Wednesday, October 22, 2014

MAMA ALIYEPIGWA MSHALE KISA MAHARI



Ghati Bunyige akiwa amekaa kwenye benchi akisubiri huduma ya matibabu katika kituo cha afya cha Sirari wilayani Tarime mkoani Mara.
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni! Mwanamke mmoja, mkazi wa Kitongoji cha Buriba, Kijiji cha Sirari wilayani Tarime, Mara aitwaye Bunyige Chacha (25) amepigwa mshale kwenye makalio na mumewe, Ghati Nyamarandi kisa kikidaiwa kuanzia kwenye pesa ya mahari na watoto. Akisimulia mkasa wake mzito uliompata Oktoba 5, mwaka huu majira ya jioni, mwanamke huyo alisema siku hiyo, mumewe alirudi na kumuuliza walipo watoto wao wawili (hakuwataja majina) ambao aliwaondoa nyumbani siku kadhaa nyuma bila kumwambia.
Akasema, alipomuuliza hivyo tu, ndipo mumewe akamjia juu na kumshambulia kwa matusi huku akisema watoto aliwapeleka kuuzwa eneo linaloitwa Nyumba Ntobu. “Mume wangu alifika nyumbani, nilipomuuliza watoto wako wapi ndipo akanifungia ndani ya chumba na kunishambulia kwa matusi.
“Kwa bahati nzuri nilibahatika kutoroka na kukimbilia kwa majirani lakini wakati nikivuka uzio wa mlango nilianguka, akapata nafasi, akanirushia mshale ulionichoma sehemu ya makalio, chini ya mguu wa kulia,”alisema mwanamke huyo. 
Ghati Bunyige akiongea na mwandishi wa habari kuhusiana na mkasa aliokumbana nao. 
Mama huyo aliongeza kuwa, watoto wake wawili waliuzwa Nyumba Ntobu na baba huyo kuchukua mahari bila kumshirikisha mke suala ambalo lilizua mtafaruku ndani ya nyumba mwanamke akidai watoto wake kila siku.
“Kwanza mume wangu alimwachisha masomo binti yetu wa kwanza ambaye alikuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Sirari, akamuoza Nyumba Ntobu na kupokea mahari yeye.
“Baadaye akamwachisha masomo binti yetu wa pili aliyekuwa akisoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Nyamaraga, nchi jirani ya Kenya, akamwozesha hukohuko Nyumba Ntobu na akapokea mahari peke yake.“Baadaye nilikuja kugundua kuwa, alikuwa akipokea mahari kwa siri kwa sababu alitaka kulipia mahari ili na yeye aoe mke wa pili ambaye anaishi naye tayari, lakini ni mke wa mtu,” alisema mwanamke huyo. 
Picha ya mama huyo akiwa katika usafiri akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Hivi karibuni, Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (Tamwa) kupitia kwa mkurugenzi wake mtendaji, Valarie Msoka alifika kumwona mwanamke huyo na kumpa pole kwa tukio lililompata. Alimtaka mama huyo kumshitaki mumewe ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake.
Msoka amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki ya mama na mtoto na kulaani vitendo vinavyofanywa na jamii vya ukatili wa kijinsia kwa madai kuwa nimila au desturi za makabila husika.
Kwa upande wake, mwanasheria msaidizi wa Kata ya Sirari, Zablani Zablani aliliambia gazeti hili kuwa, mwanamke huyo alifika ofisini kwake kuomba msaada wa kisheria baada ya kujeruhiwa kwa mshale na mumewe ambapo yeye alimpeleka Kituo cha Polisi cha Sirari ili kupata PF3 na kwenda kupata matibabu katika Zahanati ya Alpha iliyopo mji mdogo wa Sirari.

MH. MBOWE ATOLEA UFAFANUZI WA PICHA YAKE YA KIMAHABA ILIYOSAMBAA MITANDAONI!


Week iliyopita Picha hii ilienea mitandaoni ukimuonesha Freeman Mbowe na Mkewe Wakibusiana

“Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.

“Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.

MSANII WA TMK WANAUME FAMILY, YP AZIKWA MAKABURI YA CHANG'OMBE DAR


Wasanii wa Bongo Fleva wakiuaga mwili wa marehemu Yesaya Ambikile 'YP' katika Viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.

Waombolezaji wakiwa katika msiba wa msanii wa Bongo Fleva, Yesaya Ambikile 'YP' kwenye Viwanj vya TCC, Chang'ombe, Dar.…



Wasanii wa Bongo Fleva wakiuaga mwili wa marehemu Yesaya Ambikile 'YP' katika Viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.

