Thursday, November 27, 2014

SHEIKH PONDA ASHINDA RUFAA YAKE

  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo huku wakipaza sauti baada Sheikh Ponda kushinda rufaa ya kupinga hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013. (Picha na Francis Dande)
 Wafuasi wa Sheikh Ponda.
 Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kushoto) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza wakati  akitoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mfuasi wa  Sheikha Ponda akitoka Mahakamani.

 Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam wakati wa kesi ya Ponda.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakiwa wamelizunguka basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakilifukuza basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
 Gari la Polisi.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti.

KAULI YA JULIASI MTATIRO BAADA YA VIONGOZI WA DINI KUCHUKUA PESA WA IPTL


NCHI IMEOZA HADI ALTARENI.... 
Tunapokuwa na nchi iliyooza, viongozi wa dini wako mstari wa mbele kuchukua milungula na hela za rushwa zilizojaa damu na mateso ya kodi za wananchi.Ni aibu mno, sielewi hawa maaskofu wangu wanasimama kwenye altare kufanya nini...ni kufuru na aibu kwa mimi Mkatoliki na wakatoliki wote duniani.
Wakati Bunge linafukuza wezi, ni muhimu na Kanisa Katoliki lifukuze hawa maaskofu walafi na kuwapeleka mahakamani. Kisha kanisa lijivue ushenzi huu, lirejeshe pesa hizi kwa niaba ya watumishi hawa walafi wa fedha na mafisadi.
Shame on you beloved bishops, my bishops...

VIGOGO WALIOTAFUNA MABILION YA ESCROW HAWA HAPA


 Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.

Andrew Chenge (Mb)

Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4. 

 Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8. 

 Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 

 Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4 

 Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4

 Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7. 

 kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

 Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9 

 Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4 

 Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.

Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4. 

Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4
 Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow

 Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006 

Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa. 

 Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
NA HAYA NDIO MAPENDEKEZO YA KAMATI
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWAJIBISHWE KWA KUUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA - MAPENDEKEZO YA KAMATI YA ZITTO

Filikunjombe: Kamati inashauri kuzitangaza benki za Stanbic na Mkombozi kama asasi za utakatishaji fedha


Filikunjombe: Kamati inasha
uri bodi ya Tanesco ivunjwe na TAKUKURU iwafungulie mashtaka ya rushwa.

Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Naibu waziri wa nishati na madini alisema uongo bungeni naye achukuliwe hatua.

Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo amekuwa akisema uongo mara nyingi.

Filikunjombe: Kamati pia imethibitisha kuwa Waziri wa nishati na madini ndiye alikuwa dalali mkuu wa kuunganisha hawa watu

Filikunjombe: Kutokana na sababu hizo hapo juu, kamati inapendekeza kuwa Waziri wa Nishati na madini avuliwe madaraka yake.

Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali utengeuliwe mara moja na aadhibishwe maana ametumia vibaya madaraka

Filikunjombe: Kamati pasipo mashaka imejidhihirisha kuwa Waziri mkuu alikuwa akijua jambo hili ila hakuchukua tahadhari.

Filikunjombe: alisema Mwalimu Nyerere kuwa kumbadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu.

Kwa vyovyote vile, Waziri mkuu anapaswa kuwajibishwa kwa namna yoyote ile ili kurudisha heshima ya serikali maana ameudanganya umma wa Watanzania kwa kusema uongo na kuitete kampuni hewa ya PAP isiyokuwepo

Filikunjombe: Kamati yetu inaamini kuwa Bunge hili litaitumia vizuri taarifa yetu hii

Mh. Spika anna Makinda amehairisha shughuli za Bunge na kusema kuwa kesho asubuhi serikali itatoa kauli zake.

Baada ya serikali kutoa kauli zake hapo kesho asubuhi, Wabunge wengine watapata nafasi ya kuchangia.
 

JAJI WARIOBA AKOLEZA MOTO KATIBA MPYA


Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika ukumbi wa mdahalo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanaharakati wa mambo ya vijana Humphrey Polepole na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba akzungumza katika mdahalo huo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Picha zote: Francis Dande

Waliokuwa wajumbe Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameendelea kuikosoa vikali Katiba inayopendekezwa na kusema kwamba haitakuwa na manufaa kwa Watanzania.


