Wednesday, August 6, 2014

DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAYANSI KWA NCHI ZA AFRIKA NA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA, JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Nelson Mandela cha jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Nelson Mandela, Bernard Mussa, aliyetafiti kuhusu kuongeza joto katika Majiko kwa kutumia mwanga wa jua, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Masai Stove’s & Solar, Kisioki Moitiko aliyetafiti kuhusu mzunguko wau meme wa Jua kutumika katika nyumba za kabila la kimasai (Maboma) wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Hassna Founoune, kutoka Taasisi ya Tafiti ya Kilimo ya Senegal, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi.Picha na OMR
Kongamano hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha jana Agosti 5, 2014, na kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara. 

Kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee na akina mama.

Katika Hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa, dhana ya umuhimu katika uwekezaji na utanuaji wa sayansi katika Afrika, inahitaji kutazama kundi la vijana na kulihamasisha kushiriki katika masomo ya sayansi ili kuharakisha maendeleo kwa Bara la Afrika.

ZAO LA MUHOGO LAZIDI KUPATA NEEMA




ZAO la muhogo ni miongoni mwa mazao yasiyopewa kipaumbele kikubwa hapa nchini katika ulaji na kibiashara pia  huku wanasansi na watafiti wakizidi kulitangazia neema zao hilo.

Zao hilo ambalo limekumbwa na maswahibu ya magonjwa ambayo yalipelekea wakulima kukata tamaa ya kulima zao hilo limeonekana ni zao lenye manufaa kwa wakulima ikiwa watafuata maelekezo ya kilimo bora na watafiti wa kilimo

Hata hivyo imebainika kuwa zao la muhogo licha ya kwamba linalimwa kwa wingi hapa nchini lakini faida yake haijaonekana kutokana na jinsi linavyoandaliwa na kusababisha mkulima kupata faida kidogo.

Hivi sasa imebainika kuwa zao hilo ni miongoni mwa mazao yenye faida kubwa kutokana na kuonekana lina matumizi makubwa katika shughuli za viwandani ikiwa ni pamoja utengenezaji  wa sabuni ya unga, pipi, dawa, juisi  tambi,bisukuti,mafuta ya lishe,keki, kuni, mboga,nguo pamoja na bidhaa nyingine nyingi.

Hayo yalibainishwa na Bi Mariam Mtunguja ambapo alisema Tanzania inaagiza wanga (starch) kutoka nje wakati uwezekano wa kuwa na bidhaa hiyo hapa nchini ni kubwa. “ Nashangaa kuona viwanda vingi hapa Tanzania vinaagiza wanga kutoka nje ya nchi kwa bei ghali wakati uwezo wa kupata wanga kwa wingi upo kwa kutumia zao la mhogo”.


Bi Mariam Mtunguja akiendelea na kazi ndani ya maabara za MARI Dar es salaam


 Hivyo yeye kama mwanasayansi na mtafiti ameamua kuingia maabara na kufanya utafiti wa aina gani ya muhogo ambao una kiasi kikubwa na bora cha wanga ili kuwashauri wakulima na wafanyabiashara kulima zao hilo kwa manufaa yao na serikali kwa ujumla.

Alisema kuwa yeye  ameamua kufanya utafiti huo ili kupata muhogo wenye kukidhi vigezo vya wanga inayotumika viwandani ili wakulima wa zao hilo wanufaike na kilimo cha zao hilo.

“ Utafiti huu utakamilika mwezi wa tisa ambapo tayari itakuwa imefahamika ni aina gani ya muhogo inatakiwa kulimwa kwa ajili ya uzalishaji wa wanga inayohitajika viwandani” alisema Bi Mariam

Mtafiti huyo alisema kazi itabakia kwa serikali kutafuta masoko kwani anahakika wakulima wanalima mazao lakini hawana pa kuyapeleka kutokana na kutokuwa na masoko ya uhakika ya mazao yao.