Waombolezaji wakiwa katika msiba wa msanii wa Bongo Fleva, Yesaya Ambikile 'YP' kwenye Viwanj vya TCC, Chang'ombe, Dar.
Mke wa marehemu YP, Sakina Robert (mwenye kiremba cheupe) akiwa katika hali ya majonzi.
Msanii wa Bongo Fleva, Juma Nature akizungumza jambo kwa niaba ya wasanii wenzake waliofanya kazi na marehemu enzi za uhai wake.
 Juma Nature akiwa na ndugu wa marehemu 2
Baadhi ya wasanii na waombolezaji wakiwa mbele ya jeneza muda mfupi kabla ya kuuaga mwili wa marehemu.
Juma Nature akifunua jeneza tayari kwa shughuli ya kuuaga mwili huo.
Mtoto wa marehemu, Ambikile Yesaya akisogezwa mbele ye jeneza kuuaga mwili wa baba yake.
Msanii wa filamu, William Mtitu akipita kuaga mwili wa marehemu.
Msanii wa vichekesho, Mussa Kitale 'Mkude Simba' akiaga mwili.
Maombolezaji wakiwa wamebeba jeneza kwenda makaburini.
Sehemu ya mamia ya waombolezaji wakiwa makaburini.
Waombolezaji wakiwa wamebeba bango lenye picha ya marehemu.
Jeneza likishushwa kaburini.
MSANII WA TMK WANAUME FAMILY, Yesaya Ambikile 'YP' aliyefariki usiku wa kuamkia janai, amezikwa leo katika makaburi ya Chang’ombe maduka mawili jijini Dar jioni hii. Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliokuwepo kuungana na wasanii wenzao wa Bongo Fleva ni pamoja na JB, Steve Nyerere, Jacqueline Wolper, Kajala Masanja, Shilole, William Mtitu, Mkude Simba na wengineo

APIGWA RISASI NA WATU WALIODHANIWA NI MAJAMBAZI MAGOMENI

Mtu asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
....wapita njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.
Muonekano wa nyumba wa gari hilo.
...hawa jamaa nao waligongana, mwendesha pikipiki na mwenye gari katika eneo la tukio na kuanza 'kuzikunja'.
Mtu mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja amepigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kuporwa mkoba uliyokuwa garini ambao haukujulikana ulikuwa na nini ndani yake. Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana maeneo ya Magomeni Mikumi jirani na kwa Sheikh Yahaya jijini Dar es Salaam. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni akiwa kwenye gari yake Toyota Mark II (GX 100) yenye namba za usajili T487 AZW. Kwenye gari hiyo, alikuwemo mwanamke mmoja akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele cha abiria ambaye hakujeruhiwa.

ANASWA AKIMTEKA MTOTO WA SHULE


HALI bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.

Denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni (mwenye sare za shule) aliyenusurika kutekwa na njemba inayotambuliwa kwa jina moja la Omar.
Tukio hilo lililokusanya kadamnasi lilijiri wikiendi iliyopita, Magomeni-Kagera, Dar wakati mwanafunzi huyo akitokea shuleni.Kwa mujibu wa mashuhuda, denti huyo alipofika eneo hilo, baba huyo alimsalimia na baada ya kujibiwa salamu yake alianza kumchombeza kwa maneno matamu-tamu.
 Baadhi ya raia wenye hasira kali waliotoa kipigo ‘hevi’ kwa Bw. Omar wakiwa wametanda eneo la tukio.
Akizungumza na Uwazi lililofika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’, denti huyo aitwaye Laila alisema licha ya kuitikia salamu ya jibaba huyo na kumuamkia bado aliendelea kumchombeza na kila alipojaribu kumkwepa ilishindikana.Makamanda wa Polisi waliofika eneo la tukio kumuokoa mtuhumiwa.
Njemba huyo alivuka mipaka na kumshika mkono na kutaka kumvutia ndani ya gari lililokuwa karibu yake ndipo Laila alipoamua kupiga mayowe ya kuomba msaada na hatimaye kuokolewa na wasamaria wema waliokuwa wakipita njia.”
Mtuhumiwa (Omar) akiwa ndani ya gari mara baada ya kipigo.
Mwanafunzi huyo aliendelea kusema: “Alianza kunifuatilia tangu kule, akanisalimia hujambo nikamjibu sijambo, akaniambia tena kwenu hawajambo, nikamjibu hawajambo, akaendelea kuniambia eti, nimfuate akanipe lambalamba, mimi nikakataa kwa sababu mama alinikataza kukubali kupewa lifti na vitu vingine kutoka kwa watu nisiowajua tangu aliposikia habari za watoto kutekwa na Noah nyeusi.Wasamaria wema wakimuokoa mtoto huyo.
“Kila kitu nilimkatalia lakini yeye akawa anaendelea kuniambia maneno yake na kuanza kunivuta ndipo nikaona sasa naenda kufa hivyo ikanibidi nipige kelele ndiyo watu wakatokea na kumkamata kisha kuanza kumpiga mpaka walipofika polisi.”
Mmoja wa wasamaria wema akimuingiza binti huyo kwenye gari kumuondoa eneo la tukio.
Gazeti hili lilizungumza na mtuhumiwa aliyekuwa amehifadhiwa ndani ya gari, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alimuomba paparazi wetu kabla ya yote kwanza amuokoe na kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.Binti akiwa kwenye gari mara baada ya kuokolewa.
“Chondechonde ndugu yangu, naomba kwanza mnilindie usalama wangu, hao jamaa wanataka kuniua bila sababu, mimi wala sikuwa na nia mbaya na huyo binti wananizushia tu, nilikuwa namsalimia tu,” alisema Omar kupitia upenyo mdogo wa juu ya dirisha la gari alilohifadhiwa.
-GPL