Monday, August 4, 2014

PASTOR MIAMBA AJIUNGA NA CHAMA CHA WANANDOA


 

Pastor Emmanuel Myamba muigizaji maarufu Tanzania amefunga ndoa na mke "Praxceda" visiwani Zanzibar na kuweka historia tena kwa muigizaji aliyefanya harusi iliyokwenda sawa
na hadhi yake.Kwa mujibu wa ripota aliyekua kwenye eneo la tukio.....ameijuza AMESEMA harusi hiyo itakua miongoni mwa harusi zitakazo weka historia Visiwani Zanzibara kutokana na zawadi waliyopewa Pastor Myamba na mkewe ikiwemo gari jipya pamoja na pesa taslimu milioni 250

 

MWANAMKE AIBUA MSHANGAO BAADA YA KUJIFUNGUA WATOTO KWA STAILI YA KIPEKEE

MKAZI wa Kijiji cha Lupili wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, Tecla Kazimili (24), amejifungua watoto wanne, watatu wa kike na mmoja wa kiume kwa njia ya kawaida katika hospitali mbili tofauti na siku mbili tofauti.

Katika hospitali ya kwanza, ambayo ni zahanati ya Kijiji cha Lupili Agosti mosi mwaka huu, Tecla alionekana ana ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja ambapo wakati wa kujifungua, alizaliwa wa kiume akiwa na kilo 1.6, lakini kwa bahati mbaya alikufa.

Hata hivyo, wakunga walishuhudia mzazi huyo akiendelea kuwa na dalili ya kujifungua mtoto mwingine, lakini akawa amegoma kupita katika njia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Marko Mwita, alisema baada ya kutokea kwa hali hiyo, alipigiwa simu kuombwa msaada.

“Baada ya kupokea taarifa hiyo majira ya usiku, nilituma gari la wagonjwa kukimbilia kwenye zahanati hiyo iliyopo umbali wa kilometa 60 na kumleta mama huyo katika Hospitali ya Wilaya kwa huduma zaidi,” alisema.

Alisema alipofikishwa hospitalini hapo, Tecla aliendelea kujifungua mpaka kesho yake hatimaye idadi ya watoto ikafikia wanne.

“Hili ni tukio la kwanza katika hospitali hii ya Wilaya, mtu kujifungua watoto wanne, ni matukio yanayotokea mara chache, lakini tunamshukuru Mungu mzazi anaendelea vizuri huku watoto wake watatu, wote wa kike kila mmoja akiwa na uzito wa kilo mbili,” alisema.

Dk Mwita alisema watoto hao wanahitaji uangalizi na msaada wa hali ya juu, kwani ni rahisi kupata maambukizi. Alitoa mwito kwa jamii kumsaidia mama huyo, kwani watoto hao wanahitaji msaada wa hali na mali kwa kuwa maziwa ya mama pekee hayatawatosheleza.

Akizungumzia historia yake ya uzazi, Tecla alisema watoto hao ni uzazi wake wa nne na katika ule uliopita, watoto wote aliowazaa walifariki dunia katika umri tofauti, lakini wa utoto.

“Kitendo cha watoto kufa baada ya kufikisha umri fulani, kilimfanya mume wangu anifukuze, nikalazimika kurejea nyumbani kwetu ambapo nilipewa ujauzito na kijana mwingine,” alisema.

Alisema wakati anahudhuria kliniki, alielezwa kwamba alikuwa na zaidi ya mtoto mmoja baada ya kutoa taarifa kuwa anaona tabia ya ujauzito huo ni tofauti na uzazi wake uliopita.

