.
Aanza kwa kuunda timu itakayounda upya Jumuiya ya Watanzania UK na kuhusisha wadau wote;Azungumzia suala la uraia pacha na Rais Ajaye katika uchaguzi 2015;Kuunda Saccoss ya watanzania UK na Jumuiya ya Wanawake.Na Abraham Sangiwa Itikadi Siasa na Uenezi - CCM – UNITED KINGDOM.
Mwenyekiti Mpya wa CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma akitoa nasaha na shukrani zake.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM UK Ndugu Maina Owino akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti Mpya CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma.
Wajumbe,
wanachama wa CCM UK na watanzania waishio uingereza wakimsikiliza Kwa
makini Mwenyekiti Mpya wa CCM Ndugu Kapinga Kangoma (hayupo pichani).
Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Maina Owino akipiga kura yake katika Uchaguzi wa Mwenyekiti Mpya wa CCM UK.
Kaimu
Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela(mwenye koti jeupe) akichukua
taarifa ya yanayojili katika mkutano huo pembeni yake ni Ndugu John
Lyimo Katibu wa Uchumi na Fedha CCM UK.
Katibu
Itikadi Siasa na Uenezi CCM UK Ndugu Abraham Sangiwa akitekeleza haki
yake ya kikatiba kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti Mpya CCM UK.
Meza
kuu ikimkaribisha Mwenyekiti mpya wa CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma
kuchukua Nafasi yake kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti CCM UK Ndugu Sukwa
Said Sukwa, Mwenyekiti mstaafu Maina Owino na Abraham Sangiwa – Itikadi
na Uenezi CCM UK.
Katibu
wa CCM Shina la Birmingham Bi. Lilian Barongo ambaye pia anakuwa Katibu
mteule wa Jumuiya ya Watanzania UK Akibadilishana mawazo na Kaimu
Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela kabla ya kuingia katika ukumbi wa
mkutano
Wanachama, wajumbe na watanzania waliohudhuria mkutano wakipata maankuli ya ukweli.
Café 12 misosi na vinywaji palikuwa hapatoshi.
Baadhi ya wanachama na watanzania walipatiwa uhakiki kabla ya kuingia ukumbini.
==============
Mkutano mkuu wa wanachama wote
CCM UK ambao uliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM UK umefanyika
katika jiji la Reading siku ya Jumamosi tarehe 30/08/2014 ambapo wagombea
watatu walipitishwa na vikao vya awali kugombea nafasi hiyo ni Ndugu Said
Surur, Peter Gabagambi na Kapinga Kangoma na kujaa shamrashamra na nderemo
na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM UK NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI
UINGEREZA pia viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED
KINGDOM aliyeng”atuka Ndg Maina Ang'iela Owino, Makamu Mwenyekiti
Ndugu Said Sukwa, Kaimu Katibu Ndugu Leybab Mdegela, Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham
Sangiwa, Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi
na Fedha Ndugu Mohamed Upete, Viongozi wa mashina, wajumbe na wanaCCM toka
mashina ya CCM UK.
Mkutano huo ulianza kwa Katibu mwenezi ndugu Abraham Sangiwa kuwashukuru
Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni na kujiunga
na Chama Cha Mapinduzi hapa UK ili kuleta chachu ya mabadiliko ndani na nje ya
chama kwa manufaa ya watanzania wote kwa ujumla.
Ndg Sangiwa aliwakumbusha kuwa
kujiunga na CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya
juhudi za kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM.
Pia kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.
Akimkaribisha Mwenyekiti
mstaafu Ndugu Maina A Owino, Kaimu Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela
aliwashukuru wanachama wote kwa kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi ili
kufanikisha malengo ya mkutano huo na zoezi la kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM
UK na kuwafahamisha wanachama wagombea wawili Ndugu Said Surur na Peter
Gabagambi waliopitishwa na vikao vya awali wamejitoa katika kinyanganyiro hicho
hivyo mgombea pekee aliyebaki katika nafasi hiyo ni Ndugu Kapinga Kangoma, pia
ripoti ya Tawi iliwakilishwa na itasambazwa na viongozi wa mashina kwa
wanachama wote.
Katika hotuba yake Mwenyekiti
mstaafu Ndugu Maina A Owino aliwashukuru wana ccm na watanzania wote kwa ujumla
kwa ushirikiano waliompa katika awamu yake ya kwanza ya uongozi tangu
kuanzishwa kwa tawi hapa UK ambapo awamu yake imefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha
wana CCM na watanzania kwa ujumla katika miji mbalimbali hapa UK ; Aidha
alisema baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko endelevu,
kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na kwamba CCM
na serikali yake inaendelea kujiimarisha kuyakabili kwa mikakati na mipango
endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina aliwakumbusha Wana CCM UK Kuwa
mchango wao unahitajika na ni wamuhimu katika kuleta mabadiliko
yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali muhimu za kimaendeleo na
kichumi kuanzia na watanzania wanaoishi hapa UK na nyumbani.
