisa ambazo ziliidhinishwa na TRA mkoa wa Ilala, mwandiko ulipo unafanana sana na mwandiko wa nyaraka za malipo ya kodi, CRDB, tawi la Water Front—jambo linaloonyesha kwamba mtu mmoja huyo huyo ndiye aliyeandika nyaraka zote hizi.
Utata mwingine ni kuwa iweje kampuni ya VIP Engineering iliyokuwa na hisa asilimia 30 katika IPTL ilipwe dola za Kimarekani milioni 75 wakati Mechmar iuze asilimia 70 kwa sh. milioni 6 tu na PiperLink iuze kwa dola laki tatu tu ndani ya wiki tatu.
Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wake, Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi, wamekuwa wakisisitiza kwamba fedha hizo zilitolewa kwa kuzingatia hukumu ya MahakamaKuu.
Hukumu hiyo ya Jaji John Utamwa inapingwa na Kafulila na wadau wengine kuwa imetafsiriwa visivyo, kwani hakuna popote alipotaja Akaunti ya Escrow, ingawa katika muhtasari wa kikao kati ya Tanesco, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini, ndipo wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za akaunti hiyo zipewe Kampuniya PAP.
Kupitia barua kumb. No. SAB.88/417/01/5 ya Oktoba 21, 2013, Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Maswi alimwandikia Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu akimtaka aruhusu fedha hizo katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Hata hivyo, sehemu ya ripoti ya CAG kuhusu kashfa ya uchotwaji wa fedha hizo inathibitisha kuwa TRA walibaini kuwa msingi wa ukokotoaji wa kiwango cha kulipa kodi ya Ongezeko la Mtaji ulitokana na nyaraka zenye taarifa zisizo sahihi, jambo lililochangia kutolipwa kodi ya kiasi cha sh. 8,682, 521,100.
Utawala wa Rais Kikwete umeghubikwa na kashfa nzito za ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kipindi chote cha miaka tisa, lakini mara zote kumekuwa na kigugumizi cha kuwang’oa watuhumiwa mpaka pale Bunge lilipoingilia kati.
Kashfa zilizotikisa ni ile ya ununuzi wa rada mbovu kwa gharama kubwa hadi serikali ya Uingereza ikaingilia kati kushinikiza kampuni iliyouza rada hiyo irudishe chenji kwa Tanzania, pia ipo ile ya EPA iliyoaiandama serikali mwanzoni mwa utawala wa Kikwete ambapo baadaye aliyekuwa Gavana wa BoT, Daud Balali alifariki bila kuchukuliwa hatua.
Sakata lingine ni kampuni hewa ya Richmond mwaka 2008, ambapo mbali na Lowassa, mawaziri wengine waliong’oka ni Dk. Ibrahim Msabaha na Nasir Karamagi waliopata kuwa mawaziri wa Wizara ya Nishati na baadaye Baraza la Mawaziri lilivunjwa na kuundwa upya kwa Mizengo Pinda kuteuliwa kushika wadhifa wa Waziri Mkuu ambaye naye kashfa ya Escrow huenda ikamwondoa.
Zipo pia kashfa za uchangishaji fedha kinyume cha taratibu ndani ya Wizara ya Nishati na Madini iliyomhusu aliyekuwa Katibu Mkuu wake, David Jairo na kisha uchotwaji wa fedha uliyoihusisha kampuni ya Pan African Energy zaidi ya sh. bilioni 110, tuhuma ambazo ziliwangoa Jairo na Waziri wake, William Ngeleja.
Kashfa ya Buzwagi nayo ilitikisa Bunge mwaka 2007, ambapo Zitto alimtuhumu Waziri wa Nishati na Madini, Karamagi kuwa alikiuka utaratibu kwa kusaini mkataba mbovu wa mgodi huo ikiwa hotelini nje ya nchi. Hata hivyo CCM kwa kutumia wingi wa wabunge wake bungeni ilimgeuzia Zitto kibao na kumwadhibu kutohudhuria vikao kadhaa vya Bunge.
Pia zipo kashfa za ripoti ya CAG mwaka 2012 na ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu utekelezaji wa oparesheni tokomeza mwaka 2013, ambapo mawaziri Dk. Cyril Chami, Dk. Hadji Mponda, Omary Nundu, Mustafa Mkulo, Ezekiel Maige, Dk. Athuman Mfutakamba, Dk. Lucy Nkya, Balozi Khamis Kagasheki, Dk. Emmanuel Nchimbi, Shamsi Vuai Nahodha na Dk. Mathayo David waling’oka kufuatia shinikizo la Bunge.
Wabunge CCM wakamia
Wakati PAC leo ikianza kumhoji Jaji Werema kuhusu kashfa hiyo, wabunge wa CCM wanatarajia kuwa na kikao maalum kwa ajili ya kujadili sakata hilo kabla halijaingia bungeni Novemba 27.
Kashfa hiyo, itabiriwa kwamba huenda ikamwangusha Waziri Mkuu, Pinda, kutokana na wabunge wanaomuunga mkono Lowassa kujipanga kulipa kisasi cha yale ya Richmond ya mwaka 2008.
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alilieleza gazeti hili kuwa kamati yao imeshaanza kazi tangu jana, lakini leo itaanza kuhoji Jaji Werema ambaye ni mmoja wa watuhumiwa.
Mwingine atakayehojiwa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na itaendelea na kazi yake kwa kuwahoji watu wengine kadri itakavyoona inafaa.
Habari zaidi kuhusu kamati hiyo iyopiga kambi nje ya viwanja vya Bunge, zinasema kuwa itafanyakazi usiku na mchana na kukamilisha kazi yake ndani ya siku tatu.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ilikabidhiwa ripoti hiyo juzi na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Mmoja wa wabunge kutoka CCM, aliliambia gazeti hili kuwa tayari wameshajulishwa kuwapo kwa kikao hicho kitakachofanyika siku yoyote wiki hii.
“Tutakuwa na kikao wiki hii, sijui wanataka kutuambia nini. Kama kuwatetea watuhumiwa itakuwa ngumu kwa sababu taarifa ya CAG inaonyesha wazi kwamba Waziri Muhongo, Katibu Mkuu, Maswi na wengine waliotajwa kuhusika, hawaponi. Sisi tutakuwa na nguvu gani kuwatetea? Alihoji.
Wabunge wengi bila kujali vyama vyao, wamepania sana mjadala huo na kulitaka Bunge litenge muda wa kutosha ili kila mchangiaji apate muda wa kutosha.
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), jana aliomba mwongozo wa Spika kutaka Bunge litenge zaidi ya siku moja ya mjadala wa kashfa hiyo ya IPTL.
Alisema kwa jinsi hali ilivyo, inaonyesha kuwa wabunge wengi wanataka kuchangia, hivyo aliomba mwongozo wa Spika ili Bunge liongeze muda zaidi wa kuchangia.
Akijibu mwongozo huo, Ndugai alisema anachukua mawazo hayo na kuyapeleka kwenye Kamati ya Uongozi ili waweze kufanya uamuzi.
CREDIT: TANZANIA DAIMA

