Thursday, September 4, 2014

HAIJAWAHI KUTOKEA TANZANIA: MTOTO WA MFUGAJI "MWIGULU NCHEMBA" HAKUNA WA KUMFANANISHA KWA MAENDELEO JIMBONI KWAKE




Mh:Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr.Kone wakati wakukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Maabara za  Kisasa Katika Shule za Jimbo la Iramba,Hapa ni Shule ya Kijiji cha Usule.Kufikia Tar.31/09/2014 Mkuu wa Mkoa anategemea Kumkabidhi Mh:Rais Jakaya Kikwete Maabara zote za Shule za Sekondari zikiwa zimekamilika ndani ya Mkoa wa SIngida kuendana na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
 Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Usule waliofika kusikiliza mambo mbalimbali ya Utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo.Kwaya ya akina mama Kiji cha Usule wakitumbuiza mbele ya
Mgeni Rasmi Mh:Mwigulu Nchemba(hayupo pichani).Vijana wakifurahia Ushindi wao katika Michuoano ya MWIGULU CUP,Hii ni timu ya Kijiji cha Usule.Akina mama wakionesha kadi zao za Chama cha Mapinduzi kuonesha kuwa wao bila CCM haiwezekani.Wananchi wakishangilia baada ya Kuona Nguzo za Umme zikipita kijijini kwao Ishara kuwa Umeme umewafikia.
Mh:Mwigulu akimsikiliza Mmoja wa Wazee wa kijiji cha Usule.Mkutano unaendelea huku Mh:Mwigulu nchemba akiwafafanulia mambo mbalimbali ya maendeleo wanakijiji wa Usule,Kubwa ni Usambazaji wa maji hapo Kijijini ambao tayari umekwisha anza,Pia amesisitiza Kusuka nyaya za Umeme wakati huu Umeme unapowekwa kwenye nguzo,Ukiingiza Umeme wakati huu mafundi wakiwa wanasambaza nyaya ni Bei nafuu 27000/= tu.Ilikukamilisha Ujenzi wa Maabara ya Shule ya Usule Mh:Mwigulu amechangia Mifuko 100 ya Sementi na ameagiza kwenye Upungufu wowote Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi atoe taarifa.Hivyo hivyo amesaidia Uchimbaji wa Bwawa la maji kama Mpango wa Muda mfupi wakati Bomba za Maji zikiendelea Kusambazwa kijiji chote cha Usule.Baadhi ya Vijaja Kijiji cha Kibaya wakiwa kwenye Jezi zao za MWIGULU CUP.Mh:Mwigulu Nchemba akikabidhi Mchango wake wa bati 70 kwa Diwani wa kata ya Mbelekesye kwaajili ya kuezeka Madarasa ya shule ya Mbelekesye yaliyoongezwa.Pia amechangia Mifuko 100 na Mbao kwaajili ya kupau madarasa hayo.
Wakati hili likifanyika katika kijiji cha Kibaya,Mh:Mwigulu Nchemba jana alikabidhi Mabati 320 kijiji cha Misuna kwaajili ya Ujenzi wa Zahanati.Wananchi wakibaya wakifurahia na Mbunge wao.

MUME WA KAJALA...AMUOMBA MKEWE AMTOE GEREZANI

Kajala na mumewe wakiwa mahakamani.

 
Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi kama wanavyoita mastaa wa Kibongo. 
 

Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla. 

Baada ya kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa. 

Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.

SOMA HII NI MUHIMU KWAKO MTANZANIA KUJUA KILICHOELEZWA HUMU.

TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA TOKA WAJUMBE 201 KUHUSU MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

