Mkuu
wa kituo cha polisi cha Nyamboge kilichopo katika kata ya Katoma
wilayani Geita mkoani Geita amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira
kali baada ya kukutwa akitaka kufanya mapenzi na mwanafunzi katika
chumba anachoishi mwanafunzi huyo(Geto).
Tukio
hilo limetokea juzi Jumapili majira ya saa tatu usiku ambapo wananchi
wakiwa na marungu na mikuki waliweka mtego wa kumnasa mkuu huyo mwenye
namba E 2837 Koplo Venance.
Akielezea
tukio hilo binti huyo (jina linahifadhiwa)(19) anayesoma kidato cha nne
alisema siku ya jumapili mkuu huyo wa kituo alituma maaskari wawili
wiki jana wakaenda kumkamata.
"Hata
sijui kosa langu,nilikamatwa nikalazimika kwenda na nilipofika alianza
kunilazimisha natembea na mwalimu wangu,nilipokataa nilianza kupigwa na
kulazimishwa kuandika maelezo",alisema mwanafunzi huyo.
Alisema
baada ya kukataa kuandika maelezo alipelekwa rokapu na muda mfupi
baadaye alifuatwa na askari mmoja kati ya wale waliomfuata anapoishi,
alianza kuandika maelezo na kumlazimisha kusaini.
Alisema
baada ya kugoma kuandika alipigwa sana na kuamua kusaini kutokana na
kutishiwa kufungwa na baada ya kusaini aliitwa na OCS huyo na kumwambia
aende nyumbani lakini arudi jioni ana shida naye ya muhimu sana lakini
hakurudi kutokana na kuchoka na kipigo alichokipata kituoni hapo.
"Kutokana
na mkuu huyo wa kituo kutuhumiwa na mwanafunzi kuwa anamtaka kimapenzi
ilibidi awaambie wanafunzi wenzake na wananchi na baada ya hapo
wakatengeneza mtego ili wamnase",walisema mashuhuda wa tukio hilo.
"Siku
ya jumapili mkuu huyo wa kituo alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo
na kuomba wafanye mapenzi kwa kuwa wenzake anaoishi nao hawakuwepo
lakini aligoma kufanya hiyo ",walisema mashuhuda wa tukio hilo na kuongeza:
"Kutokana
na mtego wa wananzengo,muda mfupi wananchi waliokuwa wamemuona OCS
anakwenda kwa binti huyo walifika hapo na kufunga mlango kwa nje na
kuanza kupiga mwano".