Tuesday, September 16, 2014

REGINALD MENGI AINGIA FAINALI TUZO YA MFANYABIASHARA BORA AFRIKA

 

MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi ni miongoni mwa wafanyabiashara wanne waliofikia fainali ya kuwania Tuzo ya Mwaka ya Mfanyabiashara Bora Afrika (AABLA), kundi la Afrika Mashariki.


Sherehe za tuzo za AABLA, kundi la Afrika Mashariki zitafanyika Septemba 20 mjini Nairobi, Kenya na zitarushwa hewani na runinga barani Afrika.
Kwa mujibu wa chaneli ya runinga ya masuala ya fedha na biashara Afrika (CNBC Africa), ambao ndio waandaji wa sherehe hizo, tuzo hizo za kila mwaka zimebuniwa kwa ajili ya kutambua utendaji uliyotukuka katika biashara, wenye mafanikio makubwa kwenye sekta zao za biashara na vile vile kwenye jamii ambako biashara hizo zinaendeshwa.
“Tuzo hizo ni kutambua uongozi wa watu hao katika kubadilisha sekta ya biashara kwa kuendeleza ubora wa shughuli zao kwa kuzingatia desturi njema za kufanyabiashara na ubunifu,”.
“CNBC Africa, inajivunia kuendeleza utamaduni uliowekwa na tuzo hizi unaotambua na kusherekea mtazamo, msukumo wa mafanikio na ubora mkubwa wa viongozi wafanyabiashara katika bara la Afrika. AABLA inawatambua kipekee na kuwaheshimu viongozi ambao wamechangia katika kuboresha uchumi wa Afrika na waelekezi wa biashara zinazoongoza sasa,” ilisema taarifa hiyo kupitia tovuti : http://www.aabla2014.com.
Wafanyabiashara wengine watatu wateule wa tuzo hiyo ni Ofisa Mtendaji wa Britam, Benson Wairegi, Ofisa Mtendaji wa Centum, James Mworia, na Ofisa Mtendaji wa Crown Paints, Rakesh Rao (Kenya).
Watanzania wengine waliyoteuliwa katika tuzo hizo kwa makundi tofauti ni Ofisa Mtendaji wa Helvetic Solar Ltd, Patrick Ngowi, (EA Young Business Leader), na Ofisa Mtendaji wa Techno Brain Ltd, Manoj Shanker, (Entrepreneur of the Year).

WALIOKUFA KWENYE KANISA LA NABII TB JOSHUA WAFIKIA 50!


Idadi ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni liliporomoka Jumamosi  wakati ujenzi ukiendelea.Hadi kufikia jana Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka leo hii.Inaelezwa kwamba, mhubiri huyo wa kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini mwenyewe akaamua kujenga ghorofa tano.Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124 walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.
A photo taken and released by Nigeria's National Emergency Management Agency (NEMA) on September 12, 2014 shows emergency workers transporting a man after he was pulled out from the rubble of The Synagogue Church of All Nations
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos. 
 

LAGOS –

SERIKALI YASEMA BUNGE MAALUM LA KATIBA LINA UHALALI KISHERIA NA KISIASA KUENDELEA


Asha-Rose-300x257Na Magreth Kinabo,Dodoma
Serikali imesema kwamba Bunge Maalum la Katiba linaendelea kwa mujibu wa Sheria, mjadala wa hoja ya kusitishwa kwa Bunge hilo, umefungwa rasmi leo.
Aidha Serikali imewaondoa hofu wananchi kwamba hakuna mgogoro wa kisiasa, hivyo waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato(riziki) kama kawaida, pia ipo macho kupitia vyombo vyake vya usalama,itasimamia sheria na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu.
 
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha  Rose  Migiro kwenye kikao cha Arobaini cha Bunge hilo wakati akitoa tamko la Serikali  kwenye mjadala wa mwisho wa kujadili sura zote 15 zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya.
 