 Sisi Wawakilishi wa Jumuiya na Taasisi za Dini, tuliopendekezwa na Taasisi zetu na baadaye kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na kula kiapo cha utekelezaji wa jukumu hili kubwa.
Tukiamini kuandaa Katiba Mpya kwa maridhiano ya Kitaifa kwa wananchi wote, tulipokea jukumu hili kama wajibu wetu Kitaifa.  Aidha tunaamini kwamba katika kupata maridhiano ya Kitaifa ni muhimu kuheshimu kila wazo na fikra inayotolewa na kuunganisha fikra hizo kwa usahihi, kwa njia ya kidemokrasia kwa kupiga kura na kukubaliana na matokeo ya wengi.
Kama ilivyoelezwa hapo awali, kabla ya kuanza shughuli za Bunge Maalum, kila mjumbe alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo wake na ufahamu wake, kufanya kazi zinazomhusu, bila upendeleo na kumuomba Mwenyezi Mungu amsaidie. 
Tumeshangazwa na kusikitishwa sana kuona kwamba mchakato wa kutayarisha Katiba itakayopendekezwa na Bunge hili kwa wananchi, unachafuliwa taswira yake.  Bunge Maalum la Katiba linachafuliwa na, shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge, Makundi, Taasisi na Vyombo mbali mbali vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli za BungeMaalum la Katiba unapotoshwa.  Wananchi wanaaminishwa yasiyo na ukweli.
Upotoshwaji huu umezua mijadala mbali mbali katika jamii ya Watanzania na bado linaendelezwa kama ifuatavyo:
1.   Kwamba Bunge Maalum la Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hwapo, wakiwepo Bungeni basi uhalalai wake utakuwepo - utapatikana;
2.   Inadaiwa kwamba Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zinavunjwa ovyo ovyo;
3.   Inadaiwa pia, kwamba kinachojadiliwa sasa katika Bunge hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyowasilishwa rasmi Bungeni na kuanza kujadiliwa na wajumbe;
4.   Inadaiwa na watu na Taasisi mbali mbali, kwamba viongozi wa dini, wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na wajumbe wa Kundi la 201, wanapewa rushwa. Isitoshe Vyombo vya habari vimeandika tuhuma kama hizi.
5.   Inadaiwa pia kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni wachache, ukilinganisha na hao walioko nje ya Bunge hilo;
6.   Bunge hili, kwa tuhuma hizo, lazima lisitishwe au livunjwe na Mhe. Rais.
Kabla ya kuanza kuusahihisha upotoshwaji huo, sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini mbali mbali na Wajumbe wa Kundi la 201 katika Bunge Maalum la Katiba, tunapenda kufahamisha umma wa Tanzania mchakato wa kutayarisha Katiba Mpya ulivyo kisheria.
Tunapenda kuwafahamisha Watanzania wenzetu kwamba mchakato huu una hatua tatu kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.  Mpaka hivi sasa ni hatua moja imekamilika.  Hatua ya pili ndiyo inayoendelea, na hatua ya tatu bado haijaanza.
Hatua ya kwanza ni ile ya uandaaji wa Rasimu. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 iliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya kifungu cha tano cha sheria hiyo.  Tume hii ilipewa jukumu la kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba, kuanisha na kuchambua maoni ya wananchi na kisha kuandaa rasimu ya Katiba.  Kazi hiyo ilifanyika kwa kipindi cha takriban miaka miwili na hatimaye Rasimu ya Katiba ilikamilika.
Hatua ya pili ilikuwa ni kuipeleka Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum la Katiba, ambalo liliundwa kwa shughuli maalum ya kuandika Katiba inayopendekezwa, ili ifikishwe kwa wananchi ambao wataamua waikubali au waikatae kwa kuwa wao ndio wenye maamuzi ya mwisho.  Hawa ni Watanzania wote wenye uwezo wa kupiga kura kwa kutoa maoni yao.  Hoja ya Mamlaka ya Bunge hili hatujazungumzia kwa vile imefikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupata tafsiri sahihi ya mamlaka ya Bunge hili.  Tunachoweza kusema ni kwamba jukumu kuu la Bunge hili ni kutengeneza Katiba inayopendekezwa na Bunge ili ifikishwe kwa wananchi  waipigie kura ya maoni.  Hatua hii ya pili bado inaendelea.
Hatua ya tatu ni pale Bunge Maalum la Katiba tutamkabidhi Mhe. Rais Katiba inayopendekezwa ambayo itafikishwa kwa wananchi ili waikubali kama wataridhika nayo au kuikataa kama haikidhi matarajio yao.
Hatua hii ni ya mwisho wananchi wakiikubali tunapata Katiba Mpya wakiikataa, tunaendelea na Katiba tuliyonayo.
Kilichotokea ni kwamba, wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge hili wameamua kuukiuka utaratibu uliowekwa kisheria.  Badala yake wamepeleka Rasimu ya Katiba kwa wananchi wakati mchakato wa kutayarisha Katiba inayopendekezwa bado haujakamilika.
Sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini, ambao kuuhubiri, kuutangaza na kuusimamia ukweli ni moja ya majukumu yetu katika jamii, tumesikitishwa sana na taarifa potofu zinazosambazwa kwa makusudi na makundi, taasisi na vyombo vya habari mbali mbali na tukiwa wajumbe wa Bunge hili ambao tunafahamu kwa kina na tunaridhika na kila hatua ya mchakato huu.  Tuna wajibu wa kusahihisha upotofu huu, unaoendeshwa kwa makusudi na hivi kuwaeleza Watanzania ukweli na hali halisi inayojiri hapa Bungeni.  Watanzania msifadhaishwe na wala msibabaishwe.  Hali ni shwari.  Mchakato unaendelea kwa amani na utulivu.
Katika kusahihisha upotofu unaozungumzwa kupitia mijadala na midahalo mbali mbali katika jamii, tunaomba kufafanua hali ilivyo kama ifuatavyo:-
 