Kadhalika, wamesema Muungano uliopo kwa sasa upo katika hatari ya kuvunjika na kwamba hali hiyo itasababishwa na Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba (pichani), akizungumza katika mdahalo wa kujadili katiba inayopendekezwa uliofanyika ukumbi wa City jijini Dar es Salaam jana, alisema Katiba hiyo imeondoa matarajio ya wananchi waliotegemea kupata katiba ya kuwakomboa katika miaka mingine 50 ijayo.

Alisema Muungano umefika hapa ulipo, umetokana na kudra za Mwenyezi Mungu na hekima za viongozi waliopita kwa kuuendesha kwa hekima licha ya katiba hiyo kubeba changamoto lukuki.

“Mimi nimeshangaa kuona waheshimiwa hawa wananitukana na kunikashfu eti nimemsaliti Mwalimu Nyerere, wanadiriki kutumia nguvu na maneno ya kashfa kupitisha katiba. Katiba haiwezi kupitishwa kwa namna hiyo, katiba ni maridhiano ambayo pia yanashirikisha maoni ya wananchi,” alisema Warioba na kuongeza:“Hata kama Nyerere angelikuwapo leo angeipinga Katiba hii inayopendekezwa.”

Warioba alisema hata kama wataipitisha kwa nguvu, lakini wanatakiwa kufahamu kuwa italeta matatizo baadaye na ni vizuri wafahamu kuwa hata kama itapita itakuwa na matatizo.

Humphrey Polepole, aliitaka serikali kusambaza Katiba inayopendekezwa pamoja na rasimu ya Tume hiyo kwa wananchi ili waisome na kuielewa kabla ya kuipigia kura ya maoni.

Kuhusiana na suala la elimu ya wabunge, alisisitiza kuwa ni vema wabunge wawe na elimu ya kidato cha nne, tofauti na katiba inayopendekezwa inayowataka wawe wanajua tu kusoma na kuandika.

Alisema endapo Katiba itapitishwa kama ilivyo kwamba wabunge wajue kusoma na kuandika pekee, itamuwia vigumu rais kupata mawaziri wenye elimu ya kutosha ya kusimamia shughuli za maendeleo ya nchi.

“Unawezaje kusema wabunge wawe wanajua kusoma na kuandika tu, isipokuwa mawaziri, je, wakichaguliwa wabunge wote ambao uwezo wao ni wa kusoma na kuandika tu, hao mawaziri watatoka wapi na shughuli za maendeleo wataendeshaje?” alihoji Polepole.

Kadhalika, alisema kuwa anashangaa mawaziri kuipigia chapuo Katiba inayopendekezwa na kuipinga serikali tatu, wakati hata wao walitoa maoni wakiitaka muundo wa serikali hizo.

“Mimi nilishiriki katika kikao cha kukusanya maoni ya mawaziri, walipendekeza serikali tatu, na hata baadhi ya mawaziri wakuu nao walipendekeza serikali hizo, na wasitake tufikie huko wanakotaka, wakibisha tunaweza kuwataja,” alisema huku walioshiriki mdahalo huo wakitaka awataje.

Kwa upande wake, Profesa Mwesiga Baregu, alisema Katiba inayopendekezwa ni dalili ya kuvunjika kwa Muungano.

“Nilishangaa sana kuona wajumbe wa lililokuwa Bunge Maaluma la Katiba kufanya sherehe na marais kusherehekea malengo ambayo yameshindwa kufikiwa katika katiba inayopendekezwa, ambayo wananchi wakiisikia wanapata uchungu,” alisema Profesa Baregu.

Aliongeza: “Dalili inavyoonekana hivi sasa Katiba hiyo ndiyo itakuwa chanzo cha kuvunja Muungano huo na tutegemee, huko ndiyo tunakokwenda.”

Mohamed Mshamba, ambaye naye alikuwa mjumbe wa Tume ya Katiba, alisema Tume ilikusanya maoni ambayo yalilenga kulipatia taifa katiba bora, lakini lengo hilo limevurugwa baada ya kuondolewa vifungu vya msingi.