“Bunge hili linaweza kuendelea na shughuli zake. Nawaomba Watanzania wafahamu mjadala wa kusitisha Bunge umehitimishwa hii leo kisheria na Mahakama Kuu ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Dk. Migiro.
 
Dk. Migiro aliongeza kuwa  kwa taarifa walizonazo majadiliano baina na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) pamoja na vyama vyote husika yataendelea Septemba 17 na 18, mwaka huu, kwa sababu mchakato huo si wa chama kimoja, wala viwili au vitatu , bali  mchakato wa Watanzania wote kupitia mfumo ambao umewekwa  wa vyama vyote kisheria.
 
Akizungumzia kuhusu takwimu za wajumbe wa Bunge hilo, Dkt. Migiro alisema  kuwa lina wajumbe 630, kati yao waliotoka nje ya Bunge hilo ni wajumbe 130 ni sawa na asilimia 21 ya wajumbe wote.
 
“Wajumbe waliobakia ndani ya Bunge hili ni 500, sawa na asilimia 79 ya wajumbe wote, tukitazama mambo ya takwimu kwa  kutambua Kundi la 201. Imejitokeza dhana kwamba wajumbe waliobakia humu ndani ni wa aina moja, hiyo si kweli,”alisema.
 
Dk. Migiro alisema  kati ya wajumbe 500, waliobaki katika Bunge hilo, 189, wanatoka katika kundi la 201.
 
Alisema wajumbe  wengine waliobakia, 348 wanatoka upande wa Tanzania Bara, kati ya hao, wajumbe 125 ni wajumbe wanaotoka Kundi la 201.
 
“ Tukiangalia upande wa Zanzibar wajumbe waliobakia ni 152, kati yao wajumbe 64 wanatoka Kundi la 201.Tungependa kusisitiza Kundi la 201 ndio wajumbe ambao kwa wingi wao kitakwimu na kimakundi wanawakilisha Taifa  letu  kwa sura zote.
 
“ Ni dhahiri waliobakia humu ndani ni wengi, hii ina maana kwamba kwa kuzingatia matakwa ya masuala ya kisheria kwa maridhiano, kwa majadialiano na kwa kushawishi hoja.
 
“Wajumbe waliobakia  ni wengi wana uhalali kisheria na kisiasa. Tutaendelea na shughuli zetu kama sheria inavyotutaka, uwakilishi wa Bunge umetimia …  tuna wajibu  wa kisheria wa kufanya  yale tunayoyataka kuyafanya,” alisisitiza  huku akisema waliotoka nje  kwa pande zote mbili hawafikii theluthi moja.
 
Alifafanua kuwa vyama vilivyotoka nje ya Bunge hilo, ni vitatu,vilivyobakia  ndani ya ni 18 ambavyo vimesimamia na vinaendelea kusimamia umoja wa kitaifa  wa nchi yetu.
 
Akichangia mara baada ya tamko hilo, mjumbe wa Bunge hilo, John Shibuda alimpongeza mtoa taarifa hiyo ya Serikali na kuipongeza Serikali kwa kushinda kesi.
Aliwataka Watanzania kuchuja kati ya siasa na maslahi binafsi.

TRAFIKI ALIYEGONGWA NA DALADALA JANA, AFARIKI DUNIA



WP 2806 CPL Riziki, akiwa chini baada ya kugongwa na daladala eneo la Mbagala Rangi 3 jana kabla ya kukimbizwa hospitali.
ASKARI wa usalama barabarani, aliyejulikana kwa jina moja la Riziki, WP 2806 CPL Riziki, aliyegongwa na daladala aina ya DCM wakati akiwa katika harakati za kutimiza majukumu ya kazi eneo la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam jana asubuhi amefariki dunia leo.
Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikiuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili

KIJANA AJITOKEZA KWENYE KWENYE MAZISHI YAKE


DA! Duniani kuna mambo jamani! Katika hali isiyo ya kawaida, maeneo ya Tandale Kwatumbo jijini Dar, waombolezaji hawakuamini macho yao wakati walipomuona ‘marehemu’ Mohamed Salum ‘Fido’ (29) (pichani), akirejea nyumbani hapo huku maandalizi ya mazishi yake yakipamba moto na waombolezaji, hasa mkewe, mtoto na ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia ‘kifo’ chake.Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, mwaka huu, saa sita mchana wakati shughuli mbalimbali za mazishi yake zikiendelea zikiwa ni pamoja na maandalizi ya chakula cha mchana kwa waombolezaji.Iko hivi; Fido ni dereva wa bodaboda, kijiwe chake kikiwa Lumumba Mnazi Mmoja, Dar. Inadaiwa kwamba Septemba 10, mwaka huu alikamatwa na polisi wa ‘Tigo’, Lumumba kwa madai ya kutokuwa na kibali cha kuingia mjini, akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central).
Pale kituoni, habari zinadai maafande hawakumruhusu kumpigia simu mkewe ili kumweleza yaliyompata, ndipo ndugu walipoamua kumtafuta kwa siku mbili bila mafanikio.
Waombolezaji wakiwa msibani.
Septemba 11, mwaka huu, mkewe, kaka yake na baba yake mzazi walikwenda Hospitali ya Mwananyamala na kuingizwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) ambapo walioneshwa maiti moja! Vilio vikaibuka kwani wote walisema ni Fido. Marehemu huyo aliuawa kwa kugogwa na kitu kizito kichwani na maiti yake ilipelekwa hapo na polisi.
Ndugu hao walitoka na vilio hadi nyumbani na msiba ukawekwa kwa kukusanya mikeka na chakula kuanza kupikwa huku sehemu ya kuzikia makaburini ikitafutwa achilia mbali sanda kupatikana huku ndugu walio mbali wakijulishwa kuhusu msiba huo.
Siku ya tukio, watu wakiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuufuata mwili, ndipo Fido alipoibuka na kusababisha tafrani kubwa.Baadhi ya watu waliingia mitini kwa woga huku ndugu wakishangaa iweje maiti itoke mochwari yenyewe? Ndipo Fido alipotangaza kwa sauti kuwa, hakufa, alikuwa polisi.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa msibani.
Akizungumza na Uwazi huku akifakamia msosi kwa madai kuwa hakula tangu alipokamatwa, Fido alisema alikamatwa na polisi lakini akakosa njia ya kuwasiliana na familia yake.
Naye mke wa marehemu alipopewa nafasi ya kusema alikuwa na haya:
“Nimepigwa butwaa, siamini kama ndiye huyu mume wangu, watu wamekusanyika kwa ajili ya maombolezo, nilijua hatukonaye tena. Ama kweli Mungu mkubwa, nimefurahi kufika kwake nyumbani.
“Ilikuwa Jumatano saa 1.45 asubuhi mume wangu aliniaga na kwenda kazini kwake lakini hadi saa mbili usiku alikuwa hajarudi na si kawaida yake, ilikuwa nikipiga simu yake inaita tu.
“Ilibidi niende Tandale wanakohifadhia pikipiki, nilikuta wenzake wamesharudisha pikipiki lakini yeye alikuwa bado.“Tulifuatana na ndugu zangu hadi Lumumba hatukumuona, tulienda Kituo cha Polisi Msimbazi, Central, Oysterbay na Kawe lakini walituambia hakuna mtu mwenye jina hilo aliyekamatwa ama kupatwa na tatizo, ilibidi twende Hospitali ya Mwananyamala mochwari kuulizia kama kuna maiti iliyookotwa.
Chakula kikipikwa msibani.
“Uongozi wa mochwari ulitueleza kuna maiti tatu zilizopelekwa na polisi lakini hazifahamiki, moja ni kwa ajali ya pikipiki, mwizi kuuawa na wananchi na nyingine kuokotwa ufukweni mwa bahari ikiwa imefungwa kamba mikononi na kukatwa panga kisogoni.
“Mimi, baba pamoja na shemeji yangu tuliingia mochwari kuthibitisha. Tulipofika katika maiti iliyofungwa kamba na kukatwa panga kisogoni wote tulijiridhisha kuwa ndiye yeye kutokana na alama alizokuwa nazo, sikujua kilichoendelea, naamini nilipoteza fahamu baada ya kuuona mwili huo.
“Tulirudi nyumbani kuandaa msiba, kuweka maturubai, kununua sanda na kuandaa jeneza, tulipiga simu sehemu mbalimbali hadi mikoani kuwajulisha ndugu.“Tulijiandaa ili ndugu wa Morogoro na mikoa mingine wakija katika mazishi yaliyotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa (iliyopita) katika makaburi ya hapa Tandale ambapo tulishapewa eneo la kuchimba kaburi.
Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa akila.
“Kweli sijui nisemeje, tuliwataka radhi waombolezaji kwa usumbufu, baadhi walitawanyika kwa wakati huo wengine waliendelea kuwepo hata ndugu zetu wengine wako njiani wakitokea Mbeya na Mtwara.
Credit:GPL

MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI DAR ACHINJWA NA KUTUPWA KICHAKANI

Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa.
 Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi  na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar, ameuawa kwa kuchinjwa na watu  wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima matikiti.Habari zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi ambazo amekuwa akizifanya tangu afike  katika eneo  hilo mwaka 2005.
Akizungumzamke wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani),  alisema siku za nyuma kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa ajili ya kulima matikiti.
Watu hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo  hilo na wala hawajulikani walisema wanatokea Kijiji cha Lisu wilayani  Nzega, Mkoa wa  Tabora  walielekezwa  kwa  marehemu huyo.
Ilielezwa kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika  nyumbani kwa marehemu Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha eneo la ekari tatu.
Mke na watoto wa Lutebula Ndabi wakiwa na uzuni.
 Mke huyo alisema hata yeye tukio hilo limemchanganya kwani aliamini wale vijana walikuwa ni watafutaji na ndiyo maana mumewe aliwapa shamba, kumbe walikuja kutafuta roho ya mume wake.
Alisema tangu watu hao wafike, siku tatu mbele ndipo walipogundua mumewe amechinjwa na vijana hao watatu hawajaonekana tena. Alisema siku ya tukio, mume wake aliondoka na vijana hao kwa madai wanakwenda kumtolea pesa kwenye mtandao wa simu ili wamlipe kwa ajili ya shamba hilo.
Kwa mujibu wa Rehema, watoto wake wawili (mmoja miaka 7, mwingine 4) ndiyo waliogundua mwili wa marehemu baba yao akiwa amechinjwa walipokwenda kuchunga ng’ombe.

Jeneza la marehemu, Lutebula Ndabi.
 “Nikiwa bado najiuliza aliko mume wangu, mara mtoto wangu Ashura (mkubwa) akaja anakimbia huku ana wasiwasi, akasema, mama nimeona shati la baba, ndala na mguu wake. Ndipo tukaenda huko na watu lakini Ashura  alikataa kufika kwa awamu nyingine.
“Tulipofika tuliukuta mwili wa mume wangu. Niliona amekatwa kichwani na pembeni kulikuwa na panga. Baada ya hapo nilihisi mwili ukiishiwa nguvu, sikujua nini kilichoendelea,” alisema mwanamke huyo.
Mpaka sasa Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke linawashikilia  watu watatu, wawili wakiwa ni wale waliowakaribisha wale vijana huku mmoja wao akiwa mwenyeji wa kijiji cha jirani, alikamatwa kutokana na maelezo ya bahasha iliyokutwa kando ya mwili wa marehemu ikisema ‘kumbuka yaliyotokea mwaka 2013’ ambapo baadhi ya watu walisema mtuhumiwa huyo aliwahi kutofautiana na marehemu.

MWATHIRIKA WA MABOMU MBAGALA ALIPWA HUNDI YA SHILINGI 1950 TU.


