Friday, October 31, 2014

GADNER. G. HABASH KUSIKIKA EFM 93.7 KUANZIA LEO

Mtangazaji mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga na kituo cha Radio kinachokuja kwa kasi hivi sasa EFM 93.7 cha jijini Dsm ili kuongeza nguvu katika kikosi 
Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema wameamua kumchukua Gardner kwasababu ni miongoni mwa watangazaji hodari nchini mwenye kipaji cha hali ya juu hivyo kuongeza chachu ya mafanikio katika kituo hicho 
“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi wa 11 mwaka huu”alisema 
Gardner alimaarufu “KAPTENI” alianza kazi na kituo cha Radio Clouds fmna baadaye Times fm ambapo kwa sasa ametua Efm akitanguliwa na wakongwe kama Dj Majey,Dizzo One,Sos B,Denis Ssebo,Maulidi Kitenge,Omari Katanga,Scholastica Mazula na Kanky Mwaigomole.
Taarifa na
Meneja Uhusiano.
Kanky Mwaigomole.

MTANGAZAJI MAARUFU BEN KIKO AFARIKI DUNIA

Ben Kiko enzi za uhai wake. ALIYEKUWA mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania, Ben Kiko, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Oktoba 31, 2014 akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Kiko amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

BASI LA SIMBA MTOTO USO KWA SUO NA LORI


Ajali mbaya imetokea eneo la daraja la Wami basi la Simba Mtoto na Lori baada break za Lori kufeli,
Dereva wa Lori amepoteza maisha hapohapo.


Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga likiwa limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani,dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.

BROTHERS FOR CHRIST WAITAMBULISHA TANZANIA NCHINI MAREKANI KWA KUCHUKUA TUZO

 
 Kama ilivyokawaida kwa mashindano mengine watanzania kuwa wasindikizaji na washuhudiaji wa wengine kuchukua tuzo huku wao wakiambulia patupu, kwao Brothers For Christ imekuwa tofauti baada ya kuchukua tuzo katika mashindano ya PRAYZ FACTOR PEOPLE CHOICE AWARDS nchini Marekani.

Kundi hilo ambalo maskani yake ni Tegeta jijini Dar es salaam lilifanikiwa kuchukua tuzo mbili katika Afro category na International Category na kuwaacha watu kuachwa na mshangao huku wakiwa hawaamini kilichotokea. Tamasha hilo lilifanyika tarehe 22/9/2014 lilifanya nyimbo za B4C kupigwa sana na vituo vya media nchini marekani na kulifanya kundi hilo kujizolea mashabiki wengi nchini humo kitu ambacho ni tofauti na hapa Tanzania.
 
Brothers for Christ walijaribu kutupa kete yao huko baada ya kuona tangazo katika mtandao kuwa kuna mashindano hayo ndipo walipotuma Video yao ya YOTE YAWEZEKANA ili ichaguliwe kuingia katika mashindano hayo.
Waswahili husema  “kama bahati vile” wimbo huo ulichaguliwa katika vipengele viwili ambavyo nao waliwaonyesha wamarekani na wahudhuriaji wote ya kuwa hakika Yesu Kristo anahubiriwa Tanzania kupitia nyimbo.

"Tulipokuwa tumepanda jukwaani watu walionekana kuwa na mshangao wakiwa hawaamini kile kilichokuwa kinatokea baada ya umahili na ustadi tuliouonyesha katika kuimba live, wengi walituuliza tulipotoka tukawajibu Tanzania wakashangaa" alisema Justin Kaego 

Kundi  hilo ambalo liliiwakilisha vyema Tanzania halina jina kubwa nchini lakini limefanya mambo makubwa yakushangaza kwani wapo wanamuziki wakongwe waliowahi kushiriki katika mashindano kama haya na hawakuweza kurudi na tuzo.
Brothers For Christ (B4C) ni kundi la vijana 14 wakiwemo watanzania 8, wakenya 2 na wacongo 4 ambao wameunda kundi hilo likiwa chini ya Dockta Mponzi ambaye pia ni mzee wa kanisa la Mlima wa moto Asseblise of God Mikocheni Dar Ambaye ndiye mlezi wao. Ni vijana wasiojua kuimba kwa kutumia mshindo nyuma, wenyewe husema “ live bila chenga”.  Wapo tayari kwa mialiko ya aina yoyote kwani nia yao kuu ni kukiokoa kizazi cha watanzania kupitia uimbaji. Hivyo wasiliana nao kwa +255767600604 na +255753599542 wapo tayari kwenda popote kwa ajiri ya Kristo Yesu.