Mdahalo huo ulitawaliwa na ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ambao walikagua kila alieingia katika ukumbi huo kwa kutumia vifaa maalum vya ukaguzi.

Pia, ndani ya ukumbi kulikuwapo na utulivu, tofauti na ilivyokuwa katika mdahalo uliopita ambao baadhi ya watu waliumia kutokana na vurugu zilizosababishwa na kikundi cha watu walisadikika kutoka Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapindiuzi (UVCCM).

Kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza katika mdahalo wa jana, ukumbi huo ulijaa na kupelekea polisi kuwazuia baadhi ya watu kuingia ndani kutokana na kukosekana na nafasi.

Hali hiyo ilisababisha askari polisi kupata changamoto ya kuwaelewesha wananchi hao ambao hawakutaka kukubali kubaki nje.

UTETEZI MREFU WA WATUHUMIWA UKWELI WABAKI KAMATI YA ZITTO




ESCROW kila kona! Wabongo wameibuka na msemo mpya kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha za umma kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wakilitolea tafsiri iliyobeba kichwa cha habari hii kwamba Escrow ni Eneza Siasa Chota Riziki Ondoa Woga. 
Waziri mkuu Mizengi Pinda.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wananchi wamesema mtu akitaka riziki kirahisi ajiingize katika siasa na kuanza kuihubiri pia aondoe woga kama washiriki katika sakata hilo walivyofanya kwa kujipa ujasiri wa kujichotea shilingi bilioni 306 kutoka kwenye akaunti hiyo.
ISIKIE HII
“Sasa nimeamini, ukitaka kuwa tajiri mkubwa katika nchi hii, we eneza siasa, utaweza kuchota riziki (pesa) kubwa sana hususan kama utaondoa woga,” alisema Fred Jimmy ‘Fredwaa’, mkazi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Pamoja na yote hayo, wananchi hao wamesema chochote kitakachofanyika, ni lazima fedha hizo zirejeshwe kutoka kwa wahusika hao, kwani ni fedha za walipa kodi wa Tanzania ambao maisha yao ya kila siku ni ya kubangaiza.

Askofu Mkuu Msaidizi Jimbo la Kagera, Methodius Kilaini.
“Ripoti ya PAC tumeiona na utetezi wa Waziri Sospeter Muhongo pia tumeusikia, lakini hatuukubali. Anadai kuwa Tanesco haina fedha kwa kuwa haijaanza kutengeneza faida, kwamba kwa muda wote imekuwa ikidaiwa tu.
“Sawa, hatukatai Tanesco inadaiwa (bilioni 90 na capacity charge’) lakini si ni kweli pia kwamba Tanesco hiyohiyo ilikuwa inaweka yale mabilioni kwenye ile akaunti ya Escrow?” alihoji mwananchi mmoja aliyejitambulisha kama Justin Sompa, mfanyakazi serikalini jijini Dar es Salaam.
Akaendelea: “Kwa hiyo kwa akili ya kawaida, madeni yanayodaiwa Tanesco hayana uhusiano na fedha za Escrow na ukweli unabaki kuwa kwenye Kamati ya Zitto (PAC), hizi pesa zinatakiwa zirudi mara moja na waliohusika lazima wapandishwe kizimbani na ikibidi wafilisiwe mali zao.”

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
WATU WAFANYA BONGE LA SHEREHE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni jana, kuna habari kuwa, baadhi ya watu jijini Dar na Dodoma kutoka kwenye makundi ya urais 2015 ambao hawakujulikana kambi, walikesha juzi wakila na kunywa kufurahia anguko la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye mbio hizo.

“Kashfa hii kwa Pinda ni anguko kwa uchaguzi wa urais mwakani. Ripoti ya Twaweza ilimtaja kushika nafasi ya pili baada ya Edward Lowassa, sasa kachafuka  ni dhahiri ameshuka kisiasa.
“Unadhani kwa muda uliobaki kufika mwakani atatumia mbinu gani ili atakate kama zamani?” alihoji mmoja wa watu wa kambi hizo.