Mwathirika wa mabomu ya Mbagala ya mwaka 2009, Said Omary Mbonde akionyesha cheki malipo ya Tsh 1950 kutoka Benki Kuu wakati wa mkutano na waandishi, uliofanyika katika shule ya msingi Mbagala Kuu, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Rafael Lubava.....

MAMA AMTOA MWANAYE KAFARA AWE TAJIRI HUKO SONGEA!


Bwana Allan Menas Lwambano anayedaiwa kumuua mkewe.
 
 Hali huenda ikigeuka, wakati jamii inaamini akina baba ndiyo wenye tabia ya kutokuwa na uchungu kwa watoto, imekuwa tofauti kwa mama huyu!Ni mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwanamonga, Kata ya Lilambo, Manispaa ya Songea, Kasiana Komba (60) anadaiwa kuuawa na mumewe, Allan Menas Lwambano (76) kisa kikidaiwa mambo ya kumtoa kafara mtoto.Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri usiku wa Agosti 25, mwaka huu ambapo maelezo ya mume huyo yanasema ni baada ya marehemu kumtaka akubali kumuua mtoto wao mmoja (jina tunalo) kati ya saba ili walipe madeni kwa imani ya kishirikina na kufanikiwa katika kipato (utajiri). 



Ilielezwa kuwa, mwanaume huyo alikataa ombi hilo na mkewe akamwekea mgomo wa kumnyima unyumba hadi pale atakapokubali ombi lake hilo. 
Ilidaiwa kuwa, maisha ya wawili hao yakawa ya ‘sitaki nataka’, mume akitaka unyumba mke hataki kwa vile amemkatalia kumtoa mtoto wao kafara wakati yeye mke alishawaambia wenzake (kwenye ushirikina) kuwa, ameamua kumtoa mtoto huyo lakini baba yake hakutaka kufanya hivyo. 

“Siku ya tukio usiku, Lwambano alirudi nyumbani na kumkuta mkewe amelala, alianza kumshikashika mwilini kuashiria alimhitaji faragha, ndipo mke huyo alipotoka nje na kuchukuwa mchi wa kutwangia mahindi kwa lengo la kumpiga mumewe
Kasiana Komba aliyedaiwa kumtoa kafara mtoto wake ili apate utajili.

 “Mumewe aliuzuia, akamnyang’anya na kumpiga mkewe kichwani, alianguka palepale na kufariki dunia,” kilisema chanzo. 

MUME AHANGAIKA KUUZIKA MWILI
Habari za ndani zinasema kuwa, mume alipobaini ameua aliuchukuwa mwili wa mkewe na kuupeleka nyuma ya nyumba ambako kuna choo na kuuzika hukuakipanda migomba juu ili kuzubaisha watu. 

WATOTO: “BABA, MAMA YUKO WAPI?”
Agosti 26, mwaka huu, siku moja tu baada ya tukio hilo la kutisha, watoto ambao wanaishi mbali na nyumba hiyo walifika na walipoona hawamuoni mama yao, walimwuliza baba yao: “Baba, mama yuko wapi?”  akawajibu: “Mama yenu ameenda mjini Songea, atarudi.” 

WATOTO WAENDA KWA MGANGA

Ikazidi kudaiwa kuwa, Agosti 27, mwaka huu, watoto hao hawakukubaliana na majibu ya baba yao, wakaenda kwa mganga wa kienyeji (jina halikupatikana mara moja) kwa lengo la kupiga ramli ili kujua alipo mama yao.
Waombolezaji wakiwa msibani.

 “Mganga baada ya kuangalia ‘king’amuzi’ chake aliwaambia kama wanataka kujua mama yao alipo, warudi wakamchukue baba yao na kumfikisha kwa mganga huyo kwani yeye (baba) ndiye ana siri nzito.

“Watoto hao wakiongozwa na kaka yao mkubwa (Mathias) walimpa baba yao maagizo ya mganga. Ndipo baba huyo naye akawaambia kama wanataka kujua ukweli wa mama yao alipo, waongozane hadi kwa mtendaji wa kijiji akasimulie mbele yake. 