TUHUMA KWAMBA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUKOSA UHALALI
Jambo hili si kweli hata kidogo kwani kuna wajumbe wa aina tatu Bungeni ambao wamewekwa na kutambuliwa kisheria.  Hawa ni kama wafuatao:
1.   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2.   Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
3.   Wajumbe 201 walioteuliwa na Mhe. Rais, baada ya kupendekezwa na Taasisi, Mashirika na makundi mbali mbali nchini,
Uhalali wa Bunge unakuwapo wakati wajumbe kutoka makundi hayo matatu wapo Bungeni, na si Vyama vya Siasa pekee.  Iwapo kwa mfano wajumbe wa 201 wakiamua kutoshiriki katika shughuli za Bunge, basi sehemu moja muhimu ya Bunge haitakuwapo na uhalali wa Bunge hautakuwepo.
Hata hivyo, Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zimeweka idadi ya akidi ambayo ni nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.  Akidi hii ikifikiwa Bunge huendelea na shughuli zake.  Akidi hii hufikiwa kila wakati BungeMaalum linapokutana.  Hii inamaanisha kwamba Bunge Maalum la Katiba linaendesha shughuli zake kwa misingi ya sheria na taratibu zilizojiwekea.  Bunge lina uhalali wa kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria.
 
TUHUMA KWAMBA KANUNI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA ZINAVUNJWA
Suala hilo halijawahi kutokea.  Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zilipitishwa na wajumbe wote kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sheria Namba 83.  Vile vile uendeshaji wote wa shughuli za Bunge zinafanywa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalum.  Kanuni hizo zinatoa fursa ya Bunge Maalum kuzirekebisha pindi inapobainika ipo haja ya kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni Namba 87.  
 
WARAKA MWINGINE UNAJADILIWA NA SI RASIMU YA TUME
Hili nalo si kweli.  Tunawahakikishia Watanzania wote kwamba sisi kama Wawakilishi wa Taasisi za Dini miongoni mwa wajumbe wa Kundi la 201, kwa ujumla tunasema hii si kweli.  Ni upotoshaji wa makusudi.  Tunaijadili Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ibara kwa ibara.  Ibara nyingi zimeachwa kama zilivyo.  Kuna ibara ambazo zimeboreshwa au kurekebishwa, kuna ambazo zimeondolewa na kuna nyingine mpya ambazo zimewekwa ili kuweka mambo ya msingi ambayo Rasimu haikuyazingatia au haikuyaona.
 
WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI, WAJUMBE WA KUNDI LA 201 WA BUNGE LA KATIBA KUPEWA AU KUPOKEA RUSHWA
Sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini na Wajumbe wa Kundi la 201 wa Bunge hili tumesikitishwa sana na taarifa hii iliyosambazwa na baadhi ya watu, na kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari aidha kupitia kwenye mijadala, midahalo na makongamano  mbali mbali.  Baadhi yetu sisi Viongozi wa Kiroho tumeapishwa viapo vya uadilifu katika uongozi wetu wa kiroho na tuko mstari wa mbele kuongoza waumini wetu kuepuka dhambi ya tamaa ya fedha, na kusema uongo.  Taarifa kama hizo hazionyeshi heshima kwa dini au nafasi zetu za kipekee katika uongozi wa kiroho.  Taarifa hizi zinatangazwa kwa makusudi na watu mbali mbali  kupita vyombo vya habari kwa malengo ya kisiasa na kutudhalilisha sisi Viongozi wa kiroho mbele ya umma.  Tunaomba tabia hii ikomeshwe.
 