Watu hao walifurahia zaidi kwa kudai kuwa, kama ni uwanjani Pinda alikuwa akipiga mpira wa penalti ambao ameutoa nje ya uwanja na kuliacha goli (angalia mchoro ukurasa wa kwanza).
WAKATOLIKI WAMBANA KILAINI
Wakati huohuo, baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania wamemtaka Askofu Mkuu Msaidizi Jimbo la Kagera, Methodius Kilaini kujieleza alipewa kitita cha shilingi milioni 80 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Bier, James Rugemalila  kwa ajili ya kitu gani?


 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Hata hivyo, mtu mmoja alilipenyezea Ijumaa jana kuwa, Rugemalila na Kilaini ni marafiki waliosoma pamoja japokuwa bado urafiki huo haujitoshelezi kupeana kiasi hicho cha pesa.
MWANASHERIA MKUU
Aidha, wananchi wamemtaka pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kuachia ngazi na baadaye mamlaka zimpeleke mahakamani kwa kuisababishia hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 20 kama kodi, baada ya kusema uongo kuwa fedha zilizokuwa katika akaunti hiyo, hazikutakiwa kukatwa kodi ya ongezeko la thamani wala mhuri wa stempu.

“Huyu alitoa kauli ya uongo kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) waliotaka kukata kodi, lakini pia aliidanganya Wizara ya Fedha kwa kusema fedha hizo ni za IPTL wakati anajua kabisa kuwa ni za umma.
Kwa kiongozi mkubwa wa serikali kama huyu, anapodanganya na kuisababishia hasara nchi, ni mtu wa hatari sana, hafai kukalia kiti kile, amepoteza sifa,” alisema mwanafunzi mmoja wa mwaka wa pili wa shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyejitambulisha kwa jina moja la Daffa.

 
William Ngeleja.
“Huyu anaonesha jinsi serikali yetu ilivyo na watendaji waliooza, yupo tayari mamilioni ya wananchi wateseke ili mradi tu ashibishe tumbo lake na familia yake. Kwa cheo chake anapata fedha na marupurupu mengi, lakini haridhiki, nchi inatafunwa sisi tumekaa tunaangalia, tunaona kama haituhusu, tuamke jamani,” alisema Daffa akionekana kuwa na uchungu mwingi.
BOSI WA IPTL
Mtu mwingine aliyetajwa kuwa anastahili kufikishwa katika vyombo vya sheria, ni pamoja na mmiliki wa kampuni ya IPTL, Singh Harbinder Sethi ambaye licha ya ukweli kwamba alistahili sehemu ya fedha hizo, lakini kitendo chake cha kuwasilisha nyaraka za kugushi, akiidanganya serikali kuhusu manunuzi ya hisa zake na hivyo kukwepa kodi halali, ni kosa la jinai.

“Kamati ya PAC imeonyesha jinsi alivyokuwa akiidanganya serikali (TRA) kuwa ameuza hisa kwa fedha kidogo wakati ameuza kwa bei kubwa, haiwezekani tuwachekee hawa watu wakati sisi wananchi wetu wanakufa kwa kukosa dawa mahospitalini halafu fedha zetu zinaibiwa kirahisi tu,” alisema Daffa.

Jaji Werema.
Wengine waliotajwa kuhusika na fedha zilizochotwa na ambao pia wanatakiwa kufikishwa mahakamani ni pamoja na Andrew Chenge, mwanasheria mkuu wa zamani, Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, William Ngeleja na  Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba. 
Fedha za Escrow zitapazo shilingi bilioni 306 zilichukuliwa katika akaunti hiyo na kwa mara ya kwanza, liliibuliwa bungeni na mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye hata hivyo, alishambuliwa na watendaji mbalimbali wa serikali, kwa kuitwa mwongo.
Miongoni mwa waliosakama ni pamona na Mwanasheria Mkuu Jaji Werema ambaye alifikia hatua ya kumuita Tumbili. Pia Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo (Pichani), Naibu wake Steven Masele na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