Kwa habari hii ni neema kwa zao la muhogo ambalo kila ufikapo msimu wa kilimo lenyewe halifikiriwi kulimwa kama ilivyo mazao ya mahindi, mpunga Maharage na mengineyo kwani muhogo hulimwa kama zao la kuzuia njaa kutokana na uwezo wake wa kustahimili ukame hivyo wengi hulima kwa tahadhali na si kwa faida kama ilivyo kwa mazao mengine.

Hivyo kama wazalishaji wa viwandani wakiamua kukaa na wakulima wakapeana elimu ya kusindika unga wa muhogo unaotakiwa kwenye viwanda vyao, Tanzania inaweza kumaliza tatizo la njaa na umasikini kwa wakati mmoja.



Akiongea na mwandishi Bwana Athumani Idd mkulima wa mihogo katika kijiji cha Gwata mkoani Pwani alisema “serikali itutafutie soko la mihogo ili tunufaike kwani zao hili ni chanzo cha ajira kama ilivyo kwa mazao mengine”. Amesema kuwa huwa wanapata faida kiasi wakati wa mfungo wa waumini wa kiislam kwakuwa hutumia mihogo kwa ajili ya kuandaa futari vinginevyo kwao wao ni hasara tuu ila hulima kwa kuwa hawana ajira nyingine zaidi ya kilimo.

Nae Bwana Richard Kasuga afisa mawasiliano wa wizara ya kilimo na chakula alisema kuwa serikali inasubiri matokeo ya utafiti huo ili watakapo anza kutangaza bidhaa ya unga huo wawe na ukakika ya kuwa bidhaa hiyo ipo. “hatuwezi kutafuta masoko bila kuwa na uhakika wa bidhaa hiyo kuwepo,  hivyo pindi utafiti utakapokamilika watatujulisha ndipo tutukapoanza kutangaza kwa wenye viwanda na nchi zingine wanaotumia bidhaa hiyo.

 Hivi sasa zao la muhogo limezidi kupata umaarufu zaidi, ambapo  kadri siku zinavyosogea linabadilika   na kuwa zao la kibiashara hii ni kutokana na tafiti zinazoendelea kufanywa hapa nchini.

Julias James kijana anayejishughulisha na kilimo cha  mihogo mkoani Pwani alisema “tangu nizaliwe sijawahi ona zao ambalo kila sehemu ya zao ni faida kama mhogo, mzizi ni chakula, shina ni kuni wakati majani ni mboga, jamani kwani twataka kitu gani kifanyike”. Hakuishia hapo bali alizitaja faida ya kulima zao hilo ambapo alisema ni zao linalostahimili ukame na halihitaji rutuba nyingi hivyo kumpa urahisi mkulima kwa kumpunguzia gharama.

Nae mkulima wa mboga mboga katika eneo la mchicha  jijini Dar es salaam ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema kuwa anatamani sana kama serikali ingeruhusu wakulima wapewe mbegu mpya za mihogo kwani tangu watangaze kuwa utafiti wa kupatikana kwa mbegu mpya isioathiriwa na magonjwa umefanikiwa hatuioni madukani sasa nini faida ya kututangazia”?  aliuliza swali ambalo lilikosa mtu wa kulijibu.

Tanzania tumekuwa tukiachwa nyuma na nchi kama  kama vile Afrika  ya kusini, Nigeria,Ghana, na zingine za ulaya kama vile Italia, Thailand na kwingineko ambako kuna viwanda vikubwa kwa ajili   ya kusindika mihogo na kufanya wakulima wa nchi hizo kunufaika na kilimo hicho.

Ikumbukwe yakuwa katika kuijenga Tanizania salama bila njaa ni lazima  kanuni za kilimo bora zifuatwe, matumizi ya mbegu bora, bila kusahaku kufuata utabiri  wa hali ya hewa ili kuenenda sawa na kauli mbiu ya kilimo kwanza na si kwanza kilimo.