WAKULIMA BAGAMOYO WASIFIA MBEGU MPYA ZA MIHOGO.




Wakati tafiti mbalimbali zikiendelea kufanyika katika kituo cha utafiti cha MARI (Mikocheni Agricultural Research Institute)ili kulikomboa zao la Mhogo kutoka katika janga la magonjwa yaliyolikumba zao hilo,  wakulima wamendelea kusifia mbegu mpya ambazo zinaendelea kutolewa na kituo hicho kwa sasa
 Sambamba na hilo, wakulima wa mihogo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamesifia ubora wa  mbegu mpya ya mihogo itokayo MARI kuwa ni mbegu bora, ikomaayo haraka, isiyo na magonjwa na pia inazaa sana tofauti na mbegu za zamani.
Wakiongea na mwandishi kwa nyakati tofauti walisema mbegu walizokuwa wakizilima hapo awali zilikuwa ni pamoja na Jota ambayo ilikuwa inakuwa ni ndefu  na inalewesha sana ukila kwa wingi, Mzungu, yenyewe ni nyekundu kwa muonekano ambayo pia hulewesha, mbegu ya Kiruthungu na Kinyafu ambazo zenyewe ni michungu sana iliwapo. Pia walisema mbegu hizi zilikuwa zinachukua mda wa miezi minne hadi mitano kukomaa kitu ambacho ni tofauti na mbegu ya sasa.
 