WATU WASHANGAZWA NA KIJANA ALIYEVUA NGUA NA KUBAKI KAMA ALIVYOZALIWA MJINI SHINYANGA

Katika pita pita zake asubuhi hii,kamera za Malunde1 blog zimemnasa kijana ambaye hakujulikana jina lake mara moja akiwa amevua nguo zote na kubaki kama alivyozaliwa na kung'ang'ania kwenye daraja la Kidau(Ibinzamata) mjini Shinyanga barabara ya Mwanza Shinyanga.Mashuhuda wanasema kijana huyo kafika darajani leo asubuhi na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine huku wakisema kuwa huenda amepandisha majini,ama katumia madawa ya kulevya yaliyomchanganya akili
Kijana akikatisha barabarani kwenda upande wa pili wa daraja
PICHA ZAIDI>>>>

Kijana akining'inia darajani,hatukuweza kujua nini kimemsibu kijana huyo
Baadaye aliamua kutoka darajani kisha kuanza kukimbia hivyo barabarani kisha kulala barabarani

Akiwa amesemama barabarani.Mpaka tunaondoka eneo la tukio wasamaria wema walijitokeza kumkamata kisha kumvalisha nguo baada ya tukio hilo kuduma takribani  dakika 30

IPTL: JINSI BUNGE NA MAHAKAMA ZILIVOONYESHANA UBABE WA UTENDAJI KAZI


Ripoti itakayowasilishwa bungeni hii hapa.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiilinda ripoti hiyo usiku kucha.
Wajumbe wa kamati wakiipitia ripoti hiyo kabla ya kuwasilishwa leo bungeni.

Wakati mahakama ikitangaza kuzuia kashfa ya kampuni ya IPTL ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kujadiliwa na Bunge, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesisitiza kuwa mjadala kuhusu suala hilo utafanyika kama ulivyopangwa.
Makinda amesema kamwe hakuna anayeweza kulizuia Bunge kazi zake za kibunge.

”Msianze kuishi kwa wasiwasi, sisi kinga zetu ziko wazi, hakuna atakayetuzuia kufanya kazi za kibunge na zinazopatikana katika maeneo tunayopita na hatuwezi kushitakiwa,” alisema Makinda.

Kwa kauli hiyo ya Spika Makinda, vigogo waliochota, waliofaidika na mgawo na kama taratibu za kisheria za uchotwaji wa fedha hizo kutoka kwenye akaunti hiyo zilifuatwa au la, wanatarajiwa kujulikana leo.

Hiyo ni baada ya ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ya uchotwaji wa fedha hizo kwenye akaunti hiyo, kuanika kila kitu kuhusu kashfa hiyo bungeni leo.

Jana Spika Makinda aliwataka wabunge kujiamini na kujiandaa kwa kusoma ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyotokana na chunguzi wa kashfa ya uchotwaji wa fedha hizo kwenye akaunti hiyo, ili wakidhi haja ya kuchangia mjadala huo leo.

Alisema hayo akijibu miongozo iliyoombwa kwa nyakati tofauti na wabunge; John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP) na John Mnyika (Ubungo-Chadema), bungeni jana.

Cheyo alimuomba Spika Makinda atoe mwongozo ikiwa leo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) itawasilisha taarifa yake na ripoti ya CAG,kuhusu kashfa hiyo kufuatia kuwapo taarifa kwamba jana ilifunguliwa kesi mahakamani kupinga suala hilo kuingizwa bungeni.

”Naona hii hali inaanza kushamiri nchini, Bunge linapotaka kushughulikia jambo kama muhimili, wanajitokeza watu kwa kutumia ujanja ujanja, wanatumia mihimili mingine kuzuia, naomba mwongozo katika hili,” alisema Cheyo.

Makinda alitumia fursa hiyo kuwatangazia wabunge kwamba, jana mchana mara baada ya kuahirishwa bunge, kila mmoja angegawiwa ripoti ya CAG na kwamba ilitakiwa wagawiwe kabla ya bunge kuahirishwa lakini ilikuwa bado inadurufiwa.

Makinda alikiri kuwa na taarifa zilizoelezwa na Cheyo, alisisitiza kuwa wana orodha ya kesi zote zilizopo mahakamani, ambazo zinahusu IPTL hakuna hata moja inayohusu kitakachojadiliwa leo bungeni.

Mnyika pamoja na kumpongeza Makinda kwa kusema Bunge lazima lipelekewe na kujadili ripoti hiyo, alimtaka Spika Makinda kuwahakikishia kuwa hata kesi iliyofunguliwa jana na kampuni ya Pan African Power (PAP), haitapewa nafasi ya kuzima ‘moto’ huo kuwaka bungeni.