TUHUMA KWAMBA BUNGE KUWA NA WAJUMBE WACHACHE
Hili nalo si kweli.  Wajumbe wanaohudhuria Bunge wanakidhi akidi inayohitajika kwa mujibu wa kanuni.
 
HOJA YA KUSITISHWA AU KUVUNJWA KWA BUNGE MAALUM
Hii ni hoja inayozungumzwa katika mijadala mbali mbali katika jamii.  Msingi wa hoja hiyo ni kutokuueleza umma ukweli ulioko Bungeni kwa kupeleka taarifa potofu kwa wananchi kwamba Bunge Maalum limekosa mwelekeo.  Hatuoni sababu za hoja hii kutiliwa maanani kwa kuwa hakuna sababu za msingi na za kisheria za kufanya hivyo. 
 
HITIMISHO
Kumekuwa na taarifa mbali mbali zenye malengo ya ama kuingilia shughuli za Bunge hili au kutudhalilisha sisi wajumbe ambao si Wabunge au Wawakilishi.  Wajumbe 201, ambao mchango wao katika mijadala ya Kamati mbali mbali umekuwa na uzito wa pekee, hautambuliki katika taarifa hizo ambazo zimejaa malengo ya kisiasa zaidi kuliko ukamilishaji wa shughuli za Bunge Maalum.
Kuna taarifa nyingine zimesambazwa zikiwa na upotoshaji mkubwa, licha ya kwamba Taasisi zinazosambaza taarifa hizo zina wajumbe wake katika Bunge Maalum.  Wajumbe hao wangeweza kuzielimisha Taasisi zao ukweli ulipo hapa Bungeni, na hivyo kuwafikishia wasomaji wao taarifa zilizo za kweli na ili kulijengea Bunge hili heshima machoni pa umma wa Tanzania na Kimataifa.   Udhalilishaji kama huu unatuumiza hata sisi wajumbe ambao kwa hiari yetu tuliamua kubaki Bungeni na kuyatimiza hayo ambayo tulitumwa tuje tuyakamilishe.
Kama tulivyosema hapo awali ni wajibu wetu kama Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Bunge hili kuutaarifu umma hali halisi katika shughuli za Bunge Maalum na kuwasihi wapotoshaji kwamba wauheshimu ukweli na wawaheshimu watanzania kwa kuwaeleza ukweli.
Ahsanteni sana.  
…………………….                           …………………………
SHEIKH HAMID MASOUD JONGO             ASKOFU AMOS JOSEPH MUHAGACHI
           BAKWATA                                            KIKRISTO

MAJAMBAZI WATANO WAUAWA KIGOMA


Majambazi watano waliokipata cha moto katika Majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakiwa na silaha za kivita wakisubiri kuteka magari Alfajiri ya Septemba 03,2014 wakiwa chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Kasulu.
JESHI la polisi mkoa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha za kivita aina ya SMG, mabomu matatu ya kutupa kwa mkono, risasi 64 pamoja na kuwauwa watu watano wanaosadiliwa kuwa ni majambazi wakati wa purukushani za majibizano baina majambazi hao na askari polisi mkoani Kigoma.Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo kamishina msaidizi wa polisi mkoa kamanda Japhal Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:45 alfajiri Septemba 3 mwaka huu, katika barabara kuu ya Kasulu – Kibondo eneo la pori la Malagalasi Wilayani Kasulu.Kwa mujibu wa kamanda Ibrahim alisema askari polisi wakiwa katika doria walipata taarifa za majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi wakitaka kufanya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha kuteka magari ya wasafiri yaliyokuwa yakipita katika barabara hiyo.Alisema kufuatia taarifa hiyo askari polisi walijipanga na kuweka mtego katika eneo lililokusudiwa kufanyika uhalifu huo ambapo baada ya muda watu hao walifika eneo la tukio ili kukamilisha azma yao ambapo askari waliwafuata ndipo walipoanza majibizano ya risasi na askari polisi.