Walisema kuwa mbegu za sasa wamezipa majina ya Mwanamtwa, Mzuri kuonja, Kibangameno, Magimbi na kilokote, huku wakizingatia radha na uzuri wa mbegu hiyo.
Wakitofautisha mbegu mpya  walisema mbeguu mpya zote si chungu kwa kula, hukomaa ndani ya miezi mitatu mpaka mine na huzaa mihogo mikubwa kitu ambacho ni tofauti na za zamani.
“Mihogo ya siku hizi ni mitamu hata kwa kutafuna ikiwa mibichi tofauti na ile mingine ni michungu, na pia ukiipika inaunga sana mpaka inavutia wakati wa kula” alisema Ibrahim Ramadhani
Hata hivyo wananchi hao wameiomba serikali kuanzisha vipindi na majarida yanayotoa elimu ya kilimo katika vituo vya redio mbalimbali na magazeti kwani bila elimu watu wengi hufanya  tofauti na baadae kulaumu kilimo pale wanapopata hasara shambani.
“Serikali inatakiwa kurudisha vipindi vya kilimo kwani wameziacha redio zinapiga mziki asubuhi hadi asubuhi hakuna faida badala yake vijana wanaacha kufanya kazi na kukaa vijiweni kusikiliza miziki. Inatakiwa wawaambie wenye vituo vya redio kuwa na vipindi vya kilimo ili kuwabadirisha vijana wanaosubiri ajira maofisini wajue kuwa hata kilimo ni ofisi kama ofisi zingine” alisema mzee Frank Shaban.
Wakati huo huo mwandishi aliwasihi wakulima hoa kutunza mbegu hizo kwani mbegu walizopewa ni mbegu zisizokuwa na magonjwa hivyo wanatakiwa kutunza vizuri ili kupata mazao mazuri na bora kwa manufaa zaidi.
Ikumbukwe kuwa zao la muhogo lilikumbwa na magonjwa ya mnyauko fuzari pamoja na batobato ambayo yalisababisha zao hili kuwa hatarini kutoweka kitu ambacho kiliwafanya watafiti kuingia maabala na kutafuta ufumbuzi ili kukomboa mikoa inayotegemea zao la mihogo kwa chakula.
Mpaka sasa njia pekee inayotumika kuzalisha mihogo isiyokuwa na magonjwa ni tissueculturee (uzalishaji wa chupa) na njia hii haiufanyi mmea kuwa kinzani na magonjwa hivyo njia pekee ya kufanya mbegu mpya kudumu na kuzaa vizuri ni mkulima kutunza vizuri shamba lake ili kupata faida.

MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA IN LONDON FOR MISS WORLD


 Miss Tanzania Happiness  Watimanywa  ,paid  a  courtesy  call to  the  Tanzania High  Commission  in  London. She was welcomed by the High Commissioner H.E Peter Kallaghe. During  their  meeting  Miss Happiness  was  able  to  update  the  high  commissioner  about  her   mission  to  represent  Tanzania  as  a  country  at  the  famous 64th  edition of Miss  world  beauty pageant  that  will  take  place  early  December. In  return  the  High  commissioner  promised  her  the  support   and  backing  of  the  Tanzania  mission  in  London  and  wished  her  all  the  best. There after a national flag was presented to her.
Tanzania may not win the Miss World crown this  year or ever or even surpass this year’s record in many years to come but we must learn to celebrate what we have achieved now as we prepare and plan for the future. Tanzanians must not wait for Tanzania to win the Miss World before celebrating, let’s celebrate now and leave the future to take care of itself.Lets  all  support Happiness Watimanywa