Katika hotuba yake ya
ushindi Mwenyekiti Mpya wa CCM UK ndugu Kapinga Kangoma aliwashukuru wana CCM
UK kwa Imani waliyoionyesha kwake na kumpa kura za ushindi na kusema “hakika
kwangu na familia yangu ni heshima kubwa. “
Sasa tuna kila sababu
ya kuanza awamu ya pili ya Uongozi wa CCM UK Kuunganisha maisha ya watanzania
hapa UK na diaspora kwa ujumla na kutengeneza platform itakayoleta uongozi
mahiri kuelekea hiyo awamu mpya, hivyo napenda kuwajulisha kwamba awamu hiyo
imeanza leo kwa kunichagua mimi kuwa mwenyekiti wenu.
Ninaanza kazi yangu kwa
kuunda upya Jumuiya ya watanzania hapa UK hivyo CCM UK itaweka uzito wote
unaostahili kuhakikisha kuwa tunaunda jumuiya itakayotokana na Watanzania
wenyewe na sio kushirikiana na ubalozi.. hatutaki tena kukaa na ubalozi eti
kutengeneza jumuiya ya Tanzania hapa UK, uzoefu unaonyesha kuwa tukishakuwa na
ubia na ubalozi malengo ya jumuiya yanakuwa sio endelevu..hasa kama anapatikana
balozi ambaye hana interest na jumuiya za Kitaanzania; basi inakuwa rahisi sana
kuibomoa. Hivyo leo naanza kazi kwa kuunda jumuiya ya watanzania hapa UK,
ambayo itafanya kazi ya kuunganisha mikakati na taasisi zingine zenye malengo
tofauti na CCM (hapa UK) ili mradi mwisho wa siku waje na jumuiya ambayo haina
harufu ya serikali japo watafanya kazi na ubalozi kama wadau pale inakapobidi
na terms and conditions will-apply. Hivyo namteua bwana Abdulaziz Jaad kuanza
mchakato huo yeye ni msomi mzuri na ana uzoefu wa hapa na kule nyumbani kwani
sehemu zote mbili ameshafanya kazi kwenye taasisi mbalimbali nitamsaidia kwenye
kila hatua ili afanikiwe na jumuiya ipatikane haraka. Naomba nimtambulishe
kwenu ili mtakapomuona analeta mapendekezo kwenye miji yenu msimwangushe ili
tuanze rasmi kutumikia kizazi chetu na kijacho; kwa kuanzia atasaidiwa na
Hussein Chang’a toka Reading na katibu wa kamati hiyo atakuwa Mwanasheria
Lilian Barongo toka Birmingham; wote hao ni wasomi wazuri sana nina hakika
watakuja na SCIENTIFIC APPROACH kuhusu suala hilo.
Suala la pili ni
kuifanya diaspora kuwa soko au kutumia fursa za sanaa kwa vijana wetu wa
nyumbani na wa hapa ili kuendeleza vipaji walivyonavyo kwa kuunganisha soko la
UK la music na sanaa zingine na lile la nyumbani. Mfano ni wenzetu wa nchi kama
Nigeria na hata Ghana ambapo diaspora zao zimeshiriki katika kutambulisha
vipaji vya nchi zao katika masoko ya dunia. Hivyo diaspora ya Tanzania lazima
ifanye kazi za kuunganisha masoko ya nchi zetu kwa kuanza kufungua njia za bidhaa
mbalimbali ikiwemo sanaa. Nitaunda timu ya vijana wa ccmUK na wengineo ili
waanze kuandaa strategy ya mpango huo na timu nyingine ambayo itaanza kujenga
mfumo wa kuunganisha mtandao wa masoko ya bidhaa mbalmbali kwa kutumia mtandao
wetu hapa UK.
CCM na rais ajaye..
Ndugu wana-CCM-UK na
watanzania wenzangu kama mnavyojua kwamba nchi yetu mwaka ujao itaingia kwenye
kinyang’anyiro cha kumpata rais mpya baada ya mchapa kazi Jakaya Kikwete
kumaliza muda wake kikatiba..na kwa vyovyote ccm ndio itakayoleta rais
mpya..kwani vyama vingine bado vina safari ndefu mpaka kuja kuongoza TZ. Na
tukumbuke kuwa rais ndiye muhimili wa mambo yote ndani ya nchi na hivyo akija
rais bomu mafanikio yaliyopatikana katika nchi yetu yatapotea...niwakumbushe tu
kuwa rais anayemaliza muda wake ametekeleza vizuri sana majukumu yake yaliyomo
kwenye ilani ya uchaguzi hivyo chama kinahitaji mtu bora zaidi ya Jakaya ili
aweze kuendeleza pale atakapoishia Jakaya kikwete. Na sasa nchi ipo kwenye
hatua za mwisho za kuanza kuuza gesi na labda baadae mafuta hiyo ni changamoto
kubwa sana kwa rais ajaye. Sasa kuna makundi mengi yanayojionyesha kuutaka
urais wa kupitia chama chetu na wote wanasifa mbalimbali kikubwa sio wao
kujinadi maana mtu akijinadi hataji mabaya yake atajisifia na kuonyesha mambo
yako safi..kumbe anaficha mambo mengi na ukichukulia watanzania wa vijijini hawana uwezo wa kuwang’amua na
kuwapembua..Hivyo diaspora ya Tanzania tuna jukumu la kusaidia kupeleka pressure kuhakikisha watu wenye dhambi na
wasio na uwezo wasipate nafasi hiyo nyeti. Issue hapa sio tu ufisadi bali pia
uwezo wa kuongoza nchi. Maana mtu anamsema mwenzake kuwa ni fisadi as if kipimo
tumeshakiweka kwamba kama wewe sio fisadi basi hata kama ni mjinga basi
unaruhusiwa kuupata urais wa Tanzania; Hiyo sio kweli; we need a capable person with integrity. Sisi
hapa UK na sehemu zingine za huku ughaibuni tunawajua sana hawa viongozi kwani
wanafika sana na tumeshaongea nao mara nyingi. Authenticity zao tunazijua, How
reliable they are tunawajua, lakini pia tuna access ya information kuliko wale
wa vijijini..hivyo tukinyamaza hatuitendi haki jamii yetu na tunaongeza mzigo
kwa watoto wetu hapo baadae waanze tena kupambana na majanga hayohayo ya
viongozi wabovu kwani tukiwaacha leo bila ya kuwasema watawaweka na hata watoto
wao... hivyo ninaunda idara ya siasa ambayo itaratibu matamko mbalimbali ya
kichama yenye lengo la kujenga na sio kumhujumu mtu yeyote..
Hope hiyo
itasaidia kujenga siasa bora ndani ya chama cha mapinduzi. Nitaboresha idara ya fedha ili kuhakikisha chama
kinajitegemea ikiwa ni pamoja kuanzisha SACCOS itakayoanza kujenga mitaji ya
biashara na hata baadae kuwa na benki yetu hapa UK maana tunaweza kuwa na
skills lakini bila mitaji inabaki kuwa ndoto za alinacha. Pia nitaimarisha
idara ya miradi ili iweze kusaidia kuingiza
ideas za watu mbalimbali kwenye uchumi wa chama kwa ubia na watu hao.
Hivyo wanachama mnakaribishwa kuleta ideas zenu.
Nitaboresha pia idara
ya wanawake na watoto ili kupata mchango kutoka kundi letu muhimu na mnajua
uki-mpromote mwanamke umemsaidia pia mtoto. Hivyo mchango wa jumuiya ya akina
mama tunaihitaji sana hapa ccm UK. Sijapata mtu wa kuziba nafasi hiyo
nitashauriana na wadau wenzangu kumpata mama atakayefaa kusuka jumuiya hiyo ya
chama na kuieneza kwenye kila mji ambao una shina la ccm,,ndo maana sikuweza
kukurupuka na jina lolote ili kuleta maana nzuri ya nafasi hiyo. Jina au team
nzima ya UWT itafuata baadae.
Mwisho nimalize kwa
hoja ya uraia pacha kwani hivi karibuni mheshimiwa rais wa Tanzania amekuwa na
nafasi mbalimbali za kuzungumzia diaspora, kwanza kule marekani na hatimaye
juzi pale Dar es salaam. Mambo muhimu aliyoongelea ni kuhusu watu wa diaspora
kuto kuongelea mambo yetu kwa uzito unaostahili. Japo sikubaliani na mhesh.
Rais kuhusu dhana ya kuwakataza wana-diaspora kuhoji mambo mbalimbali ya
nyumbani kitu ambacho ni haki yetu ya msingi,,lakini naomba pia nimuunge mkono
mhesh.Rais kwamba ni kweli Watanzania wa diaspora hatujahamasika vya kutosha na
kushiriki kwenye uwanja wa habari muhimu za mambo yanayotuhusu bali tumekuwa
wepesi wa kujadili mambo madogomadogo tu.
wengi wetu ni wepesi sana wa kutoa
kauli nzito vichochoroni lakini hatufanyi hivyo hadharani. Woga huu lazima
tuuache kwani hoja zisipojadiliwa na mzazi zinabaki zikimsubiri mtoto wako akue
halafu aje afanye kazi hiyohiyo!!!kwanini tusimalize majadiliano sasa? Hivi
sasa kwenye mitandao ya jamii kuna hoja nyingi zinajadiliwa na watu walioko
nyumbani wakiituhumu diaspora na kuonyesha kuwa hatupaswi kupewa uraia pacha
kwani nchi haitakuwa salama..
lakini hoja za kuhoji mantiki hiyo zinakuwa chache
sana kutokea upande wa diaspora. Hivyo nichukue nafasi hii kuwahimiza tuongeze
kasi ya kutumia mitandao ya kijamii kwani hoja zinazotuhusu zinaandikwa na watu
wengine na hivyo wanapotosha.
Nawashukuruni sana wote
naomba nifunge kikao na turejee kwenye miji yetu salama.
IMETOLEWA NA ABRAHAM SANGIWA
IDARA YA ITIKADI, SIASA NA UENEZI CCM TAWI LA UINGEREZA
01.09.2014.