Katika tukio hilo askari walifanikiwa kuwauwa majambazi wote watano ambapo katika eneo la tukio hilo walikuta mabomu matatu, silaha mbili za kivita aina ya SMG No. 691220 pamoja na AK 47 no. UA40501997 magazini tatu zenye risasi 64 sambamba na mikate na juice aina ya Zaam Zam orange kutoka katika kampuni ya Monas Beverages.
Kamanda alisema miili ya majambazi hao ipo katika hospitali ya wilaya ya Kasulu ambapo majina yao hayajatambulika huku askari polisi waliokuwa katika tukio hilo wakiwa wamesalimika na hakuna aliyejeruhiwa ambapo msako unaendelea katika maeneo yote ili kukomesha vitendo vya uhalifu mkoani Kigoma.


 


 

FFU WABOMOA KIBABE OFISI YA OCD




Ofisi ya OCD ikiwa imebolewa na FFU

FFU wakisimamia zoezi la ubomoaji
Zoezi la ubomoaji  nyumba likiendelea


Kituo cha polisi cha wilaya kikiwa kimebolewa

Wananchi wakishuhudia tukio la aina yake-picha zote na 
Hilali Alexander Ruhundwa-Malunde1 blog-Kagera 
Katika hali ya kushangaza na iliyowaacha vinywa wazi wananchi, askari wa kutuliza ghasia F.F.U wamesimamia zoezi la kubomoa kituo cha polisi cha wilaya pamoja na nyumba wanazoishi askari polisi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kupisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 59.1 toka Kyaka wilayani Missenyi hadi Bugene wilayani Karagwe kwa kiwango cha lami.

Ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi (OCD) pamoja na nyumba za makazi ya askari polisi vimebomolewa na kampuni inayojenga barabara hiyo China Henan International Group (CHICO) ndiyo iliyoendesha zoezi hilo la bomoabomoa chini ya usimamizi wa F.F.U baada ya maaskari polisi kudaiwa kugoma kuhama.

Ni tukio lililovuta makini ya wengi huku minong'ono ikitawala ya ukosoaji wa kauli ya polisi "Utii wa sheria bila shuruti", wakihoji maana yake kwani nao (polisi) wamekaidi kutii sheria hadi kuletewa F.F.U kuwashughulikia endapo wangejaribu kuleta fujo.

Meneja wa TANROADS mkoa wa Kagera John Kalupare alipopigiwa simu kuelezea tukio hilo amesema yupo safarini Dar es Salaam na asingeweza kuzungumzia suala hilo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe alipopigiwa simu juu ya tatizo hilo, simu yake imeita bila kupokelewa.

Mmoja wa maofisa wa TANROADS aliyekuwa anasimamia zoezi hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe, amesema kuwa wao wanaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao.

 "Sisi TANROADS tunaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao na kituo chao hivyo waulize wao kwanini ubomoaji unafanywa chini ya ulinzi mkali". amesema.

Hata hivyo zoezi hilo limeingiwa na dosari baada ya kundi la nyuki kutokea na kuwashambulia wabomoaji, maaskari na mashuhuda wa tukio hilo huku dereva akilazimishwa na wachina kuendelea na ubomoaji licha ya kung'atwa na nyuki hao.

Ni tukio linaloshangaza na kuitia doa serikali kwa jeshi la polisi lenye dhamana ya kulinda usalama na raia ambalo daima huhubiria raia utii wa sheria bila shuruti sasa linaenda kinyume hadi kuletewa F.F.U kulisimamia.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya Karagwe hakupatikana kuzungumzia sakata hilo ambapo inadaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itaigharimu halmashauri hiyo baadhi ya ofisi zitakazobomolewa ikiwemo ofisi za wabunge wa majimbo ya Karagwe na Kyerwa.

HUU NDO USHABIKI WA DAMU

Huu ndio ushabiki unaotakiwa uzalendo mpaka siku ya harusi si mchezo




Tazama hii ndo ilikua keki