NOTES:
THE THEME AND ROLE OF MISS TANZANIA
THE THEME OF MISS TANZANIA BEAUTY PAGEANT IS BEAUTY WITH A PURPOSE. THIS THEME CLEARLY SPELLS OUT THE ULTIMATE GOAL OF THE PAGEANT. THE GOAL IS NOT PICK THE MOST BEAUTIFUL GIRL AS A WINNER JUST FOR THE SAKE OF IT BUT TO USE HER BEAUTY TO FURTHER MEANINGFUL COURSES.
ONCE MISS TANZANIA HAS BEEN SELECTED, SHE ASSUMES THE ROLE OF A GOODWILL AMBASSADOR. IT IS COMMON FOR FAMOUS PERSONS THE WORLD ALL OVER TO ACT AS GOODWILL AMBASSADOR S ON BEHALF OF VARIOUS ORGANIZATIONS IN FURTHERING THEIR COURSES. TO BE GOODWILL AMBASSADOR, ONE NEEDS TO COMMAND THE ADMIRATION OF EITHER LOCALLY OR INTERNATIONALLY.
Since the Beauty with a Purpose ethos was incorporated into Miss World, millions of pounds have been raised and countless hours of hard work have been carried out across the globe. As well as the official Beauty With A Purpose Charity, many other outlets of these selfless activities have been utilized through the years.
From the ground up thousands of contestants right from the regional heats to the global final have found countless ways to make a difference and bring about positive change to communities in need. 
Below are the latest examples of Beauty with a Purpose in action. For more details visit www.beautywithapurpose.com

MAMA AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU JIJINI DAR


My God! Mama aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa Manzese jijini Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga baada ya kujifungua kiumbe wa ajabu.

Swaumu Sadick akiwa hospitali baada ya kujifungua mtoto huyo. Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo, lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Kituo cha Afya Cha Kijiji cha Mlali kilichopo wilayani Mvomero mkoani hapa.
Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba Swaumu alijifungua kiumbe huyo wa ajabu anayedaiwa kuwa na mkia mrefu huku akiwa hana miguu. 
Ilidaiwa kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya ndugu walishikwa na taharuki kubwa huku wengine wakitoa taarifa kwa mwanahabari wetu ambaye alifunga safari kutoka mjini Morogoro na kuwasili kwenye kituo hicho cha afya majira ya saa 12:00 asubuhi. 
Katika mahojiano maalum na gazeti hili juu ya tukio hilo, nesi wa zamu aliyekutwa kituoni hapo aliyejitambulisha kwa jina moja la Consolatha alikuwa na haya ya kusema: “Nilimpokea Swaumu majira ya saa 1:00 usiku akilalamika kuwa na uchungu wa kujifungua. 
Swaumu Sadick akiuguzwa hospitali. “Nilimpa kitanda. Saa 8:00 usiku, uchungu ulizidi nikampeleka leba ambako alijifungua kiumbe huyo mwenye jinsi ya kiume. “Baada ya kujifungua na kumuona kiumbe huyu wa ajabu, nilitimua mbio usiku huo kwa woga na kwenda kuamsha manesi wenzangu wanoishi kota za kituo hiki cha afya.
“Nimefanya kazi hii ya ukunga na kuzalisha wazazi zaidi ya 50 lakini sijawahi kukutana na tukio kama hili.”
Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Beatrice alikuwa na haya ya kusema juu ya tukio hilo la kusikitisha: 
“Kimsingi si kiumbe ila ni mtoto ambaye awali tulipomcheki mzazi tulibaini ana kichwa kikubwa na alishafia tumboni zaidi ya siku tatu.“Amezaliwa akiwa na miezi nane tumboni. Tulichokifanya ni kuokoa maisha ya mama jambo ambalo tumefanikiwa.”
Mtoto wa ajabu aliyezaliwa na Swaumu. Akizungumza kwa tabu na mwanahabari wetu, Swaumu alisema: “Hii ni mimba yangu ya tatu, ya kwanza iliharibika tumboni, ya pili nilifanikiwa kuzaa salama mwanangu Maimuna.
“Hii ya tatu ndiyo nimejifungua kitu hiki cha ajabu.” 
Alipoulizwa kwa nini aliondoka Dar ambako ndiko kwenye hospitali kubwa na kwenda kujifungulia kijiji akijua ana matatizo ya uzazi, mama huyo alisema:
“Siku za kujifungua zilipokaribia mume wangu Abdallah aliniambia nije kujifungulia kwa bibi yangu Halima, kwa bahati mbaya ndiyo yametokea haya.” 
Kwa upande wake shangazi wa Swaumu aliyekutwa akimhudumia alisema: “Yameshatokea ya kutokea, tunamshukuru Mungu na tunajiandaa kumchukua mjukuu wetu tukamzike.”

BILIONEA WA BUKOBA AFARIKI GHAFLA AKIVUNJA AMRI YA SITA KWENYE GARI NA MWANAMKE






WATOTO 130000 WANAISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI


unnamed
Wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi waliohudhuria kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa kongamano hilo. Hadi sasa watoto wenye maambukizi ya VVU 130000 wameweza kufikiwa kati ya hao 39317 wamepewa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
unnamed1
Baadhi ya wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi wakimsikiliza Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF).

……………………………………………………………………………..
 TAKWIMU zinaonesha kwamba watoto 130000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kati ya hao 39317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo. 
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la VVU na UKIMWI kwa watoto linalofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar-es-salaam.
Dkt . Chana alisema asilimia 39 ya watoto walio katika hatari ya kupata maambukii ya UKIMWI hupimwa vipimo vya kubaini maambukizi ya VVU ndani ya miezi miwili baada ya kuzaliwa hivyo basi kuna umuhimu kwa watoto hawa kupata huduma za tiba mapema.
Akizungumzia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waziri huyo alisema Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lengo likiwa ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya kwa watoto wachanga.
“Mama wajawazito na wale wanaonyoyesha wanapatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya VVU mara tu wanapogundulika kuwa na maambukizo, kupitia mpango mpya unaojulikana kama ‘uwezekano namba 2 au (Option B+)”, alisema Dkt.Chana
Alisema kufikia mwezi Juni mwaka huu jumla ya akina mama 940900 kati ya 1050043 hii ni sawa na asilimia 89.6% ya waliohudhuria kliniki walipimwa UKIMWI kati ya hao 47856 takribani asilimia 5 walikutwa na maambukizi ya VVU. 
Kwa upande wa watoto 20569 walipima kipimo cha DBS kati ya hao 2063 hii ni sawa na asilimia 10 walikutwa na maambukizo ya VVU.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mbando, alisema ingawa nchi imepiga hatua katika mapambano ya kudhibiti UKIMWI hali halisi inaonyesha kuwa bado kuna maambukizo yanatokea sio tu kwa watu wazima bali na kwa watoto pia.
“Ni jukumu letu kuendelea kuweka mikakati ya dhati na kuisimamia ili kuhakikisha lengo la kutokomeza maambukizo ya VVU tunalifikia kwani mwaka 1986 maambukizi yalikuwa juu kwa asailimia 18 lakini hivi sasa yameshuka na kufikia asilimia 5.3”, alisema Dkt. Mbando
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufundi kutoka Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF) ambao ni waandaaji wa kongamano hilo Chrispin Kimario alisema ni muhimu kwa wazazi na jamii kushirikiana kwa pamoja na kulibeba jukumu la kuhakikisha kila mama mjamzito anapata huduma ya vipimo husika na matibabu kwa wakati.
Kimario alisema, “Watoto wameachwa nyuma, ni vyema tukumbuke kuwa mtoto hawawezi kujipeleka wenyewe hospitali kupima afya zao, hivyo ni jukumu letu wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma wanazostahili”.
Kauli mbiu ya kongamano hilo la siku mbili ambalo limehudhuriwa na wadau wa afya kutoka asasi za umma na binafsi za ndani na nje ya nchi ni ongeza kasi: Rahisisha upatikanaji wa utumiaji wa huduma za VVU na Ukimwi, pata matokeo chanya ya afya za mama na watoto wanaoishi na VVU.