“Umesema hakuna kesi yoyote…, nakupa taarifa mahususi kuwa PAP, leo (jana) wamefungua kesi kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania wakiomba Bunge lizuiwe kujadili suala la Escrow, tunaomba utuhakikishie hili halitatokea,” alieleza Mnyika.

Spika Makinda alisisitiza kuwa bunge ni muhimili, unaoendesha shughuli zake kwa uhuru na lina kinga na haki zake.

Alisema ikitokea mtu au chombo chochote kuamua bunge lifanye au lisifanye nini, hilo halitakuwa bunge tena.

Hata hivyo, Makinda alishindwa kuwahakikishia wabunge kuwa leo watajadili Escrow kwa maelezo kwamba, hakuwa amepokea taarifa ya maandishi kutoka PAC kama taratibu zinavyoelekeza.

MAAMUZI YA MAHAKAMA
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imezuia Bunge kujadili ripoti ya CAG kuhusu uchunguzi wa kuchotwa kwa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo BoT hadi hapo Mahakama itakaposikiliza shauri la msingi Desemba 8, mwaka huu.

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo baada ya kuridhika na maelezo yaliyotolewa na kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na kampuni tanzu ya Pan African Power, kufuatilia hati yao ya dharura namna 51 ya kusitishwa kwa mjadala huo, iliyowasilishwa Mahakamani hapo jana.

Hati hiyo ya dharura ilisikilizwa na majaji watatu ambao ni Radhia Sheikh akisaidiana na wenzake Richard Mziray na Lugano Mwandambo kuanzia saa 8:45 hadi saa 10:45.

Jopo la Mawakili upande wa watoa maombi ya hati ya dharura liliongozwa na Joseph Makandege akisaidiana na wenzake, Gabriel Mnyele na Felician Kay.

Upande wa watoa maombi, uliiomba mahakama hiyo kusitisha mjadala huo kwa maelezo kwamba mhimili wa Bunge unahusika na utungaji wa sheria, hivyo kujadili mashauri yanayohusu kesi za jinsi hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine ambao ni Mahakama.

Makandege alidai kuwa ni kweli Bunge lina kinga ya kujadili suala kama hilo kwa mujibu wa ibara ya 100, lakini ikiwa suala hilo likiwa katika ofisi ya Bunge.
Alidai kuwa Bunge likiendelea kujadili kutasababisha mashauri ya IPTL na PAP yaliyoko Mahakama Kuu na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi yataminywa na kunyimwa haki yao.

BUNGE: MJADALA LEO
Baada ya Mahakama kutangaza maamuzi hayo, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, aliliambia NIPASHE kuwa hawajapokea taarifa kwamba Mahakama ni mhimili na Bunge ni mhimili mwingine, hivyo wataendelea na na mjadala.

Wakati huohuo; mtu aliyekamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita na jeshi la polisi mkoani Dodoma, akituhumiwa kusambaza nyaraka zinazosadikiwa kuwa ni ripoti ya CAG, bado anaendelea kushikiliwa.
Nyaraka hizo, zilidaiwa kuibwa kutoka kwenye Ofisi ya Katibu wa Bunge kabla ya kupatikana zikisambazwa mitaani na mtuhumiwa huyo, kabla hajakamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misiime, alilieleza Nipashe jana kuwa kutokana na sababu za kiupelelezi, utambulisho wa mtuhumiwa bado unaendelea kuhifadhiwa.
“Siwezi kueleza upelelezi utakamilika lini, sasa tunaendelea kutumia wataalam wa maandiko ili kujiridhisha ikiwa nyaraka hizi ni za CAG au la, tukikamilisha kazi zetu tutatoa taarifa,” alisema Kamanda Misime.

KAFULILA ATISHIWA KIFO
Wakati hayo yakijiri, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alitumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) unaomtishia maisha.

Sehemu ya sms hiyo inasema: “Nadhani umeamua kifo kwa kutafuta sifa za kijinga nakuhurumia sana kwa kuwa hujui unapambana na nani huu ni ujumbe wa mwisho kwako kama huamini utaamini ukiwa kaburini.”

Kutokana na hali hiyo, jana Kafulila alikwenda makao makuu ya polisi mkoani Dodoma kutoa taarifa dhidi ya vitisho hivyo.

Alifuatana na wabunge; Khatib Said Haji (Konde-CUF), Mohammed Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF) na Moses Machali (Kasulu Mjini-NCCR-Mageuzi).Hata hivyo, Kamanda Misime alisema jana kuwa hakuwa na taarifa zozote kuhusiana na malalamiko hayo.

RIPOTI
Ripoti hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kupitia taarifa maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe, pamoja na mapendekezo ya kamati hiyo leo.

Ripoti hiyo inahusu ukaguzi wa hesabu za fedha hizo uliofanywa na CAG kwa upande mmoja na uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kwa upande mwingine, kuhusiana na kashfa hiyo.

Uchunguzi huo ulifanywa na taasisi hizo kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilolotoa bungeni, akitekeleza azimio lililopitishwa na Bunge kuhusiana na suala hilo.

Baada ya Zitto kuwasilisha taarifa maalum kuhusiana na ripoti hiyo, wabunge watapata fursa ya kuijadili.

Mjadala huo kama utafanyika unatarajiwa kuliteka Bunge kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo wingi wa fedha hizo zinazodaiwa kuchotwa kifisadi.

Fedha hizo zinadaiwa kuwa ni za umma na kwamba zingeweza kujenga miradi mingi ya maendeleo, ikiwamo ujenzi wa zahanati, ununuzi wa dawa hospitalini, ujenzi wa shule nakadhalika.

Fedha hizo zinadaiwa kuchotwa kutoka kwenye akaunti hiyo ya Escrow na vigogo mbalimbali, wakiwamo mawaziri, wabunge, majaji wa Mahakama Kuu na viongozi wa dini.
Tayari wabunge walianza kugawiwa nakala ya ripoti hiyo jana mchana ili wapate fursa ya kuipitia kabla ya kuijadili bungeni.

Spika Makinda aliliambia Bunge jana kuwa nakala za ripoti hiyo, ambazo wamegawiwa wabunge jana, ni kama kiambatanisho cha taarifa maalum inayotarajiwa kuwasilishwa na PAC leo.

Kabla ya ripoti hiyo kugawiwa wabunge, Jumapili wiki iliyopita, Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni vijana wawili kwa tuhuma za kuiiba kutoka Ofisi ya Katibu wa Bunge.

Monday, November 24, 2014

MTOTO ATUMIWA KUMWIBA MTOTO MWENZAKE, AKAMATWA..



Mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake. Tukio hilo la kushangaza lililonaswa na Ijumaa Wikienda lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 mchana maeneo ya Majengo Mapya, Kata ya Kihonda jirani na nyumbani kwa aliyekuwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, marehemu Alberth Keneth Mangweha ‘Ngwea’.Hatari! Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Kihonda mjini hapa anayesoma darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi Noto Sosario, anadaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake kisha kukamatwa na kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira zaidi ya 300.
Raia wenye hasira kali wakimsubiri kwa hamu mtoto huyo nje ya nyumba aliyohifadhiwa. 
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa kwa jirani yangu, Asha Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo kwa njia za kichawi hivyo mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia mwizi. 
Kamanda akimbana mtoto huyo kwa maswali. “Mtoto alikuwa amevaa nguo nyeusi ndipo umati ukajitokeza na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku wengine wakimpiga vibaya na kutishia kumuua.
Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto huyo kwa usalama zaidi. “Baada ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani kwangu.“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
Mtoto huyo akichukuliwa kwenye 'Defender' kuelekea kituo cha Polisi.Kwa upande wake, mtoto huyo alisema: “Bibi ndiye huwa ananituma. Kwa sasa niko kwenye ulimwengu wa giza na mateso makubwa.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Vicent alisema: “Mwanangu nilimzaa akiwa salama lakini tangu atoke Moshi (Kilimanjaro) kwa bibi yake amekuwa wa ajabu hivyo nimepanga kumpeleka kwenye maombi.”