MBELE YA MTENDAJI
Septemba 4, mwaka huu, familia hiyo ikiongozwa na baba mtu walifika kwa Mtendaji wa Kijiji cha Mwanamonga, Said Mango na Mwenyekiti wa Kijiji, Maria Kahimba ambapo katika maelezo yake , mzee huyo alikiri kumuua mkewe kwa kumpiga na mchi kichwani. 

NUKUU YA MUME

Mzee huyo ananukuliwa hivi: “Nimemuua mke wangu nikamfukia nyuma ya nyumba yangu kwenye choo (watu wakapigwa butwaa).
Polisi wakiwa eneo la tukio.

 “Sababu kubwa ya chanzo cha tukio ni mke wangu nilimkatalia ombi lake la kutaka tumuue mtoto wetu mmoja ili alipe madeni ya uchawi na kufanikiwa kimapato.

“Nilimkatalia, akawa ananinyima unyumba. Siku ya tukio nilimlazimisha kunipa unyumba, akakataa akataka kunipiga na mchi, nikamuwahi yeye na kumpiga, akakata roho.” 

NANI ANAYEJUA?
Mwanamke mmoja aliyekataa kutaja jina lake, aliliambia Uwazi kwamba, marehemu aliwahi kumlalamikia kuhusu mumewe kugoma kumtoa mtoto wao mmoja kafara ili waweze kupata  mali. Alisema mumewe haoneshi kutaka mabadiliko. 

“Alisema namwambia mume wangu tumtoe mtoto mmoja kafara tupate utajiri lakini alisema sitaki kusikia habari hizo, kwani yeye ameridhika na ufukara,” alisema mwanamke huyo akimkariri marehemu. 


POLISI WAFUKUA MWILI, WAKUTA UMEHARIBIKA 
Baada ya maelezo ya mzee huyo, vilio vilitawala, hakuna aliyeamini kisha familia kwa kushirikiana na wananchi na jeshi la polisi,

RPC wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msekela.
 walifika nyumbani kwa mzee huyo akaonyesha sehemu aliyomfukia mkewe, polisi wakaamuru mwili huo ufukuliwe ukakutwa umeharibika vibaya, hasa sehemu ambazo mchi ulipiga.Baada ya polisi na madaktari kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, waliwaruhusu wanandugu wauzike. MTUHUMIWA YUKO POLISIKamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Mihayo Msikela (pichani), amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya taratibu za kisheria.

MRITHI WA ZITT KABWE HUYU HAPA


DK SLAA,SALUM MWALIM PAMOJA NA JOHN MNYIKA Uchaguzi ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA leo usiku huu umefikia tamati kwa kamati kuu ya chama hicho kupata viongozi wake wamwisho ambao ni KATIBU MKUU ,NAIBU KATIBU MKUU BARA pamoja na NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR
MATOKEO----

KATIBU MKUU --DK WILLBROD SLAA--
NAIBU KATIBU MKUU BARA---JOHN MNYIKA
NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR--SALUM MWALIM
viongozi awa waliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kama katiba inavyosema na hatimaye baraza kuu likawapitisha wote bila kuwapinga
mh JOHN MNYIKA anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini mh ZITTO KABWE ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na kamati kuu ya chama kwa kile ambacho kilisemekana kuvunja katiba ya chama hicho
FAIDI PICHA ZA USHINDI HAPO CHINI



MCHAWI ADNDOKA KANISANI AKIWA UCHI

Mwanamke anayedaiwa kuwa mchawi akiwa amedondoka Kanisani.