“Namshukuru Mungu kwa kunipatia watoto hawa na naiomba Serikali inisaidie kuwatunza ili wakue vizuri kwani peke yangu siwezi,” alisema. Kwa mujibu wa Tecla, aliumwa uchungu kwa siku tatu na alimaliza kujifungua Agosti 

WAKULIMA WAASWA KUFUATA MBINU BORA ZA KILIMO

Kwani ni njia pekee ya mafanikio katika kilimo

Hayo yamesemwa na bi Rose Mongi ambaye ni mtafiti na mtaalamu wa ngano na maharage katika kituo cha utafiti na kilimo Uyole mkoani Mbeya ARI. Amesema wakulima wengi hawajapata mazao kama walivyokuwa wakitarajia kutokana na wao wenyewe kutokuzingatia kanuni na njia bora za kilimo ambazo wanatakiwa kuzifuata ili kupata mafanikio makubwa katika kilimo. Japo kuwa kulikuwa na mvua za kutosha sehemu nyingi za nyanda za juu kusini  laikini wakulima wengi wamepata mavuno machache kutokana na mfumo wanaoutumia wakulima wenyewe. Pia amesema kuwa wakulima wengi siku hizi wamekuwa wakaidi wa kufuata kanuni hizo kutokana na kuwa na propaganda nyingi katika sekta ya kilimo, akidai kuwa hiyo ni changamoto kati ya changamoto nyingi nambazo zinaikabili sekta ya kilimo Tanzania. 



 Bwana  Anthon Elanga msaidizi wa Bi Rose katika utafiti
 Rose Mongi mtafiti wa mbegu za ngano na maharage ARI Uyole Mbeya


 Bi Rose amesema kuwa wao kama wataalamu wapo kwa ajili ya wakulima ili wawatumie vile watakavyo, "sisi kama wataalamu tunafurahi sana pale wakulima wanapotuita ili tuwaelekeze njia bora za kilimo kwa ajili ya manufaa yao wenyewe kwani sie tupo kwa aajili yao na tumeajiriwa na serikali ili tuwatumikie wao". Pia ametoa wito kwa wakulima kufika kituoni hapo ili waweze kujifunza mengi kuhusu kilimo kwani wakifika mahali hapo waweza kujifunza hata kimatendo na mwisho wa siku kupata manufaa katika kilimo. "Tunataka kuwa na Tanzania yenye wakulima wanaojua nini wanafanya katika kazi zao, kwani kilimo chenye manufaaa bado hakijafanikiwa Tanzania, tunatamani sana tena sana"
Hata hivyo bi Rose alisema japokuwa kuna changamoto ya kuwa na mbegu feki madukani kitu ambacho kinasababisha wakulima kutokuwa na imani na mbegu za madukani, lakini amewahakikishia wakulima kuwa wanauhakika na mbegu wanazozalisha kituoni hapo.
 hivyo amewaasa wakulima kuwa waangalifi wanapokwenda madukani kwa kuzitambua nembo halisi katika pakiti za mbegu wanazonunua.


Shamba la ngano

Kituo hiki ambacho kipo mkoani mbeya kimekuwa kikifanya utafiti wa mazao mbalimbali ili kupata mbegu bora kwa ajili ya wakulima. Na pia wamekuwa wakifanya utafiti wa udongo pamoja na magonjwa kwa mimea ili kumuondoa mkulima kutoka kwenye kilimo cha kupata chakula tuu bali wanataka mkulima apate hata mazao ya ziada ili kupata faida zaidi kwa kuyauza mazao hayo. 




 
 Bi Rose akichunguza aina ya ugonjwa kwa kutumia darubini
 Bi Benadetha Rugumisa yeye ni biotechnology kituoni hapo

Akieleza kuhusu changamoto wanazozipata wakulima Bi Rose amesema kuwa wakulima wamekuwa wakiweka mambo ya imani mbaya hata katika kilimo kitu ambacho amekikemea vikali na badala yake amewasihi wakulima kutofuata maneno ya watu bali wafuate kanuni ambazo wataalamu wa kilimo wamekuwa wakiwafundisha. Ametoa mfano wa wakulima kutoamini juu ya mbegu zinazouzwa madukani kwa kusema kuwa si mbegu nzuri kwa afya za binadamu eti kwasababu tu zimeboreshwa, na badala yake Bi Rose amesema kuwa wao ni watanzania halisi na hawawezi wakafanya kitu kibaya kwa watanzania. Pia amesema hawawezi kutengeneza mbegu mbaya kwani hata wao ni watumiaji wa mbegu hizi  hivyo wako makini saana  katiaka kutafiti mbegu hizo. Hata hivyo amewasihi sana kutumia mbegu bora zinazouzwa madukani na kuachana na imani mbaya ambayo imewaacha wakulima wengi kuingia hasara kila wanapolima mazao na kuzidi kubaki katiak maisha duni siku zote.
Akifafanua kuhusu uboreshaji wa mbegu alisema kuwa mbegu zilizoboreshwa ni zile zilizochanganywa sifa za mbegu mbalimbali katika mbegu moja ambayo ndiyo iliyoboreshwa kwa kuziunganisha halisia zake {cross}. Na uboreshaji wa mbegu hufanyika kwa njia halisi bila kuongeza kitu kingine chochote ndani yake. 






 


Akiongea kuhusu maharage, Rose amesema kuwa msimu huu wa kilimo uliopita wametafuta sample ya majani ya magonjwa mbalimbali kutoka kila mahali ili kutambua magonjwa shambulizi ya maharage ili waweze kugundua magonjwa sumbufu na mwisho wa siku waweze kudhibiti magonjwa hayo kwa kuzalisha mbegu stahimilivu wa magonjwa hayo ama kwa kutafiti dawa ambayo itadhibiti magonjwa hayo.





Mwisho amewasihi wakulima kutumia maonyesho ya wakulima yajulikanayo kama nane nane amabay hufanyika kila mwezi August {8} kwa manufaa zaidi kwa kuwauliza wataalamu wa kilimo maswali yenye manufaa na kutaka kujifunza kutoka kwao hata kimatendo baddala ya kuyatumia maonyesho hayo kwa kujifurahisha. Amewasihi sana kutembelea Banda la kilimo nanenane mkoani Mbeya na wao wako tayali kwa moyo mkunjuf ili kuwasaidia wakulima, na baada ya maonyesho pia waweze kufika kituoni uyole kwa msaada zaidi. Pia ametoa wito kwa vyomba vya habari kuwaunga  mkono wataalamu wa kilimo kote nchini kuwaelimisha wananchi njia ya kilimo bora na matumizi ya mbegu bora.

MWANAMKE ALIYEJERUHIWA KWA BOMU LA POLISI AKATWA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA


Mkazi wa Mbagala Zakhiem, Mwanaharusi Hamis amepoteza kiganja chake cha mkono wa kulia baada ya kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu lililorushwa na polisi wakati wakitawanya wananchi. Mwanaharusi alilipuliwa na bomu hilo Agosti Mosi 2014, saa 3:00 usiku alipokuwa anatoka ndani kwenda msalani.Akizungumza na mwandishi jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wodi ya Mwaisela namba mbili alikolazwa, alisema tukio hilo limebadilisha kabisa mustakabali wa maisha yake.Mwanaharusi, ambaye ni mama wa watoto wawili alisema alikumbwa na madhila hayo wakati polisi walipokwenda mtaani kwao kumkamata mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki. 

Alisema walipofika, vijana waliokuwa maeneo hayo waliwarushia polisi mawe, ndipo polisi walipofyatua mabomu ya machozi na risasi kuwatanya wananchi hao.
 
“Ilikuwa saa 3:00 hivi mimi na watoto wangu tukiwa ndani hatujui nini kinachoendelea nje, ghafla tulianza kusikia milio ya risasi na mvumo wa kitu kuelekea upande wa ilipo nyumba yetu. Wakati huo nilikuwa natoka ndani kwenda msalani, nikaona kitu kimenipiga na kunichana sehemu za mkono na miguuni, baadaye nikagundua kilichonipiga kilikuwa bomu,”alisimulia Mwanaharusi.
 
Alisema baada ya tukio hilo polisi walimpelekea kituoni kwa ajili ya kupata fomu namba ya tatu ya matibabu (PF3) na baadaye Hospitali ya Temeke, alikopewa rufaa ya kwenda Muhimbili kwa kuwa alikuwa akitoka damu nyingi.
 
“Nimechanganyikiwa. Mimi ndio mtafutaji wa familia, mwanangu wa kwanza amemaliza kidato cha nne na wa pili ana miaka tisa,” alisema.
 
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Temeke, Kienya Kienya alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema ufafanuzi utatolewa leo na kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.