Binti mmoja mkazi wa
kijiji Lugombo kata
ya Kandete Wilayani Rungwe
Mkoani Mbeya Getina
Karinga miaka {24} ameingia katika wakati mgumu
baada ya kuozeshwa ndoa ya mkeka
kwa nguvu na wazazi
wake baada ya
kufuniwa na
mwanaume wakati akifanya
tendo la ndoa chumbani kwao.
Tukio hilo la kushangaza
limetokea baada ya
kijana huyo kwenda kwa
wazazi wa binti
huyo kwa lengo la
maongezi ya kawaida na
kujikuta akiambulia kipigo kikali kutoka kwa mama
mtu baada ya kufumwa wakati
akifanya tendo hilo chumbani kwa mama yake
na binti.
Hata hivyo
kutokana na hali
hiyo
mama huyo aliweza
kuangua kilio kikubwa baada
ya vijana hao kuto onyesha ishara
ya kuacghana na kitendo hicho mara baada ya kufumwa
wakati wakifanya kitendo
hicho na kwamba kabla ya
tukio mama mtu alifika
na kuwa muru kuondoka mara
moja lakini kutokana na
wapendanao kunogewa na
tendo hilo walijikuta
wakiendelea kufanya bila kujari uwepo wa
mama yao na kupelekea mama mtu
kupatwa na hasira na kuchukua
mfagio na kuwachapa .
Kwa mujibu
wa mama huyo ambaye
hakutaka kutajwa jina lake
hadharani alisema mnamo
majila ya sambili za usiku akiwa
ametokea kwenye shughuri zake za kawaida aliweza
kukuta milango ya nyumba yake
ikiwa wazi na kuamua kuingia
lakini baada ya kumwita binti
yake alijibiwa arudi aliko tokea
, lakini aliamua kupiga moyo
konde na kuamua
kosogea zaidi na kumkuta mtoto wake akifanya kitendo hicho
na kuamua kuita watu.
“Nimeona aondoke
nyumbani kwangu kwani amekuwa akinidharau bila kujari kwamba mimi ni mama yake na
hadi kufikia hatua ya kufanya
mapenzi na mwanaume mwingine nyumbani kwangu kitu ambacho ni dharau kubwa ,
na mpaka sasa nimemwozesha na
kutoa baraka zangu zote
kwani nimechoka vitendo anavyo
nifanyia kwani mda
wote amekuwa akifika nyumbani akiwa amelewa pombe
kupita kiasi na mda
mwingine nimekuwa nikimfuma
kwa macho yangu akiwa
anavuta bangi na sigara.” Alisema
mama mtu.
Kwa
upande wa binti huyo alisema yuko
tayari kuolewa na kijana
huyo na kwamba anawashukuru wazazi wake
kwa hatua walio fikia kutokana na kwamba amekaa miaka mingi sana akiwa nyumbani
kwao bila kuolewa na kwamba sasa atakuwa
huru katika kumpatia mme
huduma yake muhimu, na huku mwanaume akifurahia ndoa
hiyo kutoikana na kwamba
muda wote walikuwa wakimbania
mwanamke huyo wakidai
anatabia mbaya kitu amacho kwake si kweli..
Mtendaji wa
kata hiyo huruma mwakyusa mbali
na kukili kutokea kwa tukio
hilo alisema wameshindwa kuendelea na
kesi hiyo kutokana na kwamba
wazazi wa binti
huyo wamekataa kumpokea binti yao
kwa madai ya kuwachafua na kuamua kumuodhesha
bila mahali.