 NI kweli imetokea! Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani) anayedaiwa mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi kutembea.Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa wamezama kwenye maombi ya kufunga.
 Ilidaiwa kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maombi hayo, Nabii Gideon Parapanda aliwahakikishia kuwa usiku huo kutatokea mambo ya ajabu kufuatia maombi hayo. 
Inadaiwa ilipofika saa saba usiku mwanamke huyo akiwa na wenzake watatu, walidondokea kanisani hapo na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani. Mwanamke huyo alikuwa na kitambaa chekundu kikidaiwa ni hirizi, fimbo  nyeusi iliyozungushiwa shanga na alikuwa amejipaka masizi mwilini.
Mwanamke baada ya kudondokea kanisani na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani. 

 Akizungumza na Uwazi, Nabii Parapanda alisema watu hao walidondoka watatu, wawili walifanikiwa kukimbia akabaki huyo mmoja aliyejitambulishwa kwa jina moja la Aisha, mkazi wa Mwananyamala A jijini Dar. 

Baada ya tukio hilo vyombo vya ulinzi, askari wa JWTZ na polisi walifika kwa lengo la kuhakikisha usalama wa eneo  hilo lakini nabii huyo aliomba mtu huyo asichukuliwe hadi atapofanyiwa maombi maalum. 

Ombi la kiongozi huyo lilikubaliwa ambapo Aisha alipandishwa  madhabahuni na kukiri kuwa alikuwa na wenzake watano lakini katika kuanguka walikuwa watatu, wawili walifanikiwa kukimbia bila kusema walikuwa wakitoka wapi kwenda wapi.

Kitambaa chekundu alichokuwa nacho mwanamke huyo.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado  yuko kanisani hapo kwa maombi.”

MTOTO HUYU, MAMA YAKE AMTUPA, KISA MGONJWA!


 
Mtoto Sauda Mohamed aliyeokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake.
 MTOTO Sauda Mohamed (6) mkazi wa Kigogo, Dare s Salaam ameokotwa na wasamaria wema baada ya kutupwa na mama yake ambaye hajafahamika.

Habari zinasema mtoto huyo baada ya kuokotwa alifikishwa katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilala ambako alipokelewanakulelewa.ALIVYOOKOTWASauda aliokotwa na msamaria mwema maeneo ya Buguruni sehemu ya wazi akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi ambaye hajafahamika. 

Chanzo chetu kilisema mara baada ya kuokotwa taratibu zilifanyika kwa kumfikisha Kituo cha Polisi Buguruni kisha akapelekwa moja kwa moja katika kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo, Dar. 


Akifafanua kuhusu tukio hilo mkurugenzi wa kituo hicho, Mwanaisha Magambo alikuwa na haya ya kusema: “Sauda aliokotwa akiwa na umri wa miaka mitatu hata hivyo, walifanya vipimo vya kitaalamu ili kujua umri kwa kumpima kichwa na baadhi ya viungo vya mwili wake. 

“Alipookotwa alikuwa na hali mbaya sana kipindi hicho kwani alilazwa mwezi mzima katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anapumlia mashine na mapigo ya moyo yalikuwa juu sana. 

AGUNDULIKA MATUNDU KATIKA MOYO
“Kutokana na kuwa na hali mbaya, madaktari pale Muhimbili baada ya vipimo wakagundua kuwa ana matundu “Baada ya kugundulika tatizo alipewa dawa za kutumia na akaruhusiwa lakini hali ilibadilika na ikalazimu arudishwe tena Muhimbili ambako amelazwa.”

 
Mtoto Sauda Mohamed akiwa amelala.

 MAANDALIZI YA SAFARI YA INDIA
Magambo alisema kuwa kutokana na maradhi hayo Sauda hivi sasa hawezi kukaa wala kutembea, akitaka kusogea huwa anatambaa.“Mbaya zaidi ugonjwa huo umemfanya Sauda asiwe na uwezo wa kusema na mwili wake umedhoofu ikiwemo miguu.

“Kuna maandalizi yanafanywa ili apelekwe India kwa matibabu zaidi kutokana na ukweli kwamba tatizo lake ni kubwa maana sasa hata kula hawezi,” alisema.
  Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, mlezi wa mtoto huyo, Bi. Magambo alisema amefariki